Friday, January 25, 2013

St.Johns university walipoandamana






Wanachuo wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwa mkuu wa mkoa hii ni kushinikiza ulinzi kwa sababu ya matukio ambayo yanaendelea kutokea maana juzi alifariki mwanachuo na usiku wa kuamkia leo wanachuo walivamiwa vyumbani  baada ya kukata nondo ya dirisha na kuiba Laptop tatu na simu tano na baada ya kuchukua vitu hivyo waliacha wamewafanyia vitendo vibaya na pia waliachwa wamefungwa ili wasipige kelele.

Kwa hali hii  imesababisha maandamano ili kushinikiza ulinzi katika chuo cha St. John kilichopo Dodoma mjini.

Magazeti ya leo Ijumaa ya 25th January 2013


TAARIFA KUHUSU DHAMANA YA MWIGIZAJI LULU AMBAYO ILIKUA ITOKE LEO.

                                                         Elizabeth Michael.

Jana kwenye Exclusive on millardayo.com kulikua na stori kwamba uwezekano wa mwigizaji Lulu kuachiwa kwa dhamana january 25 2013 ulikuepo.

Ni kweli ilikua iwe hivyo lakini kwa taarifa  zilizotolewa kwa Millard Ayo ni kwamba dhamana hiyo imeshindikana kutolewa leo.

Sababu kubwa ni leo kuwa sikukuu hivyo shughuli imesogezwa mbele mpaka jumatatu january 28 2013.

Mwanzoni Lulu ambae anatuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia ilidaiwa alikua anatakiwa apate dhamana ambayo milioni 20 zilihitajika (kwa mujibu wa taarifa za ndani) ila ikashindika sababu jaji alipata udhuru.

Lulu amekua chini ya ulinzi toka kifo cha mwigizaji staa wa movie Tanzania Steven Kanumba April 2012.

Chanzo:Millard Ayo

Sitta: Nafaa kuwa Rais

“Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri nigombee,” Akizungumza katika mahojiano (soma zaidi hapa)

maalumu na gazeti hili juzi, Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri. Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

MISS UTALII VIPAJI KUFANYIKA TAREHE 27.01.2012

 Tamasha kubwa la vipaji litafanyika katika Ukumbi wa Ikondolelo Lodge  Hoteli ya Kitalii  Kibamba Jumapili hii, ambapo warembo zaidi ya Thelasini   wataingia katika kuonesha vipaji mbalimbali vikiwemo na, Kucheza ngoma, Kuimba, pamoja kuonesha mavazi mbalimbali ya Asilia.

Katika Tamasha hilo Maalum Mgeni Rasmi atakuwa Muheshimiwa Iddy Azan Zungu  Mbunge wa  Jimbo la kinondoni. Sambamba na Hayo Muheshimiwa Zungu atazindua tuzo Mbalimbali za Utalii Tanzania, kama Tuzo ya Mazingira, Tuzo ya Utamaduni, Tuzo ya Jinsia, wanawake na watoto, Tuzo ya Polisi Jamii, Tuzo ya Elimu ya Jamii, Tuzo ya Hifadhi ya Serengeti, Tuzo ya Mlima Kilimanjaro, Tuzo ya Michezo pamoja na Tuzo  zengine mbalimbali.

Viingilio katika Tamasha hilo vitakuwa kama ifuatavyo, V.I.P 20,000 , Watu wa kawaida 10,000 na watoto 5,000.

Tamasha litaanza kuanzia sa nane mchana na kuendelea.

Asante.

Fredy Tony Njeje

Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano

JAPAN YAIPA TANZANIA BILIONI 28.2 KUBORESHA BARABARA NA KILIMO, MAKUTANO YA TAZARA KUWA NA BARABARA ZA JUU KWA JUU

 SERIKALI ya Japan imepatia Tanzania msaada wa shilingi bilioni 28.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mitatu ya uboreshaji wa usafiri jijini Dar es salaam na kilimo hapa nchini.

 Msaada huo umesainiwa (leo) jijini Dar es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Masaki Okada kwa niaba ya Japan na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa kwa niaba ya Serikali ya Tanzania.

 Akizungumza mara baada ya kusaini msaada huo Waziri wa Fedha Dkt . Mgimwa alisema kuwa mradi wa kwanza utahusisha upanuzi wa barabara ya Kilwa na ile ya Bandari ambapo jumla ya shilingi bilioni 20 zitatumika katika kukamilisha mradi huo.

 Aliongeza kuwa mradi mwingine ni ule wa ujenzi wa barabara za juu(flyover) katika makutano ya TAZARA ambapo jumla ya shilingi bilioni moja (1) na milioni 26 zinatarajiwa kutumika katika kukamilisha mradi huo.

 Dkt. Mgimwa aliongeza kuwa eneo lingine ambalo litanufaika na msaada kutoka Japan ni kuunga mkono sera ya Kilimo kwanza ambapo Tanzania imepata shilingi bilioni sita(6) na milioni 92 kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwepo kwa usalama wa chakula cha kutosha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

 Alisema kuwa upande wa eneo hilo lengo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wa kipato cha chini wanaboresha kilimo ambacho kitawahakikisha uhakika wa chakula wakati wote na hivyo kuondokana na umaskini.

 Kwa upande wa Balozi wa Japan hapa nchini Masaki Okada alisema kuwa wananchi wengi wa Tanzania hasa wakazi wa Jiji la Dar es salaam wamekuwa wakisubiri kwa hamu barabara za juu ili kusaidia kupunguza msongamano wakati wa kuja na kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam.

 Alisema kuwa utakapo kamilika mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la msongamano na hivyo kupunguza saa za mwananchi kusafiri kuja na kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam.

 Balozi Okada alisema kuwa hatua hii itakuwa muhimu katika kukuza uchumi kwani wananchi watakuwa na muda wa kutosha kuzalisha mali kutoka na miundombinu kuruhusu magari kwenda kasi pasipo kikwazo.