Friday, October 12, 2012

MATOKEO YA CHAGUZI ZA CCM - WAZAZI MKOANI ARUSHA...!

CHAMA cha mapinduzi mkoa wa arusha  kimemchagua mbunge  wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Bernard Murunya,  kuwa Mwenyekiti wa Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha.

Aidha  uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa makao makuu ya CCM Mkoa wa Arusha jana, Murunya aliwashinda wenzake watatu kwa kupata kura 169 kati ya kura 334 zilizopigwa.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Mary Chatanda, ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Viti Maalum, aliwataja wagombea wengine katika nafasi hiyo na kura walizopata kwenye mabano kuwa ni Edwin Seneu (1), Mohammed Festo (68) na Musa Mkanga (69).

Kwa upande wa  nafasi ya Baraza Kuu la Taifa Wazazi/Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, aliyechaguliwa kuchukua nafasi hiyo ni John Pallangyo kwa kupata kura 211 na kuwashinda Mbunge wa Viti Maalum, Namelok Sokoine (112), Harun Matagane (6) na Baltazar Lymo (4).

Aidha nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ilikwenda kwa Fatuma Ngairo aliyepata kura 312 dhidi ya Mohammed Said Hassan (21) na Jonas Lubulu (6) na kwa upande wa Baraza la Wazazi la Mkoa ilinyakuliwa na Lucy Bongole (239) dhidi ya Mariam Athman Majengo (78) na Filemon Amo (7).

Akizungumza baada ya kuchaguliwa kwake, Murunya ambaye ni Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA), lisema Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha, inakabiliwa na tatizo la ukata ambapo ulisababisha ugumu kuwasafirisha wajumbe kutoka maeneo mbali mbali wilayani kuhudhuria uchaguzi huo muhimu.

Hata hivyo, alisema chini ya uongozi wake atahakikisha kwamba analitafutia ufumbuzi tatizo hilo ndani ya kipindi cha miaka miwili, “Tutafanya mikakati kuhakikisha Jumuiya inaondokana na ukata, tutabuni miradi ya kupata fedha na ndani ya miaka miwili mtakuja hapa mkiwa kifua mbele,” alitamba Murunya.

Bado hekaheka inaendelea kusafisha jiji

                             ilianza hivi wakizozana na mgambo na wafanyabiashara
                                                                      Wakatokea hawa
                                             Akapandisha kwenye gari huku akipewa kipondo
                                                        Je hali hii itaendelea hadi lini?

Magazeti ya Leo Ijumaa 12th October 2012

Kamati Ya Bunge Ya Masuala Ya Ukimwi Yataka Ripoti ARV Bandia Kutinga Bungeni

KAMATI ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi imeishauri serikali kutoa tamko la kuelezea ni hatua gani inaendelea kuchukua baada ya kusimamisha kazi baadhi ya viongozi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kufuatia kuwepo kwa dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi( ARV) katika kikao cha Bunge kitakachoanza mwishoni mwezi huu.

 Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Lediana Mng’ong’o wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dares Salaam kuhusu kuwepo kwa dawa hizo.

 “ Sisi tungependa kuishauri serikali kuendelea kufuatilia na hatua za kisheria pale itakapobaini katika uchunguzi huo ili tatizo hili lisiendelee kutokea,” alisema Lediana ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Iringa.

Aliongeza kuwa wanaishauri Mamlaka cha Chakula na Dawa (TFDA) kuwa na wawakilishi katika kanda mbalimbali ili kuweza kudhibiti tatizo la kuwepo kwa dawa bandia.

 Aidha kamati hiyo imelaani kampuni ambayo imeingiza dawa feki na imetaka hatua za kisheria zichukuliwe. Kamati hiyo imewataka watu wanaotumia dawa hizo kutoziacha , bali waendelee kuzitumia kwa kuwa dawa zote si feki na pia zipo za kutosha.

Jaji Manento amkaanga RPC Iringa

        ASEMA RPC KAMUHANDA ALIVUNJA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA KUZUIA      MIKUTANO YA CHADEMA, AMSHUKIA TENDWA, KAMATI YA NCHIMBI YAPINGWA


TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, imetoa ripoti yake kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi ikisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda alikiuka Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2002, huku ikiisafisha Chadema kuwa haikukosea kufanya mkutano.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Kiongozi Mstaafu, Amiri Manento alisema jana alipokuwa akisoma ripoti hiyo kuwa Kamuhanda alikiuka sheria hiyo Sura ya 322 kwa kuingilia kazi za OCD wa Mufindi kuzuia shughuli za Chadema wakati hakuwa mkuu wa polisi wa eneo hilo.

 Ripoti hiyo ni ya tatu kutolewa, baada ya juzi, Kamati ya Kuchunguza Mauaji hayo iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi iliyokuwa chini ya Jaji Steven Ihema kuwasilisha ripoti yake pamoja na Baraza la Habari Tanzania, kuweka hadharani ripoti yake.

 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2001 ikiwa na majukumu ya kulinda, kutetea na kuhifadhi haki za binadamu nchini. Jaji huyo mstaafu alisema kutokana na hilo, amri ya RPC Kamuhanda kutaka yapigwe mabomu ya machozi, haikuwa halali kwa kuwa ilitolewa na mtu ambaye hakuwa na mamlaka kisheria.

"Haya ni matumizi mabaya ya mamlaka na pia ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora," alisema. Pia Tume hiyo imeishukia hatua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa kuviandikia vyama vya siasa kuvitaka kusitisha shughuli zao kwa sababu ya sensa kuwa inakinzana na Sheria ya Takwimu Na. 1 ya mwaka 2002, inayotoa fursa kwa wananchi kuendelea na kazi zao wakati wa sensa.

"Vilevile, ni kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2002 kifungu cha cha 11(a) na (b) inayotoa fursa kwa vyama vya siasa kufanya shughuli zake bila ya kuingiliwa,"alisema. Jaji Manento alisema wamejiridhisha kuwa tukio lililosababisha kifo cha Mwangosi, limegubikwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.