Tuesday, July 2, 2013

KWA HERI BARACK ABAMA....KARIBU TENA NA SAFARI NJEMA

MAZISHI YA MANDELA YAGOMBANIWA NA VYOMBO VYA HABARI PINDI ATAKAPOFARIKI

PICHA ZA WANANCHI TOKA UBUNGO WAKISUBIRI MSAFARA WA RAIS OBAMA

MFALME MSWATI WA SWAZILAND AAONDOKA NCHINI NA AMEWATAKA WATANZANIA WABADILIKE

MAREKANI KUFUNGUA UKURASA MPYA KATIKA UWEKEZAJI BARANI AFRIKA

GEORGE BUSH NA OBAMA WATAKUTANA ANA KWA ANA KATIKA ARDHI YA TANZANIA

TANZANIA YAUMBULIWA....GAZETI MAARUFU LA MAREKANI LAANIKA UKATILI UNAOTENDEKA NCHINI

PICHA ZA RAIS OBAMA ALIPOTUA KATIKA ARDHI YA TANZANIA

MMILIKI WA FACEBOOK NA WAFANYAKAZI WAKE WASHEREHEKEA KUPITISHWA KWA SHERIA YA NDOA YA JINSIA MOJA

MKE WA OBAMA ATEMBELEA WAMA FOUNDATION NA KUKUTANA NA MAMA SALMA KIKWETE

TUJIKUMBUSHE MAMBO MACHACHE YANAYOTENDEKA KUHUSU OBAMA AMBAYE TAYARI YUPO TANZANIA

Obama ameshatua Tanzania

Saturday, June 29, 2013

HATARI LAKINI SALAMA!

 Randy Miller akicheza na chui wake Eden.
 Chui Eden akiwa amemdondosha chini mwalimu wake Randy
 Randy akiwa chini baada ya kudondoshwa na Eden.
 Marafiki hao wawili wakiwa katika pozi.Taswira hapo juu zinamwonyesha Bwana Randy Miller (45) akicheza na chui wake aitwaye Eden ambaye amemfundisha

jinsi ya kufanya mashambulio yasiyo na madhara na ambaye amekuwa akimtumia katika kucheza filamu mbalimbali.

Mambo 20 ya kusisimua kuhusu Obama

RAIS wa Marekani, Barack Obama, anatarajia kutua Tanzania Jumatatu. Watanzania wengi wanamsubiri kwa hamu, lakini je wanayafahamu mambo yanayovutia kuhusu rais huyo? Makala hii inayachambua mambo 20 ya kufurahisha kuhusu Obama.

1. Asili
Obama ni mchanganyiko wa damu ya Kenya, Ireland na England.

2. Namba 44
Ni Rais wa 44 wa Marekani. Rais wa kwanza alikuwa, George Washington, ambaye alitawala kuanzia mwaka 1789 hadi 1797.

3. Anapenda TV
Obama anapenda kuangalia televisheni. Anapenda kipindi cha ‘The Wire’. ‘The Wire’ ni tamthilia inayorushwa kwenye televisheni na inahusu upelelezi wa polisi.

4. Wa Kwanza
Obama ni rais wa kwanza wa Marekani ambaye amezaliwa Hawaii.

5. Ndugu yake
Rais Obama ana dada mmoja tu, anaitwa Maya. Hata hivyo Obama na Maya wamechangia mama tu, baba ni tofauti.

SIMULIZI ZA MZEE MADIBA; MANDELA BONDIA ALIPOKUTANA NA BONDIA…!

Ndugu zangu, Kuna simulizi nyingi za Mzee wetu Madiba. Hakika, Nelson Mandela hajawahi kuwa mpenda makuu. Mzee Mandela yuko simple sana, ni tangu enzi za ujana wake. Lakini, kuna ambao hawajui kuwa Mandela anapenda sana mchezo wa ngumi, na kuwa , yeye mwenyewe aliwahi kuwa bondia.

Kuna wakati akiwa Ikulu kama Rais, Mandela alipata habari za bondia wa Afrika Kusini aliyetwaa taji la  kimataifa. Mandela alifurahishwa sana na habari hizo. Akataka ampongeze mwenyewe bondia  huyo.Siku moja akiwa na wasaidizi wachache sana, Mandela alikwenda hadi nyumbani kwa bondia huyo. Alihakikisha kuwa bondia huyo yuko nyumbani kwake. Alipofika, Mandela aliwaambia wasaidizi wake wakamwambie bondia huyo kuwa nje kuna mtu anayehoji ubingwa wake.  Wamwambie kuwa  mtu huyo ( Nelson Mandela) anadai kuwa yeye ndiye bingwa wa uzito huo katika Afrika Kusini ( Nelson Mandela!) Kwamba anataka mkutane mpange siku ya kupigana ili apatikane mshindi halali wa taji hilo.

Basi, bondia yule akapokea habari hizo na akatamani sana amwone huyo anayedai kuwa ana ubavu wa kupambana naye. Alipotoka nje akakutana na Nelson Mandela akiwa amesimama getini na amekunja ngumi yake. Akatania; “ Nimekuja kwako tuzipige ili dunia imjue bingwa halisi!”

Ikawa ni furaha kubwa kwa bondia yule. Hakuamini macho yake. Kuwa Rais wa nchi amekuja nyumbani kwake kumpongeza.  Kumpongeza kwa jambo kubwa alilolifanya kwa taifa la Afrika Kusini.

Na Mandela akawa tayari kuingia nyumbani kwa bondia huyo na kunywa nae chai!

What a Great Leader Of Africa! Yes, Nelson Mandela!

Maggid Mjengwa,

Iringa.