Thursday, January 17, 2013
MAKAMO MWENYEIKI CCM ZANZIBAR DK. SHEIN, AZUNGUMZA NA VIONGOZI OFISI KUU YA CCM KISIWANDUI
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais wanZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisisitiza jambo alipokua akizungumza na Viongozi wa Tawi la CCM Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali mbali za Chama hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar jana,Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimiana na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai
Mama Salma Kikwete afunga kongamano la Ulimwengu la afya ya uzazi mjini Arusha
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete akifunga kongamano la Ulimwengu la Afya ya Uzazi la siku 3 Katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC mjini Arusha leo, Kongamano hilo lilewashirikisha wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi wapatao 800 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni,
SERIKALI YABARIKI FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Baraza la Sanaa la Taifa, limebariki kufanyika kwa Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 baada ya kuridhishwa na maandalizi yaliyo fanywa na Miss Tourism Tanzania Organisation waandaaji wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo kitaifa na kimataifa, pia kwa kuzingatia sheria za nchi, kanuni na Taratibu za mashindano.
Serikali pia imeridhishwa na jinsi Fainali za ngazi za mikoa na kanda zilivyofanyika kwa mafanikio,ambapo kila mkoa umepata washindi wenye sifa za kuwakilisha mkoa husika katika Fainali za Taifa mwaka

36 WACHUKUA FOMU TFF, 18 WAREJESHA
Wakati kesho ndiyo mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) waombaji 36 wameshachukua na 18 tayari wamesharejesha.Idadi hiyo ni kufikia leo mchana (Januari 17 mwaka huu). Pia Kamati ya Uchaguzi ya TFF inasisitiza kuwa wanaorejesha fomu hizo kwa email wanatakiwa kuzituma kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa email ya to= tfftz@yahoo.com" target="_blank"> tfftz@yahoo.com na si kwa email binafsi za wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi au maofisa wa TFF.
Waombaji wanne walioongezeka katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi na Rukwa, Eliud Mvella (Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na Pwani), na Omari Abdulkadir kwa Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais) wakati waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.
Waziri Simba akabidhi vyerehani kwa wajane
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba
akimsikiliza Gavana wa Lions Ukanda wa Uganda na Tanzania, Joseph
Kiwanuka, wakati alipomtembelea leo ofisini kwake akiwa na ujumbe wa
watu watano.
Waziri Simba akiangalia baadhi ya vyerehani viwili viliyotolewa na Lions kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wajane. Vyerehani hivyo ni kati ya 100 vitakavyotolewa na Lions kuwawezesha wanawake kujikimu kimaisha.
Waziri Simba akimkabidhi mmoja wa wafaidi wa vyerehani vilivyotolewa na Lions Bi. Jane Fuiko wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi zilizofanyika leo ofisini kwa Waziri.

WAFANYAKAZI OFISI YA WAZIRI MKUU WATOA MAONI YA KATIBA MPYA
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Hanifa
Masaninga (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo uandaaji wa maoni ya
wananchi katika taarifa rasmi (Hansard) kwa wafanyakazi kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)wakiongozwa
na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Jamanne Sagini (wa pili kushoto) wakati
waliotembelea ofisi za Tume hiyo
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Nenelwa Mwihambi (kulia) akitoa maelezo kuhusu mfumo wa uchambuzi wa maoni ya wanachi kwa wafanyakazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Jamanne Sagini (Kaunda suti nyeupe) wakati waliotembelea ofisi za Tume hiyo

Wednesday, January 16, 2013
Chadema sasa waanza kulipuana
KATIKA kuonyesha hali si shwari ndani ya Chadema, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha) wa chama hicho, Juliana Shonza amesema ameamua kumshtaki Mwenyekiti wake, John Heche kwa kumuita kuwa ni msaliti wa chama na kwamba anatumiwa na CCM na kuamua kumfukuza nafasi yake bila kutoa nafasi ya kusikilizwa.
Pia, amemlipua Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa akidai kuwa amefanya ufisadi ndani ya chama kwa kujikopesha Sh140 milioni ambazo hajazilipa hadi sasa.
Mbali na hilo, amemshukia Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa kudai kuwa anatoa kauli za kukurupuka ambazo zinakiyumbisha chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Shonza alitoa kauli hizo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juu ya tuhuma zilizotolewa na mwenyekiti wa Bavicha na kuhusu kufukuzwa kwake ndani ya chama akiwa na wenzake Mtela Mwampamba na Habibu Mchange.

Bus la champion lamgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo
YAH: TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA
HABARI TAREHE 15/01/2013
Mtu mmoja amefariki Dunia Mkoani Dodoma katika tukio la ajali ya gari kumgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo.
Tukio hilo limetokea tarehe 14/01/2013 majira ya saa 09:30 alasiri katika kijiji cha Kelema Wilaya ya Chemba barabara ya DODOMA -KONDOA baada ya gari lenye namba za usajili T. 769 BNP aina ya Scania Bus mali ya Kampuni ya Champion likendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la George s/o Maiko Kwayu likitokea Dodoma kuelekea Kondoa kumgonga mtembea kwa miguu na kumsababishia kifo chake papo hapo.

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AWAFANYIA SHERRY PARTY WENZA WA MABALOZI
Mama salma akisoma hotuba
Wake wa Mabalozi katika hafla hiyokatika viwanja vya Ikulu
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kwenye hafla maalumu ya kuwakaribisha wake wa Balozi nchini kwa mwaka mpya 2013, Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar- es Salaam , Jan 15,2013,
JK: Uvumilivu sasa basi
SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana. Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.
Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.
“Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha,” alisema Rais Kikwete.

MZEE MKAPA NA MZEE MSUYA WATOA MAONI LEO
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na
Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu
leo (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na
uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akiwa na wageni wake
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akiwa na wageni wake
JK: AZINDUA AWAMU YA KWANZA YA JENGO JIPYA LA HOSPITALI YA SHREE HINDU MANDAL JIJINI DAR ES SALAAM
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasha mshumaa kama ishara ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya jengo jipya na Awamu ya pili ya Hospitali ya Shree Hindu Mandal ya jijini Dar es salaam leo katika Mtaa wa Nyanza, ambapo huduma hiyo itapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali jijini na kuongeza wigo wa utoaji huduma n kuongeza vitanda vya kulaza wagonjwa, Hospitali ya Shree Hindu Mandalilianzishwa mwaka 1931 ikianza na Zahanati anayeshuhudiatukio hilowa pili katikati ni Mwenyekiti wa hospitali hiyo Bw Ramesh Patel.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi , Madaktari , Wauguzi pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya Shree Hindu Mandal mara baada ya kuzindua rasmi leo
Rais Dk. Jakaya Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa hoapitali hiyo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Manumba mahututi, alazwa Aga Khan
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba
HALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba ni mbaya na amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.
“Alitakiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu, lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu kumzindua, ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi hilo.

Subscribe to:
Posts (Atom)