Saturday, August 11, 2012

Taarifa Kwa Umma Kutoka Benki Kuu Ya Tanzania

Katika Gazeti la Business Times toleo nambari 1248 la Ijumaa, tarehe 10 Agosti 2012, ziliandikwa habari zenye kichwa cha habari chenye maana kuwa “Operesheni za NBC zawekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu”. Katika habari hiyo ilielezwa kuwa Benki Kuu imechukua hatua hiyo kufuatia ripoti za tuhuma kadhaa zihusuzo udhaifu katika uendeshaji wa benki na utawala bora.

Benki Kuu inapenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa haijaweka operesheni/shughuli za NBC chini yake. Benki hiyo inajiendesha yenyewe kwa kufuata utaratibu wa Sheria za Makampuni, 2002, Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha 2006 na miongozo itolewayo na Benki Kuu kama zilivyo benki zingine. Wateja wa NBC na Umma kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufanya biashara na benki hii kama kawaida.

IMETOLEWA NA BENKI KUU YA TANZANIA11AUGUST 2012

Magazeti ya Leo Ijumaa 11st August 2012

Ajali Ya Gari Yaua Raia 11 Wa Kenya Eneo La Wami Mkoa Wa Pwani

 Basi lililokuwa limewabeba raia wa Kenya waliokuwa wakielekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mikutano ya injili  likiwa limetumbukia katika korongo jirani na Mto Wami na kuua watu 11 katika Kijiji cha Makole Mkoa wa Pwani.

Baadhi ya abiria walionusurika wakiwa katika eneo la tukio kabla ya kupata msaada.

WATU 11 wanaoaminika kuwa raia wa Kenya wamefariki dunia papo hapo, huku wengine saba wakiwa mahututi baada ya mabasi waliyokuwa wakisafiria kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam kupata ajali katika Mto Wami mkoani Pwani.Mbali na vifo hivyo, ajali hiyo pia ilisababisha majeruhi 25 na saba kati yao waliripotiwa kuwa mahututi na walipelekwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha kwa matibabu.

Ajali hiyo ilitokea katika Kijiji cha Makole, wilayani Bagamoyo wakati abiria hao ambao ni wanakwaya walipokuwa wakisafiri kutoka Kenya kwenda Dar es Salaam kushiriki katika tamasha la uimbaji.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri ikihusisha magari manne, mawili kati yake yakiwa ni mabasi hayo yakitokea Kenya na malori mawili ya hapa nchini.Tukio hilo pia lilifunga Barabara Kuu ya Chalinze - Segera kwa zaidi ya saa nane hivyo abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea na kutoka mikoa ya Kaskazini ikiwamo nchi ya Kenya kwenda na kutoka Dar es Salaam kukwama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu alisema raia hao wa Kenya ni waumini wa Kikristo na walikuwa wakielekea Dar es Salaam kwenye tamasha la kwaya.

JK: Ahudhuria Mazishi Ya Aliyekuwa Rais Ghana John Atta Mills

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo wakati shughuli ya mazishi ya Rais John Evans Atta Mills wa Ghana katika ukumbi wa Mikutano wa Ghana jijini Accr.
                                        Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Ghana Marehemu Profesa John Evans Atta Mills katika ukumbi wa Mikutano wa Ghana jijini Accra Jana.
 Jukwaa kuu katika uwanja wa Independende Square wakati wa Shughuli mbalimbali za mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra.


 Shughuli mbalimbali za mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa  Independence Square jijini Accra jana.

Friday, August 10, 2012

TAFF YATOA TAMKO JUU YA MAHARAMIA WA FILAMU

SHIRIKISHO la Filamu nchini(TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa filamu na kazi za wasanii ‘wameapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi ya wasanii.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni kero kwa muda mrefu.

Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.

“Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao”
“Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache ndiyo wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba.

Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.

Alisema Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.

Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubaliana kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo.

Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwenda kwa haki ili wasanii na kazi zao

Tume ya Huduma za Bunge la Malawi yakutana na Spika wa Bunge la Tanzania mjini Dodoma

 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kushoto) na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (Mb) kwa pamoja wakiwa na mazungumzo ya kina leo na ujumbe wa Tume ya Huduma za Bunge la Malawi ulioko nchini hivi sasa, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia uhusiano mzuri wa mabunge ya nchi mbili hizi. Kushoto kwa Mhe. Ndugai ni Naibu Spika wa Bunge la Malawi Mhe.Juliana Mpande (Mb) ambaye ni mkuu wa msafara. Wengine ni Kamishna  Alfred Mwechumu (Mb) na Kamishna Christina Chiwowo (Mb).
Spika wa Bunge la Tanzania akiwa na mazungumzo na Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliofika ofisini kwake Dodoma leo. Spika Makinda amewataka na kuwaasa kuwa na uzalendo kwa nchi yao.

Picha na Prosper Minja - Bunge

CHAMA CHA WALIMU CWT CHATOA TAMKO LAKE KWA SERIKALI


 Rais wa Chama Cha walimu Tanzania Bw. Gratian Mukoba (Kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam kuhusiana na Tamko lao  kwa serikali kutaka iwarudishie madaraka wakuu wote waliovuliwa nyadhifa zao kwakuwa ni viongozi wa (CWT) ndio waliohamasisha mgomo.

Vilevile chama hicho kimeitaka serikali  kufuta nia yake ya kuwashitaki walimu zaidi ya 180,000 walioshiriki mgomo kati ya walimu 233,440 walioko nchini kwani kwa kufanya hivyo watoto wa maskini wanaotegemea walimu hao kufundisha watakosa haki yao ya kufundishwa.Kulia na Kaimu katibu mkuu wa chama hicho Bw, Ezekiel Olotu.

(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

Hali ya uuzaji wa madawa ya binadamu kiholela jijini Dar Es Salaam inatisha

Matokeo haya yametokana na utafuti ulifanywa na YITA Novemba 2011 na ulihusisha watafitit waliofanya ziara siri (mystery shoppers) 126 katika maduka 64 ya wilaya zote tatu za Dar es salaam. Jina la muhtasari wenye matokeo hayo ni “Ununuzi wa dawa jijini Dar es Salaam-Je, maduka ya dawa yanazingatia kanuni?” . Pamoja na mengine watafiti waliweza kuhoji yafuatayo;

    Je, dawa zinaweza kutufanya wagonjwa? Je, zinatolewa ipasavyo? Na je, mfumo wa kuwalinda wananchi kutokana na madhara ya matumizi mabaya ya dawa unafanya kazi vizuri?

    Ikumbukwe mamlaka ya dawa na chakula Tanzania imetamka wazi kwenye  Kifungu cha 31:3 ya viwango vya biashara ya dawa nchini ya mwaka 2006 (Pharmaceutical Business Standards Regulations) kuwa;

    “Hakuna mtoaji dawa yeyote atakayetoa dawa ambazo matumizi yake yanapaswa kuwa kwa maagizo ya daktari tu isipokuwa kwa agizo la matumizi ya dawa husika lililotolewa na mfanyakazi wa afya, mganga wa meno au wa mifugo au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa kuagiza matumizi ya dawa”.

    Utaafiti imedhihirisha ukiukwaji mkubwa wa kanuni za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).Ni wazi madhara yafuatayo yataliandama Taifa kama hatua za dhati hazitachukuliwa haraka;

WENGI WAZIDI KUNUFAIKA NA PROMOSHENI YA "JENGA MAISHA YAKO NA NMB"


 Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kushoto) akibofya kwenye kompyuta kuwapata washindi wa promosheni ya 'Jenga Maisha Yako na NMB' katika droo iliyofanyika, Dar es Salaam jana, ambapo baadhi ya washindi watazawadia mabati, saruji, ada ya shule, mteja kuongezewa amana maradufu na zawadi nyingine lukuki. Wanaoshuhudia ni Mratibu wa Miradi wa Selcom Wireless, Everline Simpilu (kulia) na Sadiki Elimsu ambaye ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Kusimamia Michezo ya Kubahatisha (GBT)
 Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kushoto) akibofya kwenye kompyuta kuwapata washindi wa promosheni ya 'Jenga Maisha Yako na NMB' katika droo iliyofanyika, Dar es Salaam leo.

Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kushoto) akibofya kwenye kompyuta kuwapata washindi wa promosheni ya 'Jenga Maisha Yako na NMB' katika droo iliyofanyika, Dar es Salaam jana, ambapo baadhi ya washindi watazawadia mabati, saruji ada ya shule, mteja kuongezewa amana maradufu na zawadi nyingine lukuki. Wanaoshuhudia ni Mratibu wa Miradi wa Selcom Wireless, Everline Simpilu

 PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA

"Hujafa Hujaumbika" Duniani matezo na raha zote za wanadamu aliyeguswa toa kwa moyo leo kwake kesho kwetu Naamini watanzania tunaweza na moyo tunao...

Beatrice Shimende Kantimbo (48) anaomba msaada wa pesa kwa ajiri ya matibabu ya maradhi ambayo vipimo vya kitabibu vimegundua kuwa ni matende (elephantiasis), ili kufanikisha safari yake kwenda India kwa matibabu.

Kantimbo anasumbuliwa na maradhi hayo kwa takribani miaka 12, kwahivi sasa yamemtoa kwenye mstari wa maisha yake ya kujitegemea na kumfanya awe tegemezi kwa watoto wake na mumewe ambao hata hivyo kipato chao si cha uhakika.

Kabla ya hapo alikuwa ni mama 'mchakarikaji' kweli, aliendesha maisha yake kwa biashara kadhaa ikiwemo biashara ya duka, grosari na saluni ya ususi wa nywele ambapo yeye mwenywe ni msusi mzuri wa nywele na kwa ucheshi wake na kujiamini pia alikuwa akifanya kazi za ushereheshaji (MC) kwenye sherehe kadhaa akifahamika kama MC Kimbaumbau.

Ila kwa sasa, tofauti na hapo awali alipoitwa MC na mama mchakariji, Kantimbo hawezi kufanya lolote amebakia ni mama wa kukaa mahali pamoja tu kuanzia asubuhi hadi jioni.

Kwa uchungu anasimulia namna alivyoanza kuugua…"Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa kwenye biashara zangu pale Ubungo, kuna kitu kilinichoma hapa (anaonyesh pajani) maumivu yake yalikuwa mithiri ya sindano, hata hivyo hayakudumu sana wala hapakuwa na alama yoyote.

"Baada ya dakika chache nikajihisi homa kali. nikaanza kutetemeka mwili mzima, nikaamua kwenda hospitali ya Neema, hospili ya karibu na mahali nilipokuwa nikiishi pale Ubungo. Daktari akanipima, akagundua nilikuwa na malaria.

"Wakati huo mguu haukuonyesha dalili zozote za maumivu wala jeraha. Malaria ilkuwa kali, nikalazwa kwa muda wa wiki mbili pale hospitali. Nikaruhusiwa, nikarudi nyumbani na hapo ndipo nilipoanza kuona mguu unavimba. Kaadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mguu nau unavimba"


Kuanzia mwaka 2010 mguu umezidi kuongezeka  kuvimba na maumivu makali yaliyotokana na kidonda kikubwa kilichosababishwa na kuondolewa kwa sehemu ya nyama ya mguu wake wa kuume iliyokuwa imeoza. Anasema:

"Baadhi ya madaktari wa Muhimbili walinishauri nikubali kukatwa mguu. Wanasema ya nyama imeoza na mfupa wa mguu umeharibika. Mimi sikukukubaliana na ushauri wao kwa sababu baada ya kupigwa X-ray 2007 iligunduliwa tatizo kubwa lilikuwa matatizo kwenye mishipa ya kupitisha maji kutokana na nyama kuharibika. Sio mfupa.

"Nilikataa kwa imani kuwa nitapona tu. Nikijiangalia nina uwezo wa kusimama na kutembea isipokuwa tu kinachonipa taabu kwa sasa ni nyama za mguu zimekua sana kiasi kwamba nikitembea zinagusa mguu wa kushoto" alisema.

Kwa mawasiliano namna ya kumsaidia piga simu namba 0716 850350, 0784 861031.