Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing (Kulia) akizungumza katika
hafla hiyo (kutoka kushoto)ni Mkurugenzi wa Maisha Plus, Masoud Ally na
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Monica Gorman.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Monica Gorman (Kulia) akizungumza katika
hafla hiyo, kushoto ni Mkurugenzi wa Maisha Plus, Masoud Ally.
Meneja Mawasiliano wa NMB Josephine Kulwa akifafanua jambo.
Mpango wa Mama Shujaa wa chakula unaoratibiwa na shirika la Oxfam ulianziashwa mwaka jana hapa Tanzania. Dhumuni likiwa ni kuthamini, kuwahamasisha na kuwasaidia wanawake wote katika uzalishaji wa chakula.
NMB kwa kutambua kuwa kilimo ndiyo shughuli kuu ya uchumi Tanzania na ikiwa benki yenye mtandao mpana zaidi Tanzania imetoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuunga mkono mpango huu wa Mama Shujaa wa chakula kupitia kipindi cha televisheni kiitwacho Maisha Plus kinakachotarajiwa kurushwa mapema Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bw. Mark Wiessing alisema,
udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake.
“Tumeamua kudhamini mpango huu kwa lengo la kuwasaidia kinamama ambao ni wazalishaji wadogo wa mazao mbalimbali,ili waweze kupiga hatua katika kilimo kupitia mpango huu wa Mama shujaa wa chakula”alisema Mark.
Katika kuchochea maendeleo ya kilimo, NMB ni benki ya kwanza kuanzisha akaunti maalum kwa ajili ya wakulima iitwayo NMB Kilimo Account. Pia imeanzisha huduma ya mikopo kwa ajili ya mazao mengi ya kilimo ikiwemo chai,kahawa,miwa,alizeti,korosho na mazao mengine.
Mbali ya kutoa fedha na kusaidia wakulima katika maeneo mabalimbali, NMB imeongeza mikopo zaidi katika sekta ya kilimo hasa kwa wasambazaji na watengenezaji wa chakula toka mzalishaji mdogo hadi wasambazaji wakubwa.Vilevile NMB imesaidia vyama vya ushirika zaidi 600 vyenye zaidi ya wakulima 500,000 ambao ni wanachama.
NMB kupitia mpango wa NMB Finacial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha itapata fursa ya kuwaelimisha washiriki kuhusu huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya kifedha na mengine mengi.Kama msemo wa kiswahili unavyosema” Ukimwelimisha mwanamke umeelimisha Jamii” .NMB inaamini NMB financial Fitness itamwezesha kila mwanamke kuwa na matumizi mazuri ya kifedha na kuwa na msingi mzuri wa maisha.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam ,Monica Gorman pamoja na Mkurugezi wa Maisha Plus kwa nyakati tofauti waliishukuru NMB kwa mchango wake wakiamini washiriki 15 wa Mama shujaa wa chakula na 15 toka Maisha plus watafaidika na mpango wa NMB Financial Fitness. Chanzo: www.fullshangweblo.com
No comments:
Post a Comment