Sunday, January 20, 2013

MALKIA WA NYUKI: NITASHINDANA NA MANJI





 -BILIONEA WA MAFUTA ANAYETAKA KUIFIKISHA SIMBA MBALI
-AISHI JUMBA LA MABILIONI, AELEZA NDOTO ZAKE MSIMBAZI



RAHMA Al Kharusi si jina geni katika mchezo wa soka Tanzania, wengi wanamkumbuka wakati alipoamua kuingia katika kuisaidia Twiga Stars na baadaye akaipeleka nchini Marekani lakini baadaye akapotea.
Akarejea akiwa upande wa African Lyon, akasaidia mambo mengi na kufanya timu hiyo izidi kupata umaarufu, lakini baadaye hakuonekana hadi alipokuja kuibukia Simba na kusema hapo ndiyo nyumbani.
Mfanyabiashara huyo bilionea anasisitiza ametua Simba baada ya kuombwa kukubali uteuzi wa mjumbe wa kamati ya utendaji na anaamini atakuwa mshindani mkubwa wa kuleta maendeleo.




Anataka kuiona Simba ikiwa na mambo mengi yenye mabadiliko, lakini anataka timu ya wanawake pamoja na timu imara ya vijana ambayo itaiwezesha Simba kuwa na msingi hapo baadaye.
“Simba walikuja kuniomba, sikuona kama kuna ubaya wa kukubali kuingia. Wakati tunakua nyumbani nilikuwa nikimuona baba yangu akiisaidia Simba, nasi tukajikuta tunaingia Simba. Tangu nikiwa mdogo, hii ndiyo timu yangu.




Rahma ni Rais wa Makampuni ya RBP Oil ambayo yanafanya biashara mbalimbali katika nchi tofauti za Afrika. Baadhi ya biashara hizo ni uuzaji wa mafuta ya ‘dizeli’ na petrol katika nchi mbalimbali, lakini pia vyakula pamoja na samani za ndani.



Nchi za Afrika ambazo makampuni yake yanafanya kazi ni pamoja na Tanzania, DR Congo, Sudan Kusini na Uganda lakini pia kampuni zake zinafanya biashara katika nchi za Oman na Qatar.
Rahma, maarufu kama Queen of Bees, yaani Malkia wa Nyuki, anataka Simba yenye mabadiliko makubwa huku akitumia msemo wa, “Nikianza jambo, lazima nilimalize.”




Safari Oman:
Ilikuwa Simba wapelekwe sehemu moja inaitwa Nizwa, ni kama kilomita 150 kutoka hapa Muscat, nikaona si sahihi. Natumia kama milioni 80 au zaidi kuihudumia Simba hapa maana wenyeji wao Fanja nao kama hawaihudumii vilivyo.
Sipendi wafike hapa halafu wateseke, ndiyo maana mambo yote ninayafanya kupitia RBP Group. Najua Simba inajiandaa na nina mpango wa kufanya mengi makubwa ikiwezekana.




“Huo ni ushabiki, lakini ninachotaka mimi ni maendeleo. Najua kuna presha kubwa kutoka kwa Yanga, mimi nitaichukulia kama changamoto na nitashindana kuleta maendeleo. Najua Yanga wanaye (Yusuf) Manji, nitashindana naye sana.



“Najua nikishindana na Manji nitaleta maendeleo upande wa Simba, lakini nitapenda uwe ushindani wa kimaendeleo na si zaidi. Kama nitaona ni ushindani wa kutaka kuumizana nitajiweka kando, nataka maendeleo ambayo ndiyo mafanikio.
“Sitaki ugomvi, ndiyo maana utaona nilijiondoa Twiga na African Lyon. Migogoro ni kati ya vitu nisivyopenda kabisa, halafu Manji ni mtu ninayeheshimiana naye sana. Hivyo sitaki malumbano ila ushindani wa kuleta maendeleo.
“Nitashirikiana na wenzangu kuifanyia Simba kila linalowezekana ambalo litaonekana ni kubwa. Safari ya hapa Oman nataka pia iwe ni yenye manufaa. Ndiyo maana niliwaambia wachezaji lazima wajitume na kuonyesha muda wao walioutumia hapa ulikuwa na manufaa.

Bima:
Tayari tupo katika hatua za mwisho, ndani ya siku moja wachezaji wa Simba na viongozi watakatiwa bima ya maisha. Naamini ni kitu kizuri wakiwa na bima hasa hapa ugenini.
Najua fedha nyingi pia zitatumika lakini naona ni jambo la busara kufanya hivyo, maana sisi ni binadamu na hauwezi kujua kitakachotokea kesho.

Familia, kazi, Simba:
Kweli ni kitu kigumu sana, lakini hayo tayari ni majukumu yangu. Ninapenda kufanya kazi kwa kujituma sana. Wakati mwingine nakesha nikifanya kazi hadi asubuhi maana nina ofisi nyingine Marekani, hivyo kuna vitu navifanya nikiwa hapa Oman au Tanzania, unajua tena dunia sasa ni kama kijiji.

Ugumu utakuwepo lakini sipendi kufeli katika lolote, ndiyo maana napenda kujituma ili nifanikishe kitu ambacho nimekianzisha au nimeingia na kuanza kukifanya.

Ubora:
Ninaamini Simba ni timu bora, lakini lazima wajiandae vizuri na kufanya mambo kitaalamu. Kama watajaribu kubahatisha wataharibu kila kitu. Lakini kujituma pia ni msingi wa maendeleo, hivyo lazima kuwe na watu wenye nia ya kupata mafanikio.
Sisemi Simba itashinda kila siku, lakini ikipoteza basi lazima kuwe na hali ya kukubali, pia ni lazima watu wajitathmini kwa nini wamejikwaa. Mimi pia ninapenda kuona timu yangu inashinda kama ilivyo kwa mashabiki.

Malkia wa Nyuki:
Hili jina nimebatizwa na watu kutokana na tabia yangu ya kupenda kufanya kazi kwa ushirikiano, lakini mara nyingi nimekuwa nikizungukwa na watu ambao wanapenda kuniona nipo salama.
Lakini kifamilia kuna jambo moja, karibu nyumba zangu zote, nyuki wamekuwa wakitengeneza mzinga. Hali hii imewashangaza ndugu na marafiki zangu wengi, hata mimi mwenyewe. Tayari nimelizoea hilo jina na ninaona kawaida ingawa sikulikusudia.
Rahma anaishi katika eneo la Al Kheri, moja ya vitongoji maarufu vya Jiji la Muscat, watu wengi wenye uwezo wa fedha wanaishi eneo hilo.
Nyumba yake inaweza kufikia thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1.8, imejengwa kisasa huku ikiwa na mambo kadhaa ya kuvutia utafikiri zile nyumba za mastaa wa Hollywood au wanamuziki maarufu wa Marekani.

Ingawa kuna nyumba nyingi bora katika eneo hilo, bado yake inachomoza pekee na kuonekana moja ya nyumba bora kabisa.
Ukiingia getini, gari inapanda hadi juu ghorofa ya kwanza ambako ndiko kuna sebule, kila moja ikiwa imetengenezwa kwa mfumo wake. Ndani kuna sebule tatu huku kukiwa na vyumba zaidi ya vitano vya kulala.



Kuna vyumba viwili tofauti vya kulia chakula, kuna bwawa la kuogelea lililo ndani ambamo hakuna jua na AC zinawashwa ili kuleta kipupwe. Juu ya bwawa hilo kuna maporomoko ya maji ambayo yanaongozwa na umeme na kuna ukuta wa mawe ambao unafanya eneo hilo liwe kama ziwani.
Mbele ya bwawa hilo la kuogelea kuna ukumbi mdogo ambao bendi au kikundi cha taarabu cha watu kinaweza kutumbuiza na watazamani hadi 70 wakaingia na kuburudika kwa raha zao.
Ndani ya nyumba hiyo kuna ofisi kubwa ikiwa na chumba kidogo cha mikutano ambayo mara nyingi huitumia kufanya kazi zake kama anaamua kutotoka nje.
Kwa kuwa nyumba hiyo inajitosheleza kwa kila kitu, wakati mwingine Malkia huyo wa Nyuki, mama wa watoto pacha, hujikuta akiishi ndani ya nyumba hiyo hata mwezi mzima bila kutoka nje.



Magazeti ya leo Jumapili ya 20th January 2013


Mabomu ya machozi yarindima Mtwara











    Hali mijini hapa ni tete! Mabomu yanarindima mjini mtwara kuwatawanya wananchi wanaojiandaa na mkutano mkubwa unaotarajiwa kufanyika mjini hapa kuhusu suala zima la gesi.

    Chanzo cha mabomu hayo kupingwa ni baada ya umeme kukatika/kukatwa eneo panapotarajiwa kufanyika mkutano huo uwanja wa mashujaa mjini hapa na baada ya kuona hivyo wananchi wakaamua kuandamana kuelekea Tanesco kujua chanzo cha tatizo hilo la umeme na hali hiyo kupelekea polisi kuanza kuvurumisha mabomu ya machozi.

    Ifahamike kwamba kumekuwa na mvua kubwa mjini hapa toka usiku wa leo ambayo inaweza ikawa chanzo cha kukatika kwa umeme huo (huu ni mtazamo wangu) ingawa inaweza ikawa hujuma pia.

    Eneo nilipo umeme upo hali hii ya sintofahamu imepelekea huduma muhimu za kijamii kama maduka na soko kufungwa.

    wote kwa hakika wamezungumza mengi sana na wote wameungana na wanamtwara katika kuhakikisha rasilimaliya gesi inawanuifaisha watu wa mtwara nakusini kwa ujmla kwa upande wa wasanii hakika afande sele amejitahidi sana kuongea kwa kujenga hoja. pamoja na kuwa nahali ya mvua wananchi hawakuondoka pale uwanjani kwa kweli serikali isipuuze haya madai ya watu wa mtwara kwa mfano kwa jinsi inavyoonekana vijana wako tayari kwa lolote serikalli iache kiburi. katika mkutano huo kumekusanywa saini za watu 26,000 na kuwatuma wabunge kupeleka bungeni madai yao na munge wa lindi mjini ameeleza mara baada ya mkutano huo wa bunge kma madi ya wanantwara na kusini yote watakutana lindi kwa maandamano makubwa yatakayo fanyika tarehe 23 februari mwaka huu hadi kieleweke

    lakini pia kulikuwa na jambo la kusikisha, kumetokea ajari pale njia panda ya kuelekea eapot ya mtwara gari lililokuwa linatokea tandahimba likiwa na wananchi limepata ajali na watu watatu kuumia nakupelekwa hosptali ya mkoa ligula na mmoja inaelezwa hali yake sinzuri anatakiwa kupelekwa muhimbili kwa matibabu zaidi, jambo ambalo lilimfanya bwana katani kuumba umati mkubwa uliohudhuria kutoa mchango kuwezesha safari hiyo na wananchi kuitikia jambo hilo ni hayo tu wakuu. picha zitafuata punde.

Saturday, January 19, 2013

SONY YAZINDUA "SONY Experia Z" SIMU YENYE TEKNOLOJIA YA HALI YA JUU NA ISIYODHURIKA NA MAJI!




 Kampuni kubwa na maarufu kwa utengenezaji wa vifaa vya umeme kwa matumizi mbalimbali kamavile luninga,michezo ya vedeo"Video Games",redio,nk imezindua rasmi toleo jipya ya simu za Smartphone "SONY  Experia"na sasa ni "SONY  Experia  Z".Kifaa hiki kina mambo yafuatayo

•Inaweza kustahimili maji na vumbi bila madhara yoyote
•5-inch full Touch HD screen
•Inatumia Android 4.1 aka Jelly Bean
•2GB RAM na memory ya 16GB ndani huku inauwezo wa kuendesha memory card mpaka 32GB.
•Kama zilivyo iPhone 5,Samsung Galaxy S III na vifaa vingine vyenye uwezo mkubwa,inaruhusu 4G/LTE band kwa internet yenye kasi kubwa.
•Xperia Z inakuja na kamera ya megapixel 13.1 na kamera nyingine ya mbele yenye 2.2MP.Hii ni zaidi ya iPhone 5 na Samsung Galaxy S III,zote zenye kamera ya 8 megapixel .
 Toleo jipya kabisa la simu aina ya Smartphone kutoka SONY "Experia Z" ndio inayosifika kwa mwonekano mzuri kuliko simu zote za Smartphone!
 SONY Experia Z ikiwa katika maonesho huko Las Vegas,Marekani
 SONY Expria Z haisababishiwi matatizo yoyote na maji wala vumbi.
 Simu hii kutoka SONY inafanya kazi zake zote hata ndani ya maji bila kuleta hitilafu wala kuharibika.
 Picha,muvi na kitu chochote kwenye simu hii inaweza kuonekana kwenye luninga yako bila waya wowote ule!

Mahafali ya Kidato cha Sita shule ya Sekondari Azania Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa mgeni rasmi

Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania ambapo na yeye pia alikuwa ni miongoni mwa baadhi ya viongozi waliosoma shule hapo baada ya kuwasili kwenye hafla mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita.
   Picha ya chini ni  Mstahiki Meya Jerry Silaa akipunga mkono kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Azania waliojipanga mstari kumlaki kwa furaha huku akiwa ameambatana na Mkuu wa Shule hiyo Bw. Bernard Ngoze na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Elizabeth Ngoda (kulia).


Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na kuwapongeza baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Azania
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipokea heshima kutoka kwa vijana wa skauti wa Shule ya Sekondari Azania

DK. SHEIN AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA LA ZANZIBAR ZBC

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,(kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abduhamid Yahaya Mzee,na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na  Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui,(katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Juliun Raphael,alipowasili katika Viwanja vya  Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,kuufungua Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo.

Simba yaogelea tatu Oman

MABINGWA wa Tanzania, Simba wameendelea kupokea kipigo nchini Oman baada ya jana kufungwa mabao 3-1 na timu ya Taifa ya Jeshi ya Oman.Kiungo wa Simba, Haruna Moshi alifunga bao la

kufutia machozi katika dakika ya 69 baada ya wenyeji Jeshi la Oman kufunga mabao yao kupitia Alabab Alnoaley (22), Yones Almushefrei (89) na Kassim Said.

Simba ilianza mchezo huo kwa kasi, lakini wenyeji walitumia vizuri udhaifu wa ngome wa mabingwa hao wa Tanzania katika kuokoa mipira ya kona kufunga mabao yao.

Kocha wa Simba Patrick Liewig alisema baada ya mechi hiyo kuwa mechi ni nzuri, lakini vijana wake wamezidiwa umakini.

“Inakera kwa sababu timu inacheza vizuri lakini mnafungwa kwa sababu ya uzembe.

“Yaani mtu anapiga kona anafunga mara mbili, ni tatizo, hata hivyo bora nimeliona hili mapema kwa ajili ya kulifanyia kazi.”

Kikosi

Simba: Juma Kaseja/Abel Dhaira, 2 Nassor Said ‘Cholo’/ Haruna Shamte, 3 Paul Ngalema/ Kigi Makassy, 4 Mussa Mudde, 5 Shomari Kapombe, 6 Jonas Mkude/ Abdallah Seseme, 7 Haruna Chanongo, 8 Mwinyi Kazimoto/ Amri Kiemba, 9 Felix Sunzu/ Abdallah Juma, 10 Mrisho Ngassa/Haruna Moshi na 11 Ramadhani Chombo.

Yaliyojiri leo Magazetini jumamosi ya 19th January 2013


IDADI KAMILI YA WALIO CHUKUA FOMU TFF NA KUREJESHA

Wanamichezo 50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu wamerejesha fomu hizo.

Waombaji ambao hawakurejesha fomu ni Geofrey Nyange aliyekuwa akiomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne aliyekuwa akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.

Orodha kamili ya waombaji ambao wamerejesha fomu ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais).

JK aanza ziara ya kikazi ufaransa

RAIS wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (pichani) anaanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Ufaransa leo, Jumamosi, Januari 19, 2013, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa, Mheshimiwa Francois Hollande.

Rais Kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi kuelekea Ulaya kwa ajili ya ziara hiyo.

Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja waNdege wa Charles De Gaul mjini Paris leo jioni, Rais Kikwete ambaye anafuatana na Mama Salma Kikwete atapokelewa rasmi katika Ufaransa kwa gwaride na kupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa, Mheshimiwa Paschal Canfin.

Miss utalii wawasili kambini

Washiriki wanao wanania Taji la Miss Utalii 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kuwasili Kambini, Ikondolelo Lodge Hoteli iliyopo Kibamba Jijini Dar es salaam.

Jumla ya warembo arobaini kati ya sitini wa Miss Utalii Tanzania kutoka mikoa yote ya Tanzania.tayari wameripoti kambini leo,kuanza kambi Taifa ya siku 21  kuanzia leo. Kambi hiyo mwaka huu iko katika Hoteli ya Ikondelelo Lodge iliyoko Kibamba Dar es Salaam.