Friday, July 20, 2012

HUU NDIO MKOPO CHINA ILIOTOA KWA AFRIKA.

Rais wa China Hu Jintao ametangaza mkopo wa dola Bilioni 20 kwa nchi za bara la Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hiyo na Afrika.

Mkopo huo ni mara mbili zaidi ya kiasi ambacho China iliahidi kwa kipindi cha miaka mitatu 2009.

DW wamesema ahadi hiyo inaonekana kuimarisha uhusiano mzuri wa China na bara la Afrika, ambalo ni muuzaji wa mafuta na mali ghafi kama vile shaba na uranium kwa nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu ulimwenguni na ya pili kwa ukubwa kiuchumi.

Lakini mikopo hiyo huenda isiwe habari njema kwa nchi za magharibi ambazo zinaishutumu China kwa kupuuza uiukwaji wa haki za binaadamu katika ushirikiano wake wa kibiashara na Afrika, hasa katika tamaa ya China ya kuulisha uchumi wenye njaa ya raslimali na unaozidi kukua.

President Hu alipuuzia hofu kama hiyo katika hotuba yake kwa wananchi Great Hall, mkutano uliohudhuriwa na viongozi akiwemo rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na mwenzake wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema, mtu anayeshutumiwa vikali na makundi ya haki za binaadamu kama mmoja wa viongozi mafisadi zaidi ulimwenguni.

No comments: