Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Viongozi na Waumini wa Kanisa
Katoliki la Olasiti Jijini Arusha May 7,2013 alikokwenda kutoa pole
kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo
May 5,2013 na kusababisha vifo na majeruhi.
Paroko wa Kanisa Katoliki la Olasiti la Arusha Peddy Castelino akiomba
wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipotembelea kanisa hilo May 7,2013
kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea
kanisani hapo May 6,2013 na kusabisha vifo na majeruhi.
Tuesday, May 7, 2013
VICTOR AMBROSE NDIYE ALIRUSHA BOMU KANISANI...
DEREVA wa pikipiki maarufu kama bodaboda, Victor Ambrose, anatuhumiwa kurusha bomu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti jijini Arusha, lililosababisha vifo vya watu wawili na wengine karibu 70 kujeruhiwa.
Ambrose mwenye umri wa miaka 20 na mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha, anashikiliwa pamoja na watuhumiwa wengine tisa, wakiwemo raia wanne wa Saudi Arabia kwa mahojiano zaidi ya kuhusika na tukio hilo.
Taarifa zilizopatikana jana jioni, zilieleza kuwa raia hao wa Saudi Arabia, waliingia nchini Jumamosi usiku kwa ndege kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na baada ya tukio Jumapili, waliondoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga.
Serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, ilitoa taarifa hiyo jana bungeni na kueleza namna uhalifu huo ulivyotendeka kanisani hapo juzi, muda mfupi baada ya ibada kuanza.
Kwa mujibu wa Waziri Nchimbi, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mlipuko huo ni bomu. Hata hivyo uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika, unaendelea kufanywa na Polisi na wataalamu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
“Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi. Miongoni mwao ni Victor Ambrose mwenye umri wa miaka 20 dereva wa bodaboda...ambaye anatuhumiwa kurusha bomu hilo. “Watuhumiwa wengine watano waliokamatwa ni raia wa kigeni na Mtanzania mmoja ambao wanashikiliwa kwa mahojiano,” alisema Dk Nchimbi.

Monday, May 6, 2013
Rais Jakaya Kikwete Atuma Rambirambi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha. Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa. Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake.
Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikalina vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili. Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma. Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu. Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake. Rais anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.
Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.
Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuliyao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
5 Mei, 2013

DKt. BILAL AWAFARIJI MAJERUHI WA BOMU, ARUSHA
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akiwafariji majeruhi wa mlipuko huo.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal akiwafariji majeruhiwa milipuko ya bomu jijini Arusha, kulia ni Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Dkt. Alex Malasusa na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene
Makamu wa Rais Dkt. Bilal akimsikiliza Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania Askofu Dkt. Alex Malasusa
Majeruhi wa mlipuko huo wakihangaika
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal Pamoja na Mh.Stephen Masele pichani chini na chini wakiwapa pole majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea majira ya saa 4;35 asubuhi kwenye uzinduzi wa kanisa la St.Joseph Mfanyakazi maeneo ya Olasiti jijini Arusha

JANUARY MAKAMBA NAYE AWAPONDA CLOUDS FM KWA VITISHO VYAO VYA KUGOMA KUPIGA "BONGO FLEVA " LEO
Huenda mjadala kuhusu uamuzi wa kituo cha radio cha Clouds FM, leo kutopiga Bongo Flava siku nzima haujalikuna sikio la naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Kupitia Twitter, Makamba ameandika kuwa Tanzania ina matatizo matatizo mengi ya kujadili kuliko nyimbo za kuchagua kucheza redioni. “We’ve got much bigger problems than radio playlists, ” ametweet.
Katika mahojiano maalum leo kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alidai kuwa ametoa amri leo kituo chake kisicheze Bongo Flava.
Uamuzi huo leo umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

RAIS KIKWETE AKATIZA ZIARA YAKE NCHINI KUWAIT.....ANARUDI NCHINI KUJUMUIKA NA WAHANGA WA BOMU LA JANA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.
Rais Kikwete alikuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, amekatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.
Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo la Ahmadi mjini Kuwait.
Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.

