Tuesday, April 30, 2013

LULU KURUDIA KAZI YAKE BAADA YA KUSHINDA KESI YAKE!

 HATIMAYE staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameingia mzigoni na kufyatua filamu yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu, Amani limeinyaka.
 Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu alitupia picha akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada ya kusimama kuigiza kwa muda mrefu.
Baadhi ya picha hizo zinamuonesha Lulu akiwa na staa mwingine wa filamu Bongo, Hashimu Kambi mbele ya kamera kwa ajili ya kushuti filamu hiyo ambayo jina lake halijapatikana.

TASWIRA ZA SHOW YA DIAMOND JIJINI LONDON



Pichani juu, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akifanya makamuzi ndani ya jiji la London wikiendi iliyopita. Msanii huyo bado anaendelea na ziara yake nchini England.

LEMA ASEMA HAYA BAADA YA KUACHIWA MAHAKAMANI KWA DHAMANA

 Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless lema ameachiwa huru kwa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi baada ya kusota rumande kwenye kituo kikuu cha polisi kwa siku tatu  kwa kosa la kuchochea vurugu chuoni uhasibu huku baada ya kutoka akiwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kumzomea mkuu wa mkoa.

Lema alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa Tatu na robo asubuhi akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kufikishwa mbele ya hakimu Devotha Msele  na ndipo mwendesha mashtaka Eliang’enyi Njiro alisimama kuanza kumsomewa mashtaka ya uchochezi na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani aliyoyafanya kwenye eneo la chuo cha uhasibu njiro jijini Arusha.

Baada ya kutoka mahakamani hapo alielekea kwenye ofisi za chama hicho na kuzungumza na waandishi wa habari huku akitoa malalamiko na kuwataka wanachama na wapenzi wa chadema kumzomea mkuu wa mkoa iwe kanisani,mskitini,au kwenye sherehe mbali mbali,

“Nawatakeni kumzomea huyo mkuu wa mkoa Magessa Mulongo na kuwa nia ya kumshtaki ipo pale pale ndugu zangu Makamanda wenzangu huyu jamaa awe msikitini kanisani kote tumzome hiyo itakuwa ndiyo salamu yetu kwake”alisema Lema

Katika hali nyingine jeshi la polisi liliimarisha ulinzi tangu nje ya mahakama hadi ndani ya mahakama hiyo kiasi utulivu katika mahakama hiyo ulionekana na shughuli kuendelea bila bughaa.

Hali kwenye mitaa mbali mbali ya viunga vya jiji la Arusha ilionekana kuendelea na mishughuliko ya kila siku kama kawaida kuliko ilivyokuwa ikionekana huko mwanzo kwenye kesi zilizokuwa zikimkabili mbunge huyo kwa wakazi wa jiji hili kuacha shughuli zao na kuelekea mahakamani kufuatilia kesi ya mbunge huyo.

Magazeti ya leo jumanne ya 30th April 2013




BAADA YA GODBLESS LEMA KUKAMATWA AKIHUSISHWA NA UCHOCHEZI WA FUJO WA WANAFUNZI WA UHASIBU ARUSHA BAADA YA MWENZAO KUUAWA KWA KUCHOMWA KISU HATIMAE GODBLESS LEMA AACHIWA HURU KWA DHAMANA YA MILIONI MOJA

 Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema,ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja katika mahakama kuu kanda ya Arusha.

TUNDU LISSU AHOJIWA NA RADIO TEHRAN KUHUSU SAKATA LA KUKAMATWA MBUNGE LEMA

Nchini Tanzania sakata la kukamatwa na kuwekwa mahabusu Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kwa madai ya uchochezi, limeibua sura mpya baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutajwa kuwa nyuma ya mkakati huo.

Kwa upande wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kimelaani hatua hiyo na kulilaumu jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kukandamiza upinzani.

Chama hicho kimekwenda mbali zaidi na kulituhumu jeshi la polisi Arusha kwamba, limekuwa likitumikia CCM badala ya kutumikia umma.

HUU NDO UNYAMA WALIOTENDEWA WANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

                      Marehemu  Henry  katika enzi za uhai wake....

Mwanafunzi  huyo  Alikuwa Masomoni Mida Ya Usiku Na Alipomaliza Aliondoka Na Kuelekea Maeneo Ya Esami. Kabla Hajafika Eneo La Malazi (Hostel) alipigiwa Simu na Mwenzake amsubiri Ili Waende Wote Hostel.
 
Wakati anamsubiri Rafiki Yake Kwenda Hostel, Kuna Bajaj Ilifika Eneo Hilo Na Watu Hao Wasiojulikana Wakataka Pesa Kutoka Kwa Mwanafunzi Huyo...Wakati  wakiendelea  kuzozana, rafiki  yake  naye  alifika.....
Picha  ya  marehemu  Henry Koga  baada  ya  kuchomwa  kisu  na  kufariki  hapo hapo  katika  chuo  cha  uhasibu  Arusha.....

Majibu Ya Wanafunzi Hao Hayakuwafurahisha Watu Hao Na Ndio Walipochomoa Kisu Na Kumchoma Mmoja wa Vijana Hao Tumboni Na Shingoni na Kupoteza Maisha Hapo Hapo....

Mauaji  hayo  yamesababisha  vurugu  kubwa  chuoni  hapo  zilizopelekea  kupigwa  mawe  mkuu wa  mkoa

"UREMBO SIYO KIPAJI NA SI KILA MWANAMKE MZURI ANAWEZA KUIGIZA"...JACKLINE WOLPER

Muigizaji Jacqueline “Jackie” Wolper amewashangaa wanaodhani kuwa urembo wa mwanamke ni mbadala wa kipaji hasa katika sanaa ya maigizo. Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.
 “Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper.
 Wolper aliendelea kulalama kuwa kila mtu akijona ana sura ya kuvutia na umbo zuri basi anajua anaweza kuigiza ndio maana matokeo yake wanafanya vitu sivyo na mwisho wake wanaacha fani kabisa.
 Alifafanuwa kuwa kuigiza ni zaidi ya urembo hivyo yeyote ambaye anafikiri anaweza kufanya kazi hii kwa uzuri wa sura na umbo ajaribu kama hakuchemka.

Source: Mwananchi

"SIONI TATIZO KWA LULU MICHAEL KUPIGA PICHA NA PENNY....HUO NI UMBEA WA MAGAZETI"..WEMA SEPETU

Hivi  karibuni  zilisambaa  picha  za  Lulu  Michael  akiwa  katika  picha  ya  pamoja  na  Penny....

Picha  hizo  zilizua  utata  mkubwa  miongoni  mwa  watu  huku  kundi  kubwa  likidai  kuwa  picha  hizo  zimepigwa  makusudi  kwa  lengo  la  kumuumiza  Wema  Sepetu...
 Lulu Michael  akiwa  na Penny

Madai  hayo  yaliandikwa  kwa  kina  na  gazeti  moja  la  udaku  hapa  nchini  likisimulia  ugomvi   uliopo  kati  ya Penny  na Wema Sepetu.....

"SIWAOGOPI MATAIRA WANAONIPONDA....MUNGU PEKEE ANAWEZA NA SI HAO TUMBIRI".....HII NI KAULI YA DIAMOND

Watu kadhaa  wamekuwa  wakimponda Diamond  baada ya  kwenda  LONDONI kwa  madai kuwa ni mshamba  wa  jiji  na  limbukeni ....

Madai hayo yamekuja  baada ya msanii huyu kuanza kuyashobokea  magari ya kifahari kwa kupiga nayo  picha na kuzirusha hewani.....

Baada ya kuona  mizengwe  ya watu imekuwa  mingi, Diamond  ameamua kuwajibu  kwa kupost  jumbe  huu

NAWASHUKURU SANA WADAU WANGU.

Hakika nawashukuru sana wote mliokuwa nami katika kipindi hiki cha kuumwa kwangu mungu awaongezee pale mlipotoa kwa ajili yangu.Pamoja na kwamba sikuweza kutupia vitu humu lakini hamkuacha kuperuzi habari. Nawahakikishia kuanzia sasa kila kitu kitakuwa kama kawaida habari za kumwagaaa.Nawapenda sana Asanteni kwa sapoti yenu.

Monday, April 15, 2013

MECHI YA AZAM, SIMBA YAINGIZA MIL 66/-


Na Boniface Wambura, TFF

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Aprili 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000 kutokana na watazamaji 11,458.

Viingilio katika mechi hiyo namba 155 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,849,326.14.

 WATAZAMAJI 11,021 WAZISHUHUDIA YANGA, OLJORO

Magazeti ya leo Jumatatu ya 15th April 2013






ZITTO KABWE AIKANA NAMBA YAKE YA SIMU LIVE BAADA YA CHADEMA WENZAKE KUDAI NI GAIDI NA ACHUNGUZWE

 Sasa  nashawishika  kuamini  kuwa  CHADEMA  wana  lao  juu  ya  mipango  ya  kigaidi...

Jana  Mabere  marando  alitoa  tamko refu  sana   lenye  namba  za  simu  kibao  za  watu  mashuhuri  akitaka  mahakama  ichunguze  simu  zao  ikiwemo  ya  Zitto  Kabwe.....

SWALI  LA  KUJIULIZA:

-Kwanini Mabere Marando anatoa tamko muhimu kama hili bila kuhussisha viongozi wa juu kama Zitto?

-Matamko ya nini wakati kesi iko mahakamani?

-Kwanini chadema inaendelea kulizungumzia hili swala nje ya mahakama huku wanaharakati wa chadema kama Mwanakijiji wakiwa wameshaanzisha harakati za kutaka kesi ifutwe kwa swala kuzungumziwa nje ya mahakama?

 HUU  NI  UJUMBE  WA  ZITTO  AKIKANUSHA  KUHUSIKA  NA  UGAIDI

 ( HAPA  AMEANZA  KWA  KUNUKUU  SEHEMU  YA RIPOTI  YA MABERE:)

UGOMVI WA CHADEMA NA CCM WAFIKIA PABAYA......MABERE MARANDO AYAANIKANI MAWASILIANO NYETI YA VIONGOZI WA CCM

TAMKO LA CHADEMA KUHUSU NJAMA ZA KUKICHAFUA ZINAZOFANYWA NA GENGE LA VIONGOZI WAKUU WA CCM NA VYOMBO VYA DOLA, LIMETOLEWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO, MACHI 14, 2013 NA MJUMBE WA KAMATI KUU NA MWANASHERIA WA CHAMA, MH. MABERE NYAUCHO MARANDO

Ndugu waandishi wa habari;
LEO tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushu, nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo mengi mno.

Uchunguzi huu nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na Usalama, Willifred Muganyizi Lwakatare, ambaye hivi sasa anashitakiwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi.

Nimefanya hivyo kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga mipango hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.

Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi na Mwigulu Nchemba, “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa jeshi la polisi Desemba mwaka jana. Lakini jeshi hilo halikumkamata yoyote wala kumhoji, hadi pale Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, alipovamiwa na kuumizwa.

KAULI YA MJENGWA BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI MAKAO MAKUU KUHUSU KUTEKWA KWA KIBANDA

Ndugu zangu,
Kama alivyowataarifu kaka yangu Nyaroonyo Kichehere, ni kuwa, jana Jumamosi nilikuwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuanzia saa tano asubuhi ya jana mpaka saa tatu usiku. Ilihusu mahojiano ya Polisi na mimi kuhusiana na sakata la ndugu yetu Absalom Kibanda.

Ukweli sikukamatwa mahali popote, bali niliitwa na Kamishna ( Upelelezi) Advocate Nyombi. Alhamisi nikiwa Iringa, tukakubaliana na kiungwana na Kamishna Nyombi kuwa nifike Makao Makuu hayo ya polisi Jumamosi saa tano. Ikawa hivyo.

Hapo nilipokelewa na Kamishna Nyombi. Baada ya mazungumzo mafupi ndipo akawaita maofisa wengine watano wa Upepelezi kufanya mahojiano nami.

Niliomba niwe na Mwanasheria, nikakubaliwa. Nilimpigia simu kaka yangu Nyaroonyo, naye, kwa vile ni Wakili pia wa Kibanda akanisaidia kuhakikisha napata wakili mwingine. Pamoja na kuwa ilikuwa ni Jumamosi, ndugu yangu Nyaroonyo Kichehere alifanya alivyoweza.

Ndani ya dakika 40 hivi alifika chumba nr 704 ghorofa ya saba akiwa na Wakili Jacquiline Rweyongeza na Legal Officer Dickson Mbonde. Nilimshukuru Kaka Nyaroonyo Kichehere. Na nilimuaga kwa kumwambia; “ Nenda ukaifahamishe jamii juu ya hiki kilichonitokea”.

Nachukua fursa hii pia kuwashukuru kwa dhati kabisa dada yangu Wakili Jacquiline Rweyongeza na kaka Dickson Mbonde kwa kuacha yote ya Jumamosi na kuwa tayari kuwa msaada kwangu.

Jacquiline alimuacha nyumbani mtoto wake wa miezi minne kwa ajili ya suala langu. Sina namna nyingine ya kumshukuru. Na hakika, msaada wao niliuhitaji sana.

Nawashukuru pia kwa dhati kabisa, ndugu zangu Saed Kubenea, Mbaraka Islam na wengine wote waliokuwa na utayari wa kunisaidia pale msaada wao ulipohitajika.

Kwa ufupi, nimetoa maelezo yangu bila shuruti wala kutishwa.

Na nimeweka wazi kuwa yanaweza kutumika Mahakamani kama yatahitajika au hata kama mimi nitahitajika, kwa namna yeyote ile.

Kesho saa mbili asubuhi nitaripoti Makao Makuu ya Polisi kupewa maelezo ya kitakachofuatia.Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana kwa kuwa nami katika muda wote huuMaggid,
Dar es Salaam.

MAJID MJENGWA NAYE AKAMATWA NA POLISI AKIHUSISHWA NA SAKATA LA KIBANDA

                                                                        Majid Mjengwa.
  MWANDISHI wa safu katika magazeti mbalimbali nchini, Majid Mjengwa amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.

Habari zilizoufikia mtandao huu jana mchana na baadaye kuthibitishwa na polisi zinasema Mjengwa alikamatwa muda wa asubuhi na kwamba alikuwa akihojiwa na makachero wa jeshi hilo hadi alasiri kuhusu tukio la kuteswa kwa Kibanda.

Msemaji Mkuu wa Polisi Advera Senso alisema kwamba:

“Ni kweli kwamba tunaye, tunaendelea kumhoji, tunachoomba ni kwamba mtupe nafasi ili tufanye kazi yetu na kukiwa na jambo lolote tutawajulisha.”

PICHA ZA MABAKI YA NDEGE ILIYODONDOKA JANA JIJINI ARUSHA



Eneo ambalo ndege iliyoanguka, kutoka eneo hilo mpaka landing truck ni kama 1km. Mbele ya mabaki hayo ya ndege kuna mti mmoja ambao unasadikiwa kuwa  ndege hiyo ilijigonga na kudondoka chini.

MBOWE AMKAANGA ZITO KABWE...ADAI KUWA LWAKATARE HATOFUKUZWA CHADEMA HATA KAMA NI GAIDI

 Katika hali ya kushitua,Mh.Mbowe akiongea na wanachama wa chadema leo Ubungo plaza amemkaanga  Zitto  kabwe  na  kudai  kuwa  chadema  haiko  tayari  kumtimua  Lwakatare  katika  chama  hata  kama  ni  gaidi....

"Eti nashangaa kuna watu wanataka CHADEMA kimuache Lwakatare na kumsimamisha uongozi kwa uzushi uliopandikizwa na CCM, Hilo halitafanyika"- alisema Mbowe.

IKUMBUKWE siku chache zilizopita naibu katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe alitoa mapendekezo ya kuomba Mshitakiwa mkuu kwenye kesi ya Ugaidi ambaye ni Ndugu Lwakatare aliyekuwa mkuu wa usalama wa chadema awajibike kisiasa...
 Kuwajibika kisiasa ni pamoja na kuachia ngazi ya ukurugenzi wa usalama ili kupisha uchunguzi salama na kukiacha chama salama.

Saturday, April 13, 2013

PADRI ALIYEOA KWA SIRI AFUNGWA JELA MIEZI 6

KUSHOTO: Padri William akimbusu mkewe, Beverley. KULIA: Kanisa la Mt. Clara ambamo Padri huyo alibambwa akifanya uchavu wake kwa binti wa miaka 17.

Padri mmoja wa kanisa Katoliki ambaye alifunga ndoa kwa siri amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela jana kwa kumsumbua msichana mdogo kwa kile jaji alichoelezea 'uvunjifu mkubwa wa uaminifu'.

William Finnegan, akifahamika kama 'Fadha Bill', alimpapasa binti huyo mwenye miaka 17 chini na kulazimisha kumbusu kwa nguvu katika Kanisa Katoliki la Mt Clara mjini Bradford siku ya Jumapili ya Pasaka mwaka jana.

