Tuesday, November 13, 2012

Magazeti ya leo Jumanne 13rd November 2012

Matokeo Ya Nec Yateka Dodoma

WAKATI matokeo ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), yakiwa yamevuja baadhi ya wapambe wa wagombea walioshinda wameanza kusherehekea, huku wengine wakitambiana.

Hata hivyo, matokeo hayo yamekuwa machungu kwa baadhi ya vigogo walioanguka wakiwamo mawaziri, wabunge na watu maarufu.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuunda sekretarieti mpya baada ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar utakaofanyika leo.

Kwa upande wa Zanzibar, matokeo hayo yanaonyesha kuwa walioshinda ni pamoja na Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.

Julius Magodi na Habel Chidawali,Dodoma
Endelea....www.kwanzajamii.com/?p=4241

Misaada Mingine Ya Marekani Ni fedheha

Wiki iliyopita Rais Jakaya Kikwete alizungumza neno zuri. Sina hakika kama viongozi wetu waliweza kulisikia na kulitafakari kutoka kwenye hotuba ya kiongozi huyo wakati akizindua Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, mkoani Arusha.

Alisema ujenzi wa chuo hicho ulikuwa ukwame baada ya wafadhili, wakiwamo Benki ya Dunia kukataa kutoa fedha. Kwa kutambua umuhimu wa chuo hicho kwa Tanzania na Afrika, Rais Kikwete alisema ilimlazimu kutumia mfumo uliotumika kwenye ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Mfumo huo ni wa kutumia fedha za ndani kutoka kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Sh bilioni 90 zimetolewa na Mifuho hiyo kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa Chuo cha Nelson Mandela. Tunaweza kutofautiana na Rais Kikwete kwa mengi, lakini kwa hili anastahili pongezi.

Tunapaswa kumpongeza walau kwa hilo kwa sababu Tanzania si nchi masikini kiasi cha kushindwa kujiletea maendeleo. Tanzania nikama familia iliyo na kila aina ya chakula ndani ya nyumba, lakini ikawa haiwezi kupika na kupakua, badala yake ikaenda kuhemea kwa majirani. Hiyo si aibu na fedheha tu, bali ni ujinga wa wenye nyumba hiyo.

Hatua hiyo ndiyo iliyonifanya nishawishike kuitazama picha ya maofisa wa Jeshi letu-Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Baada ya kuitazama, nikaingia kwenye mtandao na kukutana na maneno haya, “U.S. Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt (right), present's ambulance keys to the Chief of Medical Services of the Tanzania Peoples Defense Force (TPDF), Major General AS Mwabulanga, (left), during a donation ceremony held yesterday at the TPDF Headquarters in Dar es Salaam.”

Baada ya kusoma maneno hayo nikajikuta nikikosa amani kabisa rohoni. Nikaanza kujiuliza ni kwa namna gani Wamarekani au mataifa mengine ya Ulaya yanatutazama kwa kuikubali misaada ya ajabu ajabu namna hii. Thamani ya gari hilo la wagonjwa haikutajwa, lakini ni wazi kwamba si kitu kilichostahili kutolewa na “Wananchi wa Marekani” kwa chombo chetu nyeti na cha kujivunia kama JWTZ.

Umasikini ni mbaya. Lakini umasikini wa kukosa maarifa na staha ni mbaya zaidi. Naomba ndugu zangu wa JWTZ waniwie radhi kwa maneno haya. Sina nia mbaya. Ninachofanya hapa ni kujaribu kuondoa aibu hii kwa Jeshi letu mahiri pamoja na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Sijawahi kuona picha za maofisa wa Marekani wakitukabidhi misaada ya ndege vita, vifaru na mitambo mingine yenye thamani kubwa. Msaada wa gari la wagonjwa, hata kama thamani yake ni Sh milioni 300 ni aibu kubwa kwa Jeshi na kwa nchi. Tena mbaya zaidi, gari hilo linapokuwa moja tu!

Ndugu zangu, Tanzania haijawa masikini kiasi cha kubembeleza msaada wa gari la wagonjwa kutoka kwa Taifa kama Marekani. Hivi kweli Rais mstaafu George Bush aliyeishi hapa nchini kwa siku zaidi ya nne na akajionea utajiri usio kifani, atatuweka kwenye kundi gani akisikia kuwa Jeshi la Tanzania limepewa msaada wa gari la wagonjwa?

