Thursday, April 11, 2013

WAKATI RAGE WA SIMBA AKIJIANDAA KUIPELEKA MAHAKAMANI AZAM FC, CLUB HIYO IMEMJIBU NA KUMWAMBIA KUWA ITAMPATIA HADI NAULI YA KUMFIKISHA MAHAKAMANI

 KLABU ya Azam FC imetoa 'Go Ahead' kwa Simba kwenda mahakamani kwa madai ya fidia ya kuchafuliwa.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage alikaririwa mjini Dodoma alipokwenda kuhudhuria vikao vya bunge kuwa klabu yake inaandaa barua ya kuidai fidia ya Sh1.5 Bilioni.

Ni kutokana na klabu ya Azam kuwafungia wachezaji wanne kwa tuhuma za kupokea rushwa ambayo ni  Sh7 milioni ili wapange matokeo wakati wa mechi ya Simba na Azam FC Oktoba 26, mwaka jana ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo.

Magazeti ya leo Alhamis ya 11th April 2013




"KILA MTU ANAHAKI YA KUCHINJA NA KULA CHOCHOTE HATA CHURA"...HII NI KAULI MPYA YA RAIS MWINYI

RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amerejea kauli yake kuhusu mgogoro wa udini akisema kila mtu ana haki ya kuchinja kutokana na imani yake ilimradi tu asivunje sheria za nchi.

Mwinyi alisema anashangaa kuona watu wakigombania kitu kidogo kama kuchinja ilihali Tanzania ina utamaduni wa amani siku zote na kwamba kila mtu ana imani yake ya dini anayoiamini.
Kiongozi huyo mstaafu alitoa msimamo huo jana jijini Dar es Salaam katika kongamano juu ya utamaduni wa Kiislamu Afrika Mashariki ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji.

“Imani ni nafsi ya mtu na haitakiwi kumlazimisha kula nyama iliyochinjwa na mwenzie. Na kama unaona aliyochinja mwenzio ni kibudu basi usile chinja yako, kula hata ukitaka kula chura, mjusi, konokono, kula utakacho ruksa ilimradi tu usiingie katika jinai,” alisema.

Wednesday, April 10, 2013

Magazeti ya leo Jumatano ya 10th april 2013




HIVI NDIVYO UHURU KENYATA ALIVYOAPISHWA NCHINI KENYA

                                            Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akiapishwa.
                                        Rais Uhuru Kenyatta na 'First lady', Margaret Kenyatta.

MVUA YALETA MAAFA WILAYANI ARUSHA WANANCHI KADHAA HAWANA MAHALI PA KUISHI

 Hali ya mvua inayonyesha kwenye mkoa wa Arusha imewaacha wakazi wa vijiji vya Alkokola na venginevyo kadhaa kwenye kata hiyo wilaya ya Arusha wakiwa hawana makazi na mahala pakukaa baada ya mvua kunyesha usiku wa kuamkia Jumatatu.
Pichani ni maji yakiwa yanashuka kwenye maeneo ya Ngaramtoni ya Chini na Burka huku wakazi wa maeneo hayo wakiyakimbia maeneo yao kama walivyokutwa na kamera yetu.

Thatcher afariki dunia

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Thatcher (87), amefariki dunia  jijini London.

Thatcher, ambaye ni mwanamke pekee kushika nafasi hiyo Uingereza, alifariki dunia katika Hoteli ya Ritz alipokuwa akiugulia. Habari zilizopatikana zimeeleza kuwa Thatcher alifariki dunia kutokana na kuugua ghafla ugonjwa wa kiharusi.CHANZO MWANANCHI

"MIMI NDIYE NILIYEWAPELEKEA POLISI ILE VIDEO YA LWAKATARE"...MWIGULU NCHEMBA

HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba, amekiri kuhusika na video inayomwonesha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.

Nchemba amekuwa akitajwa na viongozi wa CHADEMA kuwa anahusika kutengeneza video hiyo, kwa kuwa aliwahi kutamba wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni kuwa anayo video inayowaonesha viongozi wa chama hicho wakipanga mauaji.

