Friday, January 4, 2013
TANAPA WAONGEZA MUDA WA KUWASILISHA KAZI ZA KUSHINDANIWA
Kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza na kuibuliwa na wadau wa habari nchini kuhusiana na siku ya mwisho ya kuwasilisha kazi za kushindaniwa, Waandaaji wa TANAPA Media Awards 2012 wamesogeza mbele tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kazi hizo kutoka 31.12.2012 na kuwa tarehe ya mwisho sasa itakuwa 31.01.2013.
WASHIRIKI:
Tuzo hizi ziko wazi kwa wanahabari wote nchini kutoka katika Magazeti, Redio na Runinga. Ili uweze kutimiza sifa za ushiriki wako katika tuzo za TANAPA Media Awards 2012, unatakiwa kuwasilisha kazi zote zilizochapwa na kutangazwa katika kipindi cha kuanzia tarehe 01 Januari, 2012 hadi 31 Disemba, 2012.
JINSI YA KUSHIRIKI
Wanahabari wanaweza kushiriki kwa kutuma kazi zao kwa kiwango cha juu cha kazi tatu kwa kila kundi. Wanahabari watakaoshiriki tuzo hizi watapaswa kujaza fomu maalum za ushiriki zinazopatikana katika tovuti ya shirika www.tanzaniaparks.com
MAKUNDI
A Tuzo ya Utalii wa Ndani katika Hifadhi za Taifa Redio (washindani watatu)
Runinga (washindani watatu)
Magazeti (washindani watatu)
B Tuzo ya Uhifadhi katika Hifadhi za Taifa Redio (washindani watatu)
Runinga (washindani watatu)
Magazeti (washindani watatu)
Kazi zinaweza kuwasilishwa katika lugha ya kiingereza au Kiswahili. Tuzo: Washindi kwa kila kundi watapata tuzo zifuatazo:
Mshindi wa Kwanza
Fedha taslimu Sh. 1,500,000, Ngao, Cheti na Safari ya mafunzo katika moja ya nchi za SADC
Mshindi wa Pili
Fedha taslimu Sh.1,000,000, Ngao na Cheti
Mshindi wa Tatu
Fedha taslimu Sh.500,000 na Cheti
Mwisho wa kuwasilisha
Kazi zote zinatakiwa kuwa zimewasilishwa Makao Makuu ya TANAPA hadi kufikia tarehe 31.01.2013.
Anuani ya kuwasilisha kazi:
Mkurugenzi Mkuu
Hifadhi za Taifa Tanzania
AIONE: Meneja Uhusiano- TANAPA Media Awards 2012
SL.P. 3134
Arusha, Tanzania
Au, ziletwe kwa mkono Makao Makuu ya TANAPA, Barabara ya Dodoma, Chumba Namba.32.
Au barua pepe: prm@tanzaniaparks.comImetolewa na
Pascal Shelutete
MENEJA UHUSIANO
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
04.01.2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment