Saturday, June 16, 2012

KUHUSU PREZZO KUJITOA BIG BROTHER.


Ishu ambayo imewashangaza wengi ni pale ambapo mwakilishi wa Kenya kwenye jumba la Big Brother CMB Prezzo kutangaza kwamba amechoka maisha ya kuishi kama mfungwa kwenye jumba hilo.

Mtandao wa Ghafla Kenya umeripoti kwamba hii ishu imetokea wakati Big Brother alipotangaza kupiga marufuku pombe kwa washiriki ndani ya jumba hilo, Prezzo alishikwa hasira na kusema kwamba anaweza kuondoka muda wowote, na anahisi wakati umefika.

Prezzo alimaind mpaka akawa anabishana na washiriki wenzake akiwemo Keita na kutaka mlango ufunguliwe aondoke lakini baadhi ya washiriki wenzake walimsihi asifanye hivyo.

Huu mchongo umetokea siku 30 baada ya Prezzo kuwa trending topic kwa wakenya kutokana na kuchaguliwa kwake kwenda big brother ambapo wengi walikua wanamdiss kwamba haikutakiwa apelekwe BBA.


Monday, June 11, 2012

R .I .P BOB MAKANI

Viongozi mbalimbali na wananchi wakiwa Karamjee Kuaga mwili wa mwaasisi wa CHADEMA BOB MAKANI.kwa picha zaidi tembelea www.mjengwablog.com

CCM ILIVYOFUNIKA JANGWANI Saturday, June 9, 2012

 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akihutubia
Vijana wakishangilia kwenye mkutano wa CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli akihutubia
Vijana wakichangamka kurudisha kadi za Chadema mbele ya Nape na Kinana ambazo chama cha chadema kilidai kuwa zilikuwa za fake wakihoji iweje zote ni mpya na zingine hazina hata majina.
Mamia ya kadi za vyama vya upinzani zilizorudishwa
 
Nape akichaza gita na bendi ya Vijana Jazz, Baadhi ya mabango

Wanafunzi UDOM wajitolea damu


Afisa habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosoholojia aliyemaliza rasmi muda wake leo ambaye pia ni Mmiliki wa Mtandao wa LUKAZA BLOG Mh Josephat Lukaza akiwa tayari ameshamaliza zoezi la uchangiaji wa Damu kwa Hiari ambalo liliandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuo Hapo.Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma wakiwa Wanasubiri Kwenda Kutoa damu kwa hiari

TOVUTI YA NGOMA AFRICA YARUDI HEWANI

Web ya  Ngoma Africa band aka FFU hewani tena baada ya matengenezo ya masaa machacheTovuti ya bendi maarufu ya dansi barani ulaya Ngoma Africa band hipo hewani tena baada yakufanyiwa marekebisho fulani ya kiufundi kwa masaa machache jana Juni 10 , 2012 , Kambi hiyo ya FFU at www.ngoma-africa.com inaendelea kumwaga burudani kamiliya muziki kama kawaida masaa 24 kwa siku 7 za wiki. wadau wote mnaombwa kuendelea kupata raha ya muziki bila kwikwi  bofya at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

AJALI JAMANI

Habari za Leo wadau wote. Jamani leo ningependa kuwaonya baadhi ya madereva ambao hawako makini na kazi zao siku ya jana jumapili ya tarehe 10 /6/2012 nimeshuhudia ajali nne moja kati ya hizo ndugu zetu, walipoteza maisha inasikitisha sana jamani.Embu tuwa makini sana tunapokuwa barabarani ili kupunguza vifo jamani tunazalisha yatima jamani. TARAKARI CHUKUA HATUA.

Sunday, June 10, 2012

HONGERA TAIFA STARS

 Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza mechi ya leo.
Taifa Stars imeilaza Gambia kwa bao 2-1 katika mechi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil 2014. Mabao ya Stars yamewekwa kimiani na Shomari Kapombe na Erasto Nyoni. Kwa sasa Stars ina pointi 3 na inashika nafasi ya pili katika kundi C linaloongozwa na Ivory Coast wenye pointi 4.

BOB MAKANI HATUNAYE TENA

Mzee Bob Makani enzi za uhai wake.
Naibu Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chadema, ambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Bob Makani, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam.
Habari za kifo chake zimetolewa na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye amesema kuwa, Bob Makani amefariki dunia, baada ya kuugua kwa muda mrefu, na mwili wake umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kufuatia kifo cha mwasisi huyo wa chama hicho, sasa Chadema wamekatisha ziara za kuimarisha uhai wa chama zilizokuwa zikiendelea katika mikoa ya kusini mwa Tanzania.