Utajiri wa Ngorongoro, utajiri wa Serengeti, utajiri wa Tanzanite, utajiri wa almasi, utajiri wa dhahabu, utajiri wa bahari yenye urefu wa kilometa karibu 1,000, utajiri wa maziwa -Tanganyika, Victoria, Nyasa, Rukwa-utajiri wa mito mamia kwa mamia, utajiri wa bandari zenye kupokea na kusafirisha mamilioni ya tani kila mwaka-utajiri wa hifadhi za Taifa zaidi ya 14; nchi yenye pori la akiba (Selous) kubwa kuliko yote duniani, nchi yenye Mlima mrefu uliosimama pekee duniani (Kilimanjaro), nchi yenye mabonde mazuri yanayofaa kwa kilimo cha kila aina, hifadhi za miti zisizopatikana sehemu nyingi za Afrika-utajiri wote huu bado Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linawatuma majenerali kupokea msaada wa gari la wagonjwa? Hivi kweli huu ndiyo msaada wa kuwafanya maofisa wetu wafunge ofisi ili waende kushiriki mapokezi? Kama hii si laana kwa Taifa lililojaliwa utajiri, ni nini? Je, huku si kumkufuru Mungu?

Ndugu zangu, wengi wetu, nikiwamo mimi, ni ombaomba. Lakini kuomba kunahitaji staha. Usipokuwa makini kwa kile unachokiomba, na yule anayeombwa akajiridhisha kuwa kweli unachoomba unastahili kusaidiwa, utadharauliwa.

Lakini wakati mwingine si lazima uombe. Mtu anaweza kujifanya anakuletea zawadi au msaada. Kwa mwelevu si lazima kila msaada uukubali. Mathalani, si lazima upokee samaki au mnyama usiomla kwa sababu tu yule aliyeamua kukusaidia kakuletea msaada huo.

Tatizo la JWTZ kwa msaada huu kutoka Marekani ni kwamba inaelekea sisi ndiyo tuliouomba! Kama kweli tuliketi na kuona jambo la maana kabisa kwa Jeshi letu ni kuomba msaada wa aina hii, basi tunapaswa kujitafakari upya.

Kwa nchi kama Marekani, msaada wa kuwaomba ni wa kuimarisha kiwanda kama cha Nyumbu ili siku moja tutengeneze, si magari ya suluba pekee, bali hata magari ya wagonjwa. Leo majenerali wetu wakikutana na Balozi wa Marekani, wakamwomba msaada mkubwa “wenye akili”, Balozi na Serikali ya Marekani watatuona tuna akili.

 Lakini kwa kuomba gari la wagonjwa, inadhihirisha kabisa kuwa shida yetu si wagonjwa hao tuliowambea gari, bali tatizo letu ni la kupata msaada wa kiakili ili kuzifanya bongo zetu ziwaze na kuomba misaada ya maana. Kwa maneno mengine ni kwamba tunahitaji ambulance za kuutoa ubongo wetu kwenye utegemezi hadi kufika kwenye kujitegemea.

Kuna hadithi ya kweli inayomhusu mzee mmoja aliyekuwa akiishi Msasani; pamoja na kiongozi mmoja wa kitaifa. Inaelezwa kuwa baada yam zee huyo kumsaidia kiongozi huyo eneo la shamba kwa ajili ya nyumba, kiongozi alifurahi na kumwambia, “Mzee nakushukuru sana, sasa unataka nikusaidie nini zaidi ya fedha nilizokupa?” Yule mzee hakusumbua kichwa, akamjibu; “Mheshimiwa nisaidie bia”. Akionyesha kusikitishwa na aina ya msaada alioombwa, Mheshimiwa akaagiza yule mzee epewe kreti tano za bia, na nyingine kwa idadi hiyo, za soda!

Hii ina maana gani? Hii ina maana kwamba wakati mwingine tunapokuwa tunaomba misaada, lazima tupime ni nani tunayemwomba na uwezo wake wa kusaidia unaweza kuwa katika ngazi gani? Inawezekana majenerali wetu walipoambiwa kinachowasumbua kwenye tasnia ya afya jeshini, kitu cha maana walichoomba ni gari la wagonjwa badala ya mitambo ya kuwawezesha wao wenyewe kuanza kutengeneza magari! Nasema hivyo kwa sababu haiwezekani Balozi wa Marekani aombwe mashine za kiwanda cha Nyumbu, halafu yeye akaamua kutuletea gari la wagonjwa! Haiwezekani. Na kama kweli majenerali wetu huo ndo msaada waliouomba kutoka kwa Balozi wa Marekani, kwanini tusiseme kuwa wametuaibisha?

