Monday, February 25, 2013
Sunday, February 24, 2013
MDEE AONGELEA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali
Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia” inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano. “Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo”
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Februari 24, 2013 ameungana na Wakuu wenzake wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu kutia saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mhe. Rais Kikwete alisema mara baada ya utiwaji saini wa Mpango huo kwamba: “Hii ni siku kubwa na ya kihistoria kwa watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jirani zake na Ukanda wote wa Maziwa Makuu. Ni siku ya kukumbukwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Afrika, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Jumuiya yote ya Kimataifa. “Watu wa Kongo wameteseka kwa muda mrefu sana. Wanastahili kupumua sasa. Wanastahili kuishi maisha
POLISI YATANGAZA DAU ALIYEMUUA PADRI MUSHI
MWANANCHI
WAKATI kukiwa na taarifa kwamba maofisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) wametua nchini kwa ajili ya kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi, Jeshi la Polisi limetangaza dau la Sh10 milioni kwa atakayefichua aliyemuua padri huyo.Padri Mushi aliuawa kwa
kupigwa risasi Jumapili iliyopita wakati akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia lililopo Beit el Ras nje kidogo ya mji wa Zanzibar, ambapo inadaiwa kuwa waliomuua walikuwa wamepanda pikipiki aina ya Vespa na walimfyatulia padri huyo risasi tatu akiwa ndani la gari yake.
Tuesday, February 19, 2013
KANISA LACHOMWA MOTO ZANZIBAR
Wakati Watanzania wakiendelea kutafakari tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Padre Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoriki Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadaye kulichoma moto Kanisa la Walokole la Shaloom lililoko eneo la Kiyanga kwa Sheha mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, ACP Augostine Olomi, alisema jana kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 9.30 usiku.

JOHN MNYIKA (MBUNGE) AWAJIBU NAPE NA RIDHIWANI KIKWETE JUU YA ELIMU YAKE
UTANGULIZI
- Amesoma S/Msingi Mbuyuni (Dar) | Alichaguliwa kwenda Ilboru lakini hakwenda, akaenda Maua Seminary na alipata A tisa | Alisoma A-Level Tambaza | Ana BBA toka UDSM
- Amtaka Ridhiwan aongee na 'mshua' juu ya tatizo la maji Dar!
SASA ENDELEA>>>>>>>
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM.
Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.

HUU NDO WARAKA WA UAMSHO UNAOCHOCHEA MACHAFUKO NA MAUAJI YA WAKRISTU HUKO ZANZIBAR
Huu ndo waraka uliosambazwa Zanzibar ukichochea mauaji ya wakristu ambao wao wanawaita "MAKAFIRI"....
Swali la kujiuliza ni JE, SERIKALI ILILITAMBUA HILI?..Maana hizi ni dalili za wazi kwamba mauaji haya YALIPANGWA.
NB: Hatutegemei lawama toka upande wowote.Palipo na lolote sisi hufichua kwa uwazi ili kuifahamisha jamii...
Kuna haja gani ya kuuficha ukweli?...Ni bora kuuanika ili watanzania wenzetu walioko zanzibar wachukue tahadhari wakisubiri msimamo wa serikali.
Chanzo cha waraka huu ni blog ya zanzibar.

"RAIS KIKWETE ANA HASIRA, WANAOSEMA MPOLE HAWAMJUI"...MAMA SALMA
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCN, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoboa siri kwamba mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura yake kujawa haiba ya ucheshi wa mara kwa mara lakini kwa tabia ana hasira.
Amesema, Rais Kikwete hukasirika sana anapoona au kusikia mtu au mtendaji katika Chama au serikali anafanya mambo ya hovyo au ya kizembe hasa katika masuala ya kazi.
Mama Salma Kikwete ametoboa siri hiyo, leo Februari 18, 2013, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa katika ziara ya kukagua, kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua kuwa mjumbe wao wa NEC.

"SINA KINYONGO JUU YA PENZI LA DIAMOND NA PENNY"...JOKATE
BAADA ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja kama kweli wamependana na kuridhiana.
Akizungumza katika mahojiano maalum alipobanwa kuhusiana na uhusiano wa wapenzi hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa shosti wake, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema kwamba yeye na mrembo huyo walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na urafiki wa karibu kama baadhi ya watu wanavyoamini.
Jokate ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga ya Channel O alifunguka kuwa anawatakia kila la heri na baraka zote Diamond na Penny katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi endapo tu watakuwa wamependana na kuridhiana kwa dhati.
“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.
Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.
tagazo

"SIPO TAYARI KUKUTANA NA LULU MICHAEL KUTOKANA NA UNYAMA ALIOUFANYA KWA KANUMBA"...MAYA
STAA wa filamu za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa tangu Elizabeth Michael ‘Lulu’ atolewe gerezani kwa dhamana, moyo wake unakuwa mzito kukutana naye.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Maya aliweka plain kuwa kila anapofikiria ukaribu aliokuwa nao na marehemu Steven Kanumba, moyo wake unakuwa mzito kumuona Lulu ambaye alikuwa mpenzi wa marehemu.
“Mh! Kukutana na Lulu ni ngumu sana, sijui hata najisikiaje? Moyo unakuwa mzito sana kukutana naye na sijui kwa nini,” alisema Maya.

Baba Mtakatifu aanza wiki ya kufunga na kutoonekana hadharani.
Baba Mtakatifu Benedict wa 16 ameanza wiki yake ya mafungo ya kiroho ambapo atakuwa haonekani hadharani kwa wiki nzima ikiwa ni mwanzo wa safari yake ya kuelekea kuachia rasmi uongozi wa kanisa Katoliki na kusema kuwa ana matumaini ibada zake zitakuwa na mafanikio.
Baba mtakatatifu atabakia Vatican na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu kwa ajili ya ibada za awali za sikukuu ya Pasaka na atapata mapumziko mafupi kila siku kwa ajili ya kuonana na katibu wake Georg Gaenswein, ili kuyashughulikia masuala ya dharura ya kanisa.
Baada ya wiki nzima ya ibada, Baba Mtakatifu atakutana na rais wa Italia, Giorgio Napolitano, tarehe 23 Februari kushiriki ibada ya Jumapili yake ya mwisho ifikapo tarehe 24 mwezi huu na kuzungumza hadharani kwa mara ya mwisho mbele ya waumini wapatao 10,000.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani ataachia uongozi rasmi tarehe 28 mwezi huu na inasemakana kuwa Waziri wa Utamaduni wa Vatican Kadinali Gianfranco Ravasi ndiye anayeonekana mtu mwenye nafasi kubwa ya kuchukua nafasi yake kwa muda mfupi au mrefu.

KAULI ZA SERIKALI YA ZNZ NA MAASKOFU WAKUU KATOLIKI KUHUSU MAUAJI YA PADRE.
Baada ya kifo cha Padre Evarist Mushi ambae alifariki kwa kupigwa risasi
Zanzibar jumapili iliyopita, kanisa Katoliki limewataka waumini wa
kanisa hilo na Watanzania wengine kuwa watulivu na kufanya maombi ya
amani katika kipindi hiki.
Askofu mkuu wa kanisa hilo Tanzania Muadhama Polycarp Cardinal Pengo amesema kifo cha Padre Mushi ni pigo kwa kanisa na Taifa na ni ishara ya kutoweka kwa amani hivyo hilo swala linatakiwa kufanyiwa kazi kabla ya madhara kuzidi, kwa sababu ukikosekana usalama kwa imani moja, kesho na kesho kutwa haijulikani ni imani gani ikashambuliwa.
Namkariri akisema “vyombo vya usalama vinatakiwa viwe makini, mimi sio mtaalamu wa usalama lakini naona ni jambo ambalo lingeweza kuzuilika na lisitokee kama watu wangesoma ishara za nyakati, wale wanaohusika wazuie kisitokee chochote… kuendeleza moyo wa kisasi hakutasaidia chochote na badala yake kutaleta madhara zaidi”

Saturday, February 9, 2013
Tanzania yashiriki utalii hispania
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Youssou Ndour Waziri
wa Utalii na Utamaduni nchini Senegal ambaye pia ni mwanamuziki maarufu
duniani wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho hayo ,
Youssou Ndour amewahi kufanya ziara ya kimuziki mara tatu nchini
Tanzania kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na Utamaduni nchini
mwake.
Miss Utalii Tanzania 2013 kutembelea Hifadhi za Taifa na vivutio vya utalii
Miss Utalii Tanzania 2012/13 wiki ijayo wataanza ziara ndefu ya kutembelea Hifadhi za Taifa na vivutio vya utalii katika mikoa ya Dar es salaam,Morogoro,Mtwara,Lindi na Pwani. Vivutio hivyo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Mikumi, Udizungwa, Saadani, Selous, pia maeneo ya kihistoria ya Bagamoyo, Amboni, Kijiji cha makumbusho,Makumbusho ya Taifa, Pugu sekondari,maeneo mengine ni ufukwe wa kigamboni, soko la kimataifa la Magogoni, Uwanja wa Taifa, uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere Air Port, Soko la Kariakoo, Mashule ya sekondari na msingi, pia watatembelea manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni ambapo watakutana na viongozi wakuu wa wilaya, mikoa, na wabunge katika majimbo ya mikoa hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
.jpg)