Saturday, June 9, 2012

Picha za maonesho ya Karibu Fair 2012 yaliyofunguliwa na Naibu Waziri, Nyalandu
















Zifuatazo ni picha chache kati ya nyingi kutoka kwenye blogu ya tembeatz.blogspot.com zinazohusu maonesho hayo.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu leo mchana amezindua rasmi maonesho makubwa ya sekta ya Utalii ya Karibu mjini Arusha. Baada ya kuwasili katika viwanja vya Maonesho, Nyalandu alipata wasaha wa kuzungumza na viongozi wa TTB, TATO pamoja na waandaji wa Karibu Fair 2012.
















Mhe Nyalandu akiteta jambo na mwenyekiti wa shirikisho la tour operators Tanzania, Mhe Mustapha Akunaay (kulia). Wengine ni Sam Diah mmoja wa waratibu wa maonesho sambamba na Bi Devota Mdachi, Mkurugenzi wa Masoko wa TTB















Nyalandu akipata maelezo ya kampuni inayotoa huduma za helikopta hapa Tanzania ya Whirlwind. Anayempa Maelezo ni Capt. Neels ambaye alisema kampuni yake ipo mbioni kuleta helikopta 5 mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Madhumuni ya mpango huo ni kuzitawanya katika maeneo mbalimbali ya nchi hii ili ziweze kutumika kwenye huduma za dharura haraka pale zinapohitajika. Sasa hivi wana helikopta moja nchini.


















Mojawapo ya sababu ya ziada ya kuzuru maonesho ya Karibu Fair 2012 mkoani Arusha katika Viwanja vya Magereza (karibu na Arusha Airport) ni kujionea hema la gorofa. Hema hili hutumika kwa malazi ya wageni wanapokuwa porini, hususan kwa wanaopenda kuweka kambi na kuacha kulala kwenye mahoteli. Moja ya makampuni yanayoshiriki Karibu Fair 2012 imeamua kuwaonyesha wageni na wadau bidhaa hii. Hema hili linahamishika.


















Kampuni inayotoa huduma za helikopta hapa nchini ya "Whirlwind: aviation inayoshiriki maonesho ya karibu fair ilifanya safari ya dakika kumi kuuzunguka uwanja wa maonesho, na KK wa blogu ya TembeaTz alikuwa ni mmoja wa abiria wa safari hiyo.



Friday, June 8, 2012

KITABU CHA FURAHA HUJA ASUBUHI' (JOY COMES IN THE MORNING) KIMEZINDULIWA JIJINI DAR


Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoya akitoa neno wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'FURAHA HUJA ASUBUHI' (JOY COMES IN THE MORNING) kilichoandikwa na Hopolang Phororo kinachozungumzia Mateso na manyanyaso ya wasichana wadogo wakati wa malezi yao na haki ya msingi ya jinsia ya kike katika jamii.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

USIKOSE NAKALA YAKO.


UMUHIMU WA ELIMU KATIKA TAIFA LETU

Mh.Lowasa alivyofanikisha uchangiaji wa elimu kata ya kipawa jijini dar, Jamii tuwe mfano wa kuigwa katika kuchangia maendeleo ya taifa letu.

Welcome to KARIBU FAIR 2012

http://www.karibufair.com/

Thursday, June 7, 2012

Je! Mke au Mume Waweza Kumpata DISCO? Baasi usikose "The Mboni Show" kujua undani wa swala hili. Kila Alihamis @9:00 - 10:00 @EATV 



USIKATE TAMAA .

AsiliaLive: Asante marafiki wote waliokuwa nami katika kipindi...: Asante marafiki wote waliokuwa nami katika kipindi kigumu kilichopita, Naamini yote ni mipango ya mungu mwanadamu kupitia majaribu katika du...
Asante marafiki wote waliokuwa nami katika kipindi kigumu kilichopita, Naamini yote ni mipango ya mungu mwanadamu kupitia majaribu katika dunia hii. Kila mwanadamu ana mapito yake hivyo basi yatupasa tusikate tamaa bali tumtegemee mungu pekee yake kwani yeye ndie kila kitu. USIKATEE TAMAA WAKATI BADO ASUBUHI.