Sunday, January 20, 2013
Mabomu ya machozi yarindima Mtwara

Hali mijini hapa ni tete! Mabomu yanarindima mjini mtwara kuwatawanya wananchi wanaojiandaa na mkutano mkubwa unaotarajiwa kufanyika mjini hapa kuhusu suala zima la gesi.
Chanzo cha mabomu hayo kupingwa ni baada ya umeme kukatika/kukatwa eneo panapotarajiwa kufanyika mkutano huo uwanja wa mashujaa mjini hapa na baada ya kuona hivyo wananchi wakaamua kuandamana kuelekea Tanesco kujua chanzo cha tatizo hilo la umeme na hali hiyo kupelekea polisi kuanza kuvurumisha mabomu ya machozi.
Ifahamike kwamba kumekuwa na mvua kubwa mjini hapa toka usiku wa leo ambayo inaweza ikawa chanzo cha kukatika kwa umeme huo (huu ni mtazamo wangu) ingawa inaweza ikawa hujuma pia.
Eneo nilipo umeme upo hali hii ya sintofahamu imepelekea huduma muhimu za kijamii kama maduka na soko kufungwa.
wote kwa hakika wamezungumza mengi sana na wote wameungana na wanamtwara katika kuhakikisha rasilimaliya gesi inawanuifaisha watu wa mtwara nakusini kwa ujmla kwa upande wa wasanii hakika afande sele amejitahidi sana kuongea kwa kujenga hoja. pamoja na kuwa nahali ya mvua wananchi hawakuondoka pale uwanjani kwa kweli serikali isipuuze haya madai ya watu wa mtwara kwa mfano kwa jinsi inavyoonekana vijana wako tayari kwa lolote serikalli iache kiburi. katika mkutano huo kumekusanywa saini za watu 26,000 na kuwatuma wabunge kupeleka bungeni madai yao na munge wa lindi mjini ameeleza mara baada ya mkutano huo wa bunge kma madi ya wanantwara na kusini yote watakutana lindi kwa maandamano makubwa yatakayo fanyika tarehe 23 februari mwaka huu hadi kieleweke
lakini pia kulikuwa na jambo la kusikisha, kumetokea ajari pale njia panda ya kuelekea eapot ya mtwara gari lililokuwa linatokea tandahimba likiwa na wananchi limepata ajali na watu watatu kuumia nakupelekwa hosptali ya mkoa ligula na mmoja inaelezwa hali yake sinzuri anatakiwa kupelekwa muhimbili kwa matibabu zaidi, jambo ambalo lilimfanya bwana katani kuumba umati mkubwa uliohudhuria kutoa mchango kuwezesha safari hiyo na wananchi kuitikia jambo hilo ni hayo tu wakuu. picha zitafuata punde.
Saturday, January 19, 2013
SONY YAZINDUA "SONY Experia Z" SIMU YENYE TEKNOLOJIA YA HALI YA JUU NA ISIYODHURIKA NA MAJI!
•Inaweza kustahimili maji na vumbi bila madhara yoyote
•5-inch full Touch HD screen
•Inatumia Android 4.1 aka Jelly Bean
•2GB RAM na memory ya 16GB ndani huku inauwezo wa kuendesha memory card mpaka 32GB.
•Kama zilivyo iPhone 5,Samsung Galaxy S III na vifaa vingine vyenye uwezo mkubwa,inaruhusu 4G/LTE band kwa internet yenye kasi kubwa.
•Xperia Z inakuja na kamera ya megapixel 13.1 na kamera nyingine ya mbele yenye 2.2MP.Hii ni zaidi ya iPhone 5 na Samsung Galaxy S III,zote zenye kamera ya 8 megapixel .
Toleo jipya kabisa la simu aina ya Smartphone kutoka SONY "Experia Z" ndio inayosifika kwa mwonekano mzuri kuliko simu zote za Smartphone!
SONY Experia Z ikiwa katika maonesho huko Las Vegas,Marekani
SONY Expria Z haisababishiwi matatizo yoyote na maji wala vumbi.
Simu hii kutoka SONY inafanya kazi zake zote hata ndani ya maji bila kuleta hitilafu wala kuharibika.
Mahafali ya Kidato cha Sita shule ya Sekondari Azania Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa mgeni rasmi
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania ambapo na yeye pia alikuwa ni miongoni mwa baadhi ya viongozi waliosoma shule hapo baada ya kuwasili kwenye hafla mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita.Picha ya chini ni Mstahiki Meya Jerry Silaa akipunga mkono kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Azania waliojipanga mstari kumlaki kwa furaha huku akiwa ameambatana na Mkuu wa Shule hiyo Bw. Bernard Ngoze na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Elizabeth Ngoda (kulia).

Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na kuwapongeza baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Azania
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipokea heshima kutoka kwa vijana wa skauti wa Shule ya Sekondari Azania
DK. SHEIN AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA LA ZANZIBAR ZBC
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,(kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abduhamid Yahaya Mzee,na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui,(katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Juliun Raphael,alipowasili katika Viwanja vya Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,kuufungua Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo.
Simba yaogelea tatu Oman
MABINGWA wa Tanzania, Simba wameendelea kupokea kipigo nchini Oman baada ya jana kufungwa mabao 3-1 na timu ya Taifa ya Jeshi ya Oman.Kiungo wa Simba, Haruna Moshi alifunga bao la
kufutia machozi katika dakika ya 69 baada ya wenyeji Jeshi la Oman kufunga mabao yao kupitia Alabab Alnoaley (22), Yones Almushefrei (89) na Kassim Said.
Simba ilianza mchezo huo kwa kasi, lakini wenyeji walitumia vizuri udhaifu wa ngome wa mabingwa hao wa Tanzania katika kuokoa mipira ya kona kufunga mabao yao.
Kocha wa Simba Patrick Liewig alisema baada ya mechi hiyo kuwa mechi ni nzuri, lakini vijana wake wamezidiwa umakini.
“Inakera kwa sababu timu inacheza vizuri lakini mnafungwa kwa sababu ya uzembe.
“Yaani mtu anapiga kona anafunga mara mbili, ni tatizo, hata hivyo bora nimeliona hili mapema kwa ajili ya kulifanyia kazi.”
Kikosi
Simba: Juma Kaseja/Abel Dhaira, 2 Nassor Said ‘Cholo’/ Haruna Shamte, 3 Paul Ngalema/ Kigi Makassy, 4 Mussa Mudde, 5 Shomari Kapombe, 6 Jonas Mkude/ Abdallah Seseme, 7 Haruna Chanongo, 8 Mwinyi Kazimoto/ Amri Kiemba, 9 Felix Sunzu/ Abdallah Juma, 10 Mrisho Ngassa/Haruna Moshi na 11 Ramadhani Chombo.

IDADI KAMILI YA WALIO CHUKUA FOMU TFF NA KUREJESHA
Wanamichezo 50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu wamerejesha fomu hizo.
Waombaji ambao hawakurejesha fomu ni Geofrey Nyange aliyekuwa akiomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne aliyekuwa akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha kamili ya waombaji ambao wamerejesha fomu ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais).

JK aanza ziara ya kikazi ufaransa
RAIS wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (pichani) anaanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Ufaransa leo, Jumamosi, Januari 19, 2013, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa, Mheshimiwa Francois Hollande.
Rais Kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi kuelekea Ulaya kwa ajili ya ziara hiyo.
Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja waNdege wa Charles De Gaul mjini Paris leo jioni, Rais Kikwete ambaye anafuatana na Mama Salma Kikwete atapokelewa rasmi katika Ufaransa kwa gwaride na kupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa, Mheshimiwa Paschal Canfin.

Miss utalii wawasili kambini
Washiriki wanao wanania Taji la Miss Utalii 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kuwasili Kambini, Ikondolelo Lodge Hoteli iliyopo Kibamba Jijini Dar es salaam.
Jumla ya warembo arobaini kati ya sitini wa Miss Utalii Tanzania kutoka mikoa yote ya Tanzania.tayari wameripoti kambini leo,kuanza kambi Taifa ya siku 21 kuanzia leo. Kambi hiyo mwaka huu iko katika Hoteli ya Ikondelelo Lodge iliyoko Kibamba Dar es Salaam.

Friday, January 18, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)