Tuesday, March 3, 2015
Ni kweli Hii
Jamani nimesikia kuna mtoto amezaliwa anaongea mjini morogoro na kusema kwamba kuna mvua itanyeesha kwa muda wa siku mbili hivyo watu wasitumie hayo maji baada ya hapo akafariki jamani kuna ukweli wowote juu ya hili tujuzane
Wednesday, February 18, 2015
hi nawatakia jumutano njema ya majivu
jamani nawatakia kwaresma njema na tumuombe mungu atusamehe makosa yetu leo tusisahau kwenda kanisani.
Monday, February 2, 2015
Bondia Francis Cheka amehukumiwa kwenda jela.
Bondia Francis Cheka leo February 2 2015 amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na faini ya Milioni moja laki sita kwa kosa la kumpiga mmoja kati ya wafanyakazi wake kwenye bar yake iliyopo Morogoro.
Muda mfupi uliopita Francis Cheka ameongea na kusema ndio alikua anajiandaa kuachia simu yake na vitu vingine muhimu ili achukue karandinga kuelekea gerezani ambapo namnukuu akisema ‘imeshakua hivi tayari ila hamna noma, niko na wanangu wengine wamepigwa miaka 10 nitakua nao fresh tu ila hamna noma ni miaka mitatu tu mimi’
Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Said Msuya ambapo baada ya hayo upande wa Francis Cheka unasemekana kujiandaa kukata rufaa.
millardayo.com
Muda mfupi uliopita Francis Cheka ameongea na kusema ndio alikua anajiandaa kuachia simu yake na vitu vingine muhimu ili achukue karandinga kuelekea gerezani ambapo namnukuu akisema ‘imeshakua hivi tayari ila hamna noma, niko na wanangu wengine wamepigwa miaka 10 nitakua nao fresh tu ila hamna noma ni miaka mitatu tu mimi’
Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Said Msuya ambapo baada ya hayo upande wa Francis Cheka unasemekana kujiandaa kukata rufaa.
millardayo.com
Habari njema kuhusiana na majaribio chanjo ya Ebola…
Stori kuhusu ishu ya Ebola huenda ni moja ya story zilizochukua headlines kubwa kwa mwaka wote 2014, tangu iliporipotiwa kuibuka kwa maambukizi ya ugonjwa huo Afrika Magharibi mwanzo wa mwaka 2014.
Hii inaweza kuwa habari njema kwa Waafrika na dunia nzima kwa ujumla, taarifa iliyopo ni kwamba jaribio la kwanza la chanjo ya ugonjwa wa Ebola kutarajiwa kuanza kutumika Liberia wakati wowote kuanzia sasa.

Wataalamu wanatarajia zaidi ya watu 30,000 watajitokeza katika zoezi la majaribio hayo wakiwemo wahudumu wa afya.
Katika kipindi cha mwaka mmoja zaidi ya watu elfu tisini wamefariki kutokana na ugonjwa huo ambao uliandama zaidi Mataifa ya Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Sunday, January 18, 2015
Wednesday, December 31, 2014
TAARIFA YA UFAFANUZI WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Katika gazeti la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 ziliandikwa habari kuhusu Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) chini ya kichwa cha habari "Wanaomtetea Muhongo Wajibu haya". Hoja zilizotolewa katika gazeti hilo zililenga kupotosha ukweli. Wizara inapenda kutoa maelezo kuhusu hoja zilizotolewa kama ifuatavyo:
Utendaji wa Wizara chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb)
Taarifa za gazeti hilo zilieleza kuwa utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini hasa katika uongozi wa Waziri Muhongo umekuwa ni wa kukatisha tamaa. Moja ya mifano iliyotolewa ni kuendelea kuwepo kwa wachimbaji madini wanaozidi kutorosha madini kwa nia ya kukwepa kodi.
Subscribe to:
Posts (Atom)


