Naye Mkurugenzi wa Machozi Entertainment, Gadner G Habash, alisema kwamba kutokana na vigezo vya warembo hao ni kutoka ndani ya vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga wamekuwa kambini wakijinoa kwa wiki mbili sasa katika Club ya Nyumbani Lounge, iliyopo maeneo ya Namanga, hapa Jijini.
Alisema Walimbwende hao wamekuwa akinolewa na Miss Ilala 2008, Sylvia Mashuda, ambaye pia ni mshindi wa pili Miss Tanzania 2009, akimfuatia Nasreen Karim aliyetwaa taji.
Nayo Kamati ya maandalizi ya shindano la Redd’s Miss Ilala 2012, leo inatarajiwa kuwaanika warembo 15, watakaowania umalkia wa taji hilo, linaloshikiliwa na Miss Tanzania, Salha Israel.
Hadi kufikia sasa wadhamini waliothibitisha kudhamini kudhamini shindano hilo ni pamoja na City Sports Lounge, gazeti la Jambo Leo, Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, Uhuru One, 88.4 Clouds FM na Redd’s Premium Cold.
Kinyang’anyiro cha kumsaka Redd’s Miss Ilala 2012 kitarindima Septemba 7 mwaka huu, katika sehemu ya nje ya Nyumbani Lounge.
No comments:
Post a Comment