Friday, August 17, 2012

DULLY 'MTOTO WA KARIAKOO' OFFICIAL VIDEO .


KOFFI OLOMIDE JELA KWA KUFANYA FUJO.


Stori kutoka Kinshasa Congo DRC zimetoa uthibitisho kwamba mwanamuziki maarufu ambae jina lake lina uzito ndani na nje ya Afrika Koffi Olomide, amehukumiwa kwenda jela kwa miaka mitatu au kulipa faini.

Kilichomfanya apigwe hizo nyundo ni fujo alizozifanya akiwa kwenye hoteli moja maarufu Congo DRC pamoja na kumpiga meneja wake.

Nimemsikia mwandishi wa DW kutoka Congo akisema Koffi alikua akitetewa na zaidi ya mawakili 15 ambapo mamia ya mashabiki wake walihudhuria Mahakamani kusikiliza kitatokea nini kwenye kesi yake August 16 2012.

kabla  ya kufikishwa Mahakamani Koffi alikamatwa na polisi August 15 jioni muda mfupi tu baada ya kufanya fujo hizo na kuwekwa kwenye rumande ya mahakama ndogo Kinshasa kutokana na makosa aliyofanya hotelini ikiwa ni pamoja na kumpiga meneja wake ambae amekua akiishi Ulaya.

Mwandishi wa DW amesema ugomvi huo umetokana na Koffi kumdai meneja huyo euro elfu sita ambapo mashahidi kwenye eneo la tukio wamekiri kwamba Koffi alimpiga ngumi meneja wake pamoja na kuvunja mlango wa hoteli.

Hata hivyo meneja huyo aliwasilisha Mahakamani hoja ya kuondoa mashtaka yake dhidi ya Koffi na kupendekeza kuwepo kwa maridhiano kati yao lakini majaji walilipiga chini hilo ombi lake.

Baadhi ya wananchi waliotoa maoni kuhusu hiyo kesi ya Koffi wameunga mkono adhabu hiyo na kusema amezidisha, Ulaya ni yeye na kwengine ni yeye, mwingine amesema ni safi kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa yeye kutenda kosa.

Kutokana na adhabu hiyo kiongozi wa mawakili wanaomtetea Koffi amesema wamepanga kukata rufaa lakini wanasubiri maoni ya Koffi mwenyewe.… unaweza kuiskiliza hiyo ripoti ya Dw hapo chini pia.

BELINA AWA BALOZI WA NYWELE

                                                 Mwanamitindo Belina Mgeni.

MWANAMITINDO mwenye mvuto Bongo, Belina Mgeni amelamba shavu la nguvu kutoka kwa kampuni kubwa ya nywele nchini kwa kusainishwa mkataba wa mwaka mmoja kuwa balozi wa kampuni hiyo.

‘Akisemezana’ na Motomoto Newz, Belina alisema anamshukuru  Mungu kwa kupata shavu hilo ambapo sasa picha zake zitakuwa zikionekana katika mabango ya kampuni hiyo, pia atakuwa akisuka bure nywele kwa kipindi cha mwaka mmoja na kutumia bidhaa za kampuni hiyo kama balozi.

Aidha, mwanamitindo huyo alisema ataubeba ubalozi huo kwa umakini mkubwa  kwa sababu heshima waliyompa ni kubwa sana  kwa upande wa warembo  na wanamitindo wa hapa nchini.

Na Imelda Mtema

MAIMARTHA: WAMESHAANZA KUMCHOKONOA MUME WANGU:



MTANGAZAJI wa Kituo cha Runinga cha TBC1, Maimartha Jesse ameeleza kusikitishwa kwake na baadhi ya watu wasioitakia mema ndoa yake kwa kuanza kumchokonoa mume wake kipenzi, Shaa.

 Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Maimartha alisema kuwa, kuna watu ambao mara kwa mara wanamtumia sms za kumponda mume wake huyo wakieleza kuwa, eti hawaendani na ‘ameingia chaka’.
Alisema kuwa, kibaya zaidi mumewe amekuwa akizisoma meseji hizo lakini kwa bahati nzuri ni muelewa hivyo hakasiriki badala yake humtaka kuzipuuza kwani zinatumwa na watu wasiowatakia mema.

“Wapo watu walionitabiria mabaya na sasa yanawageukia, wapo pia wengine bado wananifuatilia wanataka kuivunja ndoa yangu lakini nawaambia watashindwa,nampenda mume wangu na naamini tutadumu,” alisema Maimartha.

Magazeti Ya leo Ijumaa 17th August 2012