Friday, July 13, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete Akishiriki kikao Maalumu.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika kikao maalumu cha maandalizi ya mkutano wa Commonwealth Partnership for Technology Management (CPTM) kwenye makao makuu ya CPTM inayojiandaa kwa mkutano wake mkuu wa Global 2012 International Smart Partneship Dialogue unaotarajiwa kufanyika mwezi Mei Mwakani jijini Dar es salaam.

Netherland Kuwekeza Sekta Ya Afya Nchini

Kaimu mgaga mkuu wa serikali Dkt. Donan Mmbando akizungumza na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland  mara baada ya ujumbe huo kuwasili makao makuu ya Wizara ya Afya na Ustawi  wa jamii jana jijini Dar es Salaam.
 Watendaji wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland .

Dr.Slaa,Mbowe Na Lema Wakamatwa

Kwamba wanashikiliwa Central Dar.Tutawaletea habari kamili tutakapokuwa tumejuwa sababu ya wao kukamatwa.labda madai yao kuuawa na kukataa kupeleka madai polisi.

Taarifa Kwa Umma Juu Ya Hali Ya Utendaji Wa Viongozi Wa Bunge

CIVIL AND POLITICAL RIGHTS WATCH
The Citizens’ Parliament watch
Plot 522 Block E, Sinza Palestina, P. O. Box 522, Dar Es Salaam,
Telephone:0784417307,E-mail:ed.civilrights@yahoo.com; marcossy@yahoo.com Dated 18th JUNE, 2012.

TAARIFA KWA UMMA JUU YA HALI YA UTENDAJI WA VIONGOZI WA BUNGE
Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa shughuli za Bunge na mijadala ya Wabunge juu ya mahitaji ya umma kwao kwenye maendeleo, uongozi, kuimarisha utawala bora, uwajibikaji wa serikali na haki za binadamu na kuimarisha usimamizi wao kwa serikali kupitia mijadala yao katika vikao vya Bunge. Taarifa hii inahusika na utendaji wa viongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2011.

Kwa Ujumla:
Kumekuwa na upendeleo wa vyama katika kujadili na kuchangia hoja na kuonekana Mh Spika na Wenyeviti wa vikao kutumia vibaya kanuni za bunge kuwadhibiti wabunge kulingana na vyama vyao. Mfano ni pale Mh Spika alipomzuia Mh Tundu Lissu kumwuliza swali Mh Mizengo Pinda juu ya mauaji ya raia mikononi mwa vyombo vya dola kwa madai kuwa kuna kesi mahakamani juu ya hoja hiyo. Pamoja na Mh Lissu kujitahidi kufafanua tofauti zilizopo kati ya kesi inayomkabili yeye na wenzake na hoja anayoiulizia, bado Mh Spika ameendelea kuizuia hoja hiyo. Kulingana na maoni ya wabunge 36, Watendaji 22, wachambuzi 11 na wananchi 48 waliohojiwa, ubora wa uongozi wa bunge kwa mwaka 2011 ni kama ilivyo hapa chini:


NAFASI JINA SIFA YA KIPIMO ALAMA WASTANI MAONI YA WASHIRIKI
1 NDUGAI,
JOB
YUSTINO USIKIVU KWA WABUNGE 2.5 Amejitahidi sana kukwepa upendeleo wa kisiasa na kuilinda serikali; haoneshi utashi wake kumiliki mamlaka aliyopewa na Kanuni za Bunge anapoongoza vikao.
UZINGATIAJI KANUNI 2.625
UPENDELEO WA KISIASA 2.5625
UZINGATIAJI HOJA 2.375
USHABIKI BUNGENI 3
JUMLA KIWANGO 13.0625
WASTANI 2.6125
2 SIMBACHAWENE, USIKIVU KWA WABUNGE 2.125 Msikivu kwa Wabunge haswa wenye HOJA zenye maslahi kwa Taifa; Amejitahidi sana kukwepa upendeleo wa kisiasa na kuilinda serikali; Anayumbishwa na makundi au siasa.
GEORGE
BONIFACE UZINGATIAJI KANUNI 2.3125
UPENDELEO WA KISIASA 3.28125
UZINGATIAJI HOJA 2.09375
USHABIKI BUNGENI 3.4375
JUMLA KIWANGO 13.25
WASTANI 2.65
3 MAKINDA,
ANNE
SEMAMBA USIKIVU KWA WABUNGE 3.03125 Imara kwenye kanuni na kuzingatia hoja; Anayumbishwa na ushabiki kisiasa; si msikivu kwa wabunge.
UZINGATIAJI KANUNI 2.65625
UPENDELEO WA KISIASA 3.46875
UZINGATIAJI HOJA 2.75
USHABIKI BUNGENI 2.9375
JUMLA KIWANGO 14.84375
WASTANI 2.96875 Anajitahidi sana kuzingatia kanuni; Anayumbishwa na makundi kisiasa; si msikivu kwa wabunge.
4 MHAGAMA,
JENISTER
JOAKIM USIKIVU KWA WABUNGE 3.21875
UZINGATIAJI KANUNI 3.15625
UPENDELEO WA KISIASA 3.5
UZINGATIAJI HOJA 3.53125
USHABIKI BUNGENI 3.3125
JUMLA KIWANGO 16.71875
WASTANI 3.34375
5 MABUMBA,
SILVESTER
MASELE USIKIVU KWA WABUNGE 4.25 Haoneshi ushabiki wa wazi wa kisiasa; hushindwa kuhimili mivuto ya makundi na upendeleo wa kisiasa; Si msikivu kwa wabunge.
UZINGATIAJI KANUNI 4.25
UPENDELEO WA KISIASA 3.78125
UZINGATIAJI HOJA 3.90625
USHABIKI BUNGENI 3.25
JUMLA KIWANGO 19.4375
WASTANI 3.8875

ANGALIZO LA VIWANGO:
1.00 – 1.49 = Uongozi Mzuri Sana,
1.50 – 2.49 = Uongozi Mzuri
2.50 – 3.49 = Uongozi wa Wastani
3.50 – 4.49 = Uongozi Dhaifu
4.50 – 5.0 = Uongozi Dhaifu Sana

Kwa Ujumla
Taarifa hii imeonesha mapungufu kadhaa kwenye uongozi na utendaji wa kazi wa viongozi wa Bunge na hivyo kutoa changamoto kwa viongozi wa Bunge na wabunge kuimarisha utendaji wao iwapo wangependa kutekeleza wajibu wao kwa jamii. Ni matarajio yetu kuwa wabunge watatumia taarifa hii kuimarisha mjadala wa bajeti ya 2012/13 unaoendelea, ikiwa ni pamoja na kendeha na kusimamia vema vikao na mijadala ya Bunge na kutoa changamoto kwa utendaji wa serkali kwa maslahi ya jamii.

Tunakumbusha pia kuwa bado Bunge limeendelea kutumia muda vibaya kwa wabunge kuendeleza vijembe, kebehi, shukrani, pongezi na salamu. Hata baada ya miaka miwili sasa baada ya Uchaguzi na Serikali kuundwa bado wabunge wameendelea kutoa shukrani kwa Rais, wapiga kura wao na wengineo. Matumizi haya ya muda yanapunguza mijadala na mwendelezo wa ushiriki wa wabunge kwa ufasaha.

Mapendekezo
1. Ipo haja ya wabunge kujiangalia kwa karibu uwezo na utayari wao kujadili maswala ya maslahi kwa taifa bila kuingiza ushabiki na maslahi binafsi.
2. Iangaliwe upya akidi ya wabunge katika kupitisha hoja (angalau iwe robo tatu na sio nusu ya wabunge kama ilivyo sasa).Hii iendane na haja kwa Mhe, Spika kujiridhisha bila kuacha shaka juu ya idadi ya kura za wabunge kwenye hoja husika, na haswa walioshiriki mjadala baadala ya kuingia kwa ajili ya kupiga kura tu;
3. Spika atumie mamlaka na kanuni za Bunge ili kudhibiti maudhui, mantiki na maana ya mijadala ya Bunge bila kuathiri maslahi ya taifa. Katika hili Mhe Spika, Naibu na Wenyeviti wa Bunge,wana dhamana ya kuhakikisha ushabiki wa kisiasa haupati nafasi kuvuruga Bunge
4. Tunaona ipo nafasi kubwa kwa Spika kusaidia na kuelekeza bunge ili lifanye kazi zake vizuri zaidi. Spika atumie nafasi hii baadala ya yeye kuangukia kwenye ushabiki na kuilinda serikali.

Imetolewa na Taasisi ya Raia ya Haki za Kisiasa na Mwenendo wa Bunge,

CIVIL AND POLITICAL RIGHTS WATCH
Marcossy Albanie
Mkurugenzi Mtendaji

HAWA NDIO WATOTO WENGINE WA P DIDDY.

                                               Jessie, D’Lila na Chance.
According to blog ya Necole ni kwamba jana ilikua siku ambayo Rapper/Producer wa longtime P DIDDY alipata time ya kuspend na watoto wake mapacha wa miaka mitano baada ya mama yao ambae ni longtime girlfriend wake (Kim Porter) kukubali manake alikua hataki kabisa mapacha wake wakutane hasa na dada yao mwingine aitwae Chance ambae alizaliwa miezi mitano kabla ya mapacha hao lakini kwa mama mwingine ambae ni Sarah Chapman.

P Diddy ni miongoni mwa mastaa wenye watoto wengi lakini ndoa bado haijafungwa, Diddy tayari mpaka sasa ameshapata watoto na wanawake zaidi ya watatu huku November 4 mwaka huu akifikisha umri wa miaka 43.
Pamoja na kwamba ana watoto wengi na kila mmoja ana mama yake, Diddy amevunja rekodi ya kuwa baba anaetimiza mahitaji yote… hataki lawama au mtoto wake kupata tabu anawajibika kila anapohitajika, hii ilikua ni siku nyingine wakati wa birthday ya Chance.

                          PichaYa chini Mama (Sarah Chapman) mtoto na baba.

Huyu wa katikati tena ni mtoto wake mkubwa sasa anaitwa Justine

Thanks Millard Ayo Blog.

MADAKTARI KUANDAMANA TENA?

                              Dr Rodrick Kabangila upande wa kwanza kulia.
Kutokana na kusitishwa kwa ujasili wa madaktari zaidi ya 400 waliokuwepo kazini na wale wa mafunzo kwa vitendo Chama cha Madaktari (MAT) kimesema kimeandaa maandamano ya amani yatakayoshirikisha wanachama wake nchi nzima lengo likiwa ni kudai haki zao.

Katibu mkuu wa MAT Dr Rodrick Kabangila amesema tangu kuanza kwa vuguvugu la mgomo wa Madaktari, mambo mengi  yamekua yakifanywa kinyume na taaluma yao hivyo wameamua kukutana kesho ili kupanga maandamano.

Amesema lengo jingine la maandamano ya amani ni kuiomba serikali kuunda tume huru kufuatilia ishu ya kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka ambae kwa sasa yuko Afrika Kusini akipatiwa matibabu kutokana na huo mkasa pamoja na kupinga dhuluma na uonevu unaoendelea dhidi ya taaluma ya udaktari na madaktari wenyewe.

KAULI YA CHAMA CHA WALIMU KUHUSU KAULI YA NAIBU WAZIRI.

Chama cha walimu Tanzania CWT kimesema kimeshangazwa na kauli iliyotolewa jana bungeni na Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Kassim Majaliwa kwamba chama hicho hakina mgogoro wa kimaslahi na serikali huku akitambua kwamba hiyo ishu iko kwenye majadiliano chini ya tume ya usuluhishi.

Rais wa chama cha walimu Gratian Mukoba amesema hiyo kauli ni ya upotoshaji na ni kulidanganya bunge pamoja na Watanzania na kusisitiza kwamba nchi ya kuendeshwa kwa girba sio hii, kama girba za mwaka  70 zitaendelea kutumika 2012 ni kwamba unaishi na kichwa cha zamani katika ulimwengu mpya.

Amesema ” hizi girba hazitawasaidia kuwapa walimu mshahara, hazitawasaidia waliokata tamaa kurudisha ari ya kazi… kinachotakiwa ni kutafutwa ni ukweli utakaosaidia nchi kwenda mbele”

Kuhusu ishu ya walimu kuingia rasmi kwenye mgomo rais huyo wa Chama cha Walimu amesema hatua hiyo itafikiwa kama majadiliano yanayoendelea sasa hivi kati yao na serikali yatafikia pazuri.

Amesisitiza kwamba “katika mkutano wetu hatukumaliza majadiliano kwa sababu upande wa serikali wameomba siku mpaka tarehe 20 July 2012, ndio tutarudi mezani kuzungumza kama wametuletea tunachokihitaji na kama hatutakubaliana msajili atatupatia cheti kwamba tumeshindwa kukubaliana na tutaendelea na hatua inayofuata ambayo ni kupiga kura na kuingia kwenye mgomo”

Magazeti yaleo13th July 2012


Thursday, July 12, 2012

MAgazeti Ya leo 12th July 2012


HILI NDIO PIGO JINGINE KWA MCHEZAJI RONALDINHO WA BRAZIL.

Mkali wa soka kutoka Brazil ambae ni mwezi umepita toka aondoke kwenye club ya Flamengo aliyokua anaichezea kutokana na kushindwa kumlipa mishahara yake, amepatwa na tatizo jingine kwenye moja kati ya madili yake.

Kampuni ya vinywaji ya Coca-cola imeukatisha mkataba mnene na mchezaji Ronaldinho baada ya mchezaji huyo kuonekana akiwa na vinywaji vya Pepsi pembeni wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na club yake mpya ya Atletico Mineiro.

Mkataba wake na Coca-cola ambao hauna hata mwaka toka usainiwe, ulitakiwa kwenda mpaka 2014 ambapo malipo yake kwa mwaka ni dola za kimarekani zaidi ya  laki saba.

Pepsi ni wadhamini wa club yake mpya ya Mineiro na kuwepo kwa vinywaji hivyo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari sio chaguo au uamuzi wa Ronaldinho, ni maamuzi ya club kwa sababu ndio yenye mkataba na Pepsi na sio Dinho.

Tuesday, July 10, 2012

Mgomo Wa Wenye Mabasi Watikisa Arusha, Kilimanjaro

MGOMO mkubwa wa wamiliki wa mabasi jana uliathiri huduma za usafiri kati ya Miji ya Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro, na kusababisha adha ya usafiri kwa abiria na ulanguzi wa nauli kutoka Sh2,500 ya kusafiri kati ya miji hiyo miwili hadi kufikia Sh10,000.

Juzi, mgomo huo ulitikisa zaidi usafiri wa mabasi ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro baada ya wamiliki kupinga hatua ya Halmashauri ya Manispaa ya  Moshi kuongeza ushuru kutoka kiasi cha Sh1,000 hadi kufikia Sh2,000 bila kushirikishwa.

Mgomo huo jana, uliingia katika hatua mpya baada ya wamiliki wenzao wa Mkoa wa Arusha nao kuingia katika mgomo na kusababisha msururu wa watu barabarani, huku watoa huduma za pikipiki maarufu kama bodaboda wakineemeka na mgomo huo.

Mbali ya bodaboda kutoa huduma, baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kati ya Arusha na Moshi  walilazimika kutumia usafiri wa magari madogo aina ya Naoh, ambayo yalikuwa yakipakia abiria kwa kificho pembezoni mwa miji hiyo kuepuka kushambuliwa na wasafirishaji waliokuwa kwenye mgomo.

Abiria walioathiriwa zaidi na mgomo huo ulioanza saa 11:00 alfajiri ni wale waliokuwa wakisafiri kati ya Moshi-Arusha na wilaya nyingine za Mkoa wa  Kilimanjaro na wanaotegemea usafiri wa daladala.

Misururu mirefu ya abiria wakiwamo wanafunzi walionekana wakitembea kwa miguu kutoka majumbani kwenda shuleni, huku watu wengine wanaokwenda kazini nao wakijikuta katika adha hiyo na kulazimika kutumia usafiri wa malori na toyota aina ya Pick-Up.


Manispaa ya Moshi imepandisha ushuru kutoka Sh1,000 kwa siku kwa basi dogo hadi Sh1,500 na kutoka Sh1,000 hadi Sh2,000, sawa na ongezeko la asilimia 100.

Kauli ya Akiboa
Katibu wa Chama cha Wasafirishaji abiria Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro (Akiboa), Locken Adolf alithibitisha jana wanachama wake
kugoma kushinikiza Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kukaa nao mezani kujadili ongezeko hilo.

“Kimsingi, hatupingi ushuru wa Serikali, tunachopinga ni manispaa kuongeza ushuru wa maegesho kwenye stendi za Moshi kwa asilimia 100 kutoka Sh1,000 ya awali hadi Sh2,000 bila hata kushauriana na sisi wadau wa usafirishaji,” alisema Locken.

Alifafanua kwamba, baada ya juhudi zao kutafuta ufumbuzi wa suala hilo kupitia
vikao walivyofanya kati yao na uongozi wa Manispaa ya Moshi pamoja na
ofisi ya mkuu wa wilaya kushindikana, wameamua kusitisha huduma hadi mwafaka utakapopatikana.

Katibu huyo wa Akiboa alisema, kilichowasukuma kugoma ni kauli aliyodai kutolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Ibrahim Msengi na
uongozi wa Manispaa kuwa mfanyabiashara asiyemudu kulipa ushuru huo
aegeshe gari lake nyumbani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Akiboa, Hussein Mfinanga alisema mgomo huo unatarajiwa kudumu kwa siku tatu mfululizo.Mfinanga alisema kwa ongezeko hilo la ushuru kwa halmashauri hizo mbili, kunaamaanisha kuwa mmiliki wa mabasi atalipa ushuru mkubwa kuliko unaotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

“TRA ambako ndio sheria mama ya kodi ipo na inapitishwa na Bunge tunalipa Sh190,000 kwa Hiace na 520,000 kwa mabasi makubwa kwa mwaka, iweje ushuru wa halmashauri uwe juu ya TRA?,”alihoji.

Kiongozi huyo alisema kwa siku ya jana baadhi ya mabasi makubwa ya abiria kwenda Dar es Salaam  na Morogoro, yaliendelea na safari kwa kuwa tayari walikuwa wamewakatia abiria wao tiketi.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani  Kilimanjaro, Peter Simma alipoulizwa juu ya msimamo huo, alisema wanaopaswa kubebeshwa mzigo wa suala hilo ni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

Meya wa Manispaa hiyo, Jaffar Michael alisema ushuru huo ulipandishwa kwa nia njema ili kupanua wigo wa mapato ambayo yatatumika katika shughuli za miradi ya maendeleo ya wananchi.

Alifafanua kwamba kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuangalia kama wasitishe viwango hivyo vipya kwa muda wakati wakiendelea kujadiliana na wadau

Hata hivyo, kwa Arusha magari madogo ya abiria maarufu kama daladala yanayofanya safari zake ndani ya jiji hilo na vitongoji vyake, yaliendelea kutoa huduma wakati usafiri wa ndani ya Mkoa ya  Kilimanjaro hakukuwa na huduma hizo za usafiri baada ya daladala nazo kuingia kwenye mgomo huo.

Kwa upande wao wamiliki wa daladala, wanapinga ongezeko la ushuru kutoka Sh1,000 hadi Sh1,500 kwa madai hayo ya kutoshirikishwa kabla ya uamuzi huo kufikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

Wakati hali ikiwa hivyo, kuna madai kuwa mgomo huo una mkono wa vyama vya siasa huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikituhumiwa kuhujumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho kinaongoza halmashauri hiyo.

Hata hivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi, Alu Sigamba alikanusha tuhuma hizo akisema, chama hicho kiliingilia kati kutafuta ufumbuzi wa
mgomo huo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wasafirishaji kupitia chama chao cha Akibo

Rais wa Chama cha Madaktari Afikishwa Mahakamani Leo

Rais wa Chama cha madaktari Tanzania MAT Dr Namala Nkopi hii leo amefikishwa katika mahakama ya hakim kazi kisutu kujibu mashtaka yanayohusiana na mgomo wa madaktari.

Kwa mujibu hakimu anayesikiliza kesi hiyo Faisal Kahama, Dr Mkopi amesomewa mashtaka 2 ambayo ni
1) Kutotii amri ya mahakama ya kutangaza kusitisha mgomo
2) kuhamasisha mgomo

Hata hivyo mshtakiwa amekana mashitaka hayo na kuachiwa kwa dhamana ya watu wawili ambao ni watumishi wa serikali wakiwa na vitambulisho vya kazi na shillingi laki 5 kila mmoja.

Mawakili wa serikali walipinga masharti hayo na kuomba Hakim aongeze masharti ikiwa ni pamoja na Dr Nkopi kusalimisha hati yake ya kusafiria lakini hakim aliyakataa maombi hayo na kusisitiza kuwa maamuzi aliyoyafanya yatabaki kama yalivyo.

Saintfiet kuvuna Sh288 mil Yanga

KOCHA mpya Yanga, Tom Saintfiet aliyeingia mkataba wa kufundisha klabu hiyo ya Jangwani, atavuna Sh288 milioni iwapo mkataba wake hautaishia njiani.

Katika kipindi cha miaka mitano, Yanga imekuwa na makocha tofauti, baadhi wakishindwa kudumu klabuni kama mikataba yao ilivyokuwa ikielekeza.

Makocha waliofundisha Jangwani tangu 2007 na kuondoka kwa sababu mbalimbali, nyingi kutokana na kushindwa kutekelezwa kwa makubaliano ni Milutin Sredojovic, Dusan Kondic, Kostadin Papic na Sam Timbe.

Hata hivyo, Papic aliyekuja nchini mara ya kwanza mwaka 2009, alirejea mwaka jana baada ya Timbe aliyeipa jangwani taji la Ligi Kuu na Kombe la Kagame kutimuliwa.

Katikati ya wiki iliyopita Kocha, Saintfiet raia wa Ubelgiji
aliingia mkataba wa miaka miwili kuifundisha Yanga kwa mshahara wa Sh12 milioni.

Ina maana, katika kipindi cha mwaka mmoja, Saintfiet aliyetamba kuleta mafanikio Jangwani, tavuva Sh144 milioni.

Mshahara huo unamzidi kwa Sh730,000 kocha aliyeondoa muda mfupi baada ya kumalizika kwa msimu, Kostadin Papic kutoka nchini Serbia.

Habari za uhakika toka ndani ya klabu hiyo zimedaiwa kupanda kwa mishahara ya wachezaji, ambapo wa chini utakuwa Sh800,000 na wa juu Sh1.5milioni.

Micho ambaye sasa ni Kocha wa timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi), aliondoka nchini baada ya timu hiyo kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Ndogo mwaka 2007.
Mtihani wa kwanza wa Saintfiet katika utekelezaji wa ahadi yake ya kuleta mafanikio, Jangwani unaanza leo kwa mechi ya kirafiki dhidi ya JKT Ruvu

Yanga inashuka Uwanja wa Taifa kupambana na maafande hao katika mchezo wenye sura ya maandalizi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Kagame inayoanza Jumamosi wiki hii.

Lakini pia Bosi, Saintfiet ataitumia mechi hiyo kuwachambua wachezaji wake walioonyesha uwezo ili aweze kujenga mhimili wa kikosi cha kwanza.

Kwenye kikosi hicho kuna wachezaji wengi wameonyesha uwezo jambo ambalo ni wazi litampa wakati mgumu kuchagua kikosi cha kwanza.

Kumekuwa na ushindani mkubwa kwenye kikosi hicho chenye mchanganyiko wa wachezaji na chipukizi kadhaa wapya kama Frank Domayo, Simon Msuva na David Luhende.

Domayo na Msuva wametishia nafasi za wakongwe kama Nurdin Bakari, Juma Seif na Hamis Kiiza baada ya kuonyesha kiwango kikubwa katika pambano la kirafiki dhidi ya Express ya Uganda hivi karibuni.

Naye Luhende anayecheza nafasi beki ya kushoto ameonekana kumkuna Saintfiet baada ya kutisha katika mazoezi ya timu hiyo hivu karibuni, hivyo kuwafanya wapinzani wake wa nafasi hiyo Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua na Godfrey Taifa kuwa mtegoni.

Nayo JKT ambayo msimu uliopita ilishindwa kutamba itautumia mtanange huo kama sehemu ya kuona makali yake kabla ya kuingia katika hekaheka za Ligi Kuu msimu ujao.

POLISI KUWAHOJI KWA MATAMSHI KWAMBA WANATISHIWA MAISHA, DK NCHIMBI ASEMA WANASABABISHA CHUKI

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema huenda wakajikuta matatani kutokana na madai waliyoyatoa juzi kwamba wanatishiwa kuuawa na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa.Kutokana na matamshi hayo, jana Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ameliagiza Jeshi la Polisi kuwahoji viongozi hao ambao walidai kuwa mauaji hayo yamepangwa kufanywa kwa kuwekewa sumu kwenye chakula au kwa kutumiwa makundi ya ujambazi.

Akizungumza na waandishi wa mjini hapa jana, Dk Nchimbi alisema licha ya kudai kwamba wanatishiwa, ameshangazwa na msimamo wa viongozi hao kukataa kupeleka suala hilo polisi kwa madai ya kuhofia suala hilo halitafanyiwa kazi.

Alisema watawahoji viongozi hao kwa sababu suala la usalama wa Mtanzania yeyote si la hiari, bali ni la kikatiba na la kisheria hivyo, ni lazima polisi watimize wajibu wao.

“Ni lazima tuwahoji ili tujue ni nani amewatisha na kwa sababu zipi. Hatutamuomba mtu ruhusa ya kumlinda kwa sababu huo ni wajibu na kazi yetu kuwalinda raia, hilo halina mjadala. Hatua zitachukuliwa endapo itabainika kuwa madai yao yana ukweli,” alisema Dk Nchimbi.

Aliwataka viongozi wote wa kisiasa wakiwamo wa Chadema wanapohisi kutishiwa usalama wao, watoe taarifa polisi ili vyombo vya dola viyafanyie uchunguzi malalamiko yao ili utaratibu ufanyike kuhusu usalama wao kama sheria inavyotaka.

Alionya tabia ya viongozi kuzungumza nje ya utaratibu akisema haikubaliki kwani inaweza kuwa ni mbinu za kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

Dk Nchimbi alisema jambo hilo si jema kwani linajenga hofu miongoni mwa Watanzania na kuwafanya wasiviamini vyombo vyao vinavyowalinda kwa mujibu wa sheria.
“Ni kweli kuwa kila mwanasiasa anataka kukubalika na umma lakini, akubalike katika taratibu zinazokubalika,” alisema Dk Nchimbi na kuongeza:

“Ingekuwa Serikali inataka kukubali umaarufu kama huo, basi ingetumia mwanya wa haohao Chadema wakati mitandao ya kijamii iliposambaza taarifa kuwa Chadema ilihusika na kifo cha marehemu, Chacha Wangwe.”

Alisema Serikali haikukurupuka na kuwakamata, badala yake ilifanya uchunguzi kwanza na matokeo yake alikamatwa dereva wake ambaye ameshachukuliwa hatua.
Alisema kama Serikali ingekuwa inatafuta umaarufu, ilikuwa ni fursa nzuri kwake kujipatia umaarufu na kukivuruga chama hicho kwa kuwakamata viongozi wa Chadema hasa baada ya kuwapo kwa uvumi kwamba wamemuua kiongozi huyo.

“Viongozi wetu wa kisiasa ni lazima wafanye mambo ambayo kesho na keshokutwa watakiri mchango wao, ama katika ujenzi au uharibifu wa nchi yetu. Kila siku wakilalamika kuwa wanataka kuuawa basi ni lazima watu watawashangaa kwani badala ya kutatua matatizo ya wananchi wanabaki wakilalama wanataka kuuawa. Watu kama hawa wanafanya hivi kwa masilahi yao, wanaweza kuwagombanisha wananchi.”

Waziri Nchimbi aliwataka wananchi na viongozi wa kisiasa kuondoa hofu kwani Serikali ina wajibu wa kuwalinda na hakuna mtu atakayenufaika kwa mauaji ya wanasiasa hao.

Kuhusu madai kwamba polisi wamekuwa wakipuuza malalamiko ya wapinzani, Dk Nchimbi alikiri kuwapo kwa baadhi ya polisi wenye kasoro katika utendaji wao lakini akasema wengi ni waadilifu.
Alisema ikiwa kuna mtu haridhishwi na utendaji wa polisi kwa kutopata huduma kama inavyostahili, ana uhuru wa kutoa taarifa katika ngazi za juu hata ikiwa ni kwake.

Ikulu nayo yatoa tamko
Katika hatua nyingine, Ikulu imesema hakuna mpango wowote unaoratibiwa na Idara ya Usalama wa Taifa kwa lengo la kuwaua viongozi hao wa Chadema.
Jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alihoji sababu za Serikali kutaka kuwaua viongozi hao wakati si tishio lolote kwa nchi.

Balozi Sefue alisema Idara ya Usalama wa Taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi, bali kulinda masilahi ya taifa na kuhoji: “Sasa kwa nini wauawe? Wana nini hasa hadi Idara ya Usalama ifanye hivyo?”

Alisema ni vyema wakati mwingine kukawa na umakini kwa kuangalia namna siasa zinavyoweza kufanya kazi... “Hii inaweza kuwa siasa tu. Sisi serikalini hatuna mambo ya vyama, tunafanya kazi kwa ajili ya watu wote.”

Alisema Idara ya Usalama wa Taifa na Serikali hazifanyi kazi kisiasa, bali kwa kuangalia masilahi ya Watanzania wote: “Huku serikalini sisi hatuna ugomvi na wanasiasa. Tunafanya kazi na watu wote.”
Alisema wanaoweza kufikiria kuwa kuna siasa katika Serikali na vyombo vyake wao ndiyo wanaweza wakawa wanafanya siasa.

Tuhuma za Chadema
Kauli hizo za Serikali zinatokana na tuhuma za Chadema kwamba kimebaini njama za kuwaua viongozi wake hao waandamizi ambazo zinaratibiwa na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa na kwamba nyendo zao zimekuwa zikifuatiliwa kwa saa 24.

Tuhuma hizo za Chadema zilitolewa juzi na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni akisema: “Sisi Chadema hatuna mambo ya siri tunayotaka kufanya katika nchi hii. Matatizo ya Watanzania yapo wazi na yanajulikana na kila mmoja, Serikali ya CCM itekeleze sera na ahadi zao kwa wananchi na si vitisho.”Chanzo. Mwananchi

KOCHA MKUU WA TAIFA STARS KUWA MGENI RASMI LIGI YA KUIBUA VIPAJI

  KOCHA mkuu wa timu ya Tanzania(Taifa Stars),Kim Poulsen anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya ligi ya ya kuibua vipaji vya soka la vijana inayojulikana kama Moivaro Youth Football League(MYFL) ambayo itatimua vumbi mnamo septemba 29 mwaka huu mkoani Arusha.

Pia,viongozi mbalimbali wa ngazi za soka mkoani Arusha na nchini kwa ujumla akiwemo mtaalamu wa masuala ya ufundi wa shirikisho la soka nchini(TFF),Sunday Kayuni anatarajiwa kuwa miongoni mwa wageni walioalikwa katika ligi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi na mwasisi wa Taasisi ya Future Stars Aademy ya jijini hapa,Alfred Itaeli alisema kwamba ligi hiyo itashirikisha timu za wanawake pia ambapo usajili wa timzu zitakazoshiriki  unataraji kuanza Agosti 18 mwaka huu.

Itaeli ,alisema kwamba kabla ya  ligi hiyo kutimua vumbi wameandaa mafunzo ya wiki mbili kwa waamuzi  wenye umri  kati ya miaka 8 hadi 15 ambao watatumika kuchezesha ligi hiyo ili kuepuka gharama za kukodi waamuzi mbalimbali ambapo mafunzo hayo yatandeshwa na mwamuzi mkongwe nchini Billy Mwilima.

Alitaja lengo kuu la ligi hiyo ni kukuza vipaji vya soka nchini na kuweka ushindani kwa kila rika huku akisisitiza kuwa kwa kuwa ligi hiyo haina wadhamini wameamua kutoza kiasi cha sh,100,000 kama ada za kiingilio.

Na Ashura Mohamed-Arusha