Jaji Roger Thomas alisema kwamba Padri huyo mwenye miaka 60, alikiri wakati wa kesi hiyo kwamba alifunga ndoa kwa siri miaka 14 iliyopita.
Pia alitumia maneno makali kwa wanaparokia wa Finnegan ambao walikuwa upande wake licha ya mashitaka hayo, akisema: "Pengine baadhi yao wanaweza kuamini kesho jua litachomoza magharibi kesho kama akisema hivyo."

MWENYEKITI WA CHADEMA ATUPWA JELA MWAKA MMOJA KWA WIZI WA MIL. 1.2

Mwenyekiti wa chadema, mtaa wa isamilo kaskazini B wilayani nyamagana Philbert Bulinjiye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kujipatia shs milioni 1,250,000 kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo, imetolewa na hakimu Vaineth Mahizi wa mahakama hiyo, kufuatia kesi ya jinai namba 196/2012, iliyofunguliwa na Vedasto Mavubhi ambaye alimtuhumu mwenyekiti huyo kuchukua kwake kiasi hicho cha fedha, kwa ajili ya kumuuzia kiwanja.

Hakimu Mahizi katika hukumu yake, alidai ameridhika na ushahidi uliotolewa na upnade wa mlalamikaji, mashahidi pamoja na wazee wa baraza hivyo kumhukumu mwenyekiti kwenda jela.

Alisema mwenyekiti huyo pamoja na Balozi Robert Byagaye wanastahili kutumikia kifungo hicho cha mwaka mmoja jela kutokana na kutiwa hatiani.

"kitendo kilichofanywa na viongozi hawa, kuwaibia raia wanaowaongoza kiutapeli kwa kuwadanganya kuwauzia kiwanja na kisha kutafuta mtu bandia kwa madai kuwa kiwanja hicho kiko katika mtaa wanaouongoza, ni udanganyifu" Alisema hakimu na kuongeza kuwa Mwenyekiti huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa viongozi wengine matapeli.

NYARAKA NZITO ZA CCM ZAVUJA...

Taarifa za ndani kabisa zilizopatikana kutoka kwa Waandishi wa habari,Vyombo vya usalama na ndani ya CCM kwenyewe zinaonyesha sakata la Kuteswa kwa Kibanda na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi Mkurugenzi wa usalama wa Chadema ndugu Alfred Lwakatare linachukua sura mpya na mapya yamefichuka kwa ushahidi.

Dennis Msacky ambaye ni mhariri wa Mwananchi aliyehusishwa na kuwa mojawapo wa watu waliopangwa kutekwa,amekua akifanya mawasiliano na Ludovick Joseph Lwezaura kama ifuatavyo

Tarehe 27/12/2012: Dennis Msacky kupitia simu ya mkononi namba 07643310**  aliwasiliana kwa simu na Ludovick Joseph kupitia simu namba 07539271**  akiwa Tamal hotel,Mwenge jijini dar-Es Salaam. Hii ilikua siku moja kabla ya mkanda wa video uliowekwa youtube kurekodiwa.mkanda ulionyesha kuwa ulirekodiwa kesho yake yaani tarehe 28/12/2013

MWANAMKE MPUMBAVU HUIVUNJA NDOA YAKE MWENYEWE NA SERIKALI PUMBAVU HUBOMOA NCHI"... MH. SUGU

Wakati akichangia bajeti ya PM, Mh Mbilinyi ametumia lugha kali sana dhini ya serikali na Mwigulu Nchemba akazua ubishi mkubwa kati yake na Speaker..
Ameanza kwa kusema kuwa "Mwanamke mpumbavu huvunja nyumba yake mwenyewe" na hivyo hivyo serikali pumbavu hubomoa nchi.
Akiwa  na  jaziba  nyingi, Joseph Mbilinyi 'sugu' amemchanachana Mwigulu kuwa ni mpumbavu na kudai  kuwa anafanya dili alafu anatumia m-pesa...
Baada  ya  kumvaa  Mwigulu, Sugu  alimgeukia waziri wa elimu Mulugo na  kudai  kuwa ana elimu ya kuungaunga na ni chenga tupu...
Sugu  anadai  kushangazwa  na  tabia  ya  usalama  wa  taifa  kuifuatilia Chadema na kung'oa watu kucha na meno.
Pamoja na kukalishwa mara mbili na spika ili atumie lugha ya staha bado aliendelea

FASTJET YAKANUSHA KUNYANG'ANYWA LESENI YAKE YA BIASHARA TANZANIA

 Kampuni ya ndege ya Fast Jet imezikanusha ripoti kuwa imenyang’anywa leseni yake ya biashara katika nchi kadhaa barani Afrika ikiwemo Tanzania.Kupitia website yake kampuni hiyo imeandika:

Licha ya taarifa za leo kwenye vyombo vya habari, ni biashara kama kawaida hapa fastjet. Madai kuhusu kunyang’anywa leseni ni uongo mtupu. Tunaendelea na safari zetu kutoka Tanzania na tunaendelea kuanzisha safari mpya kama ilivyopangwa.

