Tuesday, August 21, 2012

MATOKEO YA MECHI ZA PRIMERA DIVISION AUG 20 2012.


Meles Zenawi Is Dead

July 31, 2012 — Prime Minsiter Meles Zenawi passed away from an unspecified aliment in a Brussels hospital, according to Ethiopian Satellite Radio and Television (ESAT) in its nightly raido broadcast.

Citing the International Crisis Group and western diplomatic sources for its claims, the Amsterdam-based news agency said the 57-year-old dictator's death is being covered up by the regime to buy time for a successor.

Meles, whose appearance is the daily diet of the State media, has not been publicly seen in 40 days, fueling speculations that his health has deteriorated. During his absence, he has missed key events, including the two-day AU Summit held in Addis Ababa and a number of state visits.

Last week, unnamed European diplomats told the AFP and the Telegraph news agencies that Meles was in 'critical' condition and may not survive his aliment.

The other day, veteran fighter and Tigrayan Peoples Liberation Front founder, Sehbat Nega, said Meles is still in a European hospital but is not sure to which country. This uncertainty comes two weeks after he said Meles would return within a few days.

Sources say a select few of TPLF bigwigs are in the know of Meles deteroriting health status. Even senior officials within the TPLF party are being kept in the dark to prevent a power struggle from within.

Talk of Meles' health troubles has Addis Ababa on edge. Recently, An Ethiopian court banned distribution of a newspaper that published front-page articles about premier's health on the grounds of endangering 'national security'.

Miss World Tanzania 2012 Arejea Kutoka China

 Lisa Jensen (kulia) akila pozi ya picha na mmoja wa warembo waliofika kumpokea Amisa Hassan. Lisa alifanikiwa kuingia Robo fainali za Top Model na kumi na kumi bora ya Shindano la Multmedia Award 2012.
Miss World Tanzania 2012, Lisa Jensen amerejea jijini Dar es Salaam jana akitokea nchini China alipokwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia mwaka huu na kupokelewa na viongozi kadhaa wa Kamati ya Miss Tanzania akiwepo Mkurugenzi wa Kino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) aliyefika uwanja wa ndege wa JNIA Dar es salaam kumpokea. Chanzo: www.mrokim.blogspot.com

DK.Dalali Kafumu Avuliwa Ubunge Igunga!.

Kwa habari zilizotufikia hivi punde  kutoka mahakamani kuwa mbunge wa Igunga kwa ruhusa ya CCM  Dk. Peter Dalali Kafumu  Amevuliwa Ubunge na Mahakama, Habari zaidi zitakujia hivi punde usikae mbali na blog hii

Sitta:Msiisubiri Serikali Kutaja Walioficha Mabilioni

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewataka wanaotangaza kuwafahamu vigogo walioficha mabilioni ya fedha nje ya nchi kuwataja mara moja ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao badala ya kuisubiri Serikali kufanya hivyo.Kauli hiyo ya Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), imekuja wakati baadhi ya wanasiasa, wakiwamo wabunge kutishia kuwataja watu hao, lakini wakisisitiza kuwa ni pale tu Serikali itakaposhindwa kufanya hivyo.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Fedha la Global Financial Integrity, unaonyesha kuwa tatizo la utoroshaji wa fedha nchini limekuwapo katika awamu zote za Serikali zilizoiongoza Tanzania, lakini Awamu hii ya Nne imetia fora.

Utafiti huo uliofanywa kuanzia mwaka 1970 hadi 2009, unaonyesha kuwa katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete, fedha zilizofichwa nje ya nchi ni Dola za Marekani 7,967.4 milioni (sawa Sh12.7 trilioni).
Akizungumza katika mahojiano maalumu, kuhusu nini kifanyike ili kuiokoa Tanzania isiendelee kufilisiwa na watu wachache, Sitta alisema anasikitishwa na watu hao kuogopa na kuwaficha watu wanaofisadi mali za nchi na hasa pale inapokuwa wahusika ni vigogo wa Serikali.

Alisema vigogo hao ni sababu ya watu kupata kigugumizi katika hili akihoji : “Kwa nini linapokuwa ni suala linalowahusu hawa wanaoitwa vigogo hawatajwi?”

Sitta ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini katika awamu tofauti, alisema haoni kama kuna kosa kumtaja hadharani mtu aliyeficha fedha nje ya nchi huku akisababisha Watanzania kuendelea kukabiliwa na maisha magumu.

“Watajwe! Kama ni Samuel Sitta ameficha fedha nje atajwe. Kwa kweli mimi sioni kama kuna dhambi yoyote kumtaja,” alisema Sitta huku akisisitiza kwamba huo ni msimamo wake binafsi unaotokana na uzoefu wake kwenye uongozi wa nchi na siyo kwa mamlaka aliyonayo ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Alisema njia nzuri ya kukomesha tabia hiyo ni kuwataja na vyombo husika kuwafikisha mahakamani kwa kuzingatia kuwa sheria ni msumeno, haipaswi kubagua aliye mdogo au mkubwa kwa maana ya wadhifa katika nchi.Sitta ambaye pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge alisema: “Swali la kwa nini hawatajwi, ni jambo la kushangaza.”

Alisema amesikia na kuwasoma baadhi ya wanasiasa wakitishia kuwa watawataja wahusika iwapo Serikali haitafanya hivyo, lakini akasema haoni sababu yoyote ya mtu kusita katika kuokoa taifa dhidi ya wizi wa fedha za umma.

“Haiwezekani kwa mwanasiasa yeyote katika nchi maskini kama Tanzania au kiongozi wa Serikali kuwa na utajiri wa mabilioni ya fedha.”

Alisema hata kama anafanya biashara, siyo rahisi kuwa na utajiri wa kiwango hicho hasa ikizingatiwa kuwa hutumia muda mrefu kulitumikia taifa.
“Sisi tunaofanya kazi serikalini, tunatoka saa moja usiku. Sasa muda huo wa kufanya biashara ni saa ngapi?”

Tuhuma hizo ziliibuka bungeni Jumatano iliyopita baada ya Kambi ya Upinzani kudai kwamba nawafahamu wahusika wa ufisadi huo na kutishia kuwataja ikiwa Serikali haitafanya hivyo.

Chanzo  http://www.mwananchi.co.tz

Magazeti ya Leo Jumanne 21st August 2012




















Yanga Yaicharaza African Lyon 4-0

Kikosi cha timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Taifa kabla ya kuingia uwanjani
               Kikosi cha timu ya Africa Lyon kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpambano huo kuanza.
Beki wa timu ya Yanga, Oscar Joshua (kulia) akimtoka mshambuliaji wa African Lyon, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo jioni. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa Mabao 4-0. Bao la kwanza la Yanga, limefungwa na kipa wa African Lyon, Juma Abdul, aliyejifunga katika dakika 8, kipindi cha kwanza, bao la pili limefungwa na Haruna Niyonzima kwa mkwaju wa penati, dakika ya 54, baada ya beki wa Lyon Semi Kessy, kumchezea rafu, Msuva katika eneo la hatari. Goli la tatu limefungwa na Simon Msuva, katika dakika ya 72, kufuatia pasi safi ya Frank Dumayo na bao la nne limefungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 90+2, baada ya pasi safi ya Idrisa Rashid.

Chanzo: www.fullshangweblog.com