Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani-Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Osmund Mbilinyi (Mb).
MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99 (9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)
1. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Dira ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni “kuwa na taifa lililohabarishwa vizuri, lina vijana wenye uwezo na malezi bora, linathamini utamaduni wake na linakuwa mahiri katika michezo ifikapo mwaka 2025.” Aidha, ‘dhamira’ ya wizara hii ni ‘kuendeleza utambulisho wa taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari, kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza utamaduni na michezo kwa umma kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.’
Monday, May 20, 2013
HII NDO KAULI YA SUGU ILIYOSABABISHA BUNGE LISITISHWE GHAFLA LEO KUOGOPA UCHOCHEZI
Muda mfupi uliopita spika wa bunge, Anna Makinda amelazimika kusitisha shughuli za bunge mwanzoni tu mwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyokuwa ikisomwa na waziri kivuli wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi aka Sugu.
Kauli kwenye hotuba hiyo iliyobabisha spika wa bunge asitishe shughuli za leo hadi jioni ilisema,
“Tanzania imegeuka chini ya usimamizi wa wizara ya serikali hii ya CCM kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa, kuwangoa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua.”Spika amesitisha bunge hilo ili kupata muda wa kuipitia hotuba hiyo kuondoa kauli za uchochezi.

HUYU NDO MBUGE ALIYEDONDOKA BUNGENI
MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwanamrisho Taratibu Abama jana asubuhi aliugua na kuanguka ghafla katika viwanja vya Bunge na kukimbizwa hospitali....
Tukio hilo lilitokea wakati akienda kuhudhuria semina ya wabunge kuhusu Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia kabla ya kukosa nguvu na kudondoka na kisha kusaidiwa na wenzake kumkimbiza kwenye zahanati ya Bunge.
Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza bungeni, gari la wagonjwa lilimkimbiza Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) ambako amelazwa.
Kwa mujibu wa waliomshuhudia, mbunge huyo alianza kwa kuishiwa nguvu hali ambayo waliokuwa karibu walimsaidia kumpeleka kwenye zahanati ambako alitundikiwa dripu kabla ya kupelekwa hospitalini.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma, Zainabu Chaula alikiri kumpokea mbunge huyo.

PICHA BAADHI ZA MBUNGE WA IRINGA ( PETER MSIGWA )BAADA YA KUONGOZA WANANCHI KUFANYA FUJO
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiwasili eneo la vurugu kabla ya kuanza kwa vurugu hizo
Machinga wakisukuma gari ya mbunge Msigwa
"WANAOCHOCHEA VURUGU ZA KIDINI NI WATU WALIOTUMWA NA MATAIFA YA NJE"..... RAIS KIKWETE
Rais Jakaya Kikwete amebainisha kuwa vurugu za kidini na kisiasa zinazotokea nchini, zina uhusiano na watu wa nchi za nje.
Kikwete alitoa kauli hiyo jana kwenye ibada maalumu ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mkuu wa Sitta wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dk Jacob Chimeledya.
Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye ibada hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu.
“Wanaohamasisha vurugu hizo ni watu wenye uhusiano ya karibu na watu wa nje ambao mambo yakiharibika nchini watakuwa wa kwanza kupanda ndege, ilhali wakiendelea kutoa matamko ya uchochezi wakiwa nje ya nchi wakati wengine wakiendelea kuumia,” alisema Kikwete.

WANAWAKE JIJINI MBEYA WAMVAA MCHUMBA WA DR. SLAA BAADA YA KUMKASHIFU MKE WA RAIS KIKWETE
UMOJA wa wanawake wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya(UWT) umemshukia Bi.Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba Katibu Mkuu wa chama cha
Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufuatia kauli za udhalilishaji dhidiya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Hatua hiyo inatokana na kauli za kiudhalilishaji zilizotolewa mwishoni mwa wiki na mchumba huyo wa Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mama Kikwete ameshindwa kumshauri Rais ambaye ni mume wake kuiongoza nchi vizuri .
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Bi.Priscilla Mbwaga wakati akitoa Tamko kwa waandishi wa habari juu ya Matusi ya wazi yaliyotolewa na Bi.Mushumbusi kwa Mke wa Rais katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Wilayani Mbozi Kata ya Vwawa Mkoani hapa.

Friday, May 17, 2013
CD ZA UAMSHO NA ZILE ZA SHEIKH ILUNGA ZAPIGWA MARUFUKU....
Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar inayoongozwa na Dr Shein na Makamu wake Maalim Seif kupitia Jeshi la Polisi wamepiga marufuku rasmi CD zote za mawaidha ya Kiislam za UAMSHO,MUJAHID ABOUD ROGO na SHEIKH ILUNGA.
Agizo hilo lilitolewa na OCD wa zamani Murtad MKADAM ambae kwa sasa yupo ofisi kuu ya polisi kitengo cha madawa ya kulevya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif.
Alisema cd hizo za kiislam ni chanzo cha uvunifu wa amani hapa nchini na ndio zinazosababisha uchochezi baina ya dini ya ukiristo na uislam.
OCD alibainisha kuwa mpaka sasa wameshawakamata watu kadhaa wanaojihusisha na kuuza cd hizo na kuwaonya wale wote ambao huweka kuzisikiliza maana watachukuliwa hatua kwani serikali ina mkono mrefu. ...
Akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa kwamba waliowakamata hawawaoni kuwa wamewadhulumu kwa kufanya biashara halali ya uzaji cd, Ocd alijibu cd zile za mawaidha ni Haram wala sio riziki ya halali kwa upande wa serekali kwani zinapelekea uvunjifu wa Amani katika nchi.

SERIKALI YAAHIDI KUWACHUKULIA HATUA KALI VIONGOZI WA WIZARA YA ELIMU WALIOSABABISHA UBOVU WA MATOKEO YA FORM FOUR
Mizengo Pinda.
Serikali imeahidi kuwajibisha watendaji watakaobainika kwenda kinyume katika uingizaji wa mfumo mpya wa usahihishaji mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012, ambao matokeo yake yamefutwa.
Akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kinachosubiriwa sasa, ni maelezo ya kina ya Tume ya Taifa aliyoiunda kuchunguza matokeo hayo.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Tume hiyo haijakamilisha kazi yake, lakini muda si mrefu itakuwa imekamilisha na kuwasilisha maelezo ya kina yatakayoipa Serikali majibu kwa maeneo yote.
“Tusubiri kidogo, muda si mrefu tutakuwa tumekamilisha kazi …na kama wapo watu waliosababisha jambo hili, wala haitakuwa tatizo hata kidogo kuchukua hatua za kuwawajibisha. Ni dhahiri kwamba suala hili si dogo,” alisema Waziri Mkuu.
Majibu hayo ya Pinda yalitokana na maswali ya Mbunge Sakaya, ambaye alisema uamuzi wa Serikali wa kufuta matokeo hayo kutokana na kubainika kulikuwa na mabadiliko ya upangaji wa alama bila kuandaa wanafunzi, si jambo dogo.

Beckham astaafu soka, amfuata Sir. Ferguson
Dili la kustaafu lazidi kuitikisa nchi ya Uingereza baada ya magwiji wa soka na kocha maarufu kustaafu kufundisha soka.
Wiki moja baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, Paul Scholes, leo hii mchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa England DAVID BECKHAM ametangaza kutundika daluga.
Beckham mwenye umri wa mika 38, ameisadia Paris Saint-Germain PSG Kutwaa mwari wa Ligue 1 nchini Ufaransa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 19 mwishoni mwa wiki iliyopita Pamoja na kupewa ofa ya mkataba mpya na timu hiyo ya Ufaransa, mkongwe huyo atastaafu baada ya mchezo wa mwisho tarehe 26 mwezi huu .
Alisema: “Shukrani sana kwa PSG kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwa hapa lakini sasa nadhani ni muda sahihi wa kustaafu, kucheza kwenye soka la kiwango cha juu”
Beckham alianza kucheza akiwa na Manchester United, akifunga mabao 85 katika mechi 394, kabla ya kuhamia Real Madrid. Aliondoka Spain kwa uhamisho mnono kujiunga na LA Galaxy mwaka 2007 pia aliwahi kucheza kwa mkopo mara kadhaa kwenye klabu ya AC Milan wakati akiwa kwenye Major League Soccer. Chanzo: Baraka Mpenja

Tiketi za simba na yanga kuanza kuuzwa leo
TIKETI kwa ajili ya pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Yanga litakalochezwa kesho (Jumamosi) kwenye Uwanja wa Taifa zitaanza kuuzwa leo (Ijumaa) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Vituo vitakavyouza tiketi hizo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni ni Uwanja wa Taifa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, OilCom Ubungo, kituo cha mafuta Buguruni, BMM Barbershop Sinza Madukani, Dar Live Mbagala na Sokoni Kariakoo.
Tiketi hizo zitakuwa zikiuzwa katika magari maalumu yaliyoegeshwa katika vituo hivyo. Viingilio katika mechi hiyo ya kufunga msimu ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani, sh. 7,000 viti vya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B n ash. 30,000 kwa VIP A. Chanzo: TFF

Thursday, May 16, 2013
Rais kikwete azindua kampeni ya lishe
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha kampeni ya Lishe Tanzania baada ya kukizindua leo Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Peniel Lyimo akifuatiwa na Mkurugenzi wa kwanza wa Taasisi ya Chakula na Lishe Mzee Lema. Kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere
Mama Maria Nyerere akifurahia tuzo maalumu aliyopokea kwa niaba ya Baba wa Taifa aliyotunukiwa na Taasisi ya Chakula na Lishe kwa mchango wake mkubwa kwa kukuza na kuendeleza sera ya lishe nchini wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya Lishe Tanzania leo Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Wadau wa utalii wakutana arusha
Wadau wa utalii kutoka halmashauri ya Wilaya ya Longido wamekutana leo hii katika mkutano wa Siku Mbili wenye lengo kuu la kuthamini na kutambua mchango wa Rasilamali zinazo wazunguka wafugaji wa halimashauri hiyo katika kujiletea uchumi kwa njia nyingine tofauti na ile iliyozoeleka.
Mkutano huo wa Wadau hao wa Utalii kutokandani ya Halimashauri ya Wilaya ya Longido ambao ulifunguliwa na Afisa wa Mazingira ya Ikolojia kutoka
mamlaka ya Hifadhi za Taifa Bwana Alibert Mziray ambapo amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kujua jinsi ya kutumia Rasilimali zilizopo hasa hasa kwa Wafugaji hao wa Loliondo.

MWANA FA AVUNA MILIONI 18 NDANI YA MIEZI MITATU KWENYE RINGBACK TONE
Kwa mujibu wa Mwana FA mwenyewe ambaye leo ameachia wimbo wake mpya, Kama Zamani, hivi karibuni alipokea malipo ya miezi mitatu kutoka kampuni moja ya kuuza miito ya simu aka RBT yanayofikia shilingi za kitanzania milioni 18.
Akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, FA aliyekuwa wa tatu kati ya wasanii waliopata fedha nyingi zaidi kwenye malipo hayo chini ya Rose Mhando na Diamond, amesema ameamua kuweka wazi hilo ili watu waondoe imani kuwa muziki wa hip hop hauuzi.
Tarehe 31 mwezi huu, Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.

Subscribe to:
Posts (Atom)