CLOUDS WAMJIBU LADY JAYDEE....WAMEDAI KUWA AACHE KUTAPATAPA NA BADALA YAKE AKAZE BUTI
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hatimaye mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameamua kujibu shutuma za Lady Jaydee dhidi yake. Ruge amekitumia kipindi cha Power Break Fast cha Clouds FM, kujibu rasmi shutuma hizo.
Amesema anasikitishwa na jinsi Jaydee anavyoendesha harakati zake na kudai kuwa anapigana kwenye vita isiyo sahihi.
“Jaydee akaze buti, anapigana na wrong war, vita yake ameidirect tofauti na mizinga yake, bunduki zake amezielekeza kusiko. Skylight Band inamsumbua, akubaliane na ukweli kwamba Skylight ndio iliyoisababishia Nyumbani Lounge kushuka ilivyoshuka, sio Lady Jaydee kama msanii.
Vita yake na bunduki zake azielekezee Skylight Band. Hajazungumza hata mara moja kwamba ndio kitu kinachosumbua. Mimi naamini kabisa akifanya hiyo kazi, Jaydee bado ni msanii mzuri, ana nguvu, afanye kazi kubwa ya kuweza kurudisha mapambano yake kisanii, kufanya kazi na aangalie tatizo lililotokea Nyumbani Lounge labda anaweza akatatua matatizo lakini sio kushambulia watu kwenye mitandao,” amesema Ruge.

MWANAMKE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR
Majambazi yamempora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi na kutokomea kusikojulikana....
Tukio hilo limetokea leo saa 5:16 jioni na inavyosemekana ni kuwa mwanamke huyo alikuwa akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia..
Alipotoka ,majambazi hayo yalimfuata na kuligonga gari lake makusudi na ndipo dada huyo aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa. ..

MAAGIZO ALIYOYATOA RAIS KIKWETE KUHUSU SHAMBULIO LA KIGAIDI LILILOFANYIKA HUKO ARUSHA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha. Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa.
Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake.
Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili.

RPC- ARUSHA ATHIBITISHA KUWA KILICHOLIPUA KANISA NI BOMU....WATU 3 WANAHALI MBAYA, 50 WAMEJERUHIWA
Mkuu wa Mkoa Mulongo naye amefika eneo la tukio na kuwafariji wahanga wa tukio la bomu....
RPC wa mkoa wa Arusha naye aliambatana na mkuu wa mkoa na muda huu alikuwa anatoa nasaha zake kwa wananchi....
RPC ameeleza kuwa tukio hili ni la kigaidi. Katika maelezo yake, RPC amesema kuwa aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu. ...
Amesema Polisi wanawasaka waliohusika na unyama huu na ameomba yeyote mwenye taarifa yoyote aisaide polisi. ..
Waliojeruhiwa ni 50 .Hao wana majeraha ya kawaida na 3 wako mahututi
Mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA
Saturday, May 4, 2013
MWANAFUNZI WA CHUO CHA IFM -DAR AFARIKI DUNIA KWA KULISHWA SUMU NA MKE WA MTU.....
Habari zilizotufikia toka IFM- Dar es salaam ni kwamba mwanafunzi mmoja ambaye bado hatujafanikiwa kulipata jina lake amefariki dunia kwa kulishwa sumu katika chakula alicholetewa na mpenzi wake ambaye ni mke wa mtu......
Taarifa zaidi zinadai kwamba Mwanafunzi huyo alikuwa na uhusiano wa karibu sana na mke wa mtu ambaye mbali na starehe za kimapenzi alikuwa pia anampekea chakula cha jioni
Baada ya mchezo huo kudumu kwa muda, mume wa mwanamke aliusoma mchezo mzima na kuandaa tego la kuwaangamiza wote....

Subscribe to:
Posts (Atom)