Friday, December 14, 2012

JK. Akabidhi Nyumba Mpya 35 Za Waathirika Wa Mabomu Ya Ngongo La Mboto

 Bila kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiakata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012
 Bila kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa  kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmoja wa walionufaika na hatua ya serikali ya kujenga  nyumba mpya 35 kwa ajili ya  waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala jana Desemba 13, 2012. Mama huyu ambaye alipoteza mume, amejengewa nyumba ya vyumba vitano pamoja na fremu ya duka
 Baadhi ya  nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala kama zinavyoonekana  leo Desemba 13, 2012 baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete

 Baadhi ya  nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala kama zinavyoonekqana  Desemba 13, 2012 baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete

MATOKEO YA YANGA VS OLJORO UHAI CUP DEC 14 2012


Magazeti ya leo Ijumaa ya 14th December 2012

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Thursday, December 13, 2012

Chukua Hii ......Wamependeza









TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA MADOLA

TANZANIA itakuwa mwenyeji wa mkutano wa   Vijana wa Kanda ya Afrika wa Jumuiya ya Madola kuanzia Januari 28 hadi Februari Mosi mwaka huu.

 Hayo yamesemwa (leo)  na  Mkurugenzi  wa Kanda ya Afrika ya Mpango wa Vijana wa  Jumuia ya Madola, James Odit  wakati akizungumza na  Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kuhusu  maandalizi ya mkutano  huo.

 Mkurugenzi huyo alisema mkutano utahusisha nchi 22 ambazo ni   wanachama na jumla ya washiriki 60 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo kutoka katika  wizara zinazohusiana na masuala ya vijana, viogozi wa vijana, viongozi wawakilishi wa Baraza la Vijana, wawakilishi wa kimataifa, viongozi wa kikanda wa maendeleo ya vijana na Jumuiya ya Madola.

Miongoni mwa mambo mengine waliyojadiliana ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Vijana na jinsi ya kuunda Katiba ya  Baraza la Vijana la Jumuiya ya Madola.

“Mkutano huu utajadili namna ya kuunda Barazala Vijana la Jumuiya ya Madola(CYC) na program za maendeleo ya vijana na jinsi ya kuwawezesha katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo,” alisema Odit.

 Kwa Upande wake Waziri wa wizara hiyo, Dk. Mukangara alisema  anaishukuru jumuiya hiyo kwa kuichagua Tanzania kuwa mwejeji wa mkutano huo. Huku akisema suala la uundaji wa Baraza la Taifa la Vijana hivi sasa liko katika hatua ya ngazi za juu.

Waziri huyo alizitaja changamoto za kuendeleza mipago mbalimbali ya maendedeleo ya vijana kuwa ni kukosefu wa fedha za kutosha   mfano vile kuwawezesha vijana katika shughuli za kiuchumi na kimaendeleo, kuwajengea uwezo,  kuwapatia ajira, ujuzi na elimu.

 Akifafanua kuhusu suala hilo  Mkurugenzi huyo alisema atalifikisha  suala hilo  kwa wenzake ili waweze kungalia namna ya kuweza kushirikiana.

Waziri Mukangara alishauri  jumuiya hiyo kuangalia namna ya kuweza kushirikiana katika maeneo mengine  ambayo ni sekta ya Michezo, Utamaduni na Habari.

Magazeti ya leo Alhamisi ya 13th December 2012