Mwisho, niseme kuwa sisi kama nchi, ili tupate heshima, tunapaswa kufikiria zaidi dhana ya KUJITEGEMEA. Misaada hii ya gari la wagonjwa, kusaidiwa kuchimbiwa vyoo shuleni, kuomba misaada ya madawati kwa wanafunzi wetu, kuomba msaada wa kuchimbiwa visima; kujengewa mageti kama pale Ngorongoro, ni aibu. Aina hii ya ombaomba inatufanya tuwe vilemba.

Kwa mara nyingine nasema msaada huu ambao Marekani imelipatia Jeshi letu tukufu, ni aibu na fedheha kwa Watanzania. Tuamue mgodi mmoja ugharimie vitu kama hivi! TanzaniteOne wanadaiwa kodi inayozidi Sh bilioni 3. Je, fedha hizo tukizipata haziwezi kununua magari ya wagonjwa “ya kienyeji” kama hili tulilopewa na “Watu wa Marekani?” Tutafakari.

Imetoka kwa Mjengwablog kwa kweli hii imenisikitisha sana Tujitambue Watanzania safi sana Mwandishi. 0759 488 955 manyerere@hotmail.com

Monday, November 12, 2012

Mkutano Mkuu Wa Ccm, Dodoma Leo

                         Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwasili ukumbi wa Kizota akifuatana. Kulia ni Karume, Dk. Bilal na kushoto ni Mukama na Msekwa.                              
                                                                 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiongoza Mkutano Mkuu wa CCM leo Novemba 12. Kushoto ni Karume na kulia ni Msekwa
                    Waasisi wa Tanu na baadaye CCM, Mwadawa Ali (85) na Mohammed Makber (72)
                        wakisoma gazeti ya UHURU la Chama Cha Mapinduzi, kabla ya mkutano kuanza

              Khadija Kopa (kushoto) akiimba wakati TOT ilipotumbuiza kwenye mkutano huo

Picha na Bashir Nkoromo

Chadema Yasambaza Pikipiki Nchi Nzima

 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza mkakati wa Uchaguzi Mkuu 2015 kikiahidi kumwaga pikipiki katika tarafa zote nchini kwa ajili ya kuwafikia wananchi kuelekea uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema hayo jana katika kikao cha viongozi wa chama hicho na wadau wake kilichofanyika hapa.

Mbowe alisema pikipiki hizo zitakuwa na vipaza sauti maalumu zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

“Tumeanza mkakati wa kuhakikisha tunawafikia wananchi kila mahali. Tunataka kusikiliza matatizo yao, na hata pale ambako kuna shida ya usafiri, kwa pikipiki tutafika,” alisema.

Tayari chama hicho kimezindua kampeni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), ambayo lengo lake ni kuwaandaa wananchi kwa uchaguzi ujao.

Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo unatokana na fedha za ruzuku ambazo zinatolewa na Serikali kwa chama hicho  pia marafiki na wanachama wake walioko nje ya nchi.

ngozi wa chama hicho katika ngazi zote kufanya kazi kwa kujituma ili kuhakikisha kinashika dola mwaka 2015.

“Tanzania inahitaji mabadiliko na sisi tukiwa viongozi tunapaswa kujipanga kwanza, kuhakikisha tunaongeza wanachama pia kuzitatua kero za wananchi,” alisema Mbowe.

Katika mkutano huo, Mbowe aliwapongeza viongozi wa Chadema, Wilaya ya Hanang’ kwa kazi kubwa waliyoifanya kiasi cha kupata na madiwani 17 katika halmashauri hiyo.

Awali, Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Manyara, Rose Kamili alisema chama hicho kimejipanga kutwaa Jimbo la Hanang’ katika uchaguzi ujao na Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’.

“Katika miaka hii mitano Chadema, Hanang’ tumekuwa na mafanikio makubwa na hili linatokana na mshikamano mkubwa wa viongozi katika ngazi mbalimbali,” alisema.

Na:  Mussa Juma Hanang’

BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AIPA CHANGAMOTO BODI YA UTALII TANZANIA (TTB)

 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe, wakati alipowasili katika hafla ya chakula cha jioni katika yake, Balozi na maaofisa wa Bodi ya Utalii na Taasisi zake pamoja na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ili kuagana na kutathimini mapungufu na mafanikio ya ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya dunia ya utalii World Treavel Market (WTM) yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Uingereza, ambapo zaidi ya makampuni 55 yanayouza na kutangaza utalii wa Tanzania yalishiriki katika maonyesho hayo, maonyesho hayo hufanyika kila mwaka eneo la Excel jijini London.

Balozi Khamis Kagasheki aliitaka Bodi ya Utalii Tanzania kuongeza juhudi zaidi ili kuleta mafanikio zaidi katika maonyesho hayo na menine na kuongeza idadi ya watalii kufiki milioni moja kwa mwaka, Tanzania ikijipanga vizuri na kutangza vivutio vyake zaidi duniani inaweza kupata mafanikio zaidi katika utalii na kuongeza zaidimapato yake ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii.
                                   Maofisa mbalimbali wakiingia katika hafla hiyo ya chakula cha jioni.
 Baadhi ya maofisa waliohudhuria katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Dkt. Wegoro kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha , Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Balozi mdogo wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Kilumanga na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania ubalozini Bw. Kashangwa.
                       Maofisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wakiwa katika hafla hiyo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki kulia akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maliasili, Utalii na Ardhi wakati alipokuwa kichangia mazungumzo katika hafla ya chakula cha jioni baada ya kumalizika kwa maonyesho ya WTM nchini Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita, katikati ni Balozi wa Tanzania nchini humo Balozi Peter Kallaghe.
 Ofisa Habari wa TANAPA Bw. Shelutete kulia akiwa na Maofisa wa Kituo cha biashari cha Tanzania nchini Uingereza katikati ni Dilunga na kushoto ni Mohamed
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe akizungumza katika hafla hiyo kulia ni Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili na Utalii.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika hafla hiyo ambapo aliwashukuru maofisa kutoka Bodi ya Utalii na Taasisi zake pamoja na makampuni yaliyoshiriki katika maonyesho hayo kwa maandalizi mazuri katika ushiriki huo, lakini pia akaagiza kuangalia changamoto na kuzifanyia kazi ili kuboresha zaidi ushiriki wa Tanzania katika maonyesho yajayo na mengine yanayoweza kufanyika katika nchi zingine, kulia katika picha ni Balozi Peter Kallaghe na kulia ni Mama Balozi

PICHA NA WWW.FULLSHANGWEBLOG.COM

Matokeo Wajumbe 10 Kapu La Kifo

Matokeo ya chaguzi za nafasi 10 za wajumbe wa NEC Tanzania Bara wa Chama cha Mapinduzi zinazoendela Dodoma yametoka ni kama ifuatavyo:

1. Stephen Wassira - 2,135
2. January Makamba – 2,093
3. Mwigulu Nchemba – 1,967
4. Martine Shigela – 1,824
5. William Lukuvi – 1,805
6. Bernard Membe – 1,455
7. Mathayo David Mathayo – 1,414
8. Jackson Msome - 1,207
9. Wilson Mukama - 1,174
10. Fenela Mukangara - 984

Shukurani za taarifa hii: Makongoro Nyerere (via blogu yake ya Muhunda)

Wakati huo huo, blogu ya CCM inaripoti kuwa, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kwamba uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara na Makamu Mwenyekiti Zanzibar utafanyika kesho tarehe 13 Novemba 2012.

Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,uliofanyika leo asubuhi Kizota mjini Dodoma, Nape alizungumzia kufanikiwa kwa siku ya jana, baada kila kitu kwenda vizuri kwa mujibu wa ratiba.
Pia alizungumzia ratiba ya leo, ambapo kutakuwa na Taarifa mbali mbali za kazi za chama, Taarifa za utekelezaji za ilani ya uchaguzi (Bara na Zanzibar) itasomwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar itasomwa na na Makamu wa Pili Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd.

Taarifa kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pia zitasomwa leo.
Akizungumzia mabadiliko ya Katiba, alisema kumekuwa na mafanikio sana baada ya mapendekezo yote kupitwa bila kupingwa, moja ya mapendekezo ni kuwepo kwa Baraza la Ushauri la Wazee, pamoja kubariki mapendekezo wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa watoke wilayani. Baada ya uchaguzi kutakuwa na mrejesho wa mijadala na kutoa maazimio ya Mkutano Mkuu.