Thursday, February 7, 2013

Kiongozi wa Chadema alipokwenda kumjulia hali Askofu Thomas Leizer Kabla ya Kifo chake

Askofu Thomas Leizer, katika siku za mwisho za uhai wake, akiwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya Selian Hospital Arusha Centre. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe. Picha hii ilipigwa Tarehe 3 Februari 2013, ambapo viongozi wa CHADEMA (Mbowe na Lema) walifika kumjulia hali, baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa

Picha kwa Hisani ya Jamiiforums.

Taswira bungeni leo

 Baadhi ya Maafisa Habari  Mawasiliano Serikalini  wakielekea katika Ukumbi wa Mkutano wa Bunge leo Dodoma. Maafisa hao  wamefanya ziara  Bungeni hapo ili kuona  shughuli za Bunge,
                                                   Aggrey Mwanri akijibu hoja Bungeni
Naibu Waziri, Ofisi ya  Waziri Mkuu (TAMISEMI) Aggrey Mwanri akiwakilisha hati mezani kuhusu Taarifa ya  Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha,2010/2011.

(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete azindua vitambulisho vya taifa

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyesha kitufe kuashiaria kuzindua rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofnyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu na kulia nia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said Meck Sadik.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiangalia bango lenye kitambulisho cha  taifa cha Rais Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua mfumo wa Usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya  Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi

Tanzia; askofu katoliki msarikie amefariki dunia

Askofu Mstaafu wa jimbo Katoliki la Moshi Mhashamu Amedeus Msarikie Amefariki Dunia.

WAMA yakabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 700

Taaasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) imeikabidhi hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine  kontena lenye  urefu wa futi 40 lenye mitambo na vifaa vya huduma ya afya vya kisasa  ilivyochangiwa na Shirika linayoshughulika na utoaji wa huduma za kibinadamu la  Project C.U.R.E la nchini Marekani vyenye thamani  ya shilingi milioni mia saba Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika viwanja vya...

Askofu Leizer wa KKT amefariki dunia

                            Askofu wa Kanisala KKKT Thomas Leizer enzi za uhai wake

ASKOFU  wa lKanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania ( KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer amefariki dunia alasiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha.

Askofu Leizer amefikwa na mauti ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kumjulia hali hospitalini hapo.Taarifa zilizolifikia hivi punde zinadai kwamba Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna Daktari wala ndugu aliyekuwa tayari kusema ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.

Waziri Mkuu alifika hospitalini hapo jana saa saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari wakizuiliwa kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wa Madaktari (ICU).

Hata hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiliwa kuzungumza na mgonjwa huyo.

Kabla ya Waziri Mkuu kufika katika hospitali hiyo na kumjulia ali taarifa zilizowahi nkutolewa na ndugu pamoja na watu wa karibu ikiwemo uongozi wa hospitali hiyo ilidai kwamba Askofu Laizer alihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, baada ya watu wengi kumiminika katika Hospitali ya Selian kutaka kumjulia hali.

Deni la taifa; kila Mtanzania anadaiwa Sh450,000

Baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza matokeo ya sensa, inayokaribia watu 45 milioni, siku chache baadaye deni la taifa lilitangazwa kufikia Sh21 trilioni huku katika wastani kila mtu akidaiwa Sh467,404. Fedha hizo zinatokana na mkopo baada ya Serikali kukopa kwa ajili ya kujenga miundombinu kama barabara, bomba la gesi, mishahara ya wafanyakazi, na...

miradi mingine.
Kwa mujibu wa taasisi isiokuwa ya kiserikali ya Tanzania Coalition on Debt and Development (TCDD), serikali inadaiwa ‘mzigo wa madeni’ unaofika Sh21 trilioni.

Kasi mpya ya bunge letu tukufu..


Magazeti ya leo Alhamisi 7th February 2013