Hata hivyo, tangu Nchemba atoe kauli hiyo Januari mwaka huu, Jeshi la Polisi lilikaa kimya hadi Machi 12 lilipomkamata na kumhoji Lwakatare, siku moja baada ya video hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa You tube na mtu anayejiita ‘Bukoba Boy’.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Nchemba alikiri kuwa ndiye aliyeipeleka video ya Lwakatare polisi na kwamba alifanya hivyo baada ya kuripoti kuandikiwa ujumbe wa simu wa kutishiwa maisha na baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

"NIMEAMUA KUMSAMEHE LULU MICHAEL....YALIYOTOKEA NAMWACHIA MUNGU"...MAMA KANUMBA

Mama wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amesema amemsamehe msanii Elizabeth Michael 'Lulu' kutoka moyoni .Ingawa bado kesi iko mahakamani, kwa upande wake yeye hana tatizo naye na yaliyotokea anamuachia mungu

Akizungumza katika makaburi ya Kinondoni mara baada ya kumuombea marehemu na kuweka mashada ya maua alisema kuwa yeye ni mkristo safi hivyo hawezi kuendelea kukaa na kinyongo ingawa kila anapomuona msanii huyo humkumbuka mwanaye

Alisema kuwa Kanumba alikuwa zaidi ya mtoto kwake, mume, rafiki, kaka  alimfanya kuwa mtu wa karibu sana kwake na alimfanya kuwa karibu kwake na kumzoea kwa kila kitu hali ambayo imemfanya kuwa mpweke mpaka leo

Tuesday, April 9, 2013

PARTY YA KUMKARIBISHA KAJALA URAIANI





MWAKYEMBE ASHANGAZWA NA ONGEZEKO KUBWA LA NAULI.... ..AMETOA AMRI NAULI ZA TRENI ZISIPANDE

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewatuliza Watanzania kuhusu kupanda kwa nauli akisema ameyapokea malalamiko  yao na atayafanyia kazi.

 Kwa kuanzia ameagiza nauli za treni jijini Dar es Salaam zisipande bali ziendelee kutozwa za zamani  mpaka taarifa zaidi itakapotolewa.

Mwakyembe alitoa kauli hiyo alipozungumza kwenye Bonanza la Vyombo vya Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Alisema ni kweli Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra|) ilitangaza nauli mpya, lakini kwa kilio cha Watanzania ataangalia sababu za kupandisha huku akishirikiana na wasafirishaji kujua ukweli.

WAKATI UHURU AKIAPISHWA KENYA LEO, RAILA NA WENZAKE WANADAIWA KUJA HUKU, TAZAMA PIA HII WEBSITE ILIYOFUNGULIWA KWA AJILI YA UHURU

 Wako kwenye mbuga za wanyama Afrika Kusini wanakula bata ni Raila Odinga na wenzake wawili akiwemo Kalonzo Musyoka.

Magazeti ya leo Jumanne ya 9th April 2013




SERIKALI YAKUBALI KURUDISHA ADHABU YA VIBOKO SHULENI

Serikali imesema itarudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi shuleni ili kujenga nidhamu na kujituma.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akizindua tovuti ya www.shledirect.co.tz inayowezesha wanafunzi kujisomea kwa njia ya mtandao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kumewafanya wanafunzi wengi kukosa nidhamu na wakati mwingine kujifanyia mambo kienyeji.

“Wasipotandikwa mambo hayaendi, nilipokuwa mwalimu mkuu nilikuwa nawatandika kweli ndiyo maana shule yangu ilikuwa ikiongoza Mkoa wa Mbeya hivihivi hawaendi...” alisema huku akishangiliwa na wageni waalikwa.

Alisema watoto wa siku hizi wamekuwa wakitumia vibaya teknolojia ambayo ingeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao... “Tovuti kama hiyo ingewasaidia kwa masomo, lakini wao wanakimbilia kwenye facebook na mambo mengine yasiyofaa.”

RAIS KIKWETE AWASILI NAIROBI KENYA KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA RAIS UHURU KENYATTA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani.
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani .