Thursday, January 17, 2013

SERIKALI YABARIKI FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13

Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Baraza la Sanaa la Taifa, limebariki kufanyika kwa Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 baada ya kuridhishwa na maandalizi yaliyo fanywa na Miss Tourism Tanzania Organisation waandaaji wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo kitaifa na kimataifa, pia kwa kuzingatia sheria za nchi, kanuni na Taratibu za mashindano.

Serikali pia imeridhishwa na jinsi Fainali za ngazi za mikoa na kanda zilivyofanyika kwa mafanikio,ambapo kila mkoa umepata washindi wenye sifa za kuwakilisha mkoa husika katika Fainali za Taifa mwaka

huu,ambapo jumla ya warembo 60 waingia rasmi kambini kesho katika hoteli ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam, kuanza mbio za kuwania Taji hilo la Taifa.

Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia yakiwemo ya International Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation, Miss Heritage World, Miss Tourism

University World, Miss Globe International n.k Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya

Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism Model Of The World 2008-Personality n.k Fainali za Taifa mwaka huu zimepangwa kufanyika wiki ya kwanza ya Februari ,wilaya ya Temeke na mkoa wa Dar es Salaam ukiwa umepewa

heshima ya kuwa wenyeji wa Fainali hizo.

Asante,

Erasto Gideon Chipungahelo

Rais

No comments: