Wednesday, September 12, 2012

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AZUNGUMZIA CHANAGAMOTO ZINAZOIKABILI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  pamoja na ujumbe wake na wenyeji wakiongea na wanahabari na kisha kupiga picha ya pamoja baada ya  Mazungumzo yao Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Kenya  Jumanne, 11 Septemba , 2012,  kuanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ikiwa ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa ameshawahi kufanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi, Rais Kikwete ambaye amefuatana na mkewe, Mama Salma Kikwete, amepokewa na mwenyeji wake, Rais Mwai E. Kibaki na kwa mbwembwe zote za kiprotokali zinazoambatana na ziara rasmi za kiserikali.

Baadaye mchana, Rais amekwenda Ikulu ya Kenya ambako ametia saini kitabu cha wageni, akafanya mazungumzo ya faragha na Rais Mwai Kibaki kabla ya kufanyika kwa Mazungumzo Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili majirani na wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC).

Baada ya mazungumzo hayo, Rais Kikwete na ujumbe wake amekwenda kwenye Chuo Kikuu cha Kenyatta ambako wamepokewa na Waziri wa Elimu ya Juu, Mheshimiwa Margaret Kamar, Mkuu wa Chuo hicho, Jaji Mstaafu Onesmus Mutungi na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Olive Mugendi.

Kwenye chuo hicho ambacho Desemba 8, mwaka 2008, kilimtunuku Rais Kikwete Shahada ya Uzamivu ya Heshima, amefungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shule hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa utalii ni sekta muhimu sana katika chumi za nchi za Afrika Mashariki na ambayo mchango wake unagusa maisha ya maelfu kwa maelfu ya wananchi wa nchi za ukanda huo.

Rais pia amesema kuwa nchi hizo za Afrika Mashariki sasa zimekuwa ni eneo lenye mvuto mkubwa katika nyanja ya utalii ambao unaweza kuwaingizia wananchi na mataifa ya Afrika Mashariki mapato zaidi kama changamoto zinazoikabili sekta ya utalii kwa sasa zitashughulikiwa ipasavyo na kwa pamoja na nchi hizo.

Miongoni mwa changamoto ambazo Rais Kikwete amezitaja ni ukosefu wa miundombinu ya kutosha kufanikisha kwa namna bora zaidi sekta ya utalii, ukosefu wa juhudi za pamoja kuitangaza Afrika Mashariki kama eneo muhimu la utalii, na umuhimu wa kuboresha kiwango cha usalama wa watalii.

Aidha, Rais Kikwete amezielezea changamoto nyingine kuwa ni pamoja na umuhimu wa kuwepo na viza ya pamoja ya utalii kwa nchi zote za Afrika Mashariki, kuwepo kwa safari za ndege za kutosha kutoka kwenye mataifa makubwa yanayozalisha watalii kwa wingi kuja Afrika Mashariki na umuhimu wa kupungua kwa nauli za ndege za kuja Afrika Mashariki.

Jioni, Rais Kikwete ametembelea Taasisi ya Utatifi wa Kilimo ya Kenya (KARI) ambako anatarajiwa kupokelewa na Waziri wa Kilimo wa Kenya, Mheshimiwa Dr. Sally J. Kosgei na usiku alikuwa mgeni rasmi kwenye Dhifa ya Kitaifa ambayo itaandaliwa na mwenyeji wake, Rais Mwai Kibaki.

Leo Jumatano 11 Septemba, 2012  Rais Kikwete ataweka shada la maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta, kwenye Viwanja vya Bunge la Kenya na kutembelea Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary kwenye Barabara ya Thika.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara yake, Rais Kikwete atatembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi, ambako atapokelewa na Waziri wa Nchi wa Ulinzi, Mheshimiwa Yusuf Haji na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, Jenerali Julius Karangi.

Baadaye, Rais Kikwete atakwenda kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan ambako atapokelewa na Waziri wa Huduma za Matibabu, Mheshimiwa Anyang Nyong’o.

Baadaye jioni, Rais Kikwete, ambaye anaongozana na kundi kubwa la Wafanyabiashara wa Tanzania, atashiriki chakula cha jioni ambacho ameandaliwa na Jumuiya ya Wafanya Biashara ya Kenya.

Magufuli Akagua Barabara Ya Kilwa

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akijiridhisha kwa kupima kiwango cha lami inayowekwa upya katika barabara ya Kilwa na Kampuni ya Kajima ya Japan leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki, Balozi wa Japani nchini Tanzania Masaki Okada na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Kajima.
Wafanyakazi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Kilwa leo jijini Dar es salaam Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (wa pili kutoka kulia) Mbunge wa Kigamboni Dkt.Faustine Ndugalile (wa tatu kutoka kulia) leo jijini Dar es salaam. Daraja la Kigamboni linajengwa na kampuni ya China Railways Engineering kwa gharama ya shilingi bilioni 214 na linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015

Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari-Shirikisho La Ngumi Tanzania

SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA (BFT)
S.L.P 15558
DAR ES SALAAM.
September 11, 2012,
Email:-bft.tanzania 2009@gmail.com.

                             TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Yah:- BFT YAUNDA KAMATI YA KUFANIKISHA MASHINDANO YA NGUMI YA
TAIFA 2012.TAREHE 17-22/09/2012.UWANJA WA NDANI WA TAIFA.

Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limeunda kamati ya mashindano kwa lengo la kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha taifa. Kamati hiyo imeundwa kwa kuwajumuisha wataalamu wa ufundi kutoka kamati za BFT,mabondia wa zamani na wataalam wa mipango na fedha kutoka katika taasisi na mashirika ambayo yamekuwa mtari wa mbele kusaidia kwa vitendo shughuri na matukio mbalimbali ya BFT na kupelekea kusaidia kufuzu kwa bondia Selemani Kidunda kushiriki katika michezo ya Olimpiki iliyomalizika hivi karibuni London, Uingereza.

Wajumbe walioteuliwa kuunda kamati hiyo ya mashindano ni Andrew kweyeyana ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati,Willy Issangura,Juma Suleiman,Remy Ngabo na Mohamed kasilamatwi.
Wengine ni Said Omari,Antony Mwang’onda,Joel Magori,Charles Jilaba na Undule Mwampulo.
Jukumu walilopewa ni kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa kufata taratibu zote za chama cha ngumi cha dnia AIBA na kuhakikisha fedha za kuendesha mashindano zina patikana.
Majukumu ya kamati hiyo yatamalizika baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.
Nawatakia kazi njema kwa nia ya kutangaza mashindano haya .

Habari hizi zinaletwa kwenu na
Makore Mashaga
Katibu Mkuu (BFT)Mob:-0713/0784/0763/0773- 588818
Email:- mashagam@yahoo.com.

Rais Wa Somalia Anusurika Katika Shambulizi

Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud , amenusurika jaribio la kumuua mjini Mogadishu.Milipuko miwili imetokea nje la lango la makao ya rais huyo katika hoteli ya Al-Jazeera wakati rais huyo alipokuwa anajiandaa kufanya mkutano na waandishi wa habari.Taarifa zinasema kuwa waziri wa mambo ya nje wa Kenya Sam Ongeri pia alikuwa katika hoteli hiyo wakati wa shambulizi. Hata hivyo wawili hao wamenusurika. Inaarifiwa watu wanne wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa

Magazeti ya Leo Jumatano 12th September 2012

































MKUTANO WA 14 MAWAZIRI WA MAZINGIRA BARANI AFRIKA KUANZA LEO ARUSHA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Theresia Huvisa akizungumza na wandishi wa habari jijini Arusha jana kuhusiana na maandalizi ya mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira kutoka barani Afrika Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo.



Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) nchini Tanzania Mh. Theresia Huviza anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa Rais wa Mazingira kwa Afrika katika Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa mazingira unaofanyika Arusha nchini Tanzania kuanzia leo hadi tarehe 14 mwezi huu.

Waziri Huviza ataongoza kwa kipindi cha muda wa miaka miwili ambapo baada ya hapo nafasi hiyo itachukuliwa na nchini nyingine.

Mkutano huo umefanikishwa na European Union, Ubalozi wa Norway, Global Environmental Facility, UNEP na UNDP na wajibu mwingine ukifadhiliwa na serikali yenyewe.

Bajeti ya maandilizi ya mkutano huo imegharimu takriban dola za kimarekani 350,000 sawa na shilingi za Tanzania zaidi ya milioni mia 6.

Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(kushoto) akitoa maelezo mmoja wa wadau wa mazingira aliyefika katika banda la Umoja wa Mataifa lililopo katika jengo la AICC utakapofanyika mkutano wa 14 wa mawaziri wa Mazingira.

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu aktioa maelezo kwa mmoja wa wadau ya namna Umoja wa Mataifa inavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika utunzaji wa Mazingira kupitia mpango wa mazingira (UNEP) uliopo chini ya Umoja wa Mataifa.

Banda la ROA OZONE ACTION PROGRAMME chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais na UNEP wakitoa maelezo katika kutunzaji wa mazingira kwa wananchi.

Na.MO BLOG -Arusha