Monday, August 6, 2012

KUHUSU MGOGORO WA MPAKA NA MALAWI, HII NDIO KAULI MPYA YA TANZANIA.

                         Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe.
Straight kutoka bungeni Dodoma kuhusu ishu ya mpaka wa Malawi na Tanzania ni kwamba waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe amesema Malawi wanadai kwamba mpaka wa Tanzania na wao kwenye ziwa Nyasa unapita Pwani hivyo ziwa lote kutoka kwenye mpaka wa Malawi na Mozambique hadi Kyela ni mali ya Malawi.

Amesema “serikali yetu ilipata habari za kuaminika kupitia shirika la TPDC kuwa eneo lote la ziwa Nyasa kaskazini mwa Msumbiji limegawanywa kwenye vitalu na kwamba serikali ya Malawi imevitoa vitalu hivyo kwa kampuni ya utafiti wa mafuta na gesi”

“Makampuni hayo yaliomba kibali cha kuruhusu ndege za utafiti ziwani humu ombi ambalo jeshi la Wananchi wa Tanzania lilikataa, pamoja na katazo hilo serikali yetu ilipata ushahidi kwamba ndege ndogo za utafiti zenye uwezo wa kutua majini na ufukweni zinazokadiriwa kuwa tano zilionekana zikivinjari na kutua katika ziwa Nyasa upande wa Tanzania na kwenye ufukwe wake January 29 na July 2 2012″ – Bernard Membe

“Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inathamini sana uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi mbili na ina dhamira ya kudumisha na kuimarisha uhusiano wa ujirani mwema kwa manufaa ya watu wetu, inapenda kuchukua nafasi hii tena kuitaka serikali ya Malawi kuheshimu makubaliano ya July 27 2012″ – Waziri Membe.

Pamoja na ahadi ya kuwalinda raia laki sita waliopo kwenye mwambao wa ziwa Nyasa, Waziri Membe amesema “serikali ya Tanzania inapenda kuchukua nafasi hii tena kuyaonya na kuyataka makampuni yote yanayofanya shughuli ya utafiti kwenye eneo hilo kusitisha kuanzia sasa, kuacha shughuli za utafiti katika maeneo hayo”

HUYU NDIO MCHEZAJI ALIESAJILIWA NA SIMBA NA LEO.

Klabu ya Simba imeendelea kufungua milango yake katika soko la usajili baada ya wiki iliyopita kumtwaa Mbuyi Twite na Mrisho Ngassa, leo hii klabu hiyo imemsajili kiungo wake wa zamani aliyekuwa akiichezea Azam Fc Ramadhan Chombo Redondo.

Taarifa rasmi kutoka kwa Redondo mwenyewe ni kweli amesaini mkataba na Simba akitokea Azam baada ya mkataba wake kumalizika, ambapo  Shaffihdauda.com imemkariri akisema “Nimesaini mkataba wa miaka miwili na Simba nikiwa mchezaji huru baada ya mkataba wangu na mwajiri wangu wa zamani  Azam kumalizika”

Redondo ambaye aliondoka Simba miaka 3 iliyopita, amesaini Simba kwa ada ya millioni 3 ambapo leo wakati akisaini amepewa shilingi millioni 20 na millioni 10 baadae.

Uzinduzi wa Mashine za Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester)


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akiwasha Mashine ya Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mashine hizo,zilizonunuliwa na Serikali ya Mapinduzi zikiwa jumla 14 katika kuboresha hatua za Mapinduzi ya Kilimo,katika Shamba la Mbegu Bambi,Wilaya ya Kati  Mkoa waKusini Unguja leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(wa sita kushoto)akiangalia  Mashine ya Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) baada ya kufanya  uzinduzi wa
Mashine hizo,zilizonunuliwa na Serikali ya Mapinduzi zikiwa jumla 14 katika kuboresha hatua za Mapinduzi ya Kilimo,katika Shamba la Mbegu Bambi ,Wilaya ya Kati  Mkoa waKusini Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiangalia Mpunga Ukitoka katika mashine ya  Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) baada ya kuzindua mashine  hizo katika shamba la Kilimo la Serikali huko Bambi Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini Unguja  leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiangalia Mpunga Uliovunwa kwa kutumia  mashine ya  Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) baada ya
kuzindua mashine  hizo katika shamba la Kilimo la Serikali huko BambiWilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini Unguja  leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Uongozi wa Wzara ya Kilimo na Maliasili,baada ya kuzindua rasmi  mashine za Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) katika hafla iliyofanyika leo huko shamba la Kilimo la Serikali,  Bambi Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,  akizungumza na wananchi na wakulima wa Mpunga wa Maeneo mbali mbali baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa
mashine za Kuvunia Mpunga (Combine Harvester) huko Shamba la  Kilimo la Serikali huko Bambi Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Kilimo na Maliasili Suleiman Othman Nyanga,(katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Othman Affan Maalim, baada ya kumalizika hafla ya kuzindua mashine za (Combine Harvester) leo katika shamba la Kilimo la Serikali huko Bambi Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini Unguja.

Picha na Ramadhan Othman,IKulu.

TANZANIA YAPATA NAFASI YA KUKAGUA HESABU ZA UN

 Edwin Rweyumamu kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)  akimkaribisha CAG ambaye pia ni Mkaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa (UN) Ludovick Utouh ili aweze kuongea na waandishi wa habari kuhusu  Tanzania kupata nafasi ya kukagua hesabu za UN kwa kipindi cha miaka sita. Watumishi 60 kutoka ofisi ya CAG  watafanya kazi ya kuzikagua taasisi 10 za UN.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) ambaye pia ni Mkaguzi wa hesabu za Umoja wa Mataifa  (UN) Ludovick Utouh akiongea na waandishi wa habari kuhusu  Taasisi 10 za UN ambazo zitafanyiwa ukaguzi chini ya usimamizi wake ambapo watumishi 60 kutoka ofisini yake watafanya kazi hiyo. Kwa kipindi cha miaka sita nchi za Tanzania, China na Uingereza zimepewa jukumu la ukaguzi  wa hesabu za UN.

Picha na Anna Nkinda – Maelezo

Dkt Migiro awafunda wabunge wanawake wa Tanzania

 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliyemaliza muda wake Dkt Asha Rose Migiro akiwa kwenye picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda pamoja na wanachama wa chama cha wabunge wanawake wa Tanzania. Dkt Migiro yupo mjini Dodoma kwa mwaliko wa Spika wa Bunge. Ametumia fursa hiyo kukutana na wabunge wanawake na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo ya Tanzania
Ndipo Spika wa Bunge akamwandalia na kumkaribisha mgeni wake kwenye futari maalum katika cafeteria yaBunge.

SBL Moshi wamuaga aliyekuwa mkurugenzi wao Richard Wells

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wapili kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dr. Msengi
 Richard Wells (kushoto) akiwa akitika vazi la jadi la jamii ya Wamasaa pamoja na Kisu jamii ya sime alilokabidhiwa na Wafanyakazi wa SBL mjini Moshi wakati walipomuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake na kumkaribisha Mkurugenzi Mpya Steven Gannon
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wapili kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (wapili kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda  wakati wa tafrija maalum ya kumuaga Wells iliyofanyika Kiwanda cha SBL mjini Moshi hivi karibuni.
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (katikati) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells wakati wa tafrija maalum ya kumuaga Wells iliyofanyika Kiwanda cha SBL mjini Moshi hivi karibuni.
 Mama Tundu Pinda akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL aliyemaliza muda wake, Richard Wells wakati wa tafrija ya kumuaga iliyofanyika kiwanda cha SBL mjini Moshio hivi karibuni.
                         Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi mpya wa SBL, Steven Gannon
 Mkurugemzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda akitunzwa na Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela kwa kutoa burudani ya aina yake wakati wa tafrija hiyo ya kumuga Richard Wells.
 Wafanyakazi wakiwa wanaendelea na vitu vya hapa na pale wakati wa tafrija hiyo ya mkumuga Mkurugenzi Mtendaji aliyemaliza muda wake Richard Wells mjini Moshi.
 Hapa kazi tu.....Mkurugemzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapundana Mkurugenzi wa Masoko Epraim Mafuru wakiimba wakati wa tafrija hiyo ya kumuaga Richard Wells.
 Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa SBL, Steven Gannon akisakata rumba na wafanyakazi wa SBL Kiwanda cha Moshi.
 Richard Wells akicheza mziki na Wafanyakazi wa Kiwanda cha SBL mjini Moshi wakati wa tafrija ya kumuaga.

