Thursday, May 9, 2013
MTOTO WA MIAKA 9 AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI HUKO TARIME
Polisi mkoani Tarime wameua mtoto wa miaka 9, Deo Yakob, katika kilichoripotiwa kuwa pilikapilika za kukamata majambazi wanaoiba na kuua watu mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Bado hakuna maelezo zaidi, kuhusu ni kitu kani kilichopelekea mtoto huyo kuuawa katika juhudi za polisi kukamata majambazi hayo. Pia haijafahamika kama polisi hao walifanikiwa kuwakamata majambazi...
Pichani ni wananchi wakiwa na mwili wa mtoto huyo ambaye alikua ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Mturu, mjini Tarime.

Mlipuko wa Kanisani Arusha: saba wapelekwa dar kwa matibabu zaidi
Wagonjwa saba ambao ni majeruhi wa mlipuko wa bomu kwenye kanisa la Joseph Mfanyakazi eneo la Olasiti jijini Arusha wamehamishiwa kwenye Hospitali za Muhimbili na LUgalo jijini Dar es Salaam.
Majeruhi hao wamesafirishwa mchana majira ya saa tisa kwa ndege ya shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwenda kuendelea na matibabu zaidi baada ya hali zao kuonekana bado zinahitaji vifaa vyenye uwezo wa hali ya juu.
Miongoni mwa walisafirishwa wapo watoto watatu wakike wawili na wakiume mmoja huu wakina mama walisafirishwa wakiwa wawili na kinababa wawili ambao hali zao bado mbaya licha ya matibabu walikuwa wakiyapata tokea juzi.
Wasamaria wema kutoka makampuni mbali mbali wameendelea kutoa misaada mbali mbali ya hali na mali ikiwemo madawa na vifaa tiba na mablanketi na mashuka,na Magodoro iliviisaidie hospitali za Mt.Meru na St,Elizabeth.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA DINI YENYE "VIRUSI" VYA UCHOCHEZI
Waziri wa MAmbo ya Ndani ya NChi, EMmanuel NChimbi, ameliagiza jeshi la polisi kuanzia IGP, RPC, OCD na OCS kuwachukulia hatua wale wote wanaoendesha mihadhara ya kidini yenye kuchochea vurugu na mifarakano katika jamii. ...
Nchimbi amesema kuwa kiongozi yeyote ambaye atabainika kutochukua hatua licha ya taarifa kuripotiwa kwake basi atakwenda na maji.. ...
Kauli hiyo ameitoa jijini dar es salaam jana wakati akiongea na wawakilishi wa viongozi wa dini na vyombo jeshi la polisi mkoa wa dar es salaam
Waziri Nchimbi amewatahadhalisha vijana wanaoshinda kwenye mitandao na wanaotumia simu kutuma ujumbe wenye lengo la kuhamasisha chuki za kidini. Amesema kuwa kuanzia sasa serikali itachukua hatua stahiki
Chanzo: taarifa ya habari ya TBC1

BRAKING NEWS: SHEIKH PONDA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA CHA NJE
Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam leo imemuhukumu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kifungo cha nje cha mwaka mmoja, huku washtakiwa wengine wote 49 wakiachiwa huru
Wednesday, May 8, 2013
MAHAKAMA YAFUTA KESI YA UGAIDI ILIYOKUWA INAMKABILI LWAKATARE
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.
Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.
Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari, Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

HATIMA YA ZOMBE NA LWAKATARE NI LEO
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare.
MAHAKAMA ya Rufaa nchini leo inatarajia kutoa uamuzi rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi, Abdallah Zombe, wa kuifuta au kutoifuta rufaa iliyokatwa na DPP baada ya jicho la mahakama kuona hati ya kukatia rufaa ina dosari.
Sambamba na hilo, pia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajia kutoa uamuzi wa kuifuta au kutoifuta kesi ya tuhuma za ugaidi za kutaka kumteka mhariri wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaki, inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph

RAIS KIKWETE AKIWA ARUSHA KUHANI MISIBA YA WALIOFARIKI KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISANI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakishiriki dua ya pamoja, wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7,
MSISITIZO WA KADINALI PENGO ALIOUTOA TENA JANA
Kadinali Pengo
“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:
“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,” alisema Pengo.
Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.
“Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani,” alisema Pengo.

BALOZI WA VATICAN ALIYENUSURIKA KATIKA SHAMBULIZI LA BOMU ARUHUSIWA KUONDOKA ARUSHA
Mwakilishi wa Papa akiwa na Askofu Lebulu akitoka kwenye VIP ya Arusha Airport kuelekea kwenye ndege ya Precision .
Ilikuwa ni dakika za majonzi na masikitiko kwa kundi lote lililokuwa
limemsindikiza uwanja wa ndege Balozi wa Papa ambaye ameondoka leo mjini
Arusha kuelekea Dar, baada ya kunusurika katika shambulio la bomu
lililorushwa wakati akiwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kanisa la Mt.
Joseph Mfanyakazi huko Olasiti Arusha.

Hapa akisaidiwa na wafanyakazi wa Precision kukamilisha dokomenti zake za Usafiri, huku ulinzi ukiwa umeimarishwaKwaheri Mtumishi wa Mungu, tunaomba uje tena tutakapoamua kuzindua upya Parokia Yetu ya Yosefu Mfanyakazi- Olasiti Arusha.
KINANA AJISAFICHA DHIDI YA TUHUMA ZA UJANGILI......AWATAJA WALIOHUSIKA NA SHEHENA YA PEMBE ZA NDOVU
Katibu Mkuu wa CCM ndg Abdulrahman Kinana amesema kinga ya Bunge isiwe sababu ya baadhi ya wabunge kutumia fursa hiyo kuchafua watu wasio na nafasi ya kujitetea ndani ya mhimili huo wa Dola.
Amehadharisha hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma juzi kukanusha tuhuma zilizoelekezwa kwake binafsi na chama chake na Kambi ya Upinzani Bungeni.
Tuhuma hizo zilihusu shehena ya pembe za ndovu iliyokamatwa Vietnam mwaka 2009 ambazo aliziita za kupika na za uongo. "Tuhuma hizo hazina ukweli wowote, zina nia mbaya dhidi yangu na zimelenga kuniharibia taswira yangu na ya chama changu," alisema Kinana.
Alisema hahusiki vyovyote na tuhuma hizo na kutuhumu Kambi ya Upinzani Bungeni kwa kushindwa kujadili hoja za maana za maendeleo na badala yake kujihusisha na siasa za kuchafua heshima za watu.

MUSWADA WA KUZUIA MAANDAMANO NCHINI WAANDALIWA
Katika hali ya kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi aliliambia bunge jana jioni kwamba serikali imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.
Waziri Nchimbi alisema kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa....Alisema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo Huenda azimio hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.Ikumbukwe ni hapo juzi tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kudhibiti wapinzani kuiimarisha CCM.
Credit: JF

WABUNGE WAANZA KUJIHAMI NA MILIPUKO YA MABOMU....WAMEOMBA ULINZI UIMARISHWE BUNGENI
MBUNGE wa Jimbo la Simve kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Richard Ndasa amemuomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda kuhakikisha usalama wa Bunge unaimarishwa.
Ndasa aliyasema hayo wakati akichangia hoja katika Bajeti ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kusema kuwa tukio la juzi Mjini Arusha kwa Bomu kurushwa katika sherehe za uzinduzi wa jingo la Kanisa Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasit mjini Arusha na kupelekea vifo vya watu wawili na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya.
“Mheshimiwa Spika, naomba usalama Bungeni uimarishwe na katika jingo la Bunge maana hofu ya kushambuliwa Bunge hili inaweza kutokea enbdapo ulinzi utakuwa hafifu,” alisema Ndasa.
Ndasa alitolea mfano eneo la nyuma la Bunge hilo kuwa halina ulinzi wa kutosha hivyo ni rahisi mtu kusogea jirani na kufanya uhalifu nakuleta madhara makubwa kwa taifa.
Wabunge leo wanaendelea kuchangia Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani huku kila anaesimama akilaani tukio hilo la Arusha.

Subscribe to:
Posts (Atom)