Mwili wa marehemu Nyaga Paul Mawalla ukiwa katika kanisa la Kilutheri nchini Kenya usharika wa Uhuru Highway kwa ajili ya misa
Mazishi ya Marehemu Nyaga Mawalla, aliyekuwa Mwasisi na Mkurugenzi wa
Makampuni ya Mawalla ya Jijini Arusha yamefanyika jana jijini Nairobi
Kenya katia Makaburi ya Jumuia ya Langata.
Mapema kabla ya
Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na
familia na marafiki ilifanyika Misa ya kumuombea Marehemu katika Kanisa
la KKKK, Uhuru Highway.
Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria Mazishi hayo ni Balozi wa Tanzania
nchini Kenya, Dk. Batilda Burian, Viongozi wastaafu, Sir. George Kahama,
Mwemyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Wabunge, Mawaziri wanasheria
mabalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.
Marehemu Nyaga Paul Mawalla alifariki Machi 22, 2013 jijini Nairobi alikokuwaa amelazwa kwa matibabu Hospitali ya Nairobi.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili
Lazaro Nyarandu na Sir George kahama wakiwa kanisani wakishiriki misa ya
maziko ya marehemu Nyaga Mawalla.
Picha Zaidi Chini
Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Godbless Lema Chadema ni miongoni mwa waombolezaji waliokuwa kanisani nchini Kenya.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Buriani akiwa na mwanasheria
maarufu Jijini Arusha anayemiliki kampuni ya uwakili ya Law /Access
Advocates Mosses Mahuna wakiwa nje ya kanisa la Lutherani nchini Kenya.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro wilani Simanjiro mkoani Manyara Christopher
Ole Sendeka na Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Laurence Marsha
wakiwa kanisani nchini Kenya maziko ya marehemu Poul Mawalla
Familia ya Marehemu Nyaga Mawalla wakiwa wenye simanzi nzito wakati wa Mazishi hayo.
Kiongozi wa Dini wa Kanila la Kilutheri Kenya la Uhuru Highway akiongoza Mazishi.
Sir George Kahama na mkewe wakiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu Nyaga Mawalla.
Jaji Mark bomani nae alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji walioshiriki mazishi hayo.
Mwenyejiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mkewe wakiweka shada la maua
Baadhi ya jamaa wa karibu wa Marehemu Nyaga ambao ni wabunge wakiweka Shada la Maua
Wabunge na Mawaziri mbalimbali wa serikali ya Jamhurti ya Muungano wa Tanzania, wakiweka mashada ya maua.
Watoto wa Marehemu Nyaga wakiwa na ndugu zao.
Wanafamilia wakiweka mashada ya maua
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, dk. Batilda Buriani akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Nyaga
No comments:
Post a Comment