WANAIGIZA AU, ILA TUMUOMBEE WEMA

                 Wema Sepetu akifanyiwa vipimo katika Hospitali ya Heameda, Upanga jijini Dar.

STAA wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amelazwa katika Hospitali ya Heameda, Upanga jijini Dar akiandamwa na magonjwa ya tumbo na kifua, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda limeinasa.
Awali kulazwa kwa staa huyo katika hospitali hiyo kulifanywa siri na ndugu zake ambao hawakutaka kuwaambia mapaparazi wa gazeti hili alipo Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006.

CHANZO CHA UGONJWA
Kwa mujibu wa mtu aliyenyetisha habari hiyo, alisema jamii inatakiwa kumuombea Wema kutokana na kuteseka sana na hali ya kushindwa kupumua.
Chanzo hicho kimesema kuwa Beautiful Onyinye amekula vumbi jekundu kwa wingi baada ya kwenda Kigoma hivi karibuni kwenye Tamasha la Kigoma All Stars.

ASHINDWA KUPUMUA
Vumbi hilo jekundu limembana Wema na kumfanya asumbuliwe na tumbo na kubanwa na kifua kiasi cha kumfanya ashindwe kupumua.

HOSPITALI, DOKTA WA DIAMOND
Wema amelazwa katika hospitali hiyo ambayo siku chache zilizopita alikuwa amelazwa kichaa wa Bongofleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na gazeti dada na hili la Ijumaa la wiki iliyopita kuripoti habari hiyo.
Mbali na kulazwa hospitali moja na wodi moja pia daktari anayemchunguza afya Wema ni yuleyule aliyekuwa akimtibu Diamond ambaye anadaiwa kurudisha uhusiano wa kimapenzi na Wema walipokuwa katika ziara hiyo ya Kigoma.

HUYU HAPA WEMA
Gazeti hili lilifanikiwa kupenya katika hospitali hiyo na kuonana ana kwa ana na Wema na kumuuliza kinachomsumbua.
“Kikubwa ni kifua, nahisi kama vile nina pumu, huwa kinanibana na kunifanya nishindwe kupumua vizuri, hata hivyo namshukuru Mungu naendelea vizuri.”

ANA MZIO NA VUMBI
“Kitu kingine siwezi kuvumilia hali ya vumbi, nilipokuwa Kigoma hali hiyo ilinitokea mara kwa mara kwa sababu ya lile vumbi la udongo mwekundu. Kosa nililolifanya nilivyorudi Dar sikucheki afya hadi imefikia hali hii,” alisema Wema kwa tabu.
Wema alishatoka hospitalini hapo na kurudi kwa mama yake mzazi kwa ajili ya uangalizi wa karibu wa afya yake.

Chanzona Picha: GlobalPublishers

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWEPO KWA MGONJWA WA EBOLA, WILAYA YA KARAGWE MKOA WA KAGERA, TANZANIA

                                     JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                                     WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWEPO KWA MGONJWA WA EBOLA, WILAYA YA KARAGWE MKOA WA KAGERA, TANZANIA

Utangulizi
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma, kuhusu tetesi zilizokuwa zimeenea hapa nchini kutoka kwenye vyombo mbali mbali vya habari kuhusu kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola,wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.

Mnamo tarehe 3 Agosti 2012, Wizara ya Afya na Ustawi Wa Jamii ilipokea taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya ya Karagwe ya kuwepo kwa mgonjwa aliyekuwa anahisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola, katika hospitali ya Wilaya ya Nyakahanga. Aidha,taarifa hiyo ilibainisha kuwa mgonjwa huyo alikuwa ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (6|) kutoka katika kijiji cha Nyakatundu wilayani Karagwe. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali, kulegea, kutokwa damu puani, kutapika damu, na kukojoa damu.Maelezo kutoka kwa mama mzazi zilieleza kuwa mtoto huyu alianza kuugua kuanzia tarehe 30 Agosti 2012, ambapo alipatiwa dawa ya Septrin baada ya hospitali binafsi kuonyesha kuwa ana ugonjwa wa“Typhoid”.

Uchunguzi wa awali katika hospitali ya Nyakahanga ulionyesha kuwa mtoto huyu alikuwa anasumbuliwa na uambukizo kwenye haja ndogo (Urinary Tract Infection).Vile vile alifanyiwa uchunguzi wa kimaabara na Vipimo vya malaria, Hepatitis na Typhoid havikuonyesha kuwepo kwa magonjwa haya. Hospitali inaendelea kumpatia matibabu mtoto huyu na imewaweka mgonjwa na mama yake anayemtunza kwenye chumba maalum (Isolatiom room) kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Aidha mnamo tarehe 4 Agosti 2012, timu za wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na timu ya mkoa wa Kagera imeweza kufika na kumfanyia uchunguzi wa kina pamoja na kuchukua sampuli za damu kwa ajili ya uchunguzi zaidi katika maabara ya Taifa ya uchunguzi wa magonjwa na Maabara za nje ya nchi, ili kubaini kama ameathirika na ugonjwa wa Ebola. Timu hiyo ya wataalamu imetoa taarifa kuwa hali ya mgonjwa huyu kwa sasa imeimarika ikiwa pamoja na kutokuwa na homa, kutapika na kukojoa damu kumekoma pia, uchunguzi uliofanywa kwa mama wa mtoto umeonyesha kuwa hana dalili zozote za ugonjwa wa Ebola.Vile vile hakuna taarifa ya mtu mwingine yeyote kwenye familia hiyo au kwenye maeneo ya kijiji hicho au cha jirani kuwa na dalili za ugonjwa huo.


Kufuatia taarifa hii, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Mkoa wa Kagera imechukua hatua zifuatazo;
• Imepeleka timu ya wataalamu mbali mbali kutoka Wizarani na mkoa kwa lengo la kwenda kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huo.
• Imetoa elimu ya Afya kuhusu njia za kuzuia kuenea ugonjwa wa Ebola pamoja na dalili za ugonjwa huu, kwa wananchi na watumishi wa afya katika hospitali ya Nyakahanga
• Kupeleka vifaa kinga katika hospitali ya Nyakahanga pamoja na maeneo ya mipakani
• Kutoa matangazo kwa jamii kwa kutumia vipaaza sauti na kupitia radioni (Radio Karagwe) kuhusu ugonjwa huu. Aidha, vipeperushi pia vimetolewa.


Hitimisho

Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola hapa nchini.Aidha, Wizara ya Afya imejiaanda kikamilifu kukabiliana na ugonjwa huu iwapo utatokea hapa nchini.

Kwa sasa timu za wataalum zipo katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha, kutoa elimu juu ya ugonjwa huu kwa wataalamu na kwa wananchi na vilevile kufuatilia ugonjwa huu sehemu za mipakani.

Wizara inaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa haraka kwenye kituo chochote cha kutolea huduma za afya, mara wanapoona dalili za ugonjwa huu.

Imetolewa na: kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Afya na     Ustawi wa Jamii
Tarehe 6 Agosti, 2012

Magazeti ya leo Jumatatu 6th August 2012