Saturday, January 5, 2013

Leo Chadema Wawakumbuka waliopoteza Maisha katika vurugu zilizotokea 5/1/2011 Arusha.

Kwa wakazi wa Arusha na vitongoji vyake, Leo kutakuwa na mkutano mkubwa wa kuwakumbuka ndg zetu(Denis na Ismail) walio pigwa risasi na jeshi la polisi 5.1.2011, mkutano huu utafanyika kwenye uwanja wa Ngarenaro shule ya msingi kuanzia saa tisa, vile vile utarusha na kituo cha redio ya sunrise (94.80 FM) kwa wakazi wa Arusha na mikoa jirani.






Hizi ni baadhi ya picha wakati wa kuwaaga makamanda wetu waliopoteza maisha 5.01.2011. R.I.P (Denis na Ismail)

Friday, January 4, 2013

INASIKITISHA BALI TUNASEMA WAPUMZIKE KWA AMANI.

         
 AJUAYE uchungu wa mtoto ni mzazi! Ukiwatazama akina mama watatu wa wasanii wa Tanzania waliofariki dunia kwa nyakati na sababu tofauti hivi karibuni wakilia kwa uchungu, unaweza ukadhani wazazi hao ni ndugu kwa namna nyuso zao zinavyoonekana kuwa na majonzi mazito,

Risasi Jumamosi linakuchambulia.

Makabrasha ya gazeti hili yanawaonesha mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, mama wa marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’, Zaina Mkiety na mama wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Zaituni Mzena wakilia kwa uchungu.
Wazazi hao walionekana wenye majonzi kupita maelezo kwani kila mmoja alimbeba mwanaye tumboni kwa miezi tisa, akamlea, akamtunza kwa tabu hadi akakua lakini baada ya kuanza kufaidi matunda yao tu, Mungu akawachukua.

SHELUKINDO : Namuunga mkono lowassa 2015

MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo ametangaza kuchukua kile alichokiita uamuzi mgumu ili kuhakikisha kuwa Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa anamrithi Rais Jakaya Kikwete katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.Shelukindo alitoa kauli hiyo Jumapili wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa kuchangia ujenzi wa Hosteli ya KKKT katika sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa ambazo pia zilihudhuriwa na makada kadhaa wa CCM.

Jana alipoulizwa kuhusu kauli hiyo, Shelukindo alisema: “Ni kweli mimi ni muumini wa Lowassa, ila pale (mkutanoni) sikumtaja kwa sababu najua chama kina taratibu zake na muda wa mchakato wa kumpata Rais haujafika.”

SERENGETI FREIGHT YATOA PONGEZI KWA BODI YA UTALII TANZANIA


BAADHI YA PICHA ZA MKUTANO WA CHADEMA IRINGA


TEKELEZENI AHADI MLIZOZITOA WAKATI WA KUOMBA KURA-OLE NANGOLE

 MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha(CCM)Bw Onesmo Ole Nangole amewataka Viongozi mbalimbali wa chama hasa wale ambao walitoa ahadi  kwa wananchi kwenye uombaji wa kura kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi hizo kwa haraka sana kwani wale ambao hawatekelezi ahadi wanachangia sana chama hicho kuelekezewa lawama

 Bw. Nangole aliyasema hayo Juzi wakati akifungua Kata mpya ya Chama hicho ambayo kwa sasa inajulikana kama Kata ya Majengo iliopo Meru Mkoani Arusha.

 Aidha Bw Nangole alisema kuwa tabia ya baadhi ya Viongozi ya kuwa watoa ahadi hasa nyakati za kura na kisha wakishapata kura wanasahau ahadi zao inachangia sana kuunguza Ccm kwenye jamii na kuonekana kuwa ni watoaji ahadi zisizotekelezwa.

 Alisema kuwa Viongozi wote ambao walitoa ahadi mbalimbali kwa wananchi hasa katika Nyakati za Kura wanatakiwa kuhakikisha kuwa watekeleza ahadi zao na kujijengea tabia ya kuwaangalia wapiga kura wao ili kuendelea kulinda uhai wa Chama

 Mbali na hayo aliongeza kuwa Viongozi mbalimbali wa Chama hicho wanatakiwa kuangalia zaidi ilani ya chama hicho kwa kuhakikisha kuwa wanaainisha matatizo ambayo yapo kwenye jamii na kisha kuyatatua kuanzia kwenye Ngazi za Vitongoji na Vijiji.

