Thursday, January 31, 2013

Taswira bungeni leo

  Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki(katikati) pamoja na Mbunge wa Viti maalumu  ster Bulaya(kushoto)katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
 Mbunge wa Iramba Magharibi Mwingulu Nchemba (kulia) akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari leo Dodoma katika viwanja vya Bunge-




Mwanasheria Mkuu Mkuu wa Serikali Mh. Jaji Frederick Werema (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Wazir wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla leo Bungeni mjini Dodoma.

 Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

GET WELL SOON MY LOVELY DAD.

 Mungu Akikuacha katika hali fulani,Basi mshukuru wala usilalamike! Yeye ndie Akujuae zaidi.Pia usidhani kama maisha yamekamilika kwa mtu yeyote ,kuna wenye nyumba hana gari ,kuna mwenye gari hana watoto ,kuna mwenye watoto hana pesa, kuna mwenye pesa hana afya kuna mwenye afya hana kazi ,kuna mwenye vyote lakini hana amani wala furaha, Mshukuru Mungu jinsi Ulivyo.Tunakupenda tunakuombea. GET WELL SOON MY LOVELY DAD.Jopo lote la Tanzania Asilialive ipo nawe katika Maombi Hakika mungu ni mwema Hashindwi na jambo Namtumainia yesu kila sekunde ya uhai wangu hawezi niacha kamwe.

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI NA ASKARI WENZAKE WAMDHARAU HAKIMU, WAOMBA MSAMAHA‏



 Askari  polisi wakimrejesha mahakamani mtuhumiwa  wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa Channel Ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa  wa Iringa Daudi Mwangosi, askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (aliyevaa kofia nyekundu)  baaada ya kutoroshwa  kizimbani kabla ya mahakama kumaliza shughuli zake jana.

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO


 Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mhe Freeman Mbowe (kulia), Mhe Godbless Lema (katikati- Arusha mjini) pamoja na Mbunge wa Musoma Mjini, Mhe Vicent Nyerere wakielekea katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo. Mbunge Lema amerudi tena Bungeni baada ya kushinda kesi yake.

Katuni wa KP ..........Mafuta Yakigunduliwa Tarime ITAKUWAJE...?


JK-Tunajua biashara ya dini inalipa, lakini msiivuruge Tanzania

“Kuna baadhi ya watu wanatumia vigezo vya kidini kwa ajili ya kufanya vurugu za kuhatarisha amani, Serikali haitaweza kuwavumilia, badala yake tutatumia njia mbalimbali RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa mtindo wa kufanya fujo na kusababisha uvunjifu wa amani kwa visingizio vya dini nchini ni biashara inayolipa na ndiyo maana...wakereketwa wa kufanya hivyo hawaishi.

Hata hivyo, akaonya kwamba Serikali katu haitawavumilia wanaotaka kuwavuruga Watanzania kwa kutumia dini zao.

Kikwete aliyasema hayo wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mchakato wa Nchi za Afrika Kujitathmini zenyewe katika nyanja za Demokrasia, Utawala Bora na Uchumi (APRM) nchini Ethiopia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Dr.Migiro mkuu mpya chuo kikuu huria

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.

Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

IKULU

DAR ES SALAAM

30 Januari, 2013

Magazeti ya leo Alhamisi ya 31th January 2013



AMANDA WA BONGO MOVIE AMTAMBULISHA "BWANA MISOSI" KWA WAZAZI WAKE

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Mohamed ‘Amanda’ amemtambulisha mume wake mtarajiwa, staa wa Bongo Fleva, Joseph Rushau ‘Bwana Misosi’ kwa wazazi wake.

Tukio hilo lilichukua nafasi mwishoni mwa wiki iliyopita pande za Msasani Beach, jijini Dar wakati mwigizaji huyo alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa, ndipo alipotumia nafasi hiyo kumtambulisha Bwana Misosi kwa mama yake mzazi na mjomba wake.

“Kula keki na kunywa shampeni pamoja na mama yangu, mjomba, mama Dotnata na wageni waalikwa ni ishara tosha kwamba Misosi umekubalika katika familia yetu, jisikie uko nyumbani,” alisikika Amanda.

Katika shughuli hiyo, Amanda alimuandalia mpenzi wake huyo ambaye ni mwanamuziki keki maalum yenye muonekano wa gitaa kama ishara ya upendo kwake.

"CHANZO CHA VURUGU ZA MTWARA NI MPASUKO NDANI YA CCM NA HARAKATI ZA WANASIASA ".....HII NI RIPOTI YA WAZIRI MKUU

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari kwenye makazi yake mkoani  Dodoma jana kuhusu hatua zilizochukuliwa kudhibiti vurugu za gesi mkoa wa Mtwara.Kulia ni waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel

Madai kwamba gesi hiyo inapelekwa Bagamoyo yalikuwa moja ya ujumbe mkuu uliokuwa umeandikwa kwenye baadhi ya mabango wakati wa maandamano ya Desemba 27 mwaka jana yaliyofanyika Mtwara Mjini, yakiratibiwa na baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani.

LULU MICHAEL AKATAA KUFANYIWA "SHEREHE" YA KUPONGEZWA KUINGIA URAIANI

January 29 2013 ndio msajili alithibitisha kwamba mwigizaji Lulu ametimiza masharti yote ya dhamana juu ya kesi inayomkabili ya kuua bila kukusudia na hivyo  kumwachia  kwa dhamana.....

Lulu na mama yake mzazi wote kwa pamoja waliangua vilio baada ya dhamana yao kukamilika wakati wakiwa nje ya Mahakama kabla ya kuondoka na Lulu kuingia uraiani.

Kabla  ya dhamana  hiyo kulikwa  na  tetesi  kwamba  Lulu angefanyiwa  sherehe kubwa  ya  kupongezwa  kuja uraiani.

Kwa mujibu wa ndugu yake  wa karibu, Lulu amegoma  kufanyiwa sherehe  na  badala  yake jana aliwaomba  watanzania  wamuombee  kwa  mungu  maana  kesi bado inaendelea.....

 “Nawashukuru watu wote na nilikua naomba watu waendelee kuniombea sababu hii ni dhamana tu lakini kesi bado ina safari ndefu… nawashukuru wale wote waliokua na mimi kwa hali yeyote ile na zaidi zaidi namshukuru sana Mwenyezi Mungu”....LULU

BAADHI YA PICHA ZA KIWANDA CHA CHEMICOTEX-AFRICANA, DAR KIKITEKETEA KWA MOTO JIONI JANA




WEMA SEPETU AAMUA KUTOKA KIMAPENZI NA "SERENGETI BOY" ILI KUMUUMIZA DIAMOND PLUTNUM

 Wema Sepetu  ameamua  kuhamishia majeshi  yake  kwa  kiserengeti  boy  ili  kulipiza  kiasi  kwa X wake  wa zamani, DIAMOND.....

Huyu  ni  Haidary Cavilla  ambaye  ni mchumba  wa  miss  Tanzania namba  2 ,mwaka  2000, aitwaye  Mercy Galabawa....

"NIMEANDAA FILAMU MPYA AMBAYO NITAMSHIRIKISHA LULU MICHAEL"....JACKLINE WOLPER

MSANII wa filamu Tanzania Jackline Wolper ameandaa filamu mpya atakayoshirikiana na  msanii maarufu Elizabeth Michael 'Lulu' itakayokamilika hivi karibuni baada ya msanii huyo kutoka gerezani kwa dhamana

Akizungumza na Maisha Wolpa alisema amepata faraja baada ya taaratibu na sheria kufuatwa na hatimaye Lulu kuweza kupata dhamana hivyo anatarajia kufanya naye kazi ya filamu mpya itakayoanza kurekodiwa baada ya msanii huyo kufika uraiani

Alisema kuwa anatarajia atafanya vizuri katika filamu hiyo kwani tangu awali alikuwa akifanya vizuri katika tasnia hiyo ya uwigizaji kabla ya kupatwa na matatizo

PICHA ZA LULU MICHAEL AKIWA HURU URAIANI.....

                               Lulu akiwa ndani ya gari baada ya kukamilisha dhamana yake.
                           Lulu (katikati) akitoka eneo la mahakama baada ya kukamilisha dhamana yake.
                                                 Gari lililombeba Lulu likiondoka mahakamani.
 Kutoka kushoto ni mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, wakili wa Lulu bwana Kibatala na Dk. Cheni wakijadili jambo wakati wakisubiri dhamana ya Lulu.
                                  Lulu akishuka katika gari la polisi baada ya kuwasili mahakamani.
                         Lulu akiingia katika chumba cha msajili wa mahakama ili kukamilisha dhamana yake.
               Lulu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kupata dhamana.

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba Aprili 7, 2012 bila kukusudia baada ya kukamilisha taratibu zote za dhamana.

Friday, January 25, 2013

St.Johns university walipoandamana






Wanachuo wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwa mkuu wa mkoa hii ni kushinikiza ulinzi kwa sababu ya matukio ambayo yanaendelea kutokea maana juzi alifariki mwanachuo na usiku wa kuamkia leo wanachuo walivamiwa vyumbani  baada ya kukata nondo ya dirisha na kuiba Laptop tatu na simu tano na baada ya kuchukua vitu hivyo waliacha wamewafanyia vitendo vibaya na pia waliachwa wamefungwa ili wasipige kelele.

Kwa hali hii  imesababisha maandamano ili kushinikiza ulinzi katika chuo cha St. John kilichopo Dodoma mjini.

Magazeti ya leo Ijumaa ya 25th January 2013


TAARIFA KUHUSU DHAMANA YA MWIGIZAJI LULU AMBAYO ILIKUA ITOKE LEO.

                                                         Elizabeth Michael.

Jana kwenye Exclusive on millardayo.com kulikua na stori kwamba uwezekano wa mwigizaji Lulu kuachiwa kwa dhamana january 25 2013 ulikuepo.

Ni kweli ilikua iwe hivyo lakini kwa taarifa  zilizotolewa kwa Millard Ayo ni kwamba dhamana hiyo imeshindikana kutolewa leo.

Sababu kubwa ni leo kuwa sikukuu hivyo shughuli imesogezwa mbele mpaka jumatatu january 28 2013.

Mwanzoni Lulu ambae anatuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia ilidaiwa alikua anatakiwa apate dhamana ambayo milioni 20 zilihitajika (kwa mujibu wa taarifa za ndani) ila ikashindika sababu jaji alipata udhuru.

Lulu amekua chini ya ulinzi toka kifo cha mwigizaji staa wa movie Tanzania Steven Kanumba April 2012.

Chanzo:Millard Ayo

Sitta: Nafaa kuwa Rais

“Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri nigombee,” Akizungumza katika mahojiano (soma zaidi hapa)

maalumu na gazeti hili juzi, Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri. Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

MISS UTALII VIPAJI KUFANYIKA TAREHE 27.01.2012

 Tamasha kubwa la vipaji litafanyika katika Ukumbi wa Ikondolelo Lodge  Hoteli ya Kitalii  Kibamba Jumapili hii, ambapo warembo zaidi ya Thelasini   wataingia katika kuonesha vipaji mbalimbali vikiwemo na, Kucheza ngoma, Kuimba, pamoja kuonesha mavazi mbalimbali ya Asilia.

Katika Tamasha hilo Maalum Mgeni Rasmi atakuwa Muheshimiwa Iddy Azan Zungu  Mbunge wa  Jimbo la kinondoni. Sambamba na Hayo Muheshimiwa Zungu atazindua tuzo Mbalimbali za Utalii Tanzania, kama Tuzo ya Mazingira, Tuzo ya Utamaduni, Tuzo ya Jinsia, wanawake na watoto, Tuzo ya Polisi Jamii, Tuzo ya Elimu ya Jamii, Tuzo ya Hifadhi ya Serengeti, Tuzo ya Mlima Kilimanjaro, Tuzo ya Michezo pamoja na Tuzo  zengine mbalimbali.

Viingilio katika Tamasha hilo vitakuwa kama ifuatavyo, V.I.P 20,000 , Watu wa kawaida 10,000 na watoto 5,000.

Tamasha litaanza kuanzia sa nane mchana na kuendelea.

Asante.

Fredy Tony Njeje

Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano

JAPAN YAIPA TANZANIA BILIONI 28.2 KUBORESHA BARABARA NA KILIMO, MAKUTANO YA TAZARA KUWA NA BARABARA ZA JUU KWA JUU

 SERIKALI ya Japan imepatia Tanzania msaada wa shilingi bilioni 28.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mitatu ya uboreshaji wa usafiri jijini Dar es salaam na kilimo hapa nchini.

 Msaada huo umesainiwa (leo) jijini Dar es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Masaki Okada kwa niaba ya Japan na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa kwa niaba ya Serikali ya Tanzania.

 Akizungumza mara baada ya kusaini msaada huo Waziri wa Fedha Dkt . Mgimwa alisema kuwa mradi wa kwanza utahusisha upanuzi wa barabara ya Kilwa na ile ya Bandari ambapo jumla ya shilingi bilioni 20 zitatumika katika kukamilisha mradi huo.

 Aliongeza kuwa mradi mwingine ni ule wa ujenzi wa barabara za juu(flyover) katika makutano ya TAZARA ambapo jumla ya shilingi bilioni moja (1) na milioni 26 zinatarajiwa kutumika katika kukamilisha mradi huo.

 Dkt. Mgimwa aliongeza kuwa eneo lingine ambalo litanufaika na msaada kutoka Japan ni kuunga mkono sera ya Kilimo kwanza ambapo Tanzania imepata shilingi bilioni sita(6) na milioni 92 kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwepo kwa usalama wa chakula cha kutosha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

 Alisema kuwa upande wa eneo hilo lengo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wa kipato cha chini wanaboresha kilimo ambacho kitawahakikisha uhakika wa chakula wakati wote na hivyo kuondokana na umaskini.

 Kwa upande wa Balozi wa Japan hapa nchini Masaki Okada alisema kuwa wananchi wengi wa Tanzania hasa wakazi wa Jiji la Dar es salaam wamekuwa wakisubiri kwa hamu barabara za juu ili kusaidia kupunguza msongamano wakati wa kuja na kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam.

 Alisema kuwa utakapo kamilika mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la msongamano na hivyo kupunguza saa za mwananchi kusafiri kuja na kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam.

 Balozi Okada alisema kuwa hatua hii itakuwa muhimu katika kukuza uchumi kwani wananchi watakuwa na muda wa kutosha kuzalisha mali kutoka na miundombinu kuruhusu magari kwenda kasi pasipo kikwazo.

Thursday, January 24, 2013

YANGA YADHIHIRISHA UBABE WAKE KWA BLACK LEOPARDS, YAIFUMUA 2-1 CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

 Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
                                   Umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo

RAIS WA ZANZIBAR DK. MOHAMED SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA, ALFONSO LENHARDT IKULU MJINI ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.
(Picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar)

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA FIFA MJINI ZURICH SWITZERLAND

 Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, akiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Joseph Sepp Blatter na Rais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Leodgar Chilla Tenga (kulia) wakati Rais Kikwete na ujumbe wake walipotembelea Makao Makuu ya FIFA mjini Zurich, Switzerland jana Januari 23, 2013 kwa Mwaliko maalum wa FIFA.
 Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Joseph Sepp Blatter wakiwa katika mazungumzo wakati Rais Kikwete na Ujumbe wake walipotembelea Makao Makuu ya FIFA mjini Zurich, Switzerland Januari 23, 2013 kwa Mwaliko maalum wa FIFA.
  Rais wa FIFA Joseph Sepp Blatter akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete bendera maalum ya FIFA.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, akimweleza jambo Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Joseph Sepp Blatter (kulia) kuhusiana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodgar Chilla Tenga. Tenga pia ni Mwenyeketi wa  Baraza la Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki (CECAFA).

Magazeti ya Leo Alhamisi ya 24th JAnuary 2013