Friday, January 11, 2013

magazeti ya Leo Ijumaa 11th January 2013

















Bongo movies wazindua kilimo kwanza

 Wasanii wa filamu, kutoka kushoto; Jacob Steven 'J B',  Vicent Kigosi 'Ray', Irene Uwoya, Wema Sepetu na Single Mtambalike 'Rick Rich' walipowasili Kwadelo kwa ajili ya kushiri uzinduzi huo wa kampeni ya Kilimo Kwanza kwa vijana wa Kata hiyo.
 Baadhi ya kinamama wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
 Wazee wa Kwadelo wakati wakimsubiri kuwasili kwa diwani wao pamoja wasanii hao

 Wema Sepetu akiungurumisha trekta ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Wapili Kulia ni Omary Kariat
 Wasanii hao wakimkabidhi sh. 500,000 mmoja wa wananchi wa Kwadelo walioathirika na mafuriko. Kwa mujibu wa Diwani Kariati (wapili kushoto), fedha hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Meembe ambaye ni mzee wa heshima wa kata hiyo.
Diwani Omary Kariati wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, baada ya kuwashili katika kata hiyo jana kuzindua Kampeni ya Kilimokwanza kwa Vijana wa Kata hiyo. Kutokana na juhudi za diwani huyo hivi sasa kata hiyo inayo matrekta 60 yanayotumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo ya alizeti na ufuta.

Uzinduzi wa one world football

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikabidhi Mipira kwa Ridhiwan B.Makame,wa Kaskazini A Unguja,wakati alipozindua mradi wa “ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA”,mradi wa Ugawaji wa mipira kwa vikundi mbali mbali vya vijana katika kukuza vipaji vya Mpira wa Miguu hapa Nchini uliofadhiliwa na Shirika hilo chini ya usimamizi wa Mwakilishi wake Sandra Cress,(wa pili kulia) sherehe hizo zilifanyika jana katikamUwanja wa Amaan Studium,katika kuadhimisha Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikabidhi Mipira kwa Ridhiwan B.Makame,wa Kaskazini A Unguja,wakati alipozindua mradi wa “ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA”,mradi wa Ugawaji wa mipira kwa vikundi mbali mbali vya vijana katika kukuza vipaji vya Mpira wa Miguu hapa Nchini uliofadhiliwa na Shirika hilo chini ya usimamizi wa Mwakilishi wake Sandra Cress,(wa pili kulia) sherehe hizo zilifanyika jana katikamUwanja wa Amaan Studium,katika kuadhimisha Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikabidhi Mipira kwa Ali Simai Mrisho,wa Kusini Unguja,wakati alipozindua mradi wa “ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA”,mradi wa Ugawaji wa mipira kwa vikundi mbali mbali vya vijana katika kukuza vipaji vya Mpira wa Miguu hapa Nchini uliofadhiliwa na Shirika hilo chini ya usimamizi wa Mwakilishi wake Sandra Cress,(wa pili kulia) sherehe hizo zilifanyika jana katikamUwanja wa Amaan Studium,katika kuadhimisha Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Serikali yalifufua shirika la reli

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete (yumo garini kushoto) akikagua sehemu ya kutua na kupaa ndege ya uwanja wa Tabora leo Januari 10, 2013 mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wake
 Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia)  na Waziri wa  Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe wakiongea wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Tabora leo Januari 10, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe Radhia Msuya mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataikfa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea mkoani Tabora alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku tano kukagua shughuli za maendeleo na kuzindua miradi mbalimbali

SERIKALI imetangaza hatua kubwa na kabambe za kufufua usafiri wa abiria na mizigo,  ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mabehewa na injini za treni, katika hatua kubwa za aina yake kuchukuliwa na Serikali kwa muda mrefu katika kurekebisha usafiri wa treni nchini.

Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Harrison George Mwakyembe ametangaza hatua hizo leo, Alhamisi, Januari 10, 2013, wakati alipokuwa anamkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuweka jiwe la msingi kwenye ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Ndege wa Tabora ikiwa ni tukio la mwisho la ziara yenye mafanikio makubwa ya siku tano ya Rais Kikwete katika Mkoa wa Tabora.

Mheshimiwa Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete na mamia kwa mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe ya uwekaji jiwe hilo la msingi kwenye Uwanja huo kuwa Wizara yake imeanza kubadilisha reli nyepesi, iliyochakaa na yenye uzito mdogo kwa Reli ya Kati.

Amesema kuwa kwa kupitia mashirika yake ya RAHCO na Shirika la Reli Tanzania (TRL) Serikali itafanya marekebisho hayo makubwa njia mzima ya Reli ya kati na kuwa mafundi wa mashirika hayo tayari wamefika Mkoa wa Morogoro.

Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete kuwa Serikali kupitia Wizara yake na mashirika yake hayo, imeagiza mabehewa mapya ya mizigo 274, imeagiza mabehewa mapya ya abiria 22, imeagiza mabehewa mapya ya kubebea kokoto 25 na pia imeagiza mabehewa ya breki (brake vans) 34 na tayari malipo ya awali yamefanyika.

Katika namna inayothibitisha dhamira ya Serikali kurekebisha hali ya usafiri wa reli nchini, Mheshimiwa Mwakyembe pia amewaambia wananchi kuwa Wizara yake pia imeagiza crane mpya na kubwa ya kubebea mizigo yenye uzito unaofikia kilo 100.

Kuhusu injini za treni, Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete kuwa zabuni kwa ajili ya kutengeneza upya (re-manufacturing) injini nane za treni imetolewa ili utengenezaji huo ufanyike, iwe ni ndani ama nje ya nchi.

Pia Waziri amesema kuwa oda imetolewa kwa ajili ya utengenezaji wa injini mpya 13 za treni ambazo malipo yake yatafanyika katika mwaka ujao wa fedha hata kama utengenezaji wa injini hizo utaanza.

Aidha, Waziri amesema kuwa Wizara kupitia mashirika yake hayo mawili imeagiza spea za kutosha kuweza kufanya ukarabati mkubwa wa injini tano kwenye karakana zilizoko hapa nchini.

“Mheshimiwa Rais, kwa hesabu nyepesi tu ni kwamba katika kipindi kifupi tutaweza kuwa na injini kiasi cha 26 ambazo zitarudisha uhai wa usafiri wetu wa reli kwa kiasi kikubwa sana,” Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete.

 Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

 10 Januari, 2013