Wednesday, May 1, 2013

"NITAGOMBEA URAIS MWAKA 2015 ENDAPO WANANCHI WENGI WATANIOMBA NIFANYE HIVYO"....BENARD MEMBE

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amesema atakuwa tayari kuwania urais mwaka 2015, iwapo wananchi wataona anafaa na kumtaka afanye hivyo.

Alisema hayo juzi wakati akijibu maswali ya mwandishi wa habari hii mjini Iringa, baada ya kumalizika kwa kongamano la vyuo vya elimu ya juu mkoani hapa, lililofanyika katika ukumbi wa St. Dominic.

Membe aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo, alisema ingawa muda wa kufanya uamuzi kuhusu mwaka 2015 bado na chama hakijatoa utaratibu, lakini atasubiri ushauri wa Watanzania.

"Naomba kurudia, mimi nilishapata kuueleza umma kuwa muda bado haujafika wa kutangaza kugombea urais ...ila nasema hivi natarajia sana ushauri wa Watanzania.

JK akutana na Morgan Tsvangirai ikulu, Dar

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri Mkuu wa nchi ya Zimbabwe Bwana Morgan Tsvangirai ikulu jijini Dar es Salaam. Chanzo: Freddy Maro

Bilionea wa Man city kuanzisha timu mpya MLS

                             Sheikh Mansour (katikati) anataka kuwekeza MLS dola Milioni 100

MMILIKI wa Manchester City, Sheikh Mansour wa Abu Dhabi yupo karibuni kuwekeza kiasi cha dola za Kimarekani, Milioni 100 kuanzisha timu mpya itakayoshiriki katika Ligi Kuu ya Marekani, ijulikanayo kama Major League Soccer ambayo itakuwa na maskani New York.

Bilionea huyo wa waliokuwa mabingwa wa Ligi Kuu England, amekuwa katika mazungumzo mazito na ya siri na MLS kwa miezi kadhaa juu ya kuingiza timu mpya ya nguvu USA.

Sheikh ana matumaini yeye na Maofisa wa MLS, watakuwa kwenye nafasi ya kutangaza mpango huo wakati kikosi cha Roberto Mancini kitakapokwenda Marekani kucheza na Chelsea Jijini New York katika mchezo maalum wa hisani mwishoni mwa mwezi ujao.

DEREVA WA “BODA BODA” AKAMATWA NA SHORTGUN, RISASI SITA

GEDSC DIGITAL CAMERAPichani juu ni bunduki aina ya Shortgun Mossberg ikiwa na risasi sita ambayo ilikutwa kwenye begi la dereva huyo wa Boda boda aliyekamatwa na polisi tarehe 28.04.2013 (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

Jeshi la Polisi Mkoani hapa limemkamata mtu mmoja aitwaye Ally Rashid Salimu (23) Mwendesha pikipiki za abiria maarufu kwa jina la “Boda Boda” mkazi wa kata ya Sombetini jijini hapa akiwa na bunduki aina ya shortgun Mossberg yenye namba T292166 ikiwa na risasi sita.Akizungumza na

waandishi wa habari ofisini kwake leo saa 5:30 asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas alisema kwamba, tukio hilo lilitokea juzi tarehe 28.04.2013 muda wa saa 3:00 asubuhi katika maeneo ya Shamsi yaliyopo jijini hapa.

Magazeti ya leo jumatano ya 1st May 2013





HALI ILIVYO LEO ASUBUHI JIJINI ARUSHA TUKISHEREKEA SIKU YA MEI MOSI

BAADA YA MIEZI 9 YA BILA KUONEKANA HADHARANI, HII NDIO PICHA MPYA ALIYOPIGWA MZEE MANDELA HIVI KARIBUNI

Baada ya kipindi kirefu cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela kutoonekana hadharani hatimae picha yake ya kwanza baada ya miezi tisa imeonekana.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini aliongozana na watu wengine kwenda kumtembelea Mzee Mandela ambapo baada ya kumuona, Zuma amesema afya ya Mzee iko vizuri sasa hivi japokua amekonda kidogo.

Tuesday, April 30, 2013

LULU KURUDIA KAZI YAKE BAADA YA KUSHINDA KESI YAKE!

 HATIMAYE staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameingia mzigoni na kufyatua filamu yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu, Amani limeinyaka.
 Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu alitupia picha akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada ya kusimama kuigiza kwa muda mrefu.
Baadhi ya picha hizo zinamuonesha Lulu akiwa na staa mwingine wa filamu Bongo, Hashimu Kambi mbele ya kamera kwa ajili ya kushuti filamu hiyo ambayo jina lake halijapatikana.

TASWIRA ZA SHOW YA DIAMOND JIJINI LONDON



Pichani juu, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akifanya makamuzi ndani ya jiji la London wikiendi iliyopita. Msanii huyo bado anaendelea na ziara yake nchini England.

LEMA ASEMA HAYA BAADA YA KUACHIWA MAHAKAMANI KWA DHAMANA

 Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless lema ameachiwa huru kwa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi baada ya kusota rumande kwenye kituo kikuu cha polisi kwa siku tatu  kwa kosa la kuchochea vurugu chuoni uhasibu huku baada ya kutoka akiwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kumzomea mkuu wa mkoa.

Lema alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa Tatu na robo asubuhi akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kufikishwa mbele ya hakimu Devotha Msele  na ndipo mwendesha mashtaka Eliang’enyi Njiro alisimama kuanza kumsomewa mashtaka ya uchochezi na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani aliyoyafanya kwenye eneo la chuo cha uhasibu njiro jijini Arusha.

Baada ya kutoka mahakamani hapo alielekea kwenye ofisi za chama hicho na kuzungumza na waandishi wa habari huku akitoa malalamiko na kuwataka wanachama na wapenzi wa chadema kumzomea mkuu wa mkoa iwe kanisani,mskitini,au kwenye sherehe mbali mbali,

“Nawatakeni kumzomea huyo mkuu wa mkoa Magessa Mulongo na kuwa nia ya kumshtaki ipo pale pale ndugu zangu Makamanda wenzangu huyu jamaa awe msikitini kanisani kote tumzome hiyo itakuwa ndiyo salamu yetu kwake”alisema Lema

Katika hali nyingine jeshi la polisi liliimarisha ulinzi tangu nje ya mahakama hadi ndani ya mahakama hiyo kiasi utulivu katika mahakama hiyo ulionekana na shughuli kuendelea bila bughaa.

Hali kwenye mitaa mbali mbali ya viunga vya jiji la Arusha ilionekana kuendelea na mishughuliko ya kila siku kama kawaida kuliko ilivyokuwa ikionekana huko mwanzo kwenye kesi zilizokuwa zikimkabili mbunge huyo kwa wakazi wa jiji hili kuacha shughuli zao na kuelekea mahakamani kufuatilia kesi ya mbunge huyo.

Magazeti ya leo jumanne ya 30th April 2013




BAADA YA GODBLESS LEMA KUKAMATWA AKIHUSISHWA NA UCHOCHEZI WA FUJO WA WANAFUNZI WA UHASIBU ARUSHA BAADA YA MWENZAO KUUAWA KWA KUCHOMWA KISU HATIMAE GODBLESS LEMA AACHIWA HURU KWA DHAMANA YA MILIONI MOJA

 Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema,ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja katika mahakama kuu kanda ya Arusha.

TUNDU LISSU AHOJIWA NA RADIO TEHRAN KUHUSU SAKATA LA KUKAMATWA MBUNGE LEMA

Nchini Tanzania sakata la kukamatwa na kuwekwa mahabusu Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kwa madai ya uchochezi, limeibua sura mpya baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutajwa kuwa nyuma ya mkakati huo.

Kwa upande wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kimelaani hatua hiyo na kulilaumu jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kukandamiza upinzani.

Chama hicho kimekwenda mbali zaidi na kulituhumu jeshi la polisi Arusha kwamba, limekuwa likitumikia CCM badala ya kutumikia umma.

HUU NDO UNYAMA WALIOTENDEWA WANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

                      Marehemu  Henry  katika enzi za uhai wake....

Mwanafunzi  huyo  Alikuwa Masomoni Mida Ya Usiku Na Alipomaliza Aliondoka Na Kuelekea Maeneo Ya Esami. Kabla Hajafika Eneo La Malazi (Hostel) alipigiwa Simu na Mwenzake amsubiri Ili Waende Wote Hostel.
 
Wakati anamsubiri Rafiki Yake Kwenda Hostel, Kuna Bajaj Ilifika Eneo Hilo Na Watu Hao Wasiojulikana Wakataka Pesa Kutoka Kwa Mwanafunzi Huyo...Wakati  wakiendelea  kuzozana, rafiki  yake  naye  alifika.....
Picha  ya  marehemu  Henry Koga  baada  ya  kuchomwa  kisu  na  kufariki  hapo hapo  katika  chuo  cha  uhasibu  Arusha.....

Majibu Ya Wanafunzi Hao Hayakuwafurahisha Watu Hao Na Ndio Walipochomoa Kisu Na Kumchoma Mmoja wa Vijana Hao Tumboni Na Shingoni na Kupoteza Maisha Hapo Hapo....

Mauaji  hayo  yamesababisha  vurugu  kubwa  chuoni  hapo  zilizopelekea  kupigwa  mawe  mkuu wa  mkoa

"UREMBO SIYO KIPAJI NA SI KILA MWANAMKE MZURI ANAWEZA KUIGIZA"...JACKLINE WOLPER

Muigizaji Jacqueline “Jackie” Wolper amewashangaa wanaodhani kuwa urembo wa mwanamke ni mbadala wa kipaji hasa katika sanaa ya maigizo. Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.
 “Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper.
 Wolper aliendelea kulalama kuwa kila mtu akijona ana sura ya kuvutia na umbo zuri basi anajua anaweza kuigiza ndio maana matokeo yake wanafanya vitu sivyo na mwisho wake wanaacha fani kabisa.
 Alifafanuwa kuwa kuigiza ni zaidi ya urembo hivyo yeyote ambaye anafikiri anaweza kufanya kazi hii kwa uzuri wa sura na umbo ajaribu kama hakuchemka.

Source: Mwananchi