Thursday, June 21, 2012

DOGO JANJA ANARUDI DAR KESHO, YOTE MENGINE ALIYOYASEMA NDIO HAYA.

Pamoja na kwamba aliapa hatorudi tena Dar ni bora aende kuishi kwao Arusha baada kutoridhika na vitu alivyokua akifanyiwa na Meneja Madee wa Tip Top Connection, Dogo Janja ametangaza kurudi Dar ijumaa ya kesho June 22 2012.

Exclusive na AMPLIFAYA Janja ambae amemaliza wiki moja toka arudi kwao Arusha, amesema “namshukuru Mungu amesikia kilio changu na nakuja kucheki mikataba ya kujiunga na kundi la WATANASHATI kwa Ostaz Juma na kama nitaridhika na mikataba nitajiunga nao, nimekaa na wazazi wameniambia zile zilikua hasira tu nirudi Dar es salaam kusoma na kufanya muziki kweli nikakaa nikajifikiria nikaona ni sawa”

Janja mwenye umri wa miaka 16 kwenye sentensi nyingine amesema “Ostaz kaniambia atanisomesha shule ambayo nitakua nasoma napelekwa na kurudishwa nyumbani na gari nitakua sina mawazo, kama mashabiki wangu mnanipenda njooni mnipokee Airport ijumaa nitatua na ndege pale”

KWA MASHABIKI WOTE WA MAREHEMU KANUMBA.


Bado mpaka sasa kumbukumbu za watanzania hazijalala, movie star marehemu Steven Kanumba bado anakumbukwa kwa sababu bado kazi zake nyingi alizozifanya zinaendelea kuonekana katika maisha ya kila siku ya watanzania wengi.

Wakati huu ambapo maonyesho ya sabasaba yanakaribia kuanza Dar es salaam familia yake imeamua kuchukua banda maalum kwenye viwanja vya saba saba kwa ajili tu ya kuendelea kumuenzi Marehemu Kanumba.

Seth ambae ni Mdogo wake waliekua wakiishi pamoja Sinza Dar es salaam amesema ni banda la Kanumba litakalokua na Nguo zenye alama alizokua anazitumia Kanumba ikiwa ni pamoja na jina na ujumbe, kutakua na picha zilizo kwenye frame za Kanumba zinazomuonyesha toka akiwa utotoni, pia vikombe, kanga, bazee na vitu vingine vingi vyenye alama na picha za Kanumba.

Taswira Za Mheshimiwa Godbless Lema Akiung'uruma Kwenye Mkutano Wa Hadhara Wa CHADEMA Manzese Jijini Dar es Salaam

Aliyekua Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)Mheshimiwa Godbles Lema Akiunguruma kwenye mkutano wa hadhara Manzese jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Umoja wa Baraza la Vijana wa CHADEMA John Henche(kushoto)akifwatilia kwa makini mkutano wa Chadema.
Sehemu ya Umati Mkubwa wa Wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa chadema

Omotola Kuizindua Supa Star ya Wema Sepetu Jumapili Giraffe Hotel

Ni onyesho maalum la familia
MKALI wa filamu nchini Nigeria na Afrika, Omotola Jalade atazindua filamu ya Wema Sepetu Jumapili hii katika Ukumbi wa Hoteli ya Girafee Ocean View, iliyopo Mbezi Beach.
Filamu hiyo iitwayo Super Star imechezwa na Wema, ikionyesha maisha ya mtu maarufu na changamoto anazozipata ikiwemo kuandikwa  mambo mbalimbali ikiwemo taarifa za vyombo vya habari.
Katika uzinduzi huo, bendi kutoka Tanzania House Of Talent (THT) watatoa burudani, kabla ya mashabiki kupata nafasi ya kupiga picha na msanii huyo.
Omotola, ambaye ni mke wa rubani Kapteni Matthew Ekeinde, ambao walifunga ndoa yao angani kwenye ndege atatoa nafasi ya kupiga picha na watu kadhaa.
Katika uzinduzi huo, pamoja na burudani ya muziki, mashabiki watakaofika hapo, watapata pia fursa ya kuiona filamu ya Super Star katika viwanja hivyo vya hoteli hiyo iliyoko ufukweni.
Omotola ambaye yuko kwenye ndoa kwa miaka 16 akiwa na watoto wanne, ana jumla ya albamu mbili za muziki.
Msanii huyo ambaye mwaka jana alitangaza kuachana na kucheza filamu kutokana na kuandikwa vibaya, anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwenye uzinduzi huo ambao kiingilio kitakuwa Sh 30, 000 kwa wakubwa na watoto 10,000. USIKOSE.

HONGERA MY SISTER KILA KITU KINAWEZEKANA, YOU CAN CHANGE YOUR PROFILE.


I WISH YOU COULD HELP CAPTION THIS