Saturday, June 29, 2013

HATARI LAKINI SALAMA!

 Randy Miller akicheza na chui wake Eden.
 Chui Eden akiwa amemdondosha chini mwalimu wake Randy
 Randy akiwa chini baada ya kudondoshwa na Eden.
 Marafiki hao wawili wakiwa katika pozi.Taswira hapo juu zinamwonyesha Bwana Randy Miller (45) akicheza na chui wake aitwaye Eden ambaye amemfundisha

jinsi ya kufanya mashambulio yasiyo na madhara na ambaye amekuwa akimtumia katika kucheza filamu mbalimbali.

Mambo 20 ya kusisimua kuhusu Obama

RAIS wa Marekani, Barack Obama, anatarajia kutua Tanzania Jumatatu. Watanzania wengi wanamsubiri kwa hamu, lakini je wanayafahamu mambo yanayovutia kuhusu rais huyo? Makala hii inayachambua mambo 20 ya kufurahisha kuhusu Obama.

1. Asili
Obama ni mchanganyiko wa damu ya Kenya, Ireland na England.

2. Namba 44
Ni Rais wa 44 wa Marekani. Rais wa kwanza alikuwa, George Washington, ambaye alitawala kuanzia mwaka 1789 hadi 1797.

3. Anapenda TV
Obama anapenda kuangalia televisheni. Anapenda kipindi cha ‘The Wire’. ‘The Wire’ ni tamthilia inayorushwa kwenye televisheni na inahusu upelelezi wa polisi.

4. Wa Kwanza
Obama ni rais wa kwanza wa Marekani ambaye amezaliwa Hawaii.

5. Ndugu yake
Rais Obama ana dada mmoja tu, anaitwa Maya. Hata hivyo Obama na Maya wamechangia mama tu, baba ni tofauti.

SIMULIZI ZA MZEE MADIBA; MANDELA BONDIA ALIPOKUTANA NA BONDIA…!

Ndugu zangu, Kuna simulizi nyingi za Mzee wetu Madiba. Hakika, Nelson Mandela hajawahi kuwa mpenda makuu. Mzee Mandela yuko simple sana, ni tangu enzi za ujana wake. Lakini, kuna ambao hawajui kuwa Mandela anapenda sana mchezo wa ngumi, na kuwa , yeye mwenyewe aliwahi kuwa bondia.

Kuna wakati akiwa Ikulu kama Rais, Mandela alipata habari za bondia wa Afrika Kusini aliyetwaa taji la  kimataifa. Mandela alifurahishwa sana na habari hizo. Akataka ampongeze mwenyewe bondia  huyo.Siku moja akiwa na wasaidizi wachache sana, Mandela alikwenda hadi nyumbani kwa bondia huyo. Alihakikisha kuwa bondia huyo yuko nyumbani kwake. Alipofika, Mandela aliwaambia wasaidizi wake wakamwambie bondia huyo kuwa nje kuna mtu anayehoji ubingwa wake.  Wamwambie kuwa  mtu huyo ( Nelson Mandela) anadai kuwa yeye ndiye bingwa wa uzito huo katika Afrika Kusini ( Nelson Mandela!) Kwamba anataka mkutane mpange siku ya kupigana ili apatikane mshindi halali wa taji hilo.

Basi, bondia yule akapokea habari hizo na akatamani sana amwone huyo anayedai kuwa ana ubavu wa kupambana naye. Alipotoka nje akakutana na Nelson Mandela akiwa amesimama getini na amekunja ngumi yake. Akatania; “ Nimekuja kwako tuzipige ili dunia imjue bingwa halisi!”

Ikawa ni furaha kubwa kwa bondia yule. Hakuamini macho yake. Kuwa Rais wa nchi amekuja nyumbani kwake kumpongeza.  Kumpongeza kwa jambo kubwa alilolifanya kwa taifa la Afrika Kusini.

Na Mandela akawa tayari kuingia nyumbani kwa bondia huyo na kunywa nae chai!

What a Great Leader Of Africa! Yes, Nelson Mandela!

Maggid Mjengwa,

Iringa.

OBAMA, MANDELA SIRI NZITO!


MAMBO mawili ndiyo habari ya mjini kwa sasa; umahututi wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Rolihlahla Mandela ‘Madiba’ (94) na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Husein Obama katika nchi tatu za Afrika.

NDEGE YA OBAMA NI NYUMBA INAYOTEMBEA AIR Force One ni ndege kubwa ya Rais wa Marekani. Ndege hii ina sifa nyingi kama ndege nyingine, lakini ina nyongeza ambayo kwenye ndege nyingine hakuna. Air Force One ambayo imewahi kuchezewa filamu iliyoitwa kwa jina hilohilo na staa wa muvi za Hollywood, Harrison Ford imeonekana ndiyo ndege yenye usalama zaidi duniani. SIFA KUBWA: Ndani ya ndege hiyo kuna ofisi ya rais, jiko, chumba cha mikutano, bafu, sehemu ya kuvalia nguo, eneo la kufanyia mazoezi ‘gym’ na chumba cha mawasiliano. Ndiyo maana inasemwa ni nyumba inayotembea. Pia kuna chumba cha maafisa wanaomlinda rais, sehemu yao ya kufanyia mkutano wakipata dharura na zahanati kama rais akiugua ghafla wakati ndege ipo angani. Si hayo tu, kuna chumba chenye simu 85 za mezani na Tivii 19 kwa ajili ya kupata habari za kidunia wakati ndege ipo juu. Ndege hiyo haikamiliki kuiita Air Force One bila kutambulisha sehemu maalum ambayo hutumika kijeshi kumkwepesha adui anayetaka kuilenga kwa lengo la kuilipua.

 AIR Force One ni ndege kubwa ya Rais wa Marekani. Ndege hii ina sifa nyingi kama ndege nyingine, lakini ina nyongeza  ambayo kwenye ndege nyingine hakuna.

Air Force One ambayo imewahi kuchezewa filamu iliyoitwa kwa jina hilohilo na staa wa muvi za Hollywood, Harrison Ford imeonekana ndiyo ndege yenye usalama zaidi duniani.
SIFA KUBWA:
Ndani ya ndege hiyo kuna ofisi ya rais, jiko, chumba cha mikutano, bafu, sehemu ya kuvalia nguo, eneo la kufanyia mazoezi ‘gym’ na chumba cha mawasiliano. Ndiyo maana inasemwa ni nyumba inayotembea.

Pia kuna chumba cha maafisa wanaomlinda rais, sehemu yao ya kufanyia mkutano wakipata dharura na zahanati kama rais akiugua ghafla wakati ndege ipo angani.

Si hayo tu, kuna chumba chenye simu 85 za mezani na Tivii 19 kwa ajili ya kupata habari za kidunia wakati ndege ipo juu.

Ndege hiyo haikamiliki kuiita Air Force One bila kutambulisha sehemu maalum ambayo hutumika kijeshi kumkwepesha adui anayetaka kuilenga kwa lengo la kuilipua.