Wednesday, April 3, 2013

WAZIRI MKUU AHUDHURIA MISA YA PAMOJA JIJINI ARUSHA YA KUAGA MAREHEMU WALIOFUKIWA NA KIFUSI

                                       Sehemu ya majeneza ya marehemu katika ibada hiyo maalumu leo

 Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha. Maporomoko hayo yametokea jana na kusababisha vifo vya watu13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru



 Waziri Mkuu akiwa na wabunge wa Arusha na Meya pamoja na mkuu wa mkoa kwenye msiba huo mzito. Toka Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulongo, Meya wa jiji la Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari na Mbunge wa kuteuliwa Catherine Magige
 Kiongozi wa dini akiombea marehemu waliofariki kwa kuporomokewa na Moramu
 Waziri Mkuu akipeana mkono na Askari wa Jeshi la Wananchi (jwtz) alipotembelea eneo la tukio.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoka eneo la tukio katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili.
Waziri mkuu Mizengo pindaakiongea na familia, ndugu na jamaa wa marehemu walioporomokewa na moramu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowasili mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Maunti meru.

Picha zote na Chris Mfinanga

No comments: