Platini anasema huenda ikawa bora michuano ya Euro 2020 kufanyika katika miji mbalimbali ya Ulaya
Michel Platini, rais wa shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA, amesema michuano ya Euro 2020 huenda ikafanyika katika miji mbalimbali mwaka 2020, badala ya kuwa na mji mmoja ambao utakuwa ni mwenyeji.
Utamaduni wa mashindano hayo huwa ni nchi moja, au mbili, kushirikiana katika kuwa mwenyeji, kama ilivyo wakati huu michuano hiyo kufanyika Poland na Ukraine.
Mashindano yajayo yatafanyika nchini Ufaransa, mwaka 2016.
"Euro 2020 inaweza kufanyika popote barani Ulaya," alielezea Platini. "Yanaweza kufanyika katika nchi moja yenye viwanja 12, au kufanyika katika uwanja mmoja katika miji 12 au 13 ya Ulaya."
Platini ameelezea kwamba wazo hilo pia linaweza kuokoa senti katika kuepuka gharama kubwa za ukarabati, na juhudi za kujenga viwanja vipya na kuimarisha viwanja vya ndege.
Uturuki ilitazamiwa na wengi kupata nafasi ya kuandaa mashindano ya mwaka 2020, lakini ombi la nchi hiyo limekumbwa na tatizo, kwa kuwa nchi hiyo pia ina nia ya kuandaa michezo ya Olimpiki mjini Istanbul, mwaka huohuo wa 2020.
Mataifa ya Uskochi, Wales na Jamhuri ya Ireland, rasmi pia yameelezea nia yao ya kuandaa michuano ya 2020.
Platini ametangaza kwamba uamuzi kamili utatangazwa kati ya mwezi Januari hadi Februari mwaka ujao.
Chanzo:BBC
Tuesday, July 3, 2012
Afisa Mkuu Mtendaji Wa Barclays Ajiuzulu
Afisa mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Bob Diamond hatimaye amejiuzulu.Mwenyekiti anayeondoka Marcus Agius, ambaye alitangaza kujiuzulu kwake hiyo jana, sasa atakuwa mwenyekiti wa kudumu wa benki hiyo na ataongoza mikakati ya kumtafuta afisa mkuu mtendaji mpya.Benki ya Barclays, imekumbwa na kashfa ya kuongeza viwango vya riba kinyume cha sheria.
Chanzo:BBC
Chanzo:BBC
Mgomo Wa Madaktari: JK Akoleza Moto
Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi serikalini bila ya kulipwa mshahara wa Sh3.5 milioni aache kazi, viongozi wa dini, wanasiasa, wabunge na wasomi wamemtaka apunguze jazba.Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana walisema mgogoro wa madaktari na Serikali bado unajadilika huku Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika akienda mbali zaidi na kusema Serikali iache kisingizio cha Mahakama kulizuia Bunge kujadili mgogoro baina yake na madaktari, wakati yenyewe inajadili na kutoa maelezo.
Juzi, katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alisema Serikali haiwezi kuahidi kuwa inao uwezo wa kuwalipa madaktari mshahara huo na posho zote kwani ikifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa Sh7.7 milioni kwa mwezi kitu ambacho hakiwezekani.
Jana, wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao walisema mgogoro huo kati ya Serikali na madaktari bado unajadilika na kusisitiza kuwa hotuba ya Rais Kikwete haijajibu madai ya madaktari.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally alisema ingekuwa jambo jema kama kungekuwa na uwezekano wa mazungumzo kuendelea.
Alisema kauli ya Rais ni upande wa Serikali hivyo, ingekuwa vyema kama madaktari nao wangepata nafasi ya kujieleza.
Wanasiasa
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali alimtaka Rais apunguze hasira na kuitaka Serikali ikubali kurudi katika meza ya mazungumzo hata kama ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuwapeleka mahakamani madaktari waliogoma.
Alisema kama Serikali haiwezi kulipa kiwango cha mshahara kilichopendekezwa na madaktari, irudi katika meza ya mazungumzo ili kutafuta suluhu ya mgomo huo unaowaumiza zaidi wananchi.
“Warudi kwenye meza ya majadiliano siyo kila mmoja kusema la kwake na kuacha mgomo kuendelea huku, watu wakiteseka hospitalini bila msaada wowote,’’ alisema Machali.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro alisema Serikali haipaswi kuwafukuza madaktari kwa kuwa imetumia gharama kubwa kuwasomesha.
“Ikiwafukuza madaktari italazimika kuwaleta walio nje ya nchi ambao ni gharama kubwa… Serikali itatue mgogoro huu,” alisema.
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisema Serikali iache kutumia kisingizio cha Mahakama kulizuia Bunge kujadili mgogoro wa madaktari wakati yenyewe ikitoa ufafanuzi.
“Uamuzi wa Serikali kutoa kauli kupitia hotuba ya Rais una mwelekeo wa kukwepa wabunge kujadili hotuba husika ambayo awali, ilielezwa kuwa ingetolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bungeni. Inawanyima haki wabunge wasitimize wajibu wa kikatiba wa Ibara 63 (2) wa kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi,” alisema Mnyika.
Mnyika alisema, kwa kuwa Bunge litajadili mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012/2013 kuanzia leo, ni muhimu wabunge wakajadili pia masuala ambayo Rais ameyaeleza kwa taifa na kutimiza wajibu wa kikatiba.
“Hotuba ya Rais imeendeleza kauli za upande mmoja ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali kuhusu mgogoro huo bila taifa kupewa fursa ya kupata maelezo na vielelezo vya upande wa pili, hivyo Serikali imetoa kauli yake hadharani badala ya bungeni au mahakamani.
Viongozi wa dini
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo Kibangu, Anthony Lusekelo alisema madaktari hao wanatakiwa kurudi kazini kwa kuwa tayari Serikali imeshasema kuwa haina fedha za kuwalipa na kuongeza kuwa hata kama wana madai yao, wadai wakiwa kazini.
“Asilimia kubwa ya madaktari wamesomeshwa na Serikali… Serikali hiyohiyo inawaeleza kuwa haina fedha za kuwalipa kama wanavyotaka, binafsi nawaomba tu warudi kazini kwa kuwa mgomo wao unawaathiri zaidi wananchi kuliko hata hao viongozi wa Serikali.
“Tunajua tulikotoka ila hatujui tunakokwenda, kama ni kuboreshwa kwa sekta nzima ya afya, Serikali imesema itatekeleza hilo, haiwezi kuyatekeleza kwa siku moja, haya mambo yanajadilika.
Alisema kama Serikali itakuwa na makosa yake, itayajibu mbele za Mungu... “Madaktari watekeleze wajibu wa kazi yao kwa uwezo wa Serikali iliyopo madarakani.”
Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kagera, Dk Methodius Kilaini alisema kanisa hilo haliwezi kuunga mkono mgomo huo.
Alisema pamoja na kuwa madaktari wana madai yao, jukumu lao kubwa ni kufuata maadili ya kazi yao ambayo hayawaruhusu kugoma.
Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Askofu David Mwasota alisema madaktari wanatakiwa kutenganisha siasa na maadili ya kazi yao.
“Hata kama Serikali ina makosa yake lakini, wao kuendelea kugoma si jambo zuri kwa jamii na hata mbele za Mungu, watumie njia nyingine kudai madai yao, lakini waendelee kutoa huduma. Madaktari ni watu muhimu, kurudisha viungo vya binadamu katika hali ya kawaida si kazi ndogo, warudi kazini kuokoa mamia ya Watanzania maskini.”
Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Arusha Abdulkarim Jonjo alisema ipo haja kwa Serikali kukaa meza moja na madaktari hao.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mjini Kati, Thomas Laizer alisema mgogoro wa madaktari umalizwe kwa mazungumzo.
Alisema Serikali inapaswa kuwa wazi inapozungumza na madaktari kwa kueleza ni mambo gani yanawezekana na kwa muda gani ili, kuondoa migogoro.
Akizungumza juzi katika ibada maalumu katika kanisa la KKKT Kimandolu, alisema ili kuondoa hisia kuwa Serikali inahusika na tukio la kutekwa Dk Ulimboka ni lazima iundwe tume huru.
“Nadhani ili kuondoa haya maneno ambayo si jambo dogo, Serikali inapaswa kuunda tume huru kuchunguza tukio hili, kwani inawezekana waliohusika ni watu wengine tu wenye nia mbaya na Serikali lakini ili ukweli ujulikane ni muhimu kuwepo tume huru,” alisema Askofu Laizer.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum aliwataka madaktari kutii agizo lililotolewa na Mahakama kwa kurudi kazini.
“Rais ameshaeleza wazi kwamba Serikali haina fedha za kuwalipa kama wanavyotaka, warudi tu kazini na kuweka masilahi ya Watanzania mbele na kuacha kutanguliza masilahi binafsi,” alisema Sheikh Salum.
Wanaharakati
Mkurungezi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema hotuba hiyo ya Rais haina jipya zaidi ya kurudia maelezo yake ya awali alipokutana na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.
“Nilitarajia kuwa hotuba itakuwa tofauti lakini sivyo. Amerudia maelezo yaleyale aliyoyasema Machi 12 (mwaka huu) alipokutana na wazee katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,” alisema Bisimba.
Wakili Peter Jonathan alisema kama kweli Serikali inataka kurudisha imani kwa Watanzania kuhusu tukio la Dk Ulimboka ni lazima ijisafishe kwa kuunda tume huru nje ya Serikali.
“Watafute hata Jaji mstaafu, si lazima atoke Tanzania kuongoza tume huru ikibidi tuchukue hata nje ya nchi ili wakitoa taarifa iweze kuaminiwa na jamii na hiyo ndiyo dhana sahihi ya utawala bora,” alisema.
Mjumbe wa Chama cha Watabibu wa Tiba Asili (ATME), Boniventure Mwalongo ameitaka Serikali kuacha kutumia nguvu kushughulikia madai ya madaktari badala yake ipanue wigo wa majadiliano ili kutatua tatizo hilo.
“Nimesikiliza hotuba ya Rais lakini, haijaonyesha kama kuna jawabu la mgomo hivyo wapanue wigo wa majadiliano ili kumaliza mgogoro huu,” alisema Mwalongo.
Habari hii imeandikwa na Fidelis Butahe,
Nora Damian, Bakari Kiango, Freddy Azzah, Daniel Mwingira, Dar; Daniel Mjema, Moshi; Mussa Juma, Arusha na Frederick Katulanda, Mwanza.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz

Dk. Mtaki: Usagaji Ni Starehe Kama Zingine ; Asema Ikizidishwa Inaharibu Saikolojia Ya Mchezaji
Dk. Magreth Mtaki.
GUMZO juu ya wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars kufanya vitendo vya kustareheshana, limetetewa na baadhi ya wataalam kuwa ni tendo linaloweza kufanyika kama lilivyo tendo lingine.
Mjadala ulizuka wiki mbili zilizopita juu ya kufanya vibaya kwa Twiga Stars kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1 na Ethiopia katika mechi za kuwania kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika Equatorial Guinea baadaye Novemba.
Mkwasa alisema kuwa kufanya vibaya kwa timu hiyo kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kuendekeza vitendo vya kusagana, lakini akasema kuwa waliokuwa wakifanya 'hayo mambo' (bila kuwataja) walitimuliwa.
Lakini vitendo hivyo vimetajwa kushamiri hasa katika timu zinazojumuisha wanawake ama wasichana wengi kwani kila mmoja anakuwa na tabia na mihemko yake kiasi cha kuwaathiri wengine.
Spoti Mikiki ilifanya mahojiano na Dk. Magreth Mtaki, daktari wa michezo wa siku nyingi kutoka Kurugenzi ya Michezo ambaye anasema kuwa kusagana (lesbianism) ni kama starehe nyingine ambayo watu wa jinsi mbalimbali wanafanya.
Anasema kuwa tatizo linakuja kuwa ni suala linalohusisha wasichana ama kinamama ndiyo maana linaleta mshangao, lakini hakuna tofauti na matendo mengine ama kustareheshana kwa watu wawili.
Dk. Mtaki ambaye pia ni Makamu wa Chama cha Soka ya wanawake Tanzania, TWFA, anasema kuwa kitendo cha kusagana, kwa upande mwingine kina athari kubwa kwenye timu kwani endapo kitafanywa kwa kuzidisha, inamaliza nguvu mchezaji.
"Hata ingekuwa wewe na mke wako, una mechi ya kimataifa ama ligi, halafu ukafanya tendo la ndoa kupitiliza, ni wazi itapunguza uwezo wako uwanjani, basi hata hawa wanaosagana, wakizidisha, lazima uwezo utapungua.
"Kingine ambacho naweza kusema, lakini sasa hii ni kwa mchezaji mwenyewe...hali hii itamfanya hatokuwa na hamu ya mwanaume akiamini kuwa mwanamke mwenzake anakata kiu.

Diwani wa Kata ya Makongo (Chadema), Deusdedit Jacob Mtiro.

ILIKUWA kama sinema pale Diwani wa Kata ya Makongo (Chadema), Deusdedit Jacob Mtiro alipoongoza kundi la vijana waponda kokoto kubomoa sehemu ya nyumba ya Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Kata ya Makongo, Judith Lungato Stambuli Ijumaa iliyopita nyumbani kwake Mlalakua, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Katika tafrani hiyo kiongozi huyo licha ya kuvunjiwa sehemu ya nyumba yake na kuchaniwa gauni na mtandio, habari za kipolisi zinasema Diwani Mtiro anatuhumiwa kwenda na wahuni kwa kiongozi huyo ambapo alipigwa na kusababisha mali zake kadhaa kuibiwa kutokana na vurugu kubwa iliyozuka.
Habari ambazo polisi wanazo ni kwamba mali alizoibiwa kiongozi huyo ni simu aina ya Blackberry yenye thamani ya shilingi 350,000, nguo aina ya dera na vitenge vyenye thamani kubwa, saa ya mkononi na nondo kadhaa zilizokuwa kwenye nyumba ya mama huyo.
Mwandishi wetu aliambiwa na kiongozi mmoja wa polisi kuwa tayari Diwani Mtiro amefunguliwa jalada Kituo cha Polisi Chuo Kikuu cha Mlimani lenye namba UD/RB/4045/2012 (Shambulio la mwili).
Akizungumza na mwandishi wetu, Bi Stambuli alisema sehemu iliyosababisha ashambuliwe hakujenga hivi karibuni bali imejengwa miaka zaidi ya miwili iliyopita na wala haikuwa na usumbufu wowote kwa raia.
“Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wangu aliwahi kusuluhisha suala hili baada ya watu wenye roho mbaya kuvunja, wakaamriwa wajenge, tukiwa polisi alikiri kufanya kosa na wakaamua kunijengea kwa gharama zao, nilishangaa kuona Diwani Mtiro anakuja na kunibomolea tena bila hata notisi, ” alisema katibu huyo.
Baadhi ya wananchi wa Mlalakua akiwemo mzee Kariakoo, walisema kitendo alichofanyiwa mwanamke huyo ni cha kinyama na siasa imeingizwa, “Hakuna sehemu ilikuwa nadhifu kama hii kwani mvua ikinyesha watu walikuwa hawakanyagi tope.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alipopigiwa simu alisema hajapata taarifa ya tukio hilo na akaahidi kufuatilia.
Imeandaliwa Na Haruni Sanchawa.

Mwanamke azikwa akiwa hai Mbeya
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Malamba, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
KUMEZUKA vitendo vya unyama mkoani Mbeya vya kuzika watu wanaotuhumiwa kuwa ni washirikina wakiwa hai ambapo hivi karibuni watu wawili akiwemo mwanamke mmoja wamefanyiwa unyama huo.
Mwanamke aliyezikwa akiwa hai kwa tuhuma za kujihusisha na ushirikina ni Rozina Mwadala (60) ambapo tukio hilo lilitokea Juni 2, mwaka huu.
Mwanamke huyo alichukuliwa hatua hiyo baada ya kifo cha mmoja wa ndugu yake ambaye alifariki muda mchache baada ya kulalamika kuwa alikuwa akiumwa sikio na kichwa. Hata hivyo, hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa tayari kuhojiwa na mwandishi wetu kwa hofu ya kukamatwa na polisi.
Kufuatia vitendo hivyo kushika kasi mkoani Mbeya, Mwenyekiti wa Muungano wa Jamii Tanzania (Mujata), Chifu Soja Masoko, amewaonya wananchi wa Kijiji cha Malamba, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuacha mara moja tabia za kujichukulia sheria mikononi alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara Juni 15, mwaka huu.
“Hasara yake mnaona. Sasa kufuatia kitendo hicho cha kikatili baadhi ya wananchi wamehama kijijini hapa kukwepa mkono wa sheria na shughuli za kiuchumi zimezorota,” alisema.
Mbali na mwanamke huyo kuzikwa hai, hivi karibuni mwanaume mmoja, Nyerere Kombwee naye alizikwa hai baada ya kutokea kifo cha mdogo wake kisha yeye kutohudhuria msibani ndipo wananchi wakamsaka na walipompata wakampiga na yeye akatoa vitisho kuwa damu yake isingeweza kwenda bure ndipo wakaamua kumzika akiwa hai.
DAKTARI MWINGINE ATEKWA
WAKATI Kiongozi wa Chama Cha Madaktari nchini Dk. Steven Ulimboka akiwa amesafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu, Daktari mwingine, John Chilinde ametekwa na kupigwa ambapo amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Daktari huyo ambaye ni mkazi wa Tabata Kimanga , wilayani Ilala anayetibu katika Hopitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam alitekwa Ijumaa saa tano usiku akiwa anatoka baa iitwayo Flora Pub iliyopi Tabata jijini.
Habari zinasema akiwa anatoka katika baa hiyo, Dk Chilende alitekwa na vijana watatu ambao walimshambulia huku wakimuuliza kwa nini wamegoma kutibu watu katika hospitali za serikali.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Dk. Chilende alishambuliwa kwa dakika kumi na baadaye kutekwa kisha akaenda kutelekezwa akiwa hoi hajitambui hatua chache kutoka sehemu aliyokuwa anapigiwa .
Chanzo kimesema daktari huyo aliokolewa na dereva wa kibajaji ambaye alimkuta akigagaa chini huku akivuja damu mdomoni, alimpakia na kumpeleka Kituo cha Polisi Buguruni ambako alifunguliwa jalada namba BUG/RB/7974/ 2012 (Shambulio la kudhuru mwili), baadaye alikimbizwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu zaidi.
Afisa mmoja wa polisi wa Kituo cha Buguruni ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa siyo msemaji, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akaongeza kuwa wahusika wa unyama huo wanasakwa kwani daktari huyo anamfahamu mmoja wa waliyemshambulia. Kamanda wa Kanda Maalum, Suleiman Kova hakupatikana kuzungumzia tukio hilo. Chanzo: Globalbuplisher

CHADEMA:TAARIFA KWA UMMA JUU YA MELI ZA IRAN NA BENDERA YA TANZANIA
KWA takribani muda wa juma moja sasa kumekuwepo na taarifa katika vyombo vya habari na njia mbalimbali za upashanaji habari, kuwa kampuni moja ya meli inayodaiwa kutoka Iran, inayojulikana kwa jina la NITC (National Iranian Tanker Company), inatumia bendera ya Tanzania, isivyo kihalali na kinyume kabisa na sheria za nchi na zile za kimataifa, kwa malengo ambayo hayajulikani.
Pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa taarifa kwenye Baraza la Wawakilishi tarehe 2 Julai 2012 kukanusha taarifa hizo, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Uchukuzi kutoa taarifa kwa umma juu ya hatua ilizochukua kuchunguza madai hayo.
Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ieleze iwapo utaratibu huo umezingatia kwa ukamilifu United Nations Convention law of the Sea, kifungu cha 91, Geneva Convention of Registration kifungu cha 6 na maazimio mengine ya kimataifa kuhusu usajili wa meli kubwa pamoja na usafirishaji wa mafuta.
Maelezo yaliyotolewa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inayoongozwa na CCM na CUF yanaibua maswali kutokana na kampuni ya Philtex ya Dubai inayoelezwa kupewa uwakala na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini- Zanzibar Maritime Authority (ZMA) kufanya kazi na makampuni mengine hivyo taarifa hizo hazijitoshelezi katika kuondoa uwezekano kwamba meli za NITC zilipeperusha bendera ya Tanzania.
Ili kujisafisha juu ya tuhuma hizo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilipaswa kushirikiana na Serikali ya Muungano kufanya uchunguzi wa kubaini msingi wa tuhuma hizo na kuchukua hatua iwapo meli za NITC zilipeperusha bendera ya Tanzania bila ridhaa ya serikali zote mbili.
Ikumbukwe kwamba hii si mara ya kwanza kwa baadhi ya maofisa wa ZMA kutuhumiwa kuruhusu vitendo vilivyo kinyume na sheria kama ilivyojitokeza wakati wa kashfa ya kuzama kwa meli ya Spice Islender.
Kwa upande mwingine, Serikali ya Muungano nayo haiwezi kukwepa kuwajibika kwa kuzingatia kuwa kuwa baadhi ya taarifa hizo katika vyombo vya habari vimewanukuu mawaziri wa serikali wakionekana kujikanyanga na kujikanganya juu ya suala hili nyeti la bendera ya taifa, ambayo ni moja ya utambulisho wetu rasmi kama Watanzania, kutumika kwa malengo yasiyojulikana na kampuni ya nje.
Moja ya vyombo vya habari hapa nchini, vimewanukuu mawaziri husika, Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe, juu ya suala hilo.
Wakati Waziri Mwakyembe amenukuliwa akisema kuwa anazo taarifa za suala hilo, lakini asingeweza kulitolea kauli mpaka Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Tanzania Zanzibar azungumze, Waziri Membe yeye mbali ya kukiri kuwa kitendo hicho ni kosa kisheria, anasema habari hizo zilikuwa za kushtushwa na ngeni kabisa, huku akisema kuwa vyombo husika vitalichunguza kwa makini.
Ukimya wa serikali yetu ambayo kwa hakika unatokana na udhaifu wake katika kuchukua maamuzi, sasa umesababisha kitendo hicho kutafsiriwa kuwa Tanzania inaibeba na kuisaidia Iran kukwepa vikwazo ambavyo nchi hiyo inatishiwa na mataifa ya Magharibi, hasa Marekani na Umoja wa Ulaya, kutokana na malumbano ya muda mrefu ambayo yanatokana na mataifa hayo kutumia mabavu na vitisho kuzichagulia baadhi ya nchi nyingine duniani, nini cha kufanya na rasilimali zake mathalani mzozo unaoendelea na Iran kuhusu urutubishaji wa madini ya urani.
Si nia ya CHADEMA kuingia katika mgogoro wa Iran na Mataifa ya Magharibi hapa kupitia mjadala wa madai hayo yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari; lakini CHADEMA kinatoa tamko kufuatia ukimya na kigugumizi kinachoikumba Serikali ya CCM, kila inapohitajika kufanya maamuzi ya haraka, hasa kuwalinda watu wake na hadhi ya utaifa wao na nchi yao ndani na nje ya nchi.
Ni kutokana na udhaifu wa serikali hii, ambayo umekuwa ukijidhihirisha pia kwa kushindwa kupanga bajeti inayojitegemea hasa kwa kutumia utajiri mkubwa wa rasilimali ambazo nchi hii imebarikiwa, hali inayotufanya tuonekane taifa ombaomba na kupoteza heshima mbele ya mataifa makubwa na madogo, kuwa hatuna uwezo wa akili kuweza kujitegemea.
Utegemezi huu umefanya baadhi ya raia wa Nchi nyingine mathalani Mbunge aitwaye Howard Berman wa Bunge la Marekani, akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Nje, kupata uwezo wa kuandika barua ya dharau na kejeli kwa Rais Jakaya Kikwete, juu ya suala hilo la Meli za NIT kutuhumiwa kupeperusha bendera za Tanzania.
Kupitia tamko hili, CHADEMA tunaitaka serikali kutoa kauli madhubuti juu ya suala hilo ambalo tayari limechukua sura ya mjadala wa kimataifa usiokuwa na tija yoyote kwa mustakabali wa Watanzania. Suala la bendera ambayo ni utambulisho wa taifa letu, haliwezi kuwa suala la mchezo tu, ambapo mawaziri wazima hawawezi kutoa kauli za kina na kuchukua hatua zinazostahili.
Imetolewa tarehe 2 Julai 2012 na:
Hamad Mussa Yussuf
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

Monday, July 2, 2012
HAFLA YA KUMUAGA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AFANDE AUGUSTINE NANYARO USIKU WA KUAMKIA LEO
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel Nchimbi akiwa na naibu wake Mhe Pereira Silima (wa kwanza kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Fakihi Jundu (wa pili kulia) wakiwa meza kuu na Kamishna Jenerali wa Magereza anayemaliza muda wake, Afande Augustine Nanyaro (wa tatu kulia) katika hafla ya kumuaga kiongozi huyo wa magereza anayestaafu rasmi mwishoni mwa mwezi huu baada ya kutumikia jeshi hilo kwa takriban miaka 37. Hafla hii ilifanyanyika usiku wa kuamkia leo katika Bwalo la Maafisa wa Magereza la Ukonga, Dar es salaam.
Champaigne ikiandaliwa.
Maafisa wa ngazi mbalimbali wa Magereza na taasisi zingine wakipita meza kuu kumuaga Kamishna Jenerali wa Magereza anayemaliza muda wake, Afande Augustine Nanyaro, katika hafla ya kumuaga kiongozi huyo wa magereza anayestaafu rasmi mwishoni mwa mwezi huu baada ya kutumikia jeshi hilo kwa takriban miaka 37. Hafla hii ilifanyanyika usiku wa kuamkia leo katika Bwalo la Maafisa wa Magereza la Ukonga, Dar es salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza anayemaliza muda wake, Afande Augustine Nanyaro, akijumuika na waalikwa katika hafla ya kumuaga kiongozi huyo wa magereza anayestaafu rasmi mwishoni mwa mwezi huu baada ya kutumikia jeshi hilo kwa takriban miaka 37. Hafla hii ilifanyanyika usiku wa kuamkia leo katika Bwalo la Maafisa wa Magereza la Ukonga, Dar es salaam.

ALICHOKISEMA PRESIDENT KIKWETE KUHUSU MADAKTARI NA ISHU NYINGINE KWENYE HOTUBA YAKE.
Hii ni hotube ya President Jakaya Kikwete katika utaratibu wake wa kuzungumza na watanzania kila mwisho wa mwezi..
“Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza nusu ya kwanza ya mwaka 2012 salama. Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza nanyi kila mwisho wa mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili. Jambo la kwanza ni suala la usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili ni la mgomo wa madaktari”
Usafirishaji Haramu wa Binadamu Nchini
Bila ya shaka mtakuwa mmezisikia taarifa za tukio la kushtusha na kuhuzunisha la kukutwa maiti 43 za watu wasiojulikana, zilizotupwa katika kichaka kilichopo kijiji cha Chitego, Wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma tarehe 26 Juni, 2012.
Pamoja na maiti hao, walipatikana watu 84 wakiwa hai lakini wote wakiwa wamedhoofu na baadhi yao wakiwa mahututi.
Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao hadi Dodoma ambapo wale waliokuwa mahututi walifikishwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na wengine walihifadhiwa katika Kituo cha Kati cha Polisi, Dodoma.
Maiti 22 zilipelekwa Dodoma na 21 zilipelekwa Morogoro kuhifadhiwa.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa wale walionusurika zimebainisha kuwa watu hao ni raia wa Ethiopia ambao walikuwa safarini kwenda Malawi na baadaye Afrika ya Kusini ambako wangetengenezewa utaratibu wa kwenda kuishi Marekani na Ulaya.
Kwa mujibu wa maelezo yao, safari yao ilianza miezi mitano iliyopita. Mwezi mmoja waliutumia Ethiopia na miezi minne waliitumia Kenya kabla ya kuletwa Arusha ambako walipakiwa kwenye lori na kuanza safari ya kuelekea Malawi lakini ikaishia Chitego.
Lori walilopanda lilikuwa limezibwa kabisa na hivyo kusababisha vifo kwa kukosa hewa.
Tukio la Chitego, Dodoma la wahamiaji haramu kukamatwa na wengine kukutwa wamekufa si la kwanza kutokea hapa nchini. Kwa jumla, katika kipindi cha takriban miaka 10 sasa kumekuwepo na tatizo kubwa la wahamiaji haramu kuingia nchini.
Kwa mfano, kati ya mwaka 2005 na hivi sasa jumla ya wahamiaji haramu 19,683 wamekamatwa. Karibu wote wameshaondoshwa nchini na hivi sasa wapo karibu watu 1,500 tu magerezani wanaotumikia adhabu na kusubiri kurejeshwa makwao.
Wengi wa watu hao wanatoka Ethiopia na Somalia na baadhi kutoka Pakistan na Bangladesh.
Wahamiaji haramu wamekuwa wanaingia nchini kwa kupitia njia zisizo rasmi. Wapo wanaotumia nchi kavu hasa kupitia mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
Na, wapo wanaopitia baharini kwa kutumia fukwe za Pemba, Unguja na za mikoa ya ukanda wa Pwani ya Tanzania Bara yaani Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.
Kwa mujibu wa kauli zao, watu hao wamekuwa wanaeleza kuwa hawaji nchini kuhamia bali wao ni wapita njia tu.
Wanaelekea Afrika ya Kusini ambako wameahidiwa kuwa watatengenezewa mipango ya kuhamia Marekani na Ulaya.
Watu hao pia wamethibitisha kuwepo kwa watu maalum wanaojihusisha na usafiri wao tangu nchi watokako na zote wanazopitia mpaka kule waendako.
Aidha, wamesema kuwa wao wanawalipa watu hao ili wawasafirishe na hakika si kiwango kidogo.
Kwa jumla ni kwamba hili si suala la uhamiaji haramu bali ni la biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
Ndugu Wananchi;
Kufuatia vyombo vyetu vya usalama kuwa makini na watu wengi kukamatwa ndipo wasafirishaji walipobuni njia za kuwasafirisha kama mizigo. Makontena, malori yaliyofunikwa nyuma na matenki ya mafuta na ya maji yamekuwa yanatumika kwa ajili hiyo.
Usafiri wa aina hiyo ndiyo uliosababisha vifo vilivyotokea Dodoma tarehe 26 Juni, 2012 na vya watu 21 vilivyotokea mwezi Desemba, 2011 Mkoani Morogoro, na vile vya watu 12 vilivyotokea katika matukio mawili ya Mkoa wa Mbeya, mwezi Mei, 2012.
Ndugu Wananchi;
Tarehe 27 Juni, 2012 nilikutana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuzungumzia tukio la Chitego na suala zima la biashara hii haramu na hasa mbinu mpya inayotumiwa na wasafarishaji.
Nilitoa pongezi kwa vyombo vya dola kwa kazi nzuri waifanyayo kudhibiti shughuli za biashara hii haramu hapa nchini.
Tulielewana kuwa waendelee kuimarisha udhibiti huo kwa lengo la kukomesha kabisa biashara hii.
Niliagiza pia kwamba kikundi kazi nilichokiunda mwaka 2006 kushughulikia ujambazi sasa kielekeze sehemu ya nguvu zake kukabili tatizo hili.
Aidha, kwa pamoja tulikubaliana kuwa nchi yetu ishirikiane na wenzetu wa Ethiopia, Kenya, Malawi, Msumbiji na Afrika ya Kusini kutambua mawakala na kuwabana kwa mujibu wa sheria.
Tayari nimeshaanza kufanya mawasiliano na baadhi ya Wakuu wa Nchi hizo kuhusu ushirikiano huo.
Nashukuru wote wameafiki nchi zetu zishirikiane kwa pamoja kuvunja mtandao huu mchafu na kutokomeza biashara hii haramu na inayodhalilisha utu wa mwanadamu.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wenzetu, wakazi wa vijiji vya Chitego na Mkoka kwa kazi nzuri walioifanya.
Kwa kweli, wenzetu wameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kutoa taarifa mapema juu ya jambo lenyewe, lakini pia wameonesha utu kwa kuwajali wageni waliokumbwa na janga hili.
Naushukuru pia uongozi wa Mkoa wa Dodoma na Morogoro ikiwa ni pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kulishughulikia tatizo hilo kwa umakini mkubwa.
Nimefurahishwa sana na ushirikiano ulioonyeshwa na vyombo na taasisi mbalimbali za Serikali katika kushughulikia suala hili.
Mgomo wa Madaktari
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ni kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa.
Nilipozungumza na Wazee wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 12 Machi, 2012, kuhusu mgomo wa Madaktari uliokuwa unaendelea wakati ule pamoja na kuelezea chimbuko la mgomo na hatua iliyokuwa imefikiwa, nilielezea mazungumzo yangu na viongozi wa Chama cha Madakari wakiwemo pia viongozi wa Jumuiya ya Madaktari.
Nilitoa taarifa kuwa tumeelewana kuwa watasitisha mgomo na watarudi kwenye meza ya majadiliano na Serikali.
Siku ile pia nilielezea matumaini yangu kuwa mgomo ule utakuwa wa mwisho katika nchi yetu.
Bahati mbaya matumaini yangu hayo hayakuwa na hivi sasa tunashuhudia tena wagonjwa wakiteseka, kuhangaika na wengine kufa kwa sababu ya kukosa huduma wanazostahili kwa vile madaktari wao wamegoma tena.
Ndugu Wananchi;
Kama walivyoniahidi, madaktari waliacha kugoma na viongozi wao walirudi kwenye mazungumzo na Serikali.
Kama ilivyoagizwa na Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi tarehe 8 Machi, 2012, kwa mujibu wa Sheria ya Mahusiano Kazini, Namba 6 ya mwaka 2004.
Chama cha Madaktari na Serikali walifika katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Commission for Mediation and Arbitration) kwa ajili ya majadiliano. Kwa pamoja na kwa ridhaa yao wote, pande hizo mbili ziliiomba Tume hiyo iwape fursa ya kuzungumza wao wenyewe na wakimaliza mazungumzo wataenda kusajili makubaliano yao.
Tume ikawakubalia.
Ni vizuri ikakumbukwa kuwa siku ile ya tarehe 8 Machi, 2012 Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, ilitoa zuio la mgomo pamoja na kuagiza kuwepo mazungumzo baina ya pande mbili.
Ndugu Wananchi;
Kati ya tarehe 10 Aprili, 2012 na tarehe 30 Mei, 2012, vilifanyika vikao sita vya majadiliano kati ya Serikali na Chama cha Madaktari.
Katika mazungumzo hayo hoja au madai 12 ya madaktari yalizungumzwa. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
1. Posho ya kuitwa kazini (on call allowance) iwe asilimia 10 ya mshahara.
2. Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) iwe asilimia 30 ya mshahara.
3. Madaktari wapatiwe nyumba grade A au posho ya makazi ambayo iwe asilimia 30 ya mshahara.
4. Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu iwe asilimia 40 ya mshahara.
5. Madaktari walipwe posho ya usafiri ya asilimia 10 ya mshahara au wakopeshwe magari.
6. Madaktari wanaoanza kazi walipwe mshahara wa shilingi 3,500,00/= kwa mwezi.
7. Madaktari wapatiwe Green Card za Bima ya afya.
8. Hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
9. Viongozi wa Kisiasa kulazimisha kupewa rufaa nje.
10. Madaktari waliofukuzwa warudishwe kazini.
11. Huduma za afya ziboreshwe nchini.
12. Posho ya uchunguzi wa maiti iongezwe.
Ndugu Wananchi;
Katika mambo hayo 12 pande zote mbili zilifikia muafaka na kukubaliana wa pamoja kwa mambo saba.
La kwanza, ni kuhusu usafiri wa kwenda na kurudi kazini.
Serikali ilieleza kuwa upo utaratibu kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi wa Serikali Na. 3 wa mwaka 2011 wa kuwakopesha wafanyakazi wa Serikali fedha za kununulia magari au pikipiki, samani na matengenezo ya magari.
Ilikubaliwa kuwa madaktari waitumie fursa hiyo.
Jambo la pili, ni kuhusu madaktari kupatiwa Green Card za Bima ya Afya. Jambo hili lilikubaliwa na Serikali na Wizara ya Afya imekwishachukua hatua za utekelezaji wake.
Jambo la tatu, ni kuhusu hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya.
Kwa pamoja walikubaliana kuwa suala hilo liko nje ya mamlaka ya Kamati yao ya pamoja, waziachie mamlaka husika za uteuzi.
Uongozi wa juu wa Wizara umebadilishwa na sasa kuna uongozi mpya.
Lakini, jambo la kustaajanisha hata Waziri mpya wa Afya alipowataka waonane kuzungumzia hoja walikataa kumuona.
Kwanza walisema hawaoni sababu kwa vile wameyazungumza na Kamati yake kwa miezi mitatu bila ya mafanikio
Jambo la nne walilokubaliana ni kuhusu viongozi kulazimisha kupewa rufaa ya kutibiwa nje. Walikubaliana mambo mawili.
Kwanza, kwamba maelekezo ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kuwa madaktari wazingatie maadili ya kazi zao na kukataa kutoa rufaa kwa mtu asiyestahili awe kiongozi au asiwe kiongozi.
Pili, walikubaliana kuwa hospitali zilizopo ziboreshwe ili viongozi watibiwe hapa nchini.
Ukweli ni kwamba kufanya hivyo ndiyo sera ya Serikali.
Nililieleza hili mwezi Desemba 30, 2005 katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza nchi yetu.
Tumeiongeza sana bajeti ya sekta ya afya kutoka shilingi bilioni 300 2005/2006 hadi shilingi trilioni 1.2 mwaka 2011/12 na imekuwa ya tatu baada ya miundombinu na elimu. Tumeziimarisha hospitali za Mikoa kwa vifaa tiba na wataalamu wa afya. Kazi inaendelea katika hospitali za Wilaya.
Tumewekeza katika Hospitali ya Muhimbili. Hospitali hiyo ilivyo leo sivyo ilivyokuwa miaka sita nyuma.
Na kazi inaendelea hasa katika maeneo ambayo tunapeleka wagonjwa nje.
Matunda yake yanaanza kuonekana kwa upande wa figo, moyo, kinywa na mipango inaendelea kwa upande wa ubongo na mishipa ya fahamu. Tunaendelea kuimarisha mafunzo ya madaktari na madaktari bingwa, yote kwa nia hiyo hiyo.
Hivi sasa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba,Muhimbili kinachukua wanafunzi wengi zaidi ya ilivyokuwa siku za nyuma na makazi mapya ya chuo yanaendelea kuandaliwa ili kuchukua wanafunzi wengi zaid.
Mwaka 2005 tulikuwa na madaktari bingwa 46 mwaka huu tunao 520.
Ndugu Wananchi;
Jambo la tano ambalo pande zote mbili zilikubaliana ni kuhusu madaktari waliofukuzwa. Hawa ni wale Interns waliokuwa wamerudishwa Wizarani kutoka Muhimbili na kupangiwa hospitali za Temeke, Ilala, Mwananyamala na Lugalo. Hili ni jambo ambalo lilikuwa limemalizika kitambo na wote walikuwa wamerudi Muhimbili.
Jambo la sita ni kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na madaktari kuhusu kuboresha huduma ya afya.
Mapendekezo hayo yalihusu kutathmini sera na mpango wa afya ya msingi, bajeti ya afya kuwa asilimia 15 ya bajeti ya Serikali, kuwepo na utaratibu mzuri wa kuajiri madaktari na kuboresha viwango vya ubora wa madaktari na kadhalika.
Serikali imeyaafiki mapendekezo hayo na yatafanyiwa kazi.
Jambo la saba, ambalo pande zote walilokubaliana ni kuhusu kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti.
Hili ni jambo jipya halikuwepo mwazoni. Hata hivyo, Serikali imelikubali na posho hiyo imeongezwa kutoka shilingi 10,000/= hadi kufikia shilingi 100,000/= kwa daktari na shilingi 50,000/= kwa wasaidizi wake.
Ndugu Wananchi;
Kuna masuala matatu ambayo yamekuwa na muafaka kwa kiasi fulani na kutoafikiana kwa baadhi ya mambo.
La kwanza ni suala la kufanya kazi katika mazingira hatarishi.
Serikali imekubali hoja ya kuchukua hatua ya kuwalinda madaktari wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi.
Serikali iliwaeleza kuwa watumishi wa kada zote za afya watapatiwa chanjo dhidi ya maambukizi ya Hepatitis B na fedha zimetengwa katika bajeti ya 2012/13.
Aidha, Serikali imeeleza dhamira ya kurudisha posho ya mazingira hatarishi kwa watumishi wa umma wanaostahili.
Utekelezaji wake utafanyika baada ya uchambuzi wa kina wa kubainisha mazingira hatarishi ni yepi, viwango stahiki viwe vipi na nani hasa wahusike. Madaktari wamekataa hili la kufanya uchambuzi, wanataka kiwango kiwe kama wanavyotaka wao, yaani asilimia 30 ya mshahara na kianze mara moja.
Jambo la pili ambalo wamekubaliana nusu nusu ni kuhusu nyumba za kuishi.
Serikali imekiri wajibu wake wa kuwapatia madakari nyumba za kuishi. Aidha, imeeleza mpango ulioanza wa kujenga nyumba 700 za madaktari kote nchini na kwamba hivi sasa ujenzi wa nyumba 90 unaendelea, 50 katika mkoa wa Mtwara na 40 katika mkoa wa Rukwa.
Kwa maeneo ambayo madaktari wanalipwa posho ya pango Serikali imesema waajiri wataendelea kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizopo kwa watumishi wa umma wenye stahili ya kupewa nyumba.
Jambo hilo limekataliwa na Madakari na kutaka lazima walipwe asilimia 30 ya mshahara kama posho ya nyumba.
Serikali kwa upande wake imeona vigumu kufanya hivyo na kuwasihi wakubali wanayotendewa wafanyakazi wengine wote wa umma.
Jambo lingine ambalo lilikuwa na makubaliano ya nusu nusu ni kuhusu posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu.
Pande zote mbili ziliafikiana kuwa yapo baadhi ya maeneo nchini yanayo mazingira magumu kwa watumishi wa umma hivyo hatua zichukuliwe kuwasaidia watumishi hao.
Serikali imekubali wajibu wa kuweka utaratibu wa kuboresha maisha ya watumishi katika maeneo hayo.
Kwa ajili hiyo, Serikali itatoa mwongozo kwa mamlaka za ajira kuhusu namna ya kuwasaidia watumishi hao kupunguza makali ya maisha katika kila eneo badala ya kutegemea posho peke yake.
Kuhusu posho, Serikali imeeleza kuafiki kuwepo posho ya aina hiyo ila itatekelezwa baada ya kufanya uchambuzi wa kuainisha mazingira husika, kutambua watumishi waliopo na gharama zake.
Madaktari hawajakubali kusubiri zoezi la uchambuzi lifanyike, wanataka Serikali ilipe posho hiyo sasa.
Tofauti hapa si posho hiyo kuwepo, bali ni rai ya Serikali ya kubaini maeneo yenyewe na kupanga aina ya hatua na viwango vya posho kulingana na mazingira halisi ya maeneo.
Madaktari hawaoni haja ya kufanya hayo.
Ndugu Wananchi;
Mambo mawili hayakuwa na muafaka kabisa kati ya pande zetu mbili. Jambo la kwanza ni posho ya kuitwa kazini (on call allowance).
Kwanza sina budi kueleza kuwa Serikali imekubali kuongeza posho hiyo.
Tangu Februari, 2012 posho iliongezwa kutoka shilingi 10,000/= hadi shilingi 25,000/= kwa daktari bingwa (Specialist), shilingi 20,000/= kwa dakari mwenye usajili wa kudumu (Registrars) na shilingi 15,000/= kwa madaktari waliohitimu ambao wapo katika kipindi cha mafunzo kazini (Interns).
Viwango hivyo vya posho vinatumika hivi sasa.
Madaktari kwa upande wao hawakukubali uamuzi huo wa Serikali na kusisitiza walipwe asilimia 10 ya mshahara. Ugumu wa kukubali pendekezo la madakari ni kuwa sharti la malipo haya ni mtu kuitwa kazini. Ukitaka ilipwe kiwango cha mshahara ina maana kuwa hata kama daktari hakupangwa kuitwa au alipangwa na hakutokea aendelee kulipwa. Hili haliwezi kuwa sahihi kufanya. Linaweza kuwafanya baadhi ya madaktari kutokutimiza wajibu wao kwa vile wana hakika mwisho wa mwezi malipo yako pale pale.
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ambalo muafaka haukufikiwa baina ya Serikali na madaktari ni kuhusu mshahara wa kuanzia kazi wa daktari. Madaktari wanataka uwe shilingi 3,500,000/= wakati Serikali inasema kiasi hicho hatukiwezi. Serikali imeeleza utayari wake wa kuongeza mshahara kwa kati ya asilimia 15 mpaka 20 kama ambavyo itafanya kwa watumishi wote wa umma katika mwaka huu wa fedha. Kwa kiwango cha sasa cha mshahara wao, daktari ataanzia kati ya shilingi 1,100,000/= na 1,200,000/= kutegemea kiwango kipi hatimaye kitaamuliwa. Madaktari wamekataa katakata na wameng’ang’ania shilingi 3,500,000/=.
Ndugu Wananchi;
Huo ndiyo mlolongo wa mambo yaliyozungumzwa na pande zote mbili na matokeo ya mazungumzo yenyewe. Katika kikao cha sita kilichofanyika tarehe 30 Mei, 2012, upande wa Chama cha Madaktari ulisema kuwa kwa vile hoja ya nyongeza ya mshahara haina mabadiliko hawakuona haja ya kuendelea na majadiliano mpaka watakapowasiliana na wenzao. Waliahidi kutoa taarifa ndani ya wiki mbili. Tarehe 12 Juni, 2012, Rais wa MAT aliandika barua kwa Katibu Mkuu Utumishi ambaye ndiye kiongozi wa majadiliano kwa upande wa Serikali, kuwa Madaktari wameikataa taarifa na ufafanuzi waliopewa kutoka Serikalini kwa ujumla wake.
Ndugu Wananchi;
Baada ya majibu yale ya madaktari, tarehe 19 Juni, 2012, Serikali na Madaktari walikwenda kwa Msuluhishi (CMA) kutoa taarifa kuwa mgogoro umekosa usuluhishi kama sheria inavyotaka. Kwa pamoja pande zote mbili zilikubaliana suala hilo lifikishwe Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi. Wakati pande zote zinasuburi mgogoro huu kufikishwa ngazi hiyo ya juu, upande wa Madaktari ukatangaza kuwepo kwa mgomo kuanzia saa sita ya usiku tarehe 23 Juni, 2012. Hatua hiyo haikustahili kwani suala lenyewe halijafika mwisho wa kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria za Mahusiano ya Kazi nchini.
Ndugu Wananchi;
Tarehe 22 Juni, 2012, Mwanasheria Mkuu wa Serikali akaenda Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kulifikisha suala la tishio la mgomo na kuomba zuio la muda kufanywa.
Mahakama Kuu ilikubali ombi hilo na kuagiza kuwa mgomo usitishwe. Juhudi za kumtafuta Rais wa MAT, Dkt. Namala Mkopi na viongozi wengine wa MAT hazikufanikiwa, Ofisi ya MAT ilikuwa imefungwa na simu zote za viongozi wa MAT zilikuwa zimezimwa.
Hatimaye tarehe 25 Juni, 2012, alipatikana na kupewa amri hiyo ya Mahakama. Tarehe 26 Juni, 2012, Dkt. Mkopi alifika Mahakamani ambapo alikana kuwa yeye hahusiki na kuitisha huo mgomo lakini hakumtaja aliyehusika.
Pamoja na rai hiyo, Jaji alimuamuru Rais wa MAT akawatangazie wanachama wake kusitisha mgomo.
Dkt. Namala Mkopi hajafanya hivyo hadi leo na mgomo umekuwa unaendelea kinyume cha Sheria.
Ndugu Wananchi;
Wagonjwa wanateseka na wengine kupoteza maisha kwa mgomo huu usiokuwa halali kisheria ambao pia haustahili kuwepo hata kwa mujibu wa maadili ya udaktari.
Viongozi wa MAT na wenzao wanawaingiza Madaktari katika mgogoro na Mahakama na waajiri wao isivyostahili. Ni vyema viongozi wa Madaktari na madaktari wakatambua kuwa wanashiriki katika mgomo usiokuwa halali ambao pia kiongozi wao mkuu amekana Mahakamani kuwa hahusiki nao. Madaktari lazima watambue pia kwamba ajira zao wanaziweka hatarini. Mfanyakazi ana kinga ya kutofukuzwa kazi na mwajiri kwa kushiriki mgomo unaokubalika kisheria.
Huu siyo. Watapoteza ajira, hawana pa kukimbilia, hawana cha kiwalinda.
Kwa madaktari interns, wanahatarisha maisha yao kwani hawatapata cheti cha kudumu wakishiriki mgomo usiokuwa halali.
Lazima watafakari sana kwa hayo wafanyayo.
Ndugu Wananchi;
Napenda kurudia maneno niliyoyasema tarehe 12 Machi, 2012, kuwa kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi ni Sera ya Serikali yetu kwa maelekezo ya Ilani ya Chama Tawala (CCM).
Tumeitekeleza kwa vitendo sera hiyo, hata hivyo ni ukweli ulio wazi kuwa nia yangu njema tu pekee haitoshi, lazima uwezo wa kufanya hivyo uwepo.
Kwa kulingana na uwezo uliopo, tumeendelea kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi hatua kwa hatua tangu tuingie madarakani.
Tumefanya hivyo kwa jumla kwa wafanyakazi wote na kwa kada mbalimbali za watumishi wa umma.
Miongoni mwa wafanyakazi wa umma walionufaika na hatua hizo za Serikali ni madaktari na watumishi wa kada nyingine za huduma ya afya.
Tena nadiriki kusema madaktari tumewapa upendeleo mkubwa kuliko watumishi wengine wa umma.
Upendeleo upo kwenye mafunzo ambapo wanafunzi wa udaktari wanagharimiwa na Serikali kwa asilimia mia moja wakati wanafunzi wenzao wa taaluma nyingine hawako hivyo.
Ndugu Wananchi;
Mwaka 2004/2005, mshahara wa kuanzia wa daktari ulikuwa shilingi 178,700/=, mwaka 2005/ 2006 tuliupandisha na kuwa shilingi 403,120/=. Tuliendelea kuupandisha mwaka hadi mwaka mpaka kufikia shilingi 957,700/= wanazolipwa sasa.
Kiasi hicho ni mara mbili ya mishahara ya watumishi wa taaluma nyingine wenye shahada ya kwanza wanaoanza kazi ambao kwa wastani hupata shilingi 446,100/=.
Tunafanya hivyo kwa kutambua na kuthamini nafasi maalum ya madaktari katika jamii na ukweli kwamba bado tunayo safari ndefu ya kuziba pengo la madaktari nchini.
Lakini inaonekana juhudi zetu zote hizo hazithaminiwi.
Ndugu Wananchi;
Sina budi kusisitiza kwamba tunapofanya hivyo tunaongozwa na uwezo tulio nao wa kulipa.
Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000/= na posho zote zile.
Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa shilingi 7,700,000/=.
Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari.
Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho.
Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo. Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka.
Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi.
Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu.
Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24.
Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe.
Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari.
Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma.
Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi.
Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwathibitishia kwamba dhamira ya Serikali ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wakiwemo madaktari iko wazi.
Tumekuwa tunafanya hivyo, na tutaendelea kufanya hivyo kulingana na uwezo wa kibajeti.
Ni vyema watumishi wa umma wakatambua kuwa hatuwezi kutumia fedha zote au kiasi kikubwa mno cha pesa za umma kulipana mishahara. Tukifanya hivyo, Serikali itashindwa kutoa huduma muhimu kwa wananchi ambao ndiyo wengi na wanastahili kuhudumiwa.
Hata hizo huduma za afya tunazosema ni duni tuziboreshe, hatutaweza kuziboresha kama tutatumia sehemu kubwa ya pesa za Serikali kuwalipa mishahara wafanyakazi.
Hivi sasa matumizi ya mishahara ni asilimia 48 ya bajeti ya Serikali. Kiwango hicho ni kikubwa mno.
Uwiano mzuri ni kuwa na matumizi ya mishahara yasiyozidi asilimia 35 ya bajeti na asilimia 65 zitumike kugharimia huduma na shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi na taifa.
Sisi tumezidi kwa asilimia 13. Hivyo, hatuna budi tukubali kujinyima kwa manufaa ya walio wengi.
Suala la Dkt. Steven Ulimboka
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven Ulimboka usiku wa tarehe 26 Juni, 2012.
Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo.
Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane.
Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.
Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka.
Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo.
Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari.
Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya.
Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.
Ndugu Wananchi;
Kama nilivyoeleza, mazungumzo yalienda vizuri na mafanikio makubwa yamepatikana.
Yapo maeneo machache na hasa eneo la mshahara ambalo hatukuweza kukubaliana.
Hapo tulipofikia si pabaya na tulikubaliana sote kurudi kwenye mkondo wa Sheria kusaidiwa.
Kwa nini Serikali imdhuru Dkt. Ulimboka? Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo.
Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo.
Hivi baada ya kufika hapo Serikali iwe na ugomvi na Dkt. Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru? Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali.
Ndugu Wananchi;
Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali natoa mkono wa pole kwa Dkt. Steven Ulimboka na kumuombea apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania wenzake katika ujenzi wa taifa. Kwa namna ya pekee namshukuru na kumpongeza Bwana Juma Mgaza, kwa moyo wake wa huruma na upendo na kwa hatua alizochukua za kumsaidia Dkt. Ulimboka.
Naomba kumaliza kwa kuwasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini. Watanzania wenzenu wanateseka na kupoteza maisha.
Muwe na moyo wa huruma na upendo na msaada kwa wagonjwa kama kiapo chenu kinavyowataka.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa Kunisikiliza.

UWOYA AKIRI KUPOTEZA MWELEKEO

Irene Pancras Uwoya.
Na Imelda Mtema
MWIGIZAJI Irene Pancras Uwoya amekula kiapo mbele ya Ijumaa Wikienda kuwa hataki kuonja pombe tena kwani anakiri zimempotezea mwelekeo kwa kumharibia vitu vyake vingi.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzikati, Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alisema amegundua kuwa pombe haina faida kwake.
Tujiunge na Uwoya: “Mbali na kupoteza fedha nyingi lakini wakati mwingine nashindwa kutimiza ratiba yangu na hasa nikiwa na ‘apointimenti’ muhimu nashindwa kuitimiza kwa sababu ya pombe kwa hiyo natangaza rasmi kuacha na nawasihi wasanii wenzangu nao waache.”
MAMA ULIMBOKA: NAMWACHIA MUNGU

KUFUATIA tukio la mwanaye ‘kusulubiwa’ wiki iliyopita, mama mzazi wa Dk. Steven Ulimboka ambaye hakutaka jina lake lipambe ukurasa huu, ameliambia Ijumaa Wikienda kuwa anashukuru Mungu kwa kwenda kumuona mtoto wake na kumkuta akiwa hai.
Baada ya kumuona mwanaye akipatiwa matibabu kwenye Taasisi ya Mifupa Moi katika Hospitali ya Muhimbili, Dar, mama huyo alisema tatizo lililompata mwanaye anamwachia Mungu kwani ndiye mwamuzi wa uhai wa kila mtu hapa duniani.
“Namwambia Mungu asante kwa kuwa nimemkuta yupo hai. Kwa jinsi nilivyopata taarifa niliamini mwanangu amefariki dunia japo hali yake si ya kuridhisha,” alisema kwa uchungu.
Jumamosi mchana, Dk. Ulimboka alisafirishwa kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu kufuatia kubainika kuwa ubongo wake ulikuwa umetikisika.
Dk. Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumatano wiki iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambapo alipigwa vibaya na kwenda kutupwa kwenye msitu wa Pande nje kidogo ya jiji.
Tukio hilo limekuwa ndiyo habari ya mjini kwa sasa kwani lilitokea katika kipindi ambacho madaktari wapo kwenye mgomo huku Dk. Ulimboka akiwa ndiye kiongozi wa jumuiya yao.
Subscribe to:
Posts (Atom)