Tuesday, June 25, 2013

Jeshi la Polisi limemjibu Joyce Kiria Je Majibu haya ni sawa kwa mama Huyu?

 Joyce Kiria akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo alidai hajui mume wake yuko wapi?
Inasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai. Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu (Imetolewa na Advera Senso Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania)

Mume wa Joyce Kiria Henry Kilewo akiwa ndani ya pingu na vijana wengine kwa tuhuma za ugaidi

  Bw.Henry Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza
 Ulinzi katika Mahakama hiyo uliimarishwa ipasavyo.
 Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.
Kamanda Henry Kileo ndani ya pingu akiwa ndani ya gari pamoja na wtuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013.

Inaumiza kiukweli msikia Joyce kiria alichoandika katika facebook yake

Jana baada ya kufanya hili zoezi na familia yangu namshukuru Mungu Wakili wetu Peter Kibatala alinipigia sim majira ya alasiri akanitaarifu ya kwamba Mume wangu yupo Tabora na yuko salama. isipokuwa amepandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka mawili, UGAIDI na KUM'MWAGIA MTU TINDIKALI....Am speechless familia yangu tunaitaji maombi yenu sana kuliko mnavyofikiria

Monday, June 24, 2013

Magazeti ya leo Jumatatu 24th June 2013







MWIGULU NCHEMBA NA MSIGWA NUSURA WATWANGANE NGUMI BUNGENI

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha.

Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria, baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu.

Wabunge hao wa Chadema hawakuhudhuria kikao chochote cha Bunge kutokana na kwenda mkoani Arusha kwa shughuli mbalimbali, kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wao wa kuhitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika viwanja vya Soweto, Juni 16 jijini humo.

HALI YA MANDELA NI TETE...ASHINDWA KUFUMBUA MACHO KWA SIKU KADHAA

Mzee Nelson Mandela ameendelea kuwa katika hali mbaya hospitalini jana baada ya kubainika kwamba gari la wagonjwa lililombeba Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwenda hospitali limeharibika.

Gari hilo la wagonjwa mahututi liliharibika wiki mbili zilizopita wakati Mandela alipokuwa akikimbizwa kwenye hospitali moja mjini Pretoria, na kumwacha 'njiapanda' kwa dakika 40.

Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alihamishiwa kwenye gari jingine la wagonjwa la hospitali ya kijeshi kumalizia safari iliyobaki ya dakika 50 kati ya Johannesburg na Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic.

Msemaji wa Rais Mac Maharaj alisema: "Tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha kwamba hali ya kiafya ya rais wa zamani Mandela haiathiriki na tukio hilo."

Saturday, June 22, 2013

TANZANIA NCHI BORA KWA SAFARI ZA KITALII AFRIKA

Baadhi ya watalii wakiwa katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kujioea wanyama mbalimbali ikiwemo makundi ya nyumbu wakati yakivuka mto Mara kurejea katika hifadhi hiyo kutoka Maasai Mara.

 NYOTA ya Tanzania katika sekta ya Utalii imeendelea kung’ara zaidi badaa ya hivi karibuni kuchaguliwa kuwa ndio nchi bora kwa watu mbalimbali kuweza kufanya safari za kitalii miongoni mwa nchi barani Afrika.

Kwa mujibu utafiti uliofanywa na kutolewa hivi karibuni na katika mtandao wa Kampuni ya marketplace  kwa ajili ya safari za Africa (marketplace for African safari tour)

Tanzania imepata kura nyingi zaidi ziliyotolewa kama maoni ya  watu kufuatia utafiti huo ambapo Safaribooking .com ilifanya mchanganuo huo kwa kupitia maoni 3061ya zaidi ya watalii na wasafiri waliohusishwa katika utafiti huo na kuhitimisha kuwa katika  nchi zote zilizopendekezwaa barani Africa,Tanzania ni zaidi.

SAKATA ZIMA LA KUPIGWA KWA MBUNGE WA KASULU ( MOSES MACHALI) AKIWA DODOMA JANA JIONI

Habari kutoka Dodoma zinasema Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. Moses Machali (pichani), amelazwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma kuuguza majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jana  jioni  mjini Dodoma.

Tukio hilo lilitokea jana jioni  wakati Mh. Machalli akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita ....

Kitendo hicho  kilionekana kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni ....

