Wednesday, March 6, 2013

MATUMAINI AIOMBA SERIKALI IMSAIDIE MATIBABU....

 KOMEDIANI maarufu Bongo, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ ameiomba serikali imsaidie kupata matibabu ili aweze kupona maradhi ya figo na ini yanayomkabili.

Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam alisema: “Hali yangu bado si nzuri ingawa natumia dawa lakini sijapata tiba sawasawa. Sina fedha na familia yangu kwa sasa imeishiwa kwa sababu magonjwa yanayonisumbua ni makubwa na yanahitaji fedha nyingi.

“Naiomba serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo isikie kilio changu. Hali yangu si nzuri, nahitaji msaada ili kuokoa maisha yangu. Nina imani  nikipata tiba kamili nitapona na kurejea tena jukwaani.”

Umoja wa Mataifa walaani vitendo vya kushambuliwa albino nchini Tanzania

 Umoja wa mataifa umelaani vikali vitendo vya kushambuliwa kikatili walemavu wa ngozi, albino nchini Tanzania kutokana na imani za kishirikina.

“Ninalaani vikali mauaji na mashambulio haya ambayo yamefanyika katika mazingira ya kutisha na ambayo yamehusishwa kukata viungo vya watu wakiwemi watoto wakati wakiwa hai,” alisema jana kamishna mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa Navi Pillay.

JAMES MBATIA AJITOA TUME YA KUCHUNGUZA UBOVU WA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE


    Mwenyekiti  wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amejitoa kwenye Tume ya serikali kuchunguza chanzo cha kushuka kwa kiwango cha kustisha cha matokeo ya kidato cha nne, iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

 Mbatia ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wajumbe wa tume hiyo yenye wajumbe 15, alisema kamwe hatoweza  kufanya kazi yake kwa uhuru kwa sababu  ni Mbunge wa kuteuliwa, kamati hiyo imeundwa na serikali hivyo lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.

Hatua hiyo imekuja siku tatu baada ya chama hicho kumwandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kikimuomba aunde tume ya kudumu ya elimu nchini.

MHARIRI MKUU NA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ABSALOM KIBANDA AVAMIWA USIKU WA MANANE NA KUJERUHIWA VIBAYA

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na Dimba, Absalom Kibanda amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake wakati akiingia nyumbani kwake Mbezi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kibanda alivamia majira ya saa sita usiku wa kumkia leo, akitokea kwenye majukumu yake ya kila siku. Inadaiwa kuwa alichomolewa kwene gari, akapigwa na vitu vyenye ncha kali kichwani, ametobolewa jicho lake la kushoto pamoja na kunyofolewa kucha na baadhi ya vidole na hatimaye kutupwa umbali kidogo ya nyumbani kwake.

HUYU NDO MWANAMKE ANAYEOLEWA NA 2FACE WIKI HII


Blogger maarufu wa Nigeria Linda Ikeji ameripoti kwamba staa wa muziki 2Face Idibia anatarajia kufunga ndoa ya kimila ijumaa hii tarehe 8 March 2013 na party nyingine ya harusi itafanyika Dubai.

VURUGU ZA IFUNDA SECONDARY:..MKUU WA SHULE ANUSURIKA KUUAWA.KISA NI "BARAGHASIA" DARASANI WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, jana walifanya vurugu kubwa shuleni hapo na kutaka kumuua Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shaaban Nsute. Katika vurugu hizo ambazo zilianza juzi jioni hadi saa tano usiku, wanafunzi hao ambao walivalia kininja na kuficha sura zao wakiwa na visu mkononi, walivunja vioo vya madirisha shuleni hapo. Wanafunzi hao wanadaiwa kumfuata Bw. Nsute nyumbani kwake lakini alikimbia na kwenda kujificha kwenye shamba la mahindi ambapo wanafunzi hao walimpiga mlinzi wa shule Bw. Yasini Luhala kwa mawe akiwa katika ofisi yake. Akizungumza na Majira jana, Bw. Nsute alisema chanzo cha vurugu hizo ambazo zilidhibitiwa na Jeshi la Polisi ni baada ya mwanafunzi mmoja shuleni hapo kuvaa kofia zinazotumiwa na Waislam (baraghashia). Alisema mlinzi wa shule hiyo, Bw. Luhala alimnyang'anya kofia hiyo ili asiingie nayo darasani kwa sababu si sare ya shule lakini mwanafunzi huyo alichukua uamuzi wa kwenda kuwaita wenzake na kufanya vurugu. Aliongeza kuwa, kutokana na vurugu hizo zaidi ya wanafunzi 30 wamefukuzwa shule na kuwataja baadhi yao kuwa ni Sadi Mwamed, Jamal Hashim na Athuman Ibrahim wanosoma kidato cha tano. Wengine ni Abdulazizi Hussein na Ally Abdallah wanaosoma kidato cha nne. Mwanafunzi aliyenyang'anywa kofia alidai Waislamu katika shule hii wanatengwa, kunyanyaswa na kuzuiwa wasifanye mambo yanayoendana na dini yao. Hawa wanafunzi walikuja nyumbani kwangu usiku na kugonga mlango, nilitoka mlango wa nyuma nikakimbia kwenye shamba la mahindi, mke wangu alifungua mlango na kuwaambia sipona alipowahoji wakamwambia walikuwa wakinihitaji ili niende nao Msikitini kuna kazi muhimu, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Letisia Warioba, alisema tukio hilo limemsikitisha sana. Alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufika mapema eneo la tukio, kutuliza vurugu na kuimarisha ulinzi shuleni hapo hadi asubuhi na kuwataka wanafunzi waliobaki, waendelee na masko kwa kuzingatia taratibu za shule.

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, jana walifanya vurugu kubwa shuleni hapo na kutaka kumuua Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shaaban Nsute.

Katika vurugu hizo ambazo zilianza juzi jioni hadi saa tano usiku, wanafunzi hao ambao walivalia kininja na kuficha sura zao wakiwa na visu mkononi, walivunja vioo vya madirisha shuleni hapo.

Wanafunzi hao wanadaiwa kumfuata Bw. Nsute nyumbani kwake lakini alikimbia na kwenda kujificha kwenye shamba la mahindi ambapo wanafunzi hao walimpiga mlinzi wa shule Bw. Yasini Luhala kwa mawe akiwa katika ofisi yake.

Akizungumza na Majira jana, Bw. Nsute alisema chanzo cha vurugu hizo ambazo zilidhibitiwa na Jeshi la Polisi ni baada ya mwanafunzi mmoja shuleni hapo kuvaa kofia zinazotumiwa na Waislam (baraghashia).

MAPENZI YA FACEBOOK: BIBI WA MIAKA 67 AUAWA NA MPENZI WAKE WA MIAKA 28 SIKU MOJA BAADA YA KUKUTANA LIVE...

Polisi wa Afrika Kusini bado wanaendelea kuchunguza tukio la kutisha linalodaiwa kufanywa na kijana wa Kinigeria mwenye umri wa miaka 28 ambae anatuhumiwa kumuua bibi wa kizungu mwenye umri wa miaka 67 huko Johannesburg.

Bibi kizee Jette Jacobs ambae ni raia wa Australia alisafiri mpaka Johannesburg kwa lengo la kufunga ndoa na mwanaume anayempenda lakini siku mbili baada ya kukutana na mwanaume huyo, bibi huyo amekutwa amefariki kwenye mazingira ya kutatanisha kwenye jiji hilo lililo kwenye list ya majiji hatari kwa uhalifu duniani.

MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA YAWAFANYA POLISI WAMCHUNGUZE RAY C

 ILI kuhakikisha harudi tena kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, jeshi la polisi nchini, limemweka kati mwanamuziki Rehema Yusuf Chalamila ‘Ray C’.

