Saturday, July 21, 2012

Umoja Wa Mataifa Watoa Mkono Wa Pole Kwa Watanzania

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akisaini kitabu cha Maombolezo ambacho kimefunguliwa katika Ubalozi  wa  Kudumu wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania katika Umoja wa  Mataifa.  Katika Salamu zake, Naibu Katibu Mkuu ameelezea kuguswa kwake na tukio la ajali  ya kuzama kwa meli  na  hasara iliyotokana na ajari hiyo ikihusisha pia kupotea kwa maisha ya watu. Mhe. Jan Eliasson ni miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika kutoa salamu zao za pole na kuungana na watanzania katika kipindi hiki cha majonzi.
 Naibu Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akizungumza na Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere mara baada ya kusaini kitabu cha  maombolezo ambapo   alielezea  namna gani anavyoifahamu Tanzani na mapenzi yake makubwa kwa nchi hiyo  na kwamba ni kama miaka miwili tu iliyopita alikuwa Kisiwani Zanzibar.   Katika salamu zake za pole  Mhe.  Elliasson amesema sala na dua zake anazielekeza kwa wahanga wa tukio hilo,  Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwamba Umoja wa Mataifa uko pamoja na watanzania katika  kipindi hiki kigumu.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Mhe. Jan Eliasson ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufutia ajali ya kuzama kwa meli iliyotokea hivi karibuni.

Katika salamu zake ambazo amezitoa wakati akisaini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Naibu Katibu Mkuu amesema, ameshtushwa na kuguswa sana na taarifa za tukio la kupinduka na hatimaye kuzama kwa meli, tukio ambalo limesababisha kupotea kwa maisha ya watu.

“ Ninapenda kutoa salamu zangu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wa pande zote mbili. Nimeguswa sana na taarifa hizi, sala na dua zangu zinakwenda kwa wahanga wote wa tukio hili. Mimi Binafsi na Umoja wa Mataifa tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu ” Amesema Naibu Katibu Mkuu.

Katika mazungumzo yake na Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere mara baada ya kusaini kitabu, Mhe. Jan Eliason amesema anaifahamu vema Tanzania na kwamba miaka miwili iliyopita alikuwa Kisiwani Zanzibar.

“ Ninaifahamu vizuri sana Tanzania, nimefanya kazi kwa karibu sana na Dkt. Salim Ahmed Salim, bado ninakumbukumbu nzuri sana za Tanzania. Na nililikuwa kisiwani Zanzibar kama miaka miwili hivi iliyopita. Kwa kweli tukio hili limenigusa sana”. Akasema Naibu Katibu Mkuu raia wa Sweden ambaye aliteuliwa hivi karibuni kushika nafasi iliyoachwa na Dkt. Asha-Rose Migiro.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika hapa Ubalozini kutoka salamu zao za pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwa Watanzania wote .

14 Wauawa Katika Shambulizi Marekani

                                                          Ukumbi wa Sinema mjini Denver

Rais Barack Obama na mkewe Michele wameelezea masikitiko yao kufuatia mauawaji ya watu kumi na wanne mjini denver huko colorado.

Obama alisema kuwa serikali itafanya kila juhudi kuwasaidia watu wa eneo la tukio, la Aurora wakati huu mgumu.Alikiri kuwa serikali itakahakikisha aliyehusika anakamatwa.

Mtu mmoja aliyekuwa amefunika uso wake kwa barakoa aliwauwa kwa kuwapiga risasi watu hao kumi na wanne na kuwajeruhi takriban hamsini wakati wa onyesho la filamu ya Batman,The Dark Knight Rises.

Walioshuhudia tukio hilo kwenye kitongoji cha mji huo cha Aurora walisema mtu huyo aliyekuwa amevalia kifaa cha kujikinga dhidi ya gesi aliingia ndani ya ukumbi huo na kurusha gesi ya kutoa machozi. Pindi gesi ilivyojaa kwenyen ukumbi huo mshukiwa akaanza kuwafyatulia waliokuwemo risasi.

Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

YANGA SASA INATISHA, YAWACHAPA APR 2-0 KAMA WAMESIMAMA,

                                                               Kikosi cha Yanga
Yanga SC; Yaw Berko, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Nizar Khalfan.
Benchi; Ally Mustafa ‘Barthez’, Rashid Gumbo, Shamte Ally, Jerry Tegete, Juma Seif, Idrissa Assenga, Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo na David Luhende.
Kocha; Tom Saintfiet (Ubelgiji)
                                                                    Kikosi cha APR
A.P.R.;  Jean Claude Ndoli, Mbuyu Twite, Kabange Twite, Mugiraneza Jean, Leonel St Preus, Johnson Bagoole, Iranzi Jean Claude, Ngabo Albert, Tuyizere Donatien, Suleiman Ndikumana na Olivier Karekezi.
Benchi; Ndayishimiye Jean, Kwizera Ernest, Habib Kavuma, Mubumbyi Barnabe, Ngomirakiza Herman, Danny Wagaluka na Sekamana Mzime.
Kocha; Ernest Brandy (Uholanzi).
Kocha wa APR, Ernest Brandy kulia akiwa na kocha wa Yanga, Tom Saintfiet kabla ya mechi
                                           Kiiza akiwa amembeba juu Bahanuzi kumpongeza
Yanga imechukua ushindi wa goli mbili bila kwenye mechi ya Jana na APR magoli yaliyofungwa na Said Bahanuzi kwenye dakika ya 23 na 67.

Kwa idadi hiyo ya magoli, Bahanuzi anatimiza magoli manne toka michuano ya Kagame ianze.

APR walibadilika kwenye kipindi cha pili na kulishambulia goli la Yanga pasipo mafanikio ya kufunga pamoja na nafasi nzuri walizopata, Kama goli la dakika ya 43 la Yanga lisingekataliwa basi Yanga ingeondoka na ushindi wa 3-0.

Magazeti ya leo Jumamosi 21st July 2012