Monday, December 10, 2012

Udahili Wanafunzi Wa Kitivo Cha Afya Kuongezwa


Serikali inatarajia kuongeza udahili wa wanafunzi wanaosomea masomo katika sekta ya afya nchini kutoka wanafunzi 7500 hadi 10,000 kwa mwaka ifikapo 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa wadau wa chanjo barani Afrika uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema udahili huo utasaidia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa watumishi katika sekta hiyo.

Waziri Mwinyi amesema uhaba wa wafanyakazi katika sekta ya afya umesababisha kutowafikia watoto wote nchini ili kuwapatia chanjo za magonjwa mbalimbali.

Kwa upande wake muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa Tanzania, Lufaro Chatora amesema shirika hilo likisaidiana na Wizara ya Afya wanafanya jitihada ya kuongeza magari ili kuwafikia wototo wote na kuwapatia chanjo.Mkutano huo wa siku tatu unawakutanisha wadau 200 wa huduma ya chanjo kutoka nchi mbalimbali barani afrika ambapo pamoja na mambo mengine watajadili jinsi ya kuboresha na kuimarisha huduma ya chanjo.

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

Hotuba Ya Mkuu Wa Mkoa



Ndugu wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Tarehe 11/12/2012 siku ya Jumanne kutakuwa na Sherehe za makabidhiano ya majengo ya huduma za mama na mtoto katika Hospitali za Mnazi Mmoja, Sinza na Rangi tatu.Makabidhiano hayo yatafanywa na Balozi wa Korea kusini kwa niaba ya watu wa Korea Kusini kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Ndugu wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Makabidhiano hayo yataanzia katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo katika Wilaya ya Ilala kuanzia saa 2:30 asubuhi mpaka saa 5:00 asubuhi.Baada ya hapo makabidhiano hayo yataelekea katika hospitali ya Sinza iliyopo katika Wilaya ya Kinondoni kuanzia saa 5:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana na kuishia katika hospitali ya Rangi Tatu iliyopo katika Wilaya ya Temeke kuanzia saa 7:00 mchana mpaka saa 9:00 alasili.

Ndugu wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Wakati huo huo,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete atazindua na kukabidhi nyumba 36 za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto zilizojengwa katika eneo la Msongola lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Makabidhiano hayo yatafanyika kuanzia saa 8:00 mchana mpaka saa 10:00 jioni.

Ndugu wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Nawaomba mfike kwa wingi kushuhudia makabidhiano ya majengo ya huduma za mama na mtoto katika Hospitali za Mnazi Mmoja, Sinza na Rangi tatu pamoja na uzinduzi na kukabidhi nyumba 36 za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Said Meck Sadiki
MKUU WA MKOA WA
DAR ES SALAAM
10/12/2012

Siku zote penye upendo wa kweli utakuwa huru


Kitu muhimu na kikubwa baba anachoweza kufanya kwa watoto wake ni kumpenda mama yao''

Maneno haya yamenikuna kweli leo baada ya kuyaona nikayatafakari sana.Ni kweli kabisa baba anapompenda mama watoto wanaona kwa matendo.Na baba anapokuwa sie watoto wanajua kabisa baba mzushi tu kwa mama.
Kazi kwenu kina baba,mara nyingi napenda kutumia picha za familia hii kwa sababu naipenda.

Kama una picha ya familia yako nzuri na hauna tatizo nikiitumia hapa.Basi nitumie ikiwa na ujumbe wowote ule na mie nitaiweka pasipokusahau utambulisho. 
     

Kinana Akutana Na Makatibu CCM Mikoa

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao chake cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo, Desemba 11, 2012, katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na wengine kutoka kushoto ni Makatibu wa NEC,  Asha-Rose Migoro (Siasa na Mambo ya Nje), Zakia Meghji (Uchumi na Fedha), Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao chake cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai
 Makatibu wa CCM wa mikoa wakiwa kwenye mkutano wao na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai akisalimiana na Katibu wa NEC, Siasa na Mambo ya Nje, Asha-Rose Migiro, kabla ya kuanza kikao cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Muhammed Seif Khatib.

(Picha na Bashir Nkoromo).

JK: Atunuku Nishani 40

                             Bi. Kidude akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jana
                       Bi. Kidude akiveshwa nishani na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jana
                           Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Eusebia Munuo akivishwa nishani
Rais jakaya Kikwete akimvisha nishani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue  ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana ametunuku  nishani kwa watu kutoka makundi mbalimbali yajamii waliotumikia taifa kwa uadilifu na kutoa mchango wa pekee.Miongoni wa waliotunukiwa nishani jana ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Eusebia Munuo pamoja na Msanii Mkongwe Bi.Fatma Baraka Khamis(Bi.Kidude).Wengine waliotunikiwa nishani ni pamoja na Watumishi wa umma na askari Jeshi na Polisi.
Picha na IKULU

Models For The Year 2012

 Ailinda Sawe receiving awards from Dana Banks director of pUBLIC Communication at US emnbassy in Dar es salaam
gabriel mollel receiving the DESIGNER OF THE YEAR award from Hon. jerry Silaa
FEMALE MODEL OF THE YEAR - Nadia Ali

 MALE MODEL OF THE YEAR - Benson Kwembe

EAST AFRICAN MODEL OF THE YEAR - Joseph Kimeu (KE)

DESIGNER OF THE YEAR - Gabriel Mollel

EAST AFRICAN DESIGNER OF THE YEAR - John Kaveke (KE)
MENSWEAR DESIGNER OF THE YEAR - Martin Kadinda

UPCOMING DESIGNER OF THE YEAR - Lucky Creations

INNOVATIVE DESIGNER OF THE YEAR - Gabriel Mollel

REDDS FEMALE STYLISH PERSONALITY - Nancy Sumari

MALE STYLISH PERSONALITY - Andrew Mahiga

VODACOM FASHION BLOG OF THE YEAR - Missie Popular

FASHION PHOTOGRAPHER OF THE YEAR - Osse Greca Senare

FASHION JOURNALIST OF THE YEAR - Maimuna Kubegeya (MCL)

EAST AFRICAN JOURNALIST OF THE YEAR - Susan Wong (Capital Group)

FASHION TV PROGRAMME OF THE YEAR - Nirvana (EATV)

Best Exhibition Stand – Codesh Jewellery

Origin Africa Award – Ailinda Sawe

New Face of the Year – Rachida Usuale

Emerging designer Competition Award – Phylista Oniango – Kenya

Humanitarian Award – Asia Idarous

Zakhia Meghji Lifetime Achievement Award – Farouque Abdela – Zanzibar

magazeti ya leo Jumatatu ya 10h December 2012