Kamanda wa jeshi la polisi, kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya nchini, Godfrey Nzowa, amesema kuwa Ray C kila anapotembea anakuwa katikati ya askari wanaofuatilia nyendo zake.

“Kila anapokwenda, askari wamemzunguka. Tangu alipopata nafuu, tumekuwa tukihakikisha havutiwi na makundi mabaya, vilevile tunataka kuona kweli amejirekebisha,” alisema Nzowa na kuongeza:

“Ray C mwenyewe haoni lakini kila anapotoka, askari wanamuweka katikati. Kwa kifupi kipindi hiki tumemuweka katikati yetu, kwani hata anapokuwa nyumbani, tunachunguza nani anaingia na anapeleka nini.”

Nzowa aliongeza kuwa kitengo chake kimeamua kumuweka kati Ray C kwa sababu mbili, moja ikiwa kubaini na kuwanasa wauzaji wanaomharibu mwanamuziki huyo, pili ni kufuatilia kama msaada uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete umefanya kazi yake ipasavyo.

“Mheshimiwa (JK) alitoa msaada wa matibabu kwa Ray C kwa nia njema, vilevile dada huyo aliapa mbele yake kama hatarudia tena. Sasa ni lazima kufuatilia na kudhibiti asije kuingia kwenye vishawishi, akakiuka kiapo na matokeo yake alichokifanya mheshimiwa kikaonekana hakina maana,” alisema Nzowa.

Kwa upande mwingine, Nzowa alisema, hali ya Ray C inaendelea kuimarika na akaongeza: “Akili yake imetulia, anaweza hata kutunga nyimbo tofauti na alivyokuwa. Watu ambao anafungamana nao kwa sasa ni wazuri, siyo magenge ya wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya.”

Ray C, alisharipotiwa kuwa na hali mbaya baada ya kutopea kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya.

Hata hivyo, JK aliamua kujitolea kunusuru maisha ya mwanamuziki huyo kwa kugharamia matibabu yake mpaka apone.

Takriban miezi mitatu iliyopita, Ray C alitinga ikulu na kumshukuru JK kwa msaada aliompa, vilevile akawaambia Watanzania kwamba sasa anajisikia amepona na anaweza kufanya kazi.

BAADA YA KIFO CHA HUGO CHAVEZ, HII NDIO KAULI YA MAREKANI

Baada ya taarifa za uhakika kuripotiwa kwamba Rais wa Venezuela Hugo Chavez amefariki dunia, Rais Barack Obama wa Marekani amesema nchi yake imehamasika kuanza mazungumzo ya uhusiano mpya wa nchi hizo mbili.

Rais Hugo Chavez amefariki akiwa na umri wa miaka 58 akisumbuliwa na kansa ambapo taarifa yake ilitangazwa usiku wa kuamkia march 6 2013, alietangaza ni makamu wa Rais Nicolas Maduro ambae sekunde 40 baada ya kuanza kuzungumzia kifo hicho alishindwa kuzuia hisia zake na kulazimika kuwa kimya kwa muda kutokana na machungu.

UHURU KENYATTA BADO ANAONGOZA.....

Afrika ukikuta jogoo wawili wanagombana, basi, hapo hapakosi mashabiki. Na kila shabiki aliyesimama kutazama mpambano wa majogoo hao, ujue, kuwa ana jogoo wake anayemshabikia.

Na jogoo anayemshabikia akishindwa pambano, shabiki ataondoka akisononeka. Kuna ambao watakosa hata hamu ya chakula siku hiyo. Kisa? Jogoo wake kagalagazwa!

Na kama jogoo mmoja ni mnene na mwingine ni mwembamba, ujue, kuwa jogoo mwembamba ana mashabiki wengi.

Magazeti ya leo Jumatano 6th March 2013