Tuesday, December 4, 2012

CHAMPIONS LEAGUE


STORI KUHUSU USHINDI WA KILI STARS DEC 3 2012.

Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) itacheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji 2012 Alhamisi (Desemba 6 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mandela ulioko Namboole jijini Kampala, Uganda.

Kilimanjaro Stars ambayo itacheza mechi hiyo na mshindi wa robo fainali ya Desemba 4 kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia imeingia hatua hiyo baada ya kuitoa Rwanda Desemba 3 2012.

Mabao ya Amri Kiemba dakika ya 33 na John Bocco dakika ya 53 ndiyo yaliyoifanya Kilimanjaro Stars itinge nusu fainali na kuifungisha virago Rwanda (Amavubi) inayofundishwa na Milutin ‘Micho’ Sredojovic kutoka Serbia.

Vijana wa Kilimanjaro Stars wanaonolewa na Kim Poulsen walitawala pambano hilo, hasa kipindi cha kwanza kwa pasi fupi fupi. Kilimanjaro Stars imefungwa bao moja katika mechi nne ilizocheza tangu michuano hiyo ilipoanza Novemba 24 mwaka huu jijini Kampala.

Kilimanjaro Stars ambayo katika michuano hiyo iliyofanyika Dar es Salaam mwaka jana iliishia hatua ya nusu fainali iliwakilishwa na; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Amri Kiemba, Salum Abubakar/Athuman Idd, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, John Bocco na Mrisho Ngasa.

Kwenye line nyingine mwandishi Shaffih Dauda ameandika kuhusu Michuano ya kombe la Uhai kuanza disemba 7 2012 ni kwamba michuano hiyo inayoshirikisha timu za U20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kumalizika Desemba 22 mwaka huu.

Wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ni wale tu ambao usajili wao umefanyika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata leseni. Hakutakuwa na usajili mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi Kuu.

Taratibu zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya michuano hiyo.

TAARIFA YA KILICHOENDELEA KUHUSU KESI YA MWIGIZAJI LULU DEC 3 2012.

Kesi ya mauaji ya marehemu Steven Kanumba inayomkabili movie star wa Tanzania Elizabeth Michael (Lulu) imeendelea kutajwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam huku suala la umri wa mshitakiwa huyo likiendelea kuwekwa kiporo.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu AUGUSTINA MMBANDO, Wakili wa Serikali KENNETH SEKWAO amesema upelelezi bado haujakamilika na kwa sasa ipo katika hatua ya kutajwa.

Mapema baada ya LULU kufunguliwa mashitaka ya mauaji ya msanii mwenzake STEVEN KANUMBA April mwaka huu, mawakili wanaomtetea waliwasilisha hoja ya kupinga umri wa mshitakiwa huyo na kutaka achukuliwe kama mkosaji mtoto kutokana na umri wake kuwa chini ya miaka 18 hali iliyolazimu suala hilo kupelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoamua kulirejesha jambo hilo kwenye mahakama ya Kisutu.

Pamoja na kurejeshwa kwa suala hilo katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kumekuwa na ukimya wa muda sasa, kesi ya LULU imeahirishwa mpaka Disemba 17 mwaka huu ambapo itakwenda kwaajili ya kutajwa.

Magazeti ya leo Jumanne ya 4th December 2012