 Katika hatua nyingine Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Meru Bw Langaeli Akyoo alisema kuwa bado Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa zitatuliwe kwa haraka sana ingawaje umoja na ushirikiano unaitajika kwa haraka sana

TANAPA WAONGEZA MUDA WA KUWASILISHA KAZI ZA KUSHINDANIWA



Kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza na kuibuliwa na wadau wa habari nchini kuhusiana na siku ya mwisho ya kuwasilisha kazi za kushindaniwa, Waandaaji wa TANAPA Media Awards 2012 wamesogeza mbele tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kazi hizo kutoka 31.12.2012 na kuwa tarehe ya mwisho sasa itakuwa 31.01.2013.

WASHIRIKI:

Tuzo hizi ziko wazi kwa wanahabari wote nchini kutoka katika Magazeti, Redio na Runinga. Ili uweze kutimiza sifa za ushiriki wako katika tuzo za TANAPA Media Awards 2012, unatakiwa kuwasilisha kazi zote zilizochapwa na kutangazwa katika kipindi cha kuanzia tarehe 01 Januari, 2012 hadi 31 Disemba, 2012.

JINSI YA KUSHIRIKI

Wanahabari wanaweza kushiriki kwa kutuma kazi zao kwa kiwango cha juu cha kazi tatu kwa kila kundi. Wanahabari watakaoshiriki tuzo hizi watapaswa kujaza fomu maalum za ushiriki zinazopatikana katika tovuti ya shirika www.tanzaniaparks.com

MAKUNDI

A     Tuzo ya Utalii wa Ndani katika Hifadhi za Taifa     Redio                 (washindani watatu)
Runinga             (washindani watatu)
Magazeti            (washindani watatu)
B     Tuzo ya Uhifadhi katika Hifadhi za Taifa     Redio                 (washindani watatu)
Runinga             (washindani watatu)
Magazeti            (washindani watatu)

Kazi zinaweza kuwasilishwa katika lugha ya kiingereza au Kiswahili. Tuzo: Washindi kwa kila kundi watapata tuzo zifuatazo:

Mshindi wa Kwanza    

Fedha taslimu Sh. 1,500,000, Ngao, Cheti na Safari ya mafunzo katika moja ya nchi za SADC
Mshindi wa Pili    

Fedha taslimu Sh.1,000,000, Ngao na Cheti
Mshindi wa Tatu    

Fedha taslimu Sh.500,000 na Cheti

Mwisho wa kuwasilisha

Kazi zote zinatakiwa kuwa zimewasilishwa Makao Makuu ya TANAPA hadi kufikia tarehe 31.01.2013.

Anuani ya kuwasilisha kazi:

Mkurugenzi Mkuu

Hifadhi za Taifa Tanzania

AIONE: Meneja Uhusiano- TANAPA Media Awards 2012

SL.P. 3134

Arusha, Tanzania

Au, ziletwe kwa mkono Makao Makuu ya TANAPA, Barabara ya Dodoma, Chumba Namba.32.

Au barua pepe:        prm@tanzaniaparks.comImetolewa na

Pascal Shelutete

MENEJA UHUSIANO

HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA

04.01.2013

RAIS KIKWETE AONANA NA MSHAURI WA KIJESHI WA UMOJA WA MATAIFA IKULU DAR ES SALAAM LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto ni  Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania  Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.


(PICHA NA IKULU)

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete waenda kutoa pole nyumbani kwao Sajuki

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo ambako walienda kutoa pole leo Januari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.
(PICHA NA IKULU)

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUMZIKA JUMA KILOWOKO 'SAJUKI' JIJINI DAR LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' leo.
                  Baba mzazi wa Sajuki, Mzee Kilowoko, akiweka udongo katika kaburi la mwanaye
                                                                   Mazishi ya Sajuki yakiendelea.


                                                   Umati wa watu waliohudhuria mazishi hayo.

MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam leo wamejitokeza katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kumpumzisha mpendwa wao Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' aliyefariki dunia alfajiri ya Januari 2, mwaka huu (Jumatano) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Miongoni mwa waliomzika Sajuki ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete

HAPA NDIPO ALIPOZIKWA MAREHEMU SAJUKI.


















MAJONZI, VILIO VYATAWALA WAKATI MWILI WA SAJUKI UKIOMBEWA NYUMBANI KWAKE TABATA JIJINI DAR

                                   Mwili wa Sajuki ukipelekwa uwanjani kwa ajili ya kuswaliwa na masheikh.

  Mwili wa Juma Kilowoko 'Sajuki' ukiswaliwa nyumbani kwake Tabata-Bima jijini Dar es Salaam leo kabla ya kwenda kuzikwa.
                                                              Vilio vikitawala msibani hapo.







                    Mama mzazi wa Sajuki akilia kwa uchungu wakati mwili wa mwanaye ukiswaliwa.





(PICHA: GLADNESS MALLYA NA HAMIDA HASSAN / GPL)