Saturday, January 5, 2013

Mama Bilal Mgeni Rasmi Tambaza

 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo Januari 05, 2013 katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Mama Asha amewahasa vijana hususan wanafunzi hao waliohitimu masomo kutokukubali kutumika na watu wenye maslahi binafsi na kujikuta wakisababisha uvunjifu wa amani. Aidha amewataka kutojihusisha na makundi yanayochochea uvunjifu wa amani bila kujitambua wafanyalo, badala yake amewaomba kuwa wakipima kila wanaloambiwa kuwa linamaslahi na dini yao ama maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi mhitimu wa Kidato cha Sita, Zuhura Azmin, kwa kuwa mmoja kati ya waliofanikisha sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza

Waziri Membe atangaza kutogombea Ubunge tena

                Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.

WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.

“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,” alisema Membe.

kinana akemea chokochoko za kidini

KATIBU Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana amekerwa na chokochoko za kidini zilizoanza kujipenyeza hivi karibuhi na kutoa wito kwa madhehebu ya dini na taasisi zake hapa nchini,kuendelea kuhubiri amani kwa kuliombea taifa , ili wananchi waendelee kujivunia amani iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Kinana alitoa kauli hiyo juzi kwenye maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Imam Husein, yanayoadhimishwa na dhehebu la KhojaShia Ithna Asheri Jamaat Arusha kote duniani na kufanyika kwenye msikiti wa jumuiya hiyo jijini hapa , ambapo watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa madhehemu pamoja na viongozi wa chama na Serikali walihudhuria.

Kinana alisema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa viongozi wa dini na taasisi zake kuendelea kuienzi amani kwa kuhubiri suala la kudumisha amani na kuonya kwamba Serikali haitasita kuchukua hatua za haraka kwa mtu ama kikundi chochote cha dini kitakachojihusisha na uvunjivu wa amani.

NDEGE MEDICS YAKABIDHI AMBULANCE ZA KISASA

 Head of Primary Medical Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia) ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa Afya ya Mama na Mtoto akizungumzia Malengo Makuu ya mradi huo kuwa ni kuongeza kiwango na matumizi ya Huduma ya Afya ya Mama Mjamzito na Watoto na kushirikiana na kujifunza kuhusu Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto. Kutoka kushoto ni Acting Medical Director wa Aga Khan Hospital Dr. Ambrose Chanji, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian Ndege na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo Bw. Anis Nazrani.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania
                                Wakipongezana baada ya makabidhiano hayo.
 Pichani Juu na Chini ni muonekano wa magari hayo ya kubebea wagonjwa kwa ndani yaliyotelwa kwa hospitali ya Aga Khan na NDEGE Medics kwa ajili ya mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania.

walionunua ving'amuzi star times waambiwa wavirejeshe

KAMPUNI ya Star Media Tanzania Ltd (Startime) imewataka watu ambao wamenunua ving’amuzi na kubaini kuwa havifanyi kazi kuvirejesha kwenye ofisi zao ili wapatiwe vingine.
Vilevile wamewataka wale waliouziwa kwa bei ya kulangua wafike kwenye ofisi zao pamoja na risiti walizonunulia ili hatua zinazofaa ziweze kuchukuliwa.

Hatua hiyo inatokanana malalamiko ya wananchi siku chache tangu kuanza kutumika kwa mfumo wa dijitali wa kurusha matangazo ya runiga.

Malalamiko hayo yanayolalamikiwa na kampuni hiyo ni kuhusiana na kushindwa kuonekana kwa baadhi ya chaneli licha kufunga king’amuzi kwenye Televisheni

Waziri Membe atangaza kutogombea ubunge tena

WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.

“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,” alisema Membe.

, ambapo pia aliwataka wananchi wa mikoa ya kusini, kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo Serikali inashughulikia mchakato wa kuvuna gesi asilia.

Leo ikiwa ni siku ya kuwakumbuka Denis na Ismail chadema yafanya shughuli za kijamii...

 Moja ya vituo vya kulelea watoto yatima alivyo vitembelea Godbless Lema na katibu mkoa Amani
 Mh. Lema akiwa na watoto yatima kati ya vituo alivyotembelea leo katika siku ya kuwakumbuka Denis na Ismil.
 Huyu mtoto YATIMA ameshika nafasi ya tatu ktk Wilaya Arusha matokeo ya la saba..
CHADEMA Arusha leo itakuwa na Kumbukumbu ya miaka miwili (2) ya mauaji ya makusudi ya raia wasio kuwa na hatia yaliyotokea 5/1/2011.Kumbukumbu hii itaenda sambamba na chama kufanya shughuli za kijamii,ikiwepo kutembelea vituo vitano vya watoto yatima jijini Arusha,kutoa wafungwa waliofungwa kwa kukosa faini ya ela ndogo,kisha kuhitimishwa kwa mkutano mkubwa wa hadhara.

Tunaomba wapenda haki wote kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi 5/1/2013 katika ofisi za chama Ngarenaro,kwa ajili ya kwenda kutoa misaada hiyo kwenye vituo vya Yatima,pia tunatoa wito kwa kila mmoja wetu kujitolea chochote anachoweza Sukari/mchele/sabuni/mafuta etc kama ishara ya kutoa Sadaka,kwa Mwenyenzi Mungu ili HAKI iweze kutendeka.

Tutaendelea kudai haki na usawa katika jamii yetu hata kwa gharama ya maisha yetu.Denis na Ismail pamoja na wengine wengi tutawakumbuka daima,damu yenu hakimwagika bure,

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa


 Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha kwenye mkutano wa Chadema Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni akiwa ndani ya gari ya jeshi baada ya kutiwa nguvuni,
 Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema, Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni.
 Picha juu alipopiga picha na Viongozi mbalimbali wa Chadema Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema, Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi...
                                                 

Magazeti ya leo Jumamosi ya 5th January 2013




Leo Chadema Wawakumbuka waliopoteza Maisha katika vurugu zilizotokea 5/1/2011 Arusha.

Kwa wakazi wa Arusha na vitongoji vyake, Leo kutakuwa na mkutano mkubwa wa kuwakumbuka ndg zetu(Denis na Ismail) walio pigwa risasi na jeshi la polisi 5.1.2011, mkutano huu utafanyika kwenye uwanja wa Ngarenaro shule ya msingi kuanzia saa tisa, vile vile utarusha na kituo cha redio ya sunrise (94.80 FM) kwa wakazi wa Arusha na mikoa jirani.






Hizi ni baadhi ya picha wakati wa kuwaaga makamanda wetu waliopoteza maisha 5.01.2011. R.I.P (Denis na Ismail)

Friday, January 4, 2013

INASIKITISHA BALI TUNASEMA WAPUMZIKE KWA AMANI.

         
 AJUAYE uchungu wa mtoto ni mzazi! Ukiwatazama akina mama watatu wa wasanii wa Tanzania waliofariki dunia kwa nyakati na sababu tofauti hivi karibuni wakilia kwa uchungu, unaweza ukadhani wazazi hao ni ndugu kwa namna nyuso zao zinavyoonekana kuwa na majonzi mazito,

Risasi Jumamosi linakuchambulia.

Makabrasha ya gazeti hili yanawaonesha mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, mama wa marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’, Zaina Mkiety na mama wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Zaituni Mzena wakilia kwa uchungu.
Wazazi hao walionekana wenye majonzi kupita maelezo kwani kila mmoja alimbeba mwanaye tumboni kwa miezi tisa, akamlea, akamtunza kwa tabu hadi akakua lakini baada ya kuanza kufaidi matunda yao tu, Mungu akawachukua.

SHELUKINDO : Namuunga mkono lowassa 2015

MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo ametangaza kuchukua kile alichokiita uamuzi mgumu ili kuhakikisha kuwa Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa anamrithi Rais Jakaya Kikwete katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.Shelukindo alitoa kauli hiyo Jumapili wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa kuchangia ujenzi wa Hosteli ya KKKT katika sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa ambazo pia zilihudhuriwa na makada kadhaa wa CCM.

Jana alipoulizwa kuhusu kauli hiyo, Shelukindo alisema: “Ni kweli mimi ni muumini wa Lowassa, ila pale (mkutanoni) sikumtaja kwa sababu najua chama kina taratibu zake na muda wa mchakato wa kumpata Rais haujafika.”

SERENGETI FREIGHT YATOA PONGEZI KWA BODI YA UTALII TANZANIA


BAADHI YA PICHA ZA MKUTANO WA CHADEMA IRINGA


TEKELEZENI AHADI MLIZOZITOA WAKATI WA KUOMBA KURA-OLE NANGOLE

 MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha(CCM)Bw Onesmo Ole Nangole amewataka Viongozi mbalimbali wa chama hasa wale ambao walitoa ahadi  kwa wananchi kwenye uombaji wa kura kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi hizo kwa haraka sana kwani wale ambao hawatekelezi ahadi wanachangia sana chama hicho kuelekezewa lawama

 Bw. Nangole aliyasema hayo Juzi wakati akifungua Kata mpya ya Chama hicho ambayo kwa sasa inajulikana kama Kata ya Majengo iliopo Meru Mkoani Arusha.

 Aidha Bw Nangole alisema kuwa tabia ya baadhi ya Viongozi ya kuwa watoa ahadi hasa nyakati za kura na kisha wakishapata kura wanasahau ahadi zao inachangia sana kuunguza Ccm kwenye jamii na kuonekana kuwa ni watoaji ahadi zisizotekelezwa.

 Alisema kuwa Viongozi wote ambao walitoa ahadi mbalimbali kwa wananchi hasa katika Nyakati za Kura wanatakiwa kuhakikisha kuwa watekeleza ahadi zao na kujijengea tabia ya kuwaangalia wapiga kura wao ili kuendelea kulinda uhai wa Chama

 Mbali na hayo aliongeza kuwa Viongozi mbalimbali wa Chama hicho wanatakiwa kuangalia zaidi ilani ya chama hicho kwa kuhakikisha kuwa wanaainisha matatizo ambayo yapo kwenye jamii na kisha kuyatatua kuanzia kwenye Ngazi za Vitongoji na Vijiji.

 Katika hatua nyingine Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Meru Bw Langaeli Akyoo alisema kuwa bado Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa zitatuliwe kwa haraka sana ingawaje umoja na ushirikiano unaitajika kwa haraka sana