Sunday, August 26, 2012

BINADAMU WA KWANZA KUFIKA MWEZINI AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 82

                                                                       Neil Amstrong
Buzz Aldrin yeye alikuwa wa pili kukanyaga mwezini nyuma ya Neil japo wote walikuwa katika mission moja hiyo ya Apollo 11.
Neil Amstrong alikanyaga kwa mara ya kwanza mwezini yeye akiwa wa kwanza July 20 1969
Alama hiyo ya mguu inaonyesha jinsi gani mwezini ni kama ardhi  laini sana kama poda hivi.
Mission hiyo ya Apollo 11 ilifanyika mwaka 1969 na yeye akiwa kiongozi wa msafara wa watu watatu kuelekea mwezini.
Neil Amstrong kushoto na mwenzake Buzz Aldrin kushoto wakiwa tayari mwezini na kuweka bendera ya Marekani.Walikaa mwezini kwa masaa matatu tu.
 Ilikuwa  july 6 1969 wakijiandaa kuondoka huku wakipunga kuaga na yeye mbele kabisa kuingia kwenye van iliyowapeleka kwenye rocket tayari kuanza safari kuelekea mwezini.
Neil Amstrong amefariki dunia baada ya kutokea complications akifanyiwa oparation ya moyo .Neil Amstrong amefariki akiwa na miaka 82.Dunia itamkumbika kwa rekodi yake ya kihistoria ya kuwa binadamu wa kwanza kuingia na kukanyaga mwezini.
                                                       Akiwa na Presedent Obama 2009.

Matukio ya CHADEMA-M4C Houston







                                                          Mh. Mbowe akiwasili
                                                            Wadau waliohudhuria
                                                                 Wadau wakipata picha





HII KALI JAMANI WATANZANIA MILLA NA DESTURI TUMEZITUPA WAPI??????: MTOTO AOA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA BABA YAKE KUFARIKI.

                                                Joseph Mapunda (Mtoto)
                                                     Mama Condorada Ngonyani

                                    Mama na Mtoto wake(Mume na Mke)

Mama Condorada Ngonyani mwenye umri wa miaka 70 anaishi kinyumba kama mke na mume na mwanaye wa tatu wa kumzaa mwenyewe akidai kuwa mara baada ya kufariki mume wake, Mzee Mapunda alimchagua mtoto wake amrithi baba yake.

Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na wtoto kuangalia kati sheria inayomruhusu Mtoto na Mama Mzazi kuweza kuishi kindoa

Umati wa watu wapatao 400 ulifurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo Namabengo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma wakiiomba Serikali ichukue Mkondo wa Sheria dhidi ya condorada ngonyani na joseph Mapunda.

Joseph Mapunda mwenye umuri wa miaka 40 amesema ameweza kuishi kindoa na Mama yake Mzazi Condorada Ngonyani 70 baada ya yeye kukubaliana wenyewe yeye na mama yake mzazi kuishi kindoa kama mume na mke.

Joseph Mapunda ana sema upendo ni upendo amempenda mama na anaishi kindoa wamependana nyie watu mnataka nini kwetu ?

Alipo ulizwa Mama alikiri kuwa kweli wameishi kindoa kwa miaka 10 na anampenda Mume wake ambaye ni Mtoto wake Joseph Mapunda.

Mama Condorada Ngonyani anasema mara baada ya kufariki mume wake Mzee Mapunda alimchagua mtoto wake amrithi baba yake.

Chanzo:blog ya Wananchi

Magazeti ya Leo Jumapili 26th August 2012


















Kundi La Afrika Lakutana Katika Mkutano Wa Mabadiriko Ya Tabia Nchi Nchini Thailand


Mkutano wa Kimataifa wa mabadiliko ya Tabia nchi umeanza Nchini Thailand mjini Bangkok kama mkutano wa maandalizi ambapo, kundi la nchi za Africa zimekutana na kujadili mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na namna ya kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.

Kundi hilo la nchi za Afrika, Likiongonzwa na uwenyikiti toka nchini Swazland, pia unategemeea kupata taarifa ya mikutano mbalimbali iliyofanyika baada ya ule uliofanyika mjini Bonn mwezi May 2012.

Suala la kuhimili mabadiliko ya tabianchi bado limejitokeza kuwa ni kipaumbele kwa nchi hizo za afrika.

Tanzania ambayo ni waratibu wa masuala ya hasara na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi kwa niaba ya Afrika, iliwasilisha ripoti ya mkutano wa wataalam uliofanyika Nchini Ethopia mwezi Agosti 2012 uliohusu hatua zinazofaa kumudu hasara na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabi nchi, ambapo Sudan imegusia suala la muendelezo wa washiriki katika mikutano hii ili kuweza kupata michango mizuri ya mawazo na kitaaluma wakati wa majadiliano katika mkutano huo kutokana na yaliyojitokeza Ethipia ambapo wataalam wengi hawakushiriki.

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika mjini Durban mwaka 2011 ulikubaliana kuanzishwa kwa chombo cha (ADP) ambacho, kitakachosimamia majadiliano ili kupata mkataba mpya utakaohusisha nchi zote katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkutano huu wa Bangkok ndiyo mwanzo wa mchakato wa utekelezaji wa (ADP) ambapo unatakiwa ukamilike kabla ya mwaka 2015, Mkutano huu, unategemea kusikia na kujua, chombo hicho kitafanya nini katika malengo yake ya kuhimili na kukabilianana mabadiliko ya tabia nchi, kupunguza gesi joto, kujenga uwezo katika eneo hilo pamoja na masuala ya sayansi na teknolojia na masuala ya fedha kugharamia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.

Wakati huohuo, Kundi la nchi za Afrika pia limegusia kuhusu, mkutano mkubwa wa masuala ya mazingira utakaohusisha mawaziri wa mazingira kutoka nchi za Afrika utakaofanyika mjini Arusha mwezi September, ambapo wataalam watapata nafasi ya kujadili nafasi ya Afrika katika suala zima la mazingira ikiwa ni pamoja na kipengele cha mabadiliko ya tabia nchi kuelekea mkutano wa dunia wa mabadiliko ya tabia nchi utakaofanyika mjini Dhoha mwezi disemba mwaka huu.