Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha
Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali
ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya
Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo Januari 05, 2013
katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake
Mama Asha amewahasa vijana hususan wanafunzi hao waliohitimu masomo
kutokukubali kutumika na watu wenye maslahi binafsi na kujikuta
wakisababisha uvunjifu wa amani. Aidha amewataka kutojihusisha na
makundi yanayochochea uvunjifu wa amani bila kujitambua wafanyalo,
badala yake amewaomba kuwa wakipima kila wanaloambiwa kuwa linamaslahi na
dini yao ama maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi mhitimu wa Kidato cha Sita, Zuhura Azmin, kwa kuwa mmoja kati ya waliofanikisha sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza
No comments:
Post a Comment