Hii ni njama/hujuma ‘binafsi’ dhidi ya fstjet katika jaribio wazi lililotengenezwa kuharibu brand na sifa ya Fastjet.Ofisi zetu na matawi yetu bado zipo wazi kwa booking mpya na hakuna refund zozote.

NAULI MPYA NCHINI SASA NI VURUGU TUPU

Viwango vipya vya nauli za daladala na mabasi yaendayo mikoani zimeanza kutumika jana, huku wananchi wakizipinga wakidai zinawaumiza zaidi kiuchumi.

Wakati baadhi wakilalamikia kupanda kwa nauli za dalala katika maeneo yao, baadhi ya wafanyakazi wa mabasi yaendayo mikoani wameendelea kutoza nauli ya zamani.

Zoezi la kupandisha nauli nchini lililoanza jana limewagawanya wamiliki wa magari na kufanya baadhi ya safari za mikoani kupandisha nauli, huku nyingine zikiendelea kuwa kama zamani wakati nauli za daladala Dar es salaam zikipanda kama ilivyoagizwa.

Hatua hiyo ya kupandisha nauli ilizua tafrani baina ya makondakta na abiria waliokuwa wakisafiri katika safari mbalimbali ndani ya jiji, hususan wale waliokuwa hawajui kuwa jana ndiyo siku ambapo nauli zilitakiwa kupanda.

KITENDO CHA KUWANYANG'ANYA ARDHI WANANCHI WA LOLIONDO CHAMCHANGANYA RAIS KIKWETE

Sakata la mgogoro unaorindima kwa sasa kuhusu unyang'anywaji wa Ardhi ya Loliondo kwa lengo la kumpa mwekezaji wa kiarabu umemvuruga sana Rais Kikwete na kusita kujitokeza hadharani kulitolea kauli.

Hapo awali Kupitia kikao cha baraza la mawaziri iliamriwa kuwa WAKAZI WA LOLIONDO WANYANG'ANYWE ENEO HILO na kumtuma Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kagasheki kwenda kulisimamia kwa nguvu zote....

HUU NDO UFISADI MKUBWA WA JOHN CHEYO CHINI YA "KOFIA YA BUNGE"

 John Momose Cheyo mwanasiasa wa siku nyingi ametumia cheo chake cha Uenyekiti wa Kamati ya PAC, kujinufaisha kupitia kampuni ya mdogo wake anayejulikana kwa jina la Sylvester Maghembe Cheyo ambaye anamiliki kampuni inayoitwa ATLAS PLUMBERS AND BUILDERS LTD.

Kwa kipindi ambacho Mheshimiwa Cheyo amekuwa Mwenyekiti wa Kamati hii ya Bunge kampuni ya ATLAS Plumbers amd Builders imepata miradi ifuatayo katika mashirika ya Serikali ambayo yapo chini ya Kamati iliyokuwa inaoongozwa na Bwana Mapesa.

Magazeti ya leo Ijumaa ya 13th April 2013



Friday, April 12, 2013

Magazeti ya leo Ijumaa ya 12th April 2013

             


RIPOTI KUHUSU WATOTO WA NELSON MANDELA KUGOMBANIA MALI

 Zenani ndio huyu wa nyumba ya Mzee Mandela, hawa wengine ni wajukuu na vitukuu wa Mandela.

 BBC wameandika kwamba watoto wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela Makaziwe na Zenani Mandela, wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi watatu kutoka katika makampuni anayoyamiliki  wakidai kuwa watatu hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola milioni 1.1

Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94 ambae aliondoka hospitali baada ya kutibiwa mapafu akiwa tayari kalazwa hospitali mara nne katika kipindi cha miaka miwili.

WEMA WEPETU AMFIKISHA POLISI MAMA YAKE BAADA YA KUMFANYIA VURUGU NYUMBANI

 NI kivumbi! Kuna madai kwamba, staa wa Bongo asiyechuja, Wema Sepetu amemfikisha mama yake, Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani mbalimbali...

Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.

Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.

“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,” kilisema chanzo.

Haikujulikana mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.

Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.

TATIZO LA ELIMU TANZANIA SIYO VIBOKO.....BORESHENI MIUNDO MBINU KWANZA BADALA YA KUFIKIRIA KUTEMBEZA VIBOKO

 Taifa liko katika wakati mgumu juu mustakabali wa sekta ya elimu kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili.  Kuna mengi yanazungumzwa, yamependekezwa na mengine bado yanaendelea kutolewa juu ya njia sahihi ya kukoa elimu ya watu wa taifa hili.

Kuna hoja zinatolewa kwamba sekta ya elimu imeachwa kuporomoka hadi kufikia hali mbaya ya sasa kutokana na kuminywa kwa bajeti ya sekta hiyo, matokeo yake ni janga la kufeli kwa wananfunzi wengi katika mitihani yao kama ilivyodhihirika kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza elimu ya sekondari mwaka jana kwa zaidi ya asilimia 60 kupata daraja sifuri.

HAKUNA SHERIA INAYOMLAZIMISHA MTU KUPIMA UKIMWI ILI AFUNGE NDOA AU APATIWE AJIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdul habib Fereji

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema suala la kupima Ukimwi ni la hiari kwa hivyo hakuna mwananchi wala mgeni atakayelazimishwa kufanya hivyo endapo akitaka kufunga ndoa au akipatiwa ajira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdul habib Fereji aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe ( CUF) Salim Abdalla Hamad aliyetaka kujuwa kwa nini Serikali isipime afya za wananchi kwa lazima kujuwa kama wapo salama na ugonjwa wa Ukimwi.Fereji alisema Zazibar hakuna sheria inayoilazimisha Serikali kuwapima wananchi afya zao kwa lazima kuhusu ugonjwa wa Ukimwi na kwa kuwa hilo ni suali la mtu binafsi serikali yake ni kutoa elimu na kuwahamasisha wapime afya zao lakini sio kuwalazimisha.

Thursday, April 11, 2013

Ajali Yauwa Waandishi wa Habari, Ofisa Uhamiaji Handeni

                         Marehemu, Hussein Semdoe wa Mwandishi Gazeti la Mwananchi, Handeni.

WAANDISHI wa habari wawili pamoja na Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Handeni wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo majira ya saa nne asubuhi nje kidogo ya Mji wa Handeni. Waliofariki dunia ni Hussein Semdoe wa mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Hamis Bwanga wa Radio Uhuru na Abood pamoja na Mariam Hassan ambaye ni Ofisa Uhamiaji Wilaya ya Handeni.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo pamoja na vifo vya marehemu hao. Akizungumza na www.thehabari.com mchana huu, Mkuu wa Wilaya hiyo alisema ajali hiyo imetokea wakiwa kwenye msafara kuelekea Ndolwa kupanda miti.

Akifafanua zaidi juu ya ajali hiyo, Muhingo alisema gari lililopata ajali ni la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni, STJ 4673 ambalo ndilo lililokuwa likitumiwa na Ofisa Uhamiaji, Hassan pamoja na wanahabari hao.

JK mourns Thatcher

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete signs a condolence book at British High Commissioner's Office in Dar es Salaam following the death of former British Prime Minister Margareth Thatcher who died of stroke on Monday at the age of 87

NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATANGAZA KUWASHITAKI WANAODAI KUWA "AMEGUSHI VYETI"

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema atawafikisha mahakamani watu wanaodai kuwa ameghushi vyeti vya elimu ya sekondari.  Mulugo alisema amechoshwa na kashfa hizo zinazosambazwa na baadhi ya watu atawafikisha mahakamani endapo wataendelea kumdhalilisha.

Mulugo alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO0) jijini Mbeya.

“Wanasema eti nimeghushi vyeti, mara ooh sijui natumia jina la mtu. Nimechoshwa na maneno haya… ni kweli nimerudia darasa kama walivyorudia watu wengine, kwa nini iwe tatizo kwangu. Hata hapa tulipo wapo wengi tu waliorudia darasa.

“Kama kweli ningekuwa nimeghushi vyeti hivi leo ningekuwa naibu waziri wa elimu? Sasa nimechoshwa, nitawachukulia hatua watu hawa, siwezi kusema ni lini nitafanya hivyo ila nitakapoamua nitaanza,”alisema.