Monday, August 13, 2012

Prof: Sheriff Na Jenerali Ulimwengu Wakutana Na Tume Ya Mabadiliko Ya Katiba

Mtaalamu wa historia na mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar, Profesa Abdul Sheriff (kushoto) akifafanua jambo katika mkutano wa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam (Jumatatu, Agosti 13, 2012). Wengine ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Joseph Warioba, Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid (kulia).
              
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameendelea kukutana na kubadilishana mawazo na uzoefu na Wataalam mbalimbali kuhusu Katiba Mpya kwa lengo la kuongeza uelewa wao na leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012), kwa nyakati tofauti, Wajumbe wamekutana na Prof. Abdul Sheriff na Ndg. Jenerali Ulimwengu.

Tayari Tume hiyo imeshawaalika na kukutana na kwa nyakati tofauti na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza mzalendo Jaji Mark Bomani, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Pius Msekwa na Mhadhiri wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Issa Shivji.

Prof. Sheriff ni mtaalam wa historia na mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar na kwa muda mrefu amekuwa akishiriki na kutoa mada katika makongamano mbalimbali yanayohusu Katiba. Ndg.Ulimwengu ni Mwanasheria na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi ambaye pia ameshiriki na kutoa mada katika makongamano mbalimbali yanayohusu Katiba Mpya.

Mbowe;- Siongozi Genge La Wasaka Vyeo

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe amesema kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka ndani ya chama chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.Kiongozi huyo amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea Urais au Ubunge kwa sababu huu si muda wake hata kidogo.

Mbowe amesema mwanachama yeyote makini wa Chadema kwa sasa ni muda wa kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla na wala si muda wa kuwagawa kukimbilia madaraka. Kiongozi huyo amesema ndiyo maana makamanda wote wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini kwa kazi moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C.

Chanzo: Tanzania Daima.

JK Awasili Kutoka Ghana, Afuturu Na watoto Yatima Na Walemavu Ikulu

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik muda mfupi baada ya kuwasili akitokea nchini Ghana ambapo alishiriki mazishi ya aliyekuwa Rais wan chi hiyo Marehemu John Atta Mills.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamnyange.

Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakigawa zawadi kwa watoto yatima na walemavu walohudhuria futari waliyowaandalia ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.

                         Picha na Ikulu

Magazeti ya Leo Jumatatu 13rd August 2012

Shangwe Na Majonzi Kwenye Mapokezi Ya Dr Ulimboka Alipowasili Nyumbani

 Umati wa watu wakisubiria Dr Ulimboka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere
  Amewasili jamani Dr Ulimboka alishindwa kujizuia akatokwa na machozi kwa Umati alioukuta Ukimsubiri uwanjani hapo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Tanzania, Dkt. Ulimboka Stephen, amerejea salama nchini leo mchana na kutoa shukrani za dhati kwa Watanzania kwa dua na michango yao kuinusuru afya yake na kuahidi kuendeleza mapambano dhidi ya huduma bora za afya na maslahi kwa Madaktari.

Dkt. Ulimboka, aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, saa 8:00 mchana na ndege ya Shirika la SA Airways, akitokea nchini Afrika Kusini, alipokwenda kwa matibabu.

Madaktari wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, Wanaharakati na wananchi wengine, walimlaki kwa shangwe, hoihoi, nderemo huku wakiwa na mabango yenye ujumbe ambao GlobalPublishers.info imenukuu kuwa ulisomeka:

“DR. Ulimboka karibu nyumbani.”
“DR. Ulimboka, damu yako iliyomwagika inaamsha ari ya wananchi kudai haki ya afya.”
“DR. Ulimboka wewe ni mpigania haki ya afya bora kwa wananchi wote. Mungu na Watanzania wote tuko nawe.”

Kwa upande mwingine, Dkt. Ulimboka baada ya kukuta umati mkubwa uwanjani, alishindwa kujizuia, hivyo akatoa machozi kisha akasema: “Nawashukuru sana Watanzania kwa kuwa pamoja na mimi kwa maombi, sasa nimerejea nikiwa na afya njema, mapambano yanaendelea,” na kuongeza: “Watu wacheze na watu lakini wasicheze na Mungu, hasa Mungu wangu mimi.”

Na, Waandishi wa Globalpublishers

Serikali Kulipa Mishahara Ya Wafanyakazi TAZARA

                                                 Waziri wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe

WAZIRI wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe amesema serikali itabeba jukumu la kulipa mishahara ya wafanyakazi Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA, baada ya wafanyakazi hao kucheleweshewa mshahara yao kwa kipindi cha miezi mitatu.

Kauli hiyo imekuja baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kufikisha kilio chao kwa Waziri huyo kuwa wamekuwa wakiishi maisha ya kubangaiza kutoakana ucheleweshwaji wa mishahara yao.

Akizungumza na wafanyakazi hao, kwenye ofisi za Shirika hilo (TAZARA), jijini Dar es salaam jana, Dk Mwakyembe alisema akiwa waziri wa wizara hiyo anawaahidi hatakubali kuona wanaishi bila kulipwa mishahara huku wakifanya kazikwa juhudi.

Dk Mwakyembe alibainisha kuwa serikali imepokea kilio chao hivyo italipa sh bilioni1.3 kama mshahara wa miezi miwili kati ya miezi hiyo mitatu wanayodai kuanzia leo (jana).

Aliitaja miezihiyo itakayolipwa kuwa ni pamoja na Juni na Julai ambapo amewataka viongozi wa Shirika hilo kutoa maelezo kuwa ni kwanini hadi sasa hawajalipa mishahara wafanyakazi hao.

Akizungumzia madai ya wafanyakazi hao ya kutaka kung’olewa madarakani kwa Mkurugenzi Mkuu,Mbegusita Akashambatwa na Naibu wake, Damus Ndumbalo, alisema shirika hili ni la kimataifa linalohusisha nchi mbili hivyo maamuzi yake ni lazima ya husishe viongozi wa pande zote mbili.

Aidha, alitoa onyo kuhusu vitendo vya hujuma ikiwa ni pamoja na wizi kuwa wale wote wanaojihusisha watambuwe kuwa dawa yao iko jikoni inachemka.


Katika hatua nyingine amesema amesikitishwa sana kuona kuwa wafanyakazi wa Mradi wa Ukarabati wa Train Mijini, hadi leo hawjalipwa mishahara ya miezi miwili,fedha hizo lilikwishatengwa.

“Nilisikitika sana kumkuta yule dada Mwanamisi akiwa amevaa overrol lake huku akiunganisha vyuma tena amefunga mfungo wa Ramadhani ambapo aliniambia tunafanyakazi lakini hatujalipwa mishahara inishangaza sana nataka walipwe haraka”alisema Dk Mwakyembe.
Awali Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi shirika hilo, Ernest Kiwele, alisema wamechoshwa na tabia za viongozi hao kuwa wamekuwa chanzo cha matatizo yote yanayowakabili wafanyakazi hao.

Alisema Mkurugenzi Mkuu na Naibu wake wamekuwa wakiendesha Shirika hilo kwa kujali zaidi maslahi yao na jamaa zao hata wale waliosimamishwa kazi kwa kuwalipa mishahara.

Chanzo: www.fullshangweblog.com

Mnyika Ajibu Mapigo Ya Nape...!

Katika mitandao ya kijamii kumesambazwa habari zikimnukuu msemaji wa CCM kutoa madai mbalimbali ya uzushi katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu CHADEMA baada ya CHADEMA kuendelea kutekeleza mikakati na mipango yake ya kuwaunganisha watanzania kupitia falsafa ya ‘nguvu ya umma’ katika kuchangia vuguvugu la mabadiliko (M4C) katika maeneo mbalimbali nchini.

Nitatoa tamko kamili na kueleza hatua za ziada baada ya kupata taarifa iliyotolewa kwa ukamilifu, hata hivyo kuhusu madai yaliyokwisha sambazwa kwenye mitandao ya kijamii na CCM nachukua fursa hii kutoa kauli ya awali kama ifuatavyo: Kuibuka huku kwa CCM na kufanya propaganda chafu ni ishara ya kwamba CCM inaumizwa na namna ambavyo watanzania wanajitokeza kuunga mkono CHADEMA kwa hali na mali hivyo CCM sasa inatapatapa kujaribu kudhibiti wimbi la mabadiliko kwa kutumia siasa chafu.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete anapaswa kueleza watanzania iwapo mikakati hiyo michafu ina baraka zake na za serikali anayoiongoza kwa kurejea pia madai yaliyotolewa na Waziri wa Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Steven Wassira kuwa CHADEMA itasambaratishwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa mbinu mbalimbali. CCM kwa kuwa imekuwa na kawaida ya kufanya usanii kuhalalisha fedha haramu kama ilivyofanya kwenye chaguzi zilizopita baada ya viongozi waandamizi wa CCM na makada wake kuchota fedha za chafu kifisadi kama zile za kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na vyanzo vingine vichafu na kuzisafisha kupitia harambee za hadaa zilizofanywa na CCM kwa nyakati mbalimbali; inataka kuichafua CHADEMA inayopata fedha kutoka vyanzo halali kwa njia za wazi ili kukatisha tamaa umma wa watanzania unaochangia vuguvugu la mabadiliko. Viongozi wa CCM wameamua kujidanganya, kuidanganya Serikali yao na kujaribu kuwapotosha watanzania lakini CHADEMA inatambua kwamba watu wachache wanaweza kudanganyika kwa muda mchache lakini si watu wote wakati wote; na kwamba watanzania wa leo kwa uwingi wao hawawezi kudanganyika na uzushi wa kijinga wa CCM.Ni ukweli ulio wazi kwamba CHADEMA imekuwa ikifanya harambee kwa uwazi kwa nyakati mbalimbali katika kumbi na katika mikutano ya hadhara ikiwemo ya vijijini ambapo michango hutolewa kwa uwazi, aidha michango kwa njia ya simu inaweza kufuatiliwa na kuthibitisha bila shaka yoyote kwamba watanzania wameamua kuchangia mabadiliko ya kweli.Madai ya CCM kuwa CHADEMA imepokea au itapokea mabilioni ya shilingi kutoka mataifa ya nje ni ya uzushi na narudia kwa mara nyingine tena kuitaka CCM itaje majina ya serikali, taasisi ama makampuni ya nje ambayo CCM inadai kwamba CHADEMA imepokea mabilioni ya shilingi katika siku za karibuni au inatarajia kupokea.

Tanzania Kufuta Usajili Wa Meli Za Iran

Serikali ya Tanzania inasema meli za mafuta 36 za Iran zimesajiliwa tena nchini Tanzania, ili kujaribu kukwepa vikwazo dhidi ya Iran vilivowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya.

Uchunguzi uliofaywa na serikali ya Tanzania, ambao ulionekana na shirika la habari la Reuters, unaonesha kuwa serikali haikujua lolote kuhusu shughuli hizo za kuzipatia meli za mafuta za Iran bendera ya Tanzania - shughuli iliyokuwa ikifanywa na wakala alioko Dubai.Mafuta ya Iran yamewekewa vikwazo, ili kuishawishi Iran iache mradi wake wa nuklia.Tanzania imeacha kuagiza mafuta kutoka Iran.

Uchunguzi ulifanywa na serikali ya Tanzania, baada ya mbunge mmoja wa Marekani, Howard Berman, mwenyekiti wa kamati ya Congress ya maswala ya nchi za nje, kueleza wasiwasi wake juu ya meli hizo za Iran kupatiwa bendera ya Tanzania. Tanzania sasa inasema itafuta usajili wa meli hizo.

Chanzo:  http://www.bbc.co.uk/swahili/habari