Wednesday, April 3, 2013

KAJALA MASANJA AJICHORA TATTOO YA WEMA SEPETU MGONGONI KAMA ISHARA YA KUMSHUKURU KWA ZILE MILIONI 13

Kajala ameamua kuchora Tattoo yenye jina la WEMA mgongoni mwake  baada ya kutolewa faini ya Shilingi Milioni 13 na msanii mwenzake Wema Sepetu,

hii ikiwa kama ishara ya shukrani kwa rafiki yake kipenzi Wema Sepetu.

WAZIRI MKUU AHUDHURIA MISA YA PAMOJA JIJINI ARUSHA YA KUAGA MAREHEMU WALIOFUKIWA NA KIFUSI

                                       Sehemu ya majeneza ya marehemu katika ibada hiyo maalumu leo

 Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha. Maporomoko hayo yametokea jana na kusababisha vifo vya watu13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru

LADY JAYDEE AAMUA KUFUNGUA KITUO CHAKE CHA REDIO BAADA YA KUCHOSHWA NA MANYANYASO YA CLOUDS FM

Hatimaye tumepata jibu la kwanini Judith Mbibo aka Lady Jaydee amekuwa akitweet vitu vizito weekend iliyopita. Kama hukufaniwa kuziona tweets hizo ni kwamba mwanadada huyo alishusha mfululizo wa mabomu kuelekea kwa kituo kimoja cha radio na kujikuta akiongeza aka mpya, Anaconda.

Na sasa imebainikiwa kuwa mwanamuziki huyo mkongwe na mjasiriamali anakuja na kituo chake cha radio kiitwacho Kwanza FM. Habari hiyo aliibreak mwenyewe jana na bila shaka haihusiani na April’s Fools Day.

    Kwanza FM coming soon. Yangu mwenyewee

Monday, April 1, 2013

WALIOFUKIWA NA KIFUSI KWENYE MGODI WA MORRUM JIJINI ARUSHA YAFIKIA 20

WATU zaidi ya 20 wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi wakati wakichimba  mchanga aina ya Moramu katika machimbo  yaliyopo Moshono nje kidogo ya jiji la Arusha.

Tukio hilo ambalo limegubikwa na simanzi na vilio kwa ndugu jamaa na wananchi, limetokea leo majira ya saa 5 asubuhi wakati marehemu hao wakichimba na kupakia Moramu hiyo kwenye magari .

Pamoja na vifo hivyo magari mawili aina ya Fuso na Scania yameharibiwa vibaya baada ya kufukiwa na kifusi kilichoporomoka umbali unaofikia mita 50 kutoka usawa wa bahari.

Tayari kikosi cha uokoaji ambao ni  Jeshi la Wananchi Kambi ya Tanganyika Parkers kimefanikiwa kuopoa miili ya marehemu 16 waliofukiwa.

Baadhi ya miili ya marehemu  imetambulika kwa majina kuwa ni  Alex Maliaki, Gerald Hamis, Sauli Rafael (Mbu), Barick Loselian, Kababuu Lowasale, Mwenda Kibobori, Japhet Mjivaine na Garald Masai.

Taarifa za mashuhuda zimebainisha kwamba chanzo cha kuporomoka kwa kufusi hicho ni mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Arusha zilizosababisha kukatika kwa Ngema baada ya kuzidiwa na maji ya mvua.


KIJIJI CHA MISUKULE FEKI CHAFICHULIWA BAGAMOYO, WACHUNGAJI FEKI WADAIWA KUWATUMIA ILI KUWAHADAA WAUMINI WAO

 INATISHA na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo  mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi  wa dini kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.

Uchunguzi umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini kuteua kijiji hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni kuwalaghai waumini kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na kuchukuliwa kimazingara.

Uchunguzi  zaidi umebaini kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.

BREAKING NEWS: ZAIDI YA WATU 18 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI KATIKA MACHIMBO YA MORRUM HUKO ARUSHA

                                         Wananchi wa eneo hilo wakiwa na simanzi baada ya ajali hiyo.
                                                 Mwili wa mmojawapo wa marehemu.
                                                         Majeruhi aliyeokolewa.
Watu zaidi ya 18 wanahofiwa kuwa wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi wakiwa ndani ya mgodi wa Morrum huko Moshono jijini Arusha.

Kwa sasa wanajeshi wanaendelea na zoezi la uokoaji na tayari majeruhi mmoja ameokolewa na miili ya watu watatu.

Tukio hili linatokea ikiwa ni siku siku tatu baada ya maafa mengine kutokea jijini Dar es Salaam ambapo watu zaidi ya 30 wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka.

Magazeti ya leo Jumanne ya 2April 2013




JACK WOLPER AJIPANGA KUMUENZI KANUMBA

STAA wa  Bongo Movies, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa anatarajia kumuenzi marehemu kwa kuachia vipande vya filamu ya After Death ambayo ni mwendelezo wa filamu ambayo ilichezwa na marehemu Steven Kanumba, Uncle JJ.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Wolper alibainisha kuwa anatarajia kuonesha vipande vya filamu hiyo katika siku ya Kumbukumbu ya Kanumba itakayofanyika Aprili 7, mwaka huu katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar.

 “Ni filamu ambayo nimeiandaa katika mazingira maalum kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba ambaye kila Mtanzania anatambua mchango wake kwenye sanaa,” alisema Wolper.

HIZI NDO PICHA ZA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI- ZANZIBAR

  Hapo ndio tujue kuwa wenzetu hawabahatishi na hawana siasa kwenye kazi zao proffessional....kazi kweli kweli!!wamehadithiwa tu wamemchora mtu yule yule!!Angalia Mchoro wa Polisi Hapo chini na Ufananishe na mtu Huyu..

LADY JAYDEE ADAI KUWA CLOUDS FM NI WANAFIKI....WANATAKA WAHONGWE ILI WAPIGE NYIMBO ZA WASANII

                                                                    Lady Jay Dee
East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter leo kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.

"Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. #JotoHasira"

"MI NAJITUMA KWA BIDII..Q-CHIEF ANAKAA NA KUVUTA BANGI HALAFU ANADAI NATUMIA NYOTA YAKE....NAOMBA ANIKOME"...DIAMOND

Hii  ni  kauli  ya  msanii Diamond kuhusu Q chief: mi nafanya kazi, mazoezi na dancers, nahangaika kutafuta sare, kuandika nyimbo nzuri, wakati nafanya yote hayo we unakula unga, halafu unakuja kusema nasafiria nyota yako, nisafirie nyota ya mla unga? mi staki, staki, agombane na wakubwa wenzake kina dully mi aniache na wadogo wenzangu staki...?

MIILI YA WATU ILIYOPATIKANA KWENYE GHOROFA LILILOANGUKA DAR IMEFIKIA 21 MPAKA SASA

 Miili ya watu iliyoopolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo lenye ghorofa 16 lililoanguka jana katikati ya jiji la Dar es Salaam, imefikia 21.

MAHAKAMA YASEMA Uchaguzi Kenya ulikuwa huru na wa haki

                                  Willy Mutunga rais wa mahakama ya juu zaidi Kenya
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki.
Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane.

Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia ya huru na wazi na kuwa Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.

Saturday, March 30, 2013

Kwaya ya Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali Rwanda kutua Dar es salaam


KUNDI la muziki wa kiroho la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda linatarajia kutua Dar es Salaam leo (Jumamosi) kwa ajili ya Tamasha la Pasaka kesho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa kundi hilo pamoja na mambo mengine litazindua albamu yao iitwayo Kaeni Macho katika tamasha hilo litakalofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Tayari mambo yetu yanaenda vizuri na Kwetu Pazuri watawasili Jumamosi wakiwa wamepania kufanya mambo makubwa kwenye tamasha letu,” alisema Msama na kuzitaja nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo kuwa ni Kaeni Macho, Mungu Wangu, Tugireurukundo, Ewe Ndugu, Tuombeane, Umwamini Yesu, Msalaba, Twawona, Okuswala na Huruma.

Alisema kundi hilo limefurahi sana kuja hapa Tanzania na ndiyo sababu wakaipa heshima Tanzania kuzindua albamu yao wakiwa na imani mashabiki wataipenda na kwamba hivi sasa wanatamba na albamu ya Mtegemee Yesu na wamemhakikishia watang’arisha tamasha la mwaka huu.

Alibamu yao hiyo ina nyimbo nane ambazo ni JY’ Ushima Uwite, Mtegemee Yesu, Ndifuza Kugerayo, Iyana Iby’ Isi, Yesu Niwe Mungeri, Parapanda, Abasaruzi na Nenda.

Licha ya kundi hilo, wasanii wengine wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza tamasha hilo ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.

Wasanii wa Tanzania waliothibitisha hadi sasa ni Rose Muhando, Upendo Nkone,  Bonny Mwaitege, Upendo Kilahiro, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam kesho na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Magazeti ya leo Jumamosi ya 30th March 2013