Friday, November 30, 2012

Basata Yatoa Salaam Za Rambirambi Kufatia Vifo Vya Wasanii..!

                                                       Yah: Salaam za Rambirambi
Baraza la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za misiba ya wasanii watatu wa tasnia ya filamu na muziki nchini.

“ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya vifo hivi vya wasanii hawa John Mganga, Mlopelo na Hussein Mkeity a.k.a Sharo Milionea ambao mchango wao unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo waliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wao bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa pole kwa familia za marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na wapendwa wetu.

Tunaomba mwenyezi Mungu azipumzishe mahala pema peponi roho za marehemu. Baraza liko pamoja na familia za marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

Imetolewa na
Ghonche materego
Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.
Reactions::    

Magazeti ya leo Ijumaa 30th November 2012



























ACHA KUJIKATISHA TAMAA, UNA THAMANI KUBWA KWENYE MAPENZI!

NI Ijumaa nyingine tena tunakutana katika Let’s Talk About Love, lengo likiwa ni lilelile; kupeana elimu zaidi juu ya mambo ya uhusiano na mapenzi. Sina shaka marafiki zangu wote mtakuwa wazima wa afya njema.

Kuna baadhi ya wanawake au wanaume wanakaa kipindi kirefu bila ya kutamkiwa kuwa wanapendwa, kutokana na hali hiyo wanakuwa wapweke na wakati mwingine kufikiria kuwa wao ni wabaya na wasiostahili kabisa kuwa na wapenzi.
Wengine huanza kujiona hawafai kutokana na sababu ambazo wenyewe wanaziweka ambazo kwa kiasi kikubwa huwa za kujikosoa.

Wakati mwingine huanza kufikiria kuwa huenda kwa sababu yupo katika hali fulani ndiyo maana hapati mtu wa kumpenda na fikra nyingine mbaya juu yake ambazo huwa ni za kujikatisha tamaa.

Tambua kitu kimoja, kuna wasichana warembo na wavulana watanashati wengi ambao hawajapata pumziko la kweli katika mioyo yao kwa muda mrefu sasa, wamekuwa wakitafuta watu wenye mapenzi ya dhati kwa muda mrefu bila mafanikio na sasa wamekata tamaa ya kupata wapenzi wa kweli na badala yake wamegeuka vyombo vya starehe.

Wavulana watanashati au wasichana warembo mara nyingi watu wa upande wa pili huwatamani zaidi kuliko kuwa na mapenzi ya kweli, kwa maana hiyo baada ya kushiriki naye ngono mara kadhaa huamua kuachana naye na kumuacha muhusika akiwa na sononeko katika moyo wake.

Watu wa aina hii huachwa na dhiki ya moyo na wakati mwingine hukata tamaa na kuamua kutokuwa na uhusiano mwingine kabisa na wapenzi wapya. Jaribu kufikiri kama kuna mtu wa aina hii ambaye amekuwa akitoneshwa mara kadhaa na wapenzi na wewe ambaye una miezi karibu sita sasa hujapata akupendaye nani mwenye matatizo zaidi? Nadhani jibu yakinifu utakuwa nalo.

Inawezekana wewe ni mmoja kati ya hao ambao wana sononeko la moyo kwa kutopata faraja ya kweli kwa wapenzi wao. Hakika hizi ni mada mbili tofauti lakini leo nitaanza na hili la kutopata mpenzi kwa muda mrefu na sasa umekata tamaa ya kupedwa, kuoa au kuolewa katika siku zote za maisha yako.

Wakati mwingine inawezekana hujafahamu chanzo cha wewe kutopata mpenzi, lakini kuna mambo mengi ya kuzingatia ili uweze kupata mpenzi na hivyo kuepuka upweke katika moyo wako.

JAMBO LA KWANZA
Jiulize mwenyewe, unajijali? Inawezekana ukawa na maswali lukuki kutokana na ninavyouliza swali hilo? Nataka utambue kitu kimoja, kuwa kuna baadhi ya watu hawajipendi! Hivi unadhani kama wewe mwenyewe hujipendi, hujithamini nani atakupenda?

Ninaposema ujipende namaanisha ujipe upendo ule wa kawaida wewe mwenyewe kabla ya kuhitaji upendo wa mtu mwingine. Mwingine anaweza akawa anavaa nguo chafu, hapigi pasi, nywele zipo timtim nani atakupenda kwa muonekano huo?
Hakuna anayependa kuwa na mtu ambaye hana desturi ya usafi kwanza hata kama ni mzuri kiasi gani unapokuwa upo rafu hakuna mtu atakayeusumbua moyo wake kuanza eti kukufikiria wewe usiyejipenda.

Siyo lazima wakati wote uwe ‘smart’, kwa kuwa inawezekana wengine wanafanya kazi ngumu ambazo mazingira yake lazima anakuwa mchafu, lakini baada ya kazi unapaswa kuwa msafi kabisa mbele za watu.

Upande wa wasichana siyo lazima uweke nywele zako dawa au usuke rasta wakati vitu hivyo huna uwezo navyo, unaweza ukasuka nywele zako vizuri au wakati mwingine ukanyoa mtindo mzuri unaokubalika ambao hautakutafsirisha vibaya kwa jamii.

Anza kujipenda kabla ya kuhitaji upendo kutoka kwa mtu mwingine, hiyo itakusaidia kuwa na mvuto na mwonekano mzuri kiasi cha kuweza kumpagawisha mtu mwingine kuanza kuhisi cheche za moto wa mapenzi katika moyo wake.
Nina mengi ya kuzungumza nanyi kuhusu mada hii,lakini kutokana na changamoto ya nafasi finyu, vuta subira hadi wiki ijayo tutaendelea, USIKOSE! kusoma globalpublishers

UVUMI KIFO CHA RAY C

WAKATI msanii Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ akizikwa kijijini kwao, Muheza, Tanga Jumatano iliyopita, uvumi mkubwa umelitikisa Jiji la Dar es Salaam kuwa, mwanamuziki wa  Kizazi Kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ naye ameaga dunia ghafla.

Uvumi huo ulizagaa kwa kasi kuanzia saa kumi na mbili jioni kupitia mitandao ya kijamii na ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kupitia simu za mkononi huku wengine wakidai ni ‘komfemdi’.
Baadhi ya watu walianza kuamini uzushi huo na kujiuliza kulikoni katika burudani Bongo kuwapoteza mastaa wao mfululizo.
“Juzi tu Mlopelo, halafu John Maganga, jana (Jumatatu) Sharo Milionea. Leo tena Ray C, kuna nini kwa mastaa wetu?” alihoji mmoja wa  watu waliotumiwa ujumbe huo huku akishika kichwa kuonesha hali ya majonzi.

Hata hivyo, hadi kufikia saa 4 usiku, mama mzazi wa Ray C, Margaret Mtweve alijitokeza hadharani kupitia Radio Clouds FM na kukanusha vikali taarifa hizo huku akisema:
 “Mwanangu ni mzima, tena anaendelea vizuri kwa sasa. Hao wanaoneza uzushi huo washindwe kwa jina la Yesu.”
Awali, mchana wa siku
hiyo, zilienea tetesi eti msanii nyota wa sinema Bongo, Juma Sadiki Kilowoko ‘Sajuki’ naye amefariki dunia wakari si kweli.

Watu waliozungumza na gazeti hili jana walionesha wasiwasi wao mkubwa juu ya ufahamu wa baadhi ya Watanzania ambao wamekuwa na tabia ya kueneza uvumi mara kwa mara kwamba mtu f’lani, hasa maarufu amefariki dunia.
“Nahisi kuna Watanzania si wazima vichwani kwani sasa imekuwa fasheni. Mtu anaamua tu, anaandika ujumbe kwenye simu kwamba staa f’lani amefariki dunia wakati si kweli,” alisema Hamad Hussein, mkazi wa Magomeni-Kagera, Dar.

Thursday, November 29, 2012

VIONGOZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA BARABARA YA ARUSHA-NAMANGA-ATHI RIVER

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan naye alikuwepo hapo uwanjani.
                            Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikata utepe kwa pamoja kuzindua  rasmi wa Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye  urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania




 Baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu wa Tanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye  urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania
              Rais Jakaya Kikwete akitoaa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo





Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wa barabara hiyo kwa kukata utepe.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki  wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga      

Makamu Wa Rais Dkt. Bilal Aagana Na Rais Wa Kenya Mwai Kibaki

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, mara baada ya ufunguzi wa Jengo la ofisi za Jumuiya hiyo iliyofanyika Jijini Arusha jana, Nove 28, 2012.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi baada ya kumsindikiza Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, mara baada ya ufunguzi wa Jengo la ofisi za Jumuiya hiyo iliyofanyika Jijini Arusha jana, Nove 28, 2012

Maadhimisho Kupinga Ukatili Dhidi Ya Wanawake

                                                                  Mkuu wa mkoa wa singida
 Kikundi cha nyota njema kikitumbuiza ngoma ya asili ya kabila la Kinyaturu wakati wa maadhimisho ya siku ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia

SERIKALI imeyataka mashirika ya kiraia kushirikiana pamoja, ili kupiga vita na hatimaye kutokomeza kabisa vitendo vinavyosababisha ukatili wa kijinsia, hususani wanavyofanyiwa wanawake na watoto wadogo nchini.

Hayo yamebainishwa mjini Singida na mkuu wa mkoa huo, Dk. Parseko Kone, kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake, yaliyoadhimishwa kitaifa katika viwanja vya Peoples, mjini Singida, jana.

Maadhimisho hayo, yamefanyika mkoani Singida, kwa ushirikiano wa mashirika 16 hapa nchini, yaliyoipa dhamana ya kusimamia sherehe hizo, shirika la Action Aid-Singida,huku kauli mbiu yake ikiwa ‘FUNGUKA! Kemea ukatili dhidi ya wanawake, sote tuwajibike’.

Dk. Kone alisema kuwa, kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili wanawake ikiwemo ukatili wanaofanyiwa na wanaume, serikali kwa kushirikiana na mashirika ya kirai bado yanayo kazi kubwa katika kuungana pamoja ili kutokomeza unyanyasaji huo.

“Madhara yatokanayo na ukatili kwa wanwake katika jamii hupunguza nguvu kazi ya Taifa, baadhi ya madhara ya ukatili huo ni mauaji ya wanawake, ulemavu wa kudumu wa viungo…kupungua kwa uzalishaji kwa kuwa mwanamke ndiye mzalishaji mkuu kwenye kaya nyingi hapa nchini,”alisema Dk. Kone.

Mapema akimkaribisha mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, mkuu wa wilaya Singida mwalimu Queen Mlozi aliagiza kuwa ni vema sherehe kubwa kama hiyo inapofanyika mkoani hapa, wahusika wakashirikisha serikali ili iweze kufana zaidi.

Mwalimu Mlozi alilazimika kutoa amri hiyo, baada ya maadalizi, husani hamasa kuwa katika kiwango cha chini sana, hali iliyochangia uwanja kuonekana mtupu kutokana na watu wachache sana kujitokeza, vikiwemo vikundi vichache vya hamasa.

“Jamani ni vizuri maadhimisho makubwa kama haya yanapoletwa mkoani kwetu, basi wahusika wajitahidi kushirikisha serikali washirikiane pamoja kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi na wafurike kwenye sherehe,”alisema kwa masikitiko Mlozi.

Akizungumzia maadhimisho hayo, Juliana Bwire, afisa usawa na jinsi wa shirika la Concern worldwide kutoka jijini Dar es Salaam alisema siku 16 walizokuwa Singida, walizitumia vijijini kuielimisha jamii madhara ya ukatili, ikiwemo unyanyasaji, ukeketaji, na wanawake kunyimwa haki.

Aidha mmoja wa wanawake waliohudhuria sherehe hizo, Happynes Juma(30) mzaliwa wa Kigoma, alieleza kwa masikitiko ukatili aliofanyiwa na mumewe ikiwemo kudaiwa hajui kufanya mapenzi, hali iliyoleta mgogoro wa kifamilia na suala hilo lipo ustawi wa jamii, tayari kwa ajili ya kutengana.

Alisema maadhimsho hayo yatahitimishwa jijini Dar es Salaam siku ya desemba 8, mwaka huu.

Na Elisante John;Singida
Novemba 28,2012.

Hotuba Ya JK Bunge La Afrika Mashariki

Honourable Speaker;
Invited Speakers here present;
 Honourable Members of the East African Legislative Assembly, Distinguished Guests; Ladies and Gentlemen;

 I thank you, Hon. Speaker for giving me this rare opportunity to address this august Assembly at its 3rd sitting since its inauguration this year. I also thank you for the kind words you have spoken about me and my dear country, the United Republic of Tanzania.

Honourable Speaker; Since I am speaking to Members of East African Legislative Assembly for the first time since you were elected, let me take this opportunity to extend to you all my warm congratulations on your well deserved election. Your election is a testimony of the immense confidence and trust reposed in you. More so I wish to .... Read More... http://www.kwanzajamii.com

Jengo La Jumuiya Ya Afika Mashariki Lazinduliwa

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiangalia mfano wa jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya hiyo pamoja na maelezo yake baada ya kulifungua rasmi  Novemba 28, 2012 jijini Arusha
                     Mfano wa  jengo la Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifunua pazia  kufungua rasmi jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya  Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wabunge wa Afrika Mashariki

PICHA NA IKULU

Mkuu Wa Wilaya Na Nape Wamzika Sharobaro

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi, kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa pole za Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nauye, akitupa mchanga kaburini, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga.
 Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za Shirika la Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) la Mama  Anna Mkapa, kwenye msiba huo. Pamoja naye ni Nape

 (Picha na Bashir Nkoromo).