Monday, March 25, 2013

WEMA SEPETU AJITOLEA KUTOA MILIONI 13 KUMUOKOA KAJALA ALIEHUKUMIWA MIAKA MITANO ....

Leo imesomwa hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili mcheza filamu za Kitanzania anayefahamika kwa jina la 'Kajala Masanja' na mumewe mbele ya Hakimu 'Sundi Fimbo' kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam.

 Katika hukumu hiyo 'Kajala'  amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.

Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe 'Faraji Agustino' kukumbwa na makosa ya kutakatisha fedha haramu.

Hata hivyo baada ya hukumu hiyo kutolea mahakamani hapa, mwanadada mwenye michejo mingi hapa Bongo anayefahamika kwa jina la Wema Sepetu' aliweza kujitolea yeye mwenyewe kiasi cha Tsh. milioni 13 kutoka mfukoni mwake kwa ajili ya kumlipia msanii mwenzake wa filamu 'Kajala' asiweze kutumikia adhabu ya kifungo hicho cha miaka 5 jela.

 Hii ni mara ya pili kwa msanii 'Wema Sepetu' kujitolea kiasi kikubwa cha fedha kusaidia msanii mwenzake.!

BREAKING NEWS: MSANII KAJALA MASANJA AHUKUMIWA MIAKA 5, MUMEWE MIAKA 7

Habari  njema kwa mashabiki wa muigizaji Kajala Masanja ambaye leo hukumu yake imesomwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200. Taarifa kutoka mahakamani zinadai kuwa wasanii wa bongomovie wanachanga fedha hizo ili wazilipe na tayari inasemekana Wema Sepetu amezitoa fedha hizo zote kutoka mfukoni mwake.

Mrembo huyo na mumewe Faraja Chambo walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu ambayo ni pamoja na kula njama ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa kwa kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam.

Shtaka la pili ni ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010 waliamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007. Shitaka la tatu ni la kutakatisha fedha ambalo walilitenda Aprili 14 mwaka 2010 huku wakijua ni kinyume cha sheria.

AFYA YA KIBANDA YAANZA KUIMARIKA NA AMEWEZA KUSIMAMA

 Hope all is well.
Salamu nyingi saaana toka JBG!
I could not resist! Yes I cried! But Absalom is the same person I knew last two months! Amesimama! Mungu ni Mwema!!!
Anaomba watanzania wamwombee na amesema anaendelea vizuri kwa sasa…
Cheers,
Hoyce Temu.

KAULI YA RAIS KIKWETE KUHUSU UCHAWI KWENYE SOKA LA BONGO

Moja kati ya kauli ambazo zimeingia kwenye headlines za michezo kwa wiki iliyokwisha ni kauli ya President Jakaya Kikwete, kauli kuhusu ushirikina kwenye soka la bongo aliyoitoa wakati akizindua uwanja mpya wa club ya soka ya Azam Chamazi Dar es salaam.

Namkariri akisema “najua mtapata tabu sana mkiwaleta hapa watasema kiwanja hiki kina namna, yote ni ushirikina tu…. ni wale ambao hawataki kuwekeza kwenye maendeleo ya mchezo, wanataka kuwekeza kwenye mambo ya kipuuzi… we tangu lini uchawi ukacheza mpira? ingekua uchawi unacheza mpira Afrika ingekua ina kombe la dunia na hatunyang’anywi, nyie hamjajua kwamba jambo hili la kipuuzi? mnawekeza pesa nyingi kwenye kamati ya ufundi hakuna chochote, haiwafikishi kokote”

Rais aliongeza  kwa  kusema “wekeza kwa kocha mzuri, vifaa vizuri, mafunzo mazuri, wachezaji walale mahali pazuri, Uwanja wa Azam Complex ni mzuri na wa kisasa, kuna sehemu ya mazoezi, vijana wanalala sehemu nzuri… ndio maana naamini nyinyi hakuna sababu ya kutofanikiwa"

" RAY AFUNGUKA KUHUSU SAKATA LA FILAMU YAKE YA "SISTER MARRY" ILIYODAIWA KUFUNGIWA

Mwigizaji mahiri wa Bongo Movies Vicent Kigosi maarufu kama Ray amewatoa hofu mashabiki wake kuhusu filamu yake ya ‘Sister Mary’ kuwa haijafungiwa japo kuna baadhi ya sehemu wameambiwa wazifanyie marekebisho na baadaye itakuja kutoka.

Ray amekuwa akilalamikia wahakiki wa kazi za wasanii kutowatendea haki pale wanapowapelekea kazi ambazo zinawagusa wahakiki na kushindwa kuzitendea maamuzi yalio sahihi.

“Kuna udhaifu mkubwa katika kuhakiki kazi ya mwisho ya msanii kwa kuwa wanaohakiki mara nyingi hawapendi filamu inayowagusa na kuwakosoa,” amesema Ray.

Sister Mary ilidaiwa kuwa inalidhalilisha kanisa katoliki na hivyo mapadre kutaka ipigwe marufuku.