Magazeti ya leo Jumamosi 22nd June 2013





Thursday, June 20, 2013

"NASSARI NI MUONGO NA NI MNAFIKI, TUMEMRUHUSU KWA AMANI NA BADALA YAKE KADAI ETI KATOROKA ILI TUSIMUUE"...KAULI YA DAKTARI

 UONGOZI wa hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya Selian jijini Arusha umekanusha vikali taarifa zilizotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema John Mnyika kuwa serikali ilipeleka maafisa wa usalama hospitalini hapo kwa lengo la kumdhuru mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari pamoja na majeruhi wa mabomu waliolazwa katika hospitali hiyo na kusema ni uzushi mtupu.

Mnyika alisema kufuatia kitendo hicho mbunge Nassari alipiga kelele (yowe) akiwa katika korido ya wodi namba 14 aliyokua amelazwa ili kuomba msaada baada ya maafisa hao wa usalama waliokua wamevalia mavazi ya kitabibu na kubeba vifaa vya kitabibu kumtundikia drip aliyohisi ilikua na lengo la kumdhuru ambayo aliitoa na kuitupa.

Wednesday, June 19, 2013

Magazeti ya leo Jumatano 19th June 2013






JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WABUNGE 4 WA CHADEMA KWA KUSABABISHA VURUGU ARUSHA

Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia viongozi wanne wa CHADEMA na watu wengine huku likiendelea kuwatafuta wabunge wawili na watu wengine.

Jeshi la Polisi limesema limewatua nguvuni watu hao kwa makosa ya kuhutubia mkutano haramu wakati wa kuwaaga marehemu waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa bomu uliotokea katika eneo la Soweto jijini humo mwishoni mwa wiki.

Makosa mengine ni wanayotuhumiwa kwayo ni kufunga barabara na kuwashambulia askari polisi.
Amesema wataendelea kubaki korokoroni hadi uchunguzi utakapokamilika.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amewataja Wabunge wanaoshikiliwa ni pamoja na Tundu Lissu na Mustapha Akunai.

Wanaotafutwa ni pamoja na Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambao waliponyoka mikono ya polisi.

NAPE , GODBLESS LEMA NA MBOWE WATAKIWA KUPELEKA ASHAHIDI WAO POLISI, VINGINEVYO SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE

Jeshi la Polisi limetishia kuwakamata Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na limesema litamhoji Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya wanasiasa hao kudai kufahamu watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja aliwataka wanasiasa hao kuwasilisha ushahidi wa kile wanachofahamu kuhusu kulipuliwa kwa bomu hilo.

Juzi, Mbowe akiwa na Lema, alisema wana ushahidi wa picha za video zikiwahusisha polisi na kulipuliwa kwa bomu hilo katika Uwanja wa Soweto wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani kwa Chadema, Jumamosi iliyopita.

Mkwara wa Chagonja
Kamishna Chagonja aliwataka Mbowe na Lema kupeleka ushahidi ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.

VURUGU ZA ARUSHA: CHADEMA YAGOMA KUTOA USHAHIDI POLISI, LEMA AJIFICHA KWA MCHOMA NYAMA ....WAANDISHI WAAMBULIA KICHAPO

Wabunge wanne wa Chadema, Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu) wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na mkusanyiko usio halali kwenye Uwanja wa Soweto jana.

Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jana kwamba pamoja na wabunge hao pia wamewakamata watu wapatao 60 kutokana na vurugu zilizozuka jana baada ya Polisi kuwatawanya kwenye uwanja huo waliokuwa wamekusanyika kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea kwenye uwanja huohuo, Jumamosi iliyopita.

Mbali ya viongozi hao, alisema wanawasaka Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Tuesday, June 18, 2013

Serikali imezuia mazishi ya waliouwawa kwa bomu arusha, polisi wanafukuza watu

Ni simanzi na taharuki kubwa zimetanda katika Jiji la Arusha baada ya Serikali kukataza kusanyiko lolote jambo ambalo limesababisha mazishi ya waliouwawa kwa bomu katika kampeni za udiwani za CHADEMA yasiweze kufanyika maanaa Polisi wanatawanya watu kwa mabomu ya machozi na vipigo.

    Ili kupinga uonevu huu, mabalozi 23 wa CCM huko Arusha wamejitoa katika chama hicho (CCM) na walikuwa watangaze rasmi kujiondoa katika hadhara ya kuaga miili ya marehemu. Jambo hili, kwa kuwa lingekuwa pigo kwa CCM, basi chama hicho pamoja na serikali yake kwa kutumia polisi wamepiga marufuku kusanyiko lolote Arusha.

    Aidha, wananchi wa Arumeru wamefunga barabara na kuanza kuandamana kwenda Arusha Mjini kwa Miguu ili kuupinga uonevu na unyanyasaji dhidi ya wananchi unaofanywa na Serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI.