Wednesday, October 3, 2012

UNHCR Yaunga Mkono Wakimbizi Walioko Tanzania Kurudi Kwao

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limeipongeza na kuihakikishia Tanzania kwamba linaunga mkono mpango wa Serikali hiyo kuwarejesha nyumbani wakimbizi kutoka Burundi walioko katika kambi ya wakimbizi ya Mtabila na kuifunga rasmi kambi hiyo ifikapo mwezi Desemba, 2012 Aidha Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limeipongeza Tanzania kwa kwa jitihada zake za kuwahifadhi wakimbizi kutoka nchi za Maziwa Makuu na nchi mbalimbali duniani pamoja na kudumisha amani nchini humo.

 Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Geneva Mkurugenzi Mkuu wa UNHCR Bw. Antonio Gutteres wakati wa mkutano wa Kamati Tendaji(Executive Committee )ya shirika hilo uliofanyika Geneva Uswisi. Mkurugenzi huyo wa UNHCR alihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa UNHCR na Jumuia ya kimataifa inaunga mkono mpango wa Serikali ya Tanzania kuwarejesha Burundi wakimbizi wa Kambi ya Mtabila na kuifunga Kambi hiyo ifikapo Desemba 31 mwaka huu. Naye Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt .

Emmanuel Nchimbi alisema kuwa Tanzania inahifadhi jumla ya wakimbizi 100,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) na Burundi ambao wako nchini kutokana na vita vilivyokuwa nchini mwao.

 Aliongeza kuwa katika kutafuta suluhisho la wakimbizi nchini , Serikali kwa kushirikiana na UNHCR mwaka uliopita iliendesha mahojiano katika Kambi ya Mtabila inayowahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoko wilayani ya Kasulu mkoani Kigoma ili kutaka kujua idadi ya wakimbizi wanaotaka kurejea nchini mwao kwa hiari.

 Dr. Nchimbi alisema kuwa mahojiano hayo yaliyozingatia Sheria ya Kimataifa ya wakimbizi na Sheria za Kimataifa inahusika masuala ya ubinadamu ambapo wakimbizi 2,400 waliomba kuendelea kupata hifadhi hapa nchini na hivyo kuhamishiwa kambi nyingine.

 Aidha wakimbizi 38,050 walionyesha nia ya kurudi kwao kwa hiari na hivyo kupewa muda hadi Desemba 31 mwaka huu ili waweze kujiandaa kurejea katika nchi yao. Kufuatia hali hiyo Waziri huyo alitoa wito kwa wadau kuungana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa wakimbizi hao 38050 wanarudishwa kwao ifikapo Desemba 31 mwaka huu.

 Aidha kuhusu suala la wakiingia nchini mnamo mwaka 1972 , Waziri huyo alisema kuwa bado suala lao linajadiliwa ili kuangalia kweli wapewe uraia wa Tanzania au wasipewe. Mhe. Nchimbi aliwashukuru wadau mbalimbali kwa jitihada zao za kuisaidia Tanzania katika kukabiliana na wakimbizi na kuahidi kuendelea kuwapokea wakimbizi watakaohitaji hifadhi nchini Tanzania.

TWIN BRIDES MARRY TWIN GROOMS!!

                                                         Hawa ndio bi harusi pacha wa kike!!                                       
                                                        Wakiwa na waume zao pacha wa kiume!!!
                                        
                                                                      Mapambo Nice....................

UTAMADUNI WA VITU ASILI VYAIPANDISHA RWANDA KIUCHUMI

 Kwa hali ya kawaida utaona ni ngumu kuamini kwamba kitu kama utamaduni kinaweza kuwa chanzo kikubwa cha uchumi kukua katika nchi husika.
 Nchi ya Rwanda imekuwa moja kati ya nchi baarani Afrika ambayo imefanikiwa kukuza na kuendeleza utamaduni na sanaaa mbao tayari imekuwa ikichangia kalibia asilimia 60 ya mapato ya nchini na kuwapatia ajira vijana kwa urahisi.
 Mapato haya yamekuwa yakitokana  na fedha za kigeni ambazo wamekuwa wakitoa watalii kutoka nje ambao hasa wamekuwa wakihamasika kununua vitu vizuri vya asili ambavyo vinatengenezwa kiasilia na wasanii wa sanaa za utamaduni nchini humo.
  Mbali na  kuteka soko la watalii wamekuwa na vivutio  vya asili ikiwemo vyakula na ngoma.Taasisi zinazohusika na mambo ya utalii wamekuwa mstali wa mbele kutangaza vivutio hivyo ndani na nje ya nchi ukilinganisha na sisi wabongo ambao tunavivutio lukuki na tumeshindwa kunufaika navyo
Sijui idara zetu hapa Tanzania zenye dhamana ya mambo haya ya utamaduni  zinafanya nini.Inafahamika sisi ni the best more than Rwanda kwa vivutio,sijui tunakwama sehemu gani ama tatizo liko wapi! tunapaswa kujifunza kutoka kwa majirani zetu??? au wao wanapaswa kujifunza kutoka kwetu hii ni kweli kabisa watanzania tumebarikiwa sana Amani yetu ni moja ya kujivunia pili sisi tunaweza vijana wawezeshwa tu hasa kwenye sekta hizi za utamaduni wanafanya vizuri sana Serekali iangalie sekta ya utamaduni kwa jicho la pili...

MATUKIO KATIKA SEMINA YA VIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI

 Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, pia Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abduhamid Yahaya Mzee,wakati alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Zanzibar Beach Resort,kuiongoza  Semina ya Kuimarisha Uhusiano Baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar,ikiwa ni siku ya pili.
 Katibu Mtendaji  Tume ya Mipango Bi Amina Khamis Shaaban,alipokuwa akitoa mada ya nne ya Mpango wa Miaka mitano wa Utekelezaji wa Mkuza II,katika  Semina ya Kuimarisha Uhusiano Baina ya
Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar,ikiwa ni siku ya pili katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,akichangia Mada katika Semina ya Kuimarisha Uhusiano Baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar,ikiwa ni siku ya pili katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,ikiongozwa na Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani),na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee,(kulia).
 Baadhi ya Watendaji wa Idara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi wakisikiliza Mada zilizotolewa katika Semina ya Kuimarisha Uhusiano Baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar,ikiwa ni siku ya pili katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani).
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,akichangia Mada katika Semina ya Kuimarisha Uhusiano Baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar,ikiwa ni siku ya pili katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,ikiongozwa na Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani),na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee,(kulia).
Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiongoza Semina ya Kuimarisha Uhusiano Baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali ya Mainduzi ya
Zanzibar,ikiwa ni siku ya pili katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,(kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee.
                           
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Rufani Ya Lema Yatikisa Arusha

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akiwahutubia wafuasi wake baada ya Jaji MKuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman kuahirisha kesi ya rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.Picha Zote na Jackson Odoyo Mussa Juma, Arusha MAWAKILI wanaomtetea aliyekuwa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema wamedai mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuwa mteja wao yuko huru kwa kuwa mahakama haikutengua ubunge wake.Katika kesi hiyo, Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande anawaongoza wenzake wa Mahakama ya Rufani, Salum Massati na Natalia Kimaro kusikiliza maombi ya rufani hiyo, inayopinga Lema kuvuliwa ubunge.

Mawakili hao wa Lema jana walitoa hoja ya kupinga hukumu hiyo kufuatia mabishano baina yao na upande wa utetezi kwa maelezo kuwa taratibu za ufunguaji wa rufaa hiyo zimekosewa. Awali wakili Alute Mughwai aliiomba mahakama hiyo kutupilia mbali rufani hiyo kwa kile alichoeleza kuwa ina upungufu mwingi wa kisheria na kikanuni. Wakili huyo alitaja baadhi ya kasoro za rufani hiyo kuwa ni hati ya kukaza hukumu (tuzo) ambayo imewasilishwa mahakamani hapo kutokuwa na mhuri wa Jaji Gabriel Rwakibarila aliyetoa hukumu ya kesi hiyo.

 Alidai kuwa katika rufani hiyo pia kuna upungufu kuhusu tarehe za kuwasilishwa kwa rufani, pia baadhi ya vifungu vimekosewa.Wakili Mughwai alitoa kumbukumbu ya kesi kadhaa ambazo mahakama ya rufani ilizitupa baada ya kukosa hadhi ya kisheria kusikilizwa.

 “Mawakili wa Lema walipaswa kabla ya kuwasilisha mahakamani rufani yao, kujiridhisha kama kuna upungufu katika nyaraka ambazo wanawasilisha mahakamani.” Alisema kubwa katika makosa ambayo amebaini katika rufani hiyo ni kuwasilishwa bila kuwekwa mhuri hati ya kukaza hukumu (tuzo) iliyotolewa na Jaji aliyetoa hukumu katika kesi ya awali. “Hapa nani ambaye anajua sahihi ya Jaji? Alihoji. Hawa mawakili walipaswa kushinikiza kuwekwa mhuri wa mahakama katika hukumu hiyo ili kuthibitisha uhalali wake,” alisema Alute. Hata hiyo, wakili huyo alisema badala yake, mawakili hao waliwasilisha mahakamani rufani hiyo ndani ya siku 29 tu baada ya hukumu, badala ya siku 60 ambazo walipewa.

 “Kwa kuwasilisha mahakama ya rufani, hukumu ambayo bado haina mhuri wa Jaji ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za mahakama.” Mughwai alidai kuwa katika mazingira ya sasa hakuna cha kurekebishwa katika rufani hiyo, badala yake itupwe na kuwataka wakata rufani kulipa gharama zote za kesi. Hata hivyo, hoja hizo zilipingwa na mawakili wa Lema ambao ni Tundu Lissu na Method Kimomogoro, ambao walidai kuwa hawakuwa na mamlaka ya kumlazimisha Jaji Rwakibarila kuweka mhuri.

Lissu alidai "Kama inaonekana sasa kuwa ni batili, basi hata uamuzi wa kumvua ubunge Lema ni batili," alisema. Wakili Kimomogoro Kwa upande wake, Wakili Kimomogoro alisema kisheria kasoro hizo ya mhuri wa mahakama na tarehe, haziwezi kusababisha rufani hiyo kutupwa kwani haziathiri madai ya msingi katika rufani.

Alidai kesi hiyo ya Lema ilikuwa ya kipekee kwani mara tu baada ya hukumu kutolewa faili lilipelekwa jijini Dar es Salaam na maombi ya nyaraka kadhaa za kesi hiyo yalitumwa kutoka Dar es Salaam. “Katika mazingira kama haya hatuwezi kuepuka makosa ya kibinadamu ambayo yanatambulika kisheria,” alidai Kimomogoro. Aliongeza kuwa katika hoja hiyo, waliandika kifugu namba 114 badala ya 113 kimakosa ya kiuchapaji, lakini hakipotoshi kitu chochote kwani kifungu hicho hakipo. Wakili Kimomogoro alisema wakili mwenzake, Mughwai ameshindwa kuzungumzia uamuzi ya kesi ambazo, hazikufutwa kutokana na kuwa na upungufu mdogo wa aina hiyo ambao kimsingi hauathiri rufani.

Hata hivyo, alisema kama wakili huyo alibaini makosa hayo, katika uwasilishaji wa hoja zake, alipaswa pia kurekebisha kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2009 ya mahakama. Kimomogoro pia aliwasilisha mahakamani hoja kadhaa za kisheria na uamuzi ya Mahakama ya Rufani za ndani na nje ya nchi, ambazo hazikutupilia mbali rufani ambazo zilikuwa na upungufu mdogo, kwani lengo la mahakama hizo ni kutafuta haki.

 “Siyo kila kasoro au usumbufu kwenye hukumu unaweza kusababisha kutupwa rufani kwani kasoro zote zilizotajwa ni za makosa na uchapaji na nyingine ni za kiutaratibu tu,” alisema. Alifafanua kuwa makosa ambayo yanaweza kusababisha rufani kutupwa ni kama aina namba ya kesi, majina na wadhifa wa wadau katika shauri husika, mambo yanayolalamikiwa na mahakama imeamua nini.

Wakili huyo alifafanua kuwa jambo la kukosekana mhuri wa mahakama wa Jaji siyo kubwa na kusababisha kutupwa rufani kwani hakuna ambaye anapinga hukumu iliyowasilishwa mahakamani. Kwa upande wake, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Vitalis Timoth alisema anaunga mkono hoja za mawakili wa Lema, kuwa pingamizi ya wakili Mughwai haina msingi wa kisheria.

Alisema hati ya kukaza hukumu (Tuzo) inatolewa chini ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai na siyo chini ya sheria ya masijala za mahakama. Alisema siyo kazi ya jaji aliyetoa hukumu, kuweka mhuri hukumu yake bali hiyo ni kazi ya msajili wa mahakama na masijala za mahakama.

 “Kama hati ya kukaza hukumu ina matatizo anayepaswa kulaumiwa siyo mawakili bali ni mahakama ambayo ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kuweka mhuri,” alisema. Alidai kuwa pingamizi ya awali ya rufani inapaswa kuwa na sifa mbili, kwanza iwe na suala la kisheria na pili iendane na kesi ya msingi. “Katika hoja za wakili Mughwai ni wazi inathibitika pingamizi hili halina matakwa ya kisheria kwani hata kama ikipitwa siyo kuwa itazuia kurejeshwa tena na kusikilizwa kwa rufani ya msingi.” Alidai ni busara kuacha kuwa na pingamizi ambazo zinaongeza gharama za kesi na muda wa kusikiliza.

 “Ushauri wangu kila shauri liamuliwe kwa mazingira yake na uamuzi wa sasa uzingatie mahakama katika kutenda haki,” aliongeza. Alidai kwamba kutupwa kwa hoja ya kutaka waomba rufani wachapwe mijeledi kwani kazi ya mahakama siyo kuchapa watu bali ni kutoa haki. “Tunashauri kusikilizwa rufani kwa kuzingatia sheria na ushahidi,” alisema. Jopo la Majaji Baada ya kutolewa kwa hoja za pande zote za mawakili, Jaji Chande na Jaji Massati waliwauliza maswali kadhaa mawakili hao na kujieleza na baadaye Jaji Chande alitangaza kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi hapo itakapotangazwa. Jaji Chande alisema vikao vya Mahakama ya Rufani Kanda ya Arusha vimemalizika jana, hivyo uamuzi wa kutupwa kwa pingamizi la rufani hiyo au la utatolewa siku itakayopangwa na mahakama.

 Baada ya uamuzi huo umati wa wafuasi wa Chadema, uliokuwa ndani na nje ya mahakama ulianza kuimba nyimbo mbalimbali kama vile Lema Jembe na bila Lema patachimbika. Katika hatua ya kuepuka vurugu, Lema alizungumza na wafuasi hao nje ya mahakama na kuwataka kuondoka kwa amani kwenda katika ofisi ya Chadema iliyopo Ngarenaro kwa amani bila vurugu.

Warufaniwa katika kesi hiyo ni makada wa CCM, Happy Kivuyo, Mussa Mkanga na Agnes Mollel ambao walishinda kesi ambayo hukumu yake ilimvua ubunge Lema Aprili 4, mwaka huu.

 Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari

YAliyojiri Magazetini leo Jumatano